Steve Nyerere Ameongelea Urafiki Wake na Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie na mwanasiasa Steven Nyerere amefunguka kuhusiana na urafiki na uhusiano wake na muigizaji mwenzake, Wema Sepetu.

Mapema mwaka huu kulikuwa na sintofahamu kati ya Wema na Steve Nyerere zilizotokana na kampeni za uraisi wa mwaka 2015, Hapo nyuma Wema, Steve na wasanii wengine wengi wa Bongo movie walipiga kampeni Chama cha mapinduzi (CCM) lakini habari zilikuja kutoka kutoka kuwa walilipwa fedha nyingi ili wapige kampeni hizo taarifa zilizoleta mkanganyiko lakini pia baada ya Wema kuhama chama cha CCM na kuhamia Chadema, mambo yalizidi kwenda kombo Kati ya Steve na Wema.

Alipohojiwa na Bongo 5 na kuulizwa kuhusu urafiki wake na Wema kwa sasa Steve alisisitiza kuwa Wema atabaki kuwa Wema kwake;

Mimi na Wema hatuwezi kuacha urafiki kwa sababu kwangu mimi Wema ni dada ni mtu ambaye tumesurvive naye tumehangaika naye kuhakikisha kwamba tunafika hapa tulipo na ni mzalendo kwaiyo mimi nataka kusema kwa sasa labda tumegawanyika tu kwenye vyama kwaiyo mimi nataka kusema kuwa Wema ataendelea kuwa Wema na Steve ataendelea kuwa Steve kwa sababu sisi wote ni binadamu na hujui kesho yako ukifa nani atakuzika yule ni Dada yangu na bado tunawasiliana na bado tunaendelea kupendana kama dada na kaka”.

 

Bongo Movie Nzima Hakuna Mwanamke Aliyetulia Kama Aunty Ezekiel- Steven Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie na mdau Mkubwa wa siasa, Steven Nyerere aliye maarufu zaidi kwa uwezo wake Mkubwa wa kuigiza sauti ya Marehemu baba wa taifa, Julius Nyerere amefunguka na kudai hakuna mwanamke aliyetulia kama Aunty Ezekiel.

Siku mbili zilizopita mkongwe mwingine wa Bongo movie Adam Haji au maarufu Kama Baba Haji alidai kuwa Aunty Ezekiel amepitiwa na wanaume wengi Kama Kanumba lakini yeye ndo alikuwa ana uhusiano naye wa kweli akimaanisha yeye ndo mwanaume pekee aliyetulia Nate ingawa wanaume wengi kwenye maarufu walimpitia.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Star Mix, Steven Nyerere alidai kuwa mwanamke anayemheshimu hivi sasa kwenye bongo movie ni Aunty Ezekiel kutokana na kuwa ni mwanamke ambaye hajajibweteka na amejitahidi sana kukusanya pesa anazozipata kufanya mambo ya maana kama alivyojenga nyumba maeneo ya Kigamboni tofauti na mastaa wengine hasa wanawake:

Yaani kusema ukweli kwa bongo movie kwa Bongo movie nampa sana heshima Aunty Ezekiel ni mdada aliyetulia na mzazi mwenzie amepata mtoto lakini bado ni mtafutaji tofauti na wanawake wengine hasa mastaa lakini pamoja na hayo yote ameweza kujitumia na kujenga nyumba tofauti na mastaa wengi wa Bongo Movie”.