Kilio Cha Madee Kwenda Kwa Waziri Mwakyembe

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba na miondoko yake ya kuchana Madee Ali ‘Rais wa Manzese’ ametuma ujumbe mzito kwa Waziri Mwakyembe.

Madee amemtumia ujumbe  Waziri wa Habari, Sanaa, utamaduni na Michezo Dkt Harison Mwakyembe wa kumtaka kuliangalia suala la uchezwaji wa nyimbo za wasanii Kwenye vyombo vya habari.

Madee ameonekana kusikitishwa na vitendo vya asilimia kubwa ya vyombo vya habari kucheza ngoma za nchi za nje kuliko ngoma za wasanii wa Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Madee amemuomba Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo Dkt Harison Mwakyembe kuliangalia swala hilo huku wengi wakiamini kuwa linashusha hadhi ya muziki wa Bongofleva pia inawakatisha tamaa wasanii.

Mh Waziri wa habari na Utamaduni baba yetu Harrison Mwakyembe ngoma zetu hazionekanai kwenye television za nyumbani tunaangalia mangoma ya nje tu yanayopigwa na television zao tafadhali chezesha baba”.

 

Waziri Mwakyembe Amsifia Flaviana Matata

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amempongeza Mwanamitindo wa Kimataifa, Flaviana Matata kwa jitihada zake za kila siku katika kusaidia jamii.

Flaviana Matata ambaye makazi yake kwa sasa ni nchini Marekani ambapo ndipo anafanya kazi zake za uanamitindo amekuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi mbali mbali za kijamii.

Kwenye mazungumzo yake  na waandishi wa habari Jijini Dodoma Dkt. Mwakyembe amewataka vijana wa kitanzania kuiga mfano wa mwanamitindo huyo ili kuchangia katika ujenzi wa taifa.

Nawasihi vijana wengine wenye fursa kama za Flaviana Matata kuzitumia vizuri kwa kuhakikisha jamii inanufaika na mafanikio waliyoyapata.

 Lakini pia Mwanamitindo huyo amekuwa ni Balozi mzuri katika kupeperusha bendera ya Taifa katika nchi mbalimbali za Ulaya”.

Flaviana ameleza kuwa mbali na kujishughulisha na mitindo, ameweza kuanzisha kampuni ya Flaviana Matata Foundation ambayo inasaidia kutoa vifaa vya shule, ambapo hadi sasa amefanikiwa kutoa vifaa zaidi ya 5000 katika shule mbalimbali nchini.

Waziri Mwakyembe Azidi Kumfagilia Diamond

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezidi kumfagilia staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kudai kuwa yupo Kwenye listi ya wasanii 10 duniani wenye Sauti nzuri.

Mwakyembe amesema hayo kwenye mahojiano yake na kipindi cha KAA HAPA cha Mrisho Mpoto na kueleza kuwa Diamond kwenye video zake hana haja ya kutumia picha za ajabu ajabu kwani sauti yake ni dhahabu inajiuza.

“Kwenye tasnia yetu ya sanaa  vijana wetu  nyimbo nzuri sana, wana vipaji vya hali ya juu. kinacholeta matatizo hapa ni  picha ambazo haziendani na maadili yetu, kuchanganya na utupu ndani yake hivi vitu kwa kweli wafanye wengine lakini sio hapa. Tuchukulie kijana kama Diamond sauti yeke pekee yake inatosha kabisa kumuuza. Ukisema wasanii 10 duniani tuwe wakweli tuu! wenye sauti nzuri, Diamond huwezi kumtoa pale. Lakini huitaji kuuza ukaongeza na picha za ajabu ajabu wanaofanya hivyo ni wale wenye mapungufu ili kuficha ma’flat flat kwenye nyimbo zao Diamond yeye haitaji kufanya hivyo”.

Suala hili limekuja baada ya serikali kuingilia kati kazi za wasanii mbali mbali na hata kufungia baadhi ya wasanii kama Roma Mkatoliki na baadae kumfungulia.

Waziri Mwakyembe amesisitiza kuwa serikali haina ugomvi wowote na wasanii bali wapo katika jitihada za kulinda maadili ya nchi yetu.