Taiya Haoni Shida Kufananishwa na Thea,
Baadhi ya mashabiki wa filamu na maigizo nchini Tanzania wamekuwa wakimfananisha mwigizaji Taiya Odero na Thea kuwa wanafanana kwa muonekano na jinsi wanavyoigiza katika filamu mbalimbali.
Akiongea na Clouds Radio Taiya anasema kuwa kwake yeye sio mbaya pale wanapomfananisha na msanii mkubwa na mkongwe kama Thea kwa sababu kwanza katika wasani aliokuwa akipenda kuwaangalia kipindi anaingia katika tasnia alikuwepo thea pia hiyo kwake anajivunia.
Watu wengi wamekuwa wakinifananisha na thae kutokana na ninavyoigiza japo mimi nafanya kama mimi lakini kunifananisha na mwigizaji mkubwa kama thea sioni shida kwa sababu ni moja kati a wasanii niliokuwa nawaangalia sana na kutamani kufanya nao kazi.–Alisema Taiya ambae kwa sasa anacheza vizuri nafasi zake katika tamthiliya ya Kapuni.
Hata hivyo mwanadada thea alipowahi kuulizwa kuhusu kufanana na mwigizaji huyo alisema kuwa haoni kama amefanana nae kwa sababu kila mtu ana utofauti wake.