Tanasha Avunja Ukimya Kuhusu Kupambanishwa na Zari
Mpenzi mpya wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh mrembo kutoka Kenya amefunguka kuhusu kupambanishwa na Baby mama wa Mpenzi Wake Zari The Bosslady.
Tangu Diamond aweke hadharani kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Tanasha Baada ya kuachana na Zari kumekuwa na mgongano katika ya timu hizo mbili za ushabiki wa Zari na Tanasha.
Lakini Tanasha ameibuka na kuzima tetesi zote za kuwepo na Bifu kati yake na Zari na kuweka wazi kuwa yeye una tatizo binafsi na mwanamama huyo na kuwataka watu wasiwachokonoe.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shabiki mmoja alimuuliza Tanasha kama anamfahamu Zari na yeye moja kwa moja alijibu:
Hapana simfahamu Zari lakini naamini ni mama wa Watoto wawili ambaye ni mchapakazi na watu tafadhali was he kutupambanisha na kuanza kututengenezea maugomvi yasiyokuwa na maana badala yake watuinue wote kwa pamoja”.