Alichokisema Zaiid Kuhusu Darasa

Msanii wa muziki wa bongo fleva Zaiid anaetamba kwa sasa na wimbo wake wa picha amefunguka na kusema kuwa watu wasikae wakimsema vibaya Darasa kwa kitendo cha kukaa kimya  na kumsema kuwa amefulia lakini kitu cha kuzingatia ni kwamba kuna wimbo mmoja ambao msanii yoyote anaweza kufanya vizuri kuliko mwingine.

Darasa alichofanya katika wimbo wa muziki ni muziki mzuri kwaio haikuwa raisi , ku-hiy isiwe sababu ya kumshusha mtu vyeo hata siku moja , kuhit ni matokeo tu , kuna watu hawajui hata kuimba lakini wanaweza kutoa wimbo uka-hit.

ku-hit saa zingine kunaendana na matukio na kiki pia,kunaendana na vitu vingi sana , ukiona wimbo wako umefanya vizuri bila changamoto yoyote ujue kuwa wewe ni msanii mzuri na mkubwa sana.

Ikumbukwe kuwa baada ya Darasa kutoa wimbo wa muziki alitoa wimbo wa hasara roho na kisha kukaa kimya kabisa na hii iliwafanya mashabiki kuuliza sana huku wengie wakisema kuwa amefulia.

Wowowo Kumzungusha Zaiid Mikoa Yote Tanzania .

Msanii wa muziki bongo,Zaiid  amefunguka na kusema kuwa wimbo wake wa Wowowo Umefanya vizuri kiasi kwamba wimbo huo umeweza kumfanya afany show mikoa yote ya tanzania kwa mafanikio makubwa zaidi.Zaiid anasema kuwa kutokana na kufanya vizuri kwa wimbo huo na kuwa na show nyngi ndio sababu iliyomfanya ashindwe kutoa wimbo mwingine hivi karibuni kutokana na kuwa na u-busy mkubwa.

Mpaka ninavyoongea sasa hivi nilishazunguka almost mikoa yote ,ama basi umebaki mmoja au miwiwli tu na nimezunguka karibia mikoa yote na kufanya show tatu au nne kwa kila mkoa .

Hata hivyo mwanamuziki huyo anasema kuwa mpaka sasa ameshatoa video zaidi ya tatu lakini bado kuzitoa tu .