Siku za nyuma kidogo Steve Nyerere alikuwa ni moja ya wasanii wa bongo movies ambao walikuwa wakilalamikia sana tasnia hiyo na kusema kuwa kwa muda mrefu tasnia hiyo imekuwa ikifanya kazi na wasanii wale wale na kurudia makosa makubwa kila siku kiasi kwamba watu wamechoka kuona wakifanya hayo hivyo hiyo ni sababu kubwa ya kufakwa bongo movies.
Lakini siku za hapa karibuni msaniii huyo ambae ndio amekuwa kama baba katika bongo movies anasema kuwa kwa sasa kazi za tamthiliya zimekuwa zikifanya vizuri sana kiasi kwamba inawezekana kabisa kuwa Afrika Mashariki ikawa ndio inaongoza kwa tamthiliya nzuri na zenye ubora kuliko sehemu nyingine yoyote ile.
Steve Nyerere anasema kuwa kwa sasa wasanii wameanza kujirekebisha na kutaka kuinuka tasnia hiyo , hivyo wameanza kujituma na kujitutumuanili kufanya kazi itakayowalipa lakini pia kuwaweka mashabiki wao katika nafasi nzuri ya kuangalia tamthiliya.
Tumesimama sana kwa afrika mashariki na hata magharibi sisi ndio tunaongoza kwa kuonyesha tamthiliya zenye ubora ,inaonyesha ni kwa jinsi gani Tanzania kuna vipaji.
Msanii wa maigizo na filamu bongo ambae pia ni mchekeshaji Steve Nyerere amekanusha taarifa zinazosambaa kuwa anaumwa UKIMWI.Steve Nyerere ambae wiki chache zilizopita alitangaza kuwa anaumwa sana na kwamba kama kuna mtu yeyote amemloga basi amsamehe kwa sababu maumivu hayo yamekuwa yakimtesa sana na kwamba mpaka sasa bado hajajua chanzo cha ugonjwa huo.
Steve Nyerere alipokuwa anaongea na waandishi wa habari alisema kuwa amesikia watu wakimuongelea na kusema kuwa anaumwa ukimwi lakini yeye kitu kinachomsumbua sio ukimwi bali ni maumivu ya mgongo na miguu inayomfanya kushindwa kuendelea na kazi zake lakini wale wanaokaa na kumsema kuwa anaumwa ukimwi wanampa kiki ya kuongelewa katika mitandao ya kijamii.
Ukiachana na Steve Nyerere kutangaza kuwa anaumwa sana , kuna baadhi ya wanawake waliojitokeza katika mitandao ya kijamii siku za nyuma na kusema kuwa Steve Nyerere ana umwa ugonjwa wa ukimwi na kusema kuwa wanauthibitisho kwa sababu hata wao wameupata ugonjwa huo kupitia yeye,
Steve Nyerere hivi karibuni amekumbwa na tuhuma hizo na kusemekana kuwa amekuwa akiwasadia wasanii wachanga kwa kuomba kufanya nao ngono na kusababisha kuwaambiza uginjwa huo alionao.
Msanii wa bongo movies steven nyerere amemuandikia barua msanii mwenzie Wastara Juma na kumpa pole juu ya matatizo ya maradhi yanayomkuta na kumtia moyo kuvumilia na kupambana na ugonjwa huo ikiwa yeye mwenyewe pia ni mgonjwa hoi kitandani.
Steve Nyerere amemwambia Wastara kuwa bongo movies ni wanafiki sana hivyo asikae akitegemea msaada mkubwa sana kutoka kwa wasanii zaidi ya kumuomba mwenyezi mungu amsaidie kukabiliana na hiyo hali ya ugonjwa.
Hata hivyo Steve amemwambia Wastara kuwa hata yeye ni mgonjwa na yupo kitandani anapambana na hali hiyo kwaio asikate tamaa maana hata yeye anaamini kuwa ipo siku atapona na kurudi tena barabara.”nipo tu kitandani napigania uhai wangu mama angu hakika miguu inanisumbua sana lakini ninaamini kuwa siku moja nitasisima tena , hakuna kukata tamaa na maneno ya binadamu kata tamaa na muumba wako tu”.
Steve amemwambia kuwa kwa kuwa ameomba msaada kwa watu, wapo wataotokeza kwa ajili ya kumsaidia lakini pia aangalie wapo wwatakaotokeaza kwa ajili ya kupata jina kupitia yeye ili jamii ijue kuwa alitoa msaada kwa familia yake”.kuna watu watajitokeza saahii kwa ajili ya kupata jina kupitia mguu wako kataa lakini wapo watakaojitokeza kwa ajili ya kukusaidia simama kuumwa ni ibada tosha.”
Akiendelea kmtia moyo steve nyerere amemwambia wastara kuwa watanzania wengi ni wenye huruma hivyo ipo siku mungu atamfungulia njia na watanzani watapata moyo wa kumsaidia wala hana haja ya kukata tamaa.”watanzania hawajawahi kukuacha, wewe kwangu ni malkia wa nguvu asante.”
Wiki kadhaa zilizopita Wastaar Juma aliomba msaada kwa watanzania na viongozi kusaidia kupata ela ya matibabu kwa ajili ya kurudi nchini India ambap alitakiwa kwenda tangu mwezi wa pili mwaka jana lakini ilishindikana kwa sababu ya kukosa pesa.
Msanii mkongwe wa filamu za Bongo movie na mwanasiasa mashuhuri Steve Nyerere ameongea kwa mara ya kwanza baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu na kudai kuwa anaumwa sana na kumsihi aliyemroga amsamehe.
Steve amefunguka na kusema kuwa anasumbuliwa sana maumivu makali kichwani na kwenye miguu yanayomtesa sana. Hivyo anaomba kama kuna mtu yoyote anayemroga amsamehe kwani maumivu aliyonayo ni makali sana.
Baada ya habari kusambaa mitandaoni kuwa Steve yuko hoi kitandani haraka sana habari za chini chini za kimbea zilidai kuwa Steve anasumbuliwa Ukimwi jambo ambalo Steve amedai kuwa wanaoendelea kuzusha waendelee tu kwani wanazidi kumpa umaarufu.
Steve amefanya mahojiano na Enews ya East Africa TV na amezidi kufunguk yafuatayo kuhusu maradhi yanayomsumbua:
Nasikia maumivu miguuni na kichwani lakini pia nilikuja kugundulika nina matatizo kwenye upande wa kushoto wa mapafu yangu lakini sahivi miguu hasa ndio bado inanisumbua. Nimeona kwenye mitandao yapo mengi yanayozungumzwa kuna wengine wanadai ni uchawi wengine wanasema nimeathirika na Ukimwi lakini sio mbaya mimi ni staa kwaiyo wacha waseme wanazidi kuniongezea umaarufu na wanataka kujua naumwa nini mimi naumwa miguu na ninachowaambia wanisamehe na kama wapo walinitupia hivo vitu au kuniroga naomba wanisamehe”.
Steve pia amewajia juu waliotangaza habari za yeye kuwa na ngoma kwani hakuna mtu aliyempima mpaka kutia taarifa hizo za uongo lakini pia Steve ameomba watu wamuombee maana gonjwa hill linamsababishia matatizo siyo kwake tu bali hata familia yake maana anashindwa kufanya kazi yoyote.
Ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuzagae kwa picha zikionyesha msanii wema sepetu na Mh.Paul Makonda wakiwa pamoja na kwamba wamemaliza tofauti walizokuwa nazo baada ya wema kuamiha chadema na baadae kurudi tena CCM, Steve Nyerere ambae inasemekana kuwa ndiye alifanikisha zoezi la Wema Sepetu kurudi CCM amefunguka na kuongelea swala la Paul Makonda kumsamehe Wema Sepetu.
Akiongea kwa njia ya simu na GPL, Steve Nyerere ambao alisema kuwa kwa wakati huo alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Dar alisema kuwa ni kweli tofauti za wawili hao zieisha na kila kitu kiko sawa sasa hivi wamejikita zaidi katika kujenga taifa na sio kufanya upinzani.
Hakuna uadui wa kudumu katika haya maisha ,isitoshe wale wote ni vijana wamekutana na kuombana msamaha na mambo yamebaki kuwa historia tu.wanaangalia maisha mengine ya mbele kwa sababu safari ni ndefu .Alisema Steve.
Steve anasema kuwa hata kama kulikuwa na tofauti kubwa kati ya wawili hao zilishaisha na ugomvi ule umebaki kuwa historia kwa sababu watu hao wameamua kukubaliana na kuwa kitu kimoja hakuna kilichobaki cha kutenganisha tena.
hili ni funzo kubwa sana hasa kwa wasanii kwamba watu wakogombana wasiongee mambo yote wakamaliza , kuna wasanii watu wakigombana wanaanza kuogea maneno ya ovyo ovyo kwa mkuu wa mkoa kupitia kwa wema sasa leo hao wamepata haya wao sura zao wanazipeleka wapi.-Alifunguka Steve
Hata hivyo kulikuwa na tetesi kuwa mama mzazi wa Wema haonekani nyumbani kwake Sinza Mori na kuwa inawezekana mama huyo amefichwa sehemu, Steve Nyerere amekanusha habari hizo na kusema kuwa mama huyo yupo nyumbani kwake hakuna alipofichwa kokote.
Nani amekwambia mama hayupo,mama yupo pale pale na mambo yanaendelea vizuri wala watu hawana haja ya kumtafuta popote-Alimalizia Steve Nyerere
Muigizaji na mwanasiasa Steven Nyerere amefunguka kuhusiana na tuhuma zinazomkabili rafiki yake Wema Sepetu kuhusu tuhuma za kuhamia CCM Kisa kuogopa kuvunjiwa nyumba.
Mapema wiki hii Wema alitangaza kuwa anahama Chadema chama alichohamia miezi michache iliyopita baada ya kuhama CCM. Baada ya kukaa Chadema kwa miezi michache Wema alitangaza kuwa ameamua kurudi nyumbani CCM jambo ambalo lilizua mijadala mingi kupita kiasi kwani kuna mengi yalisemwa.
Moja Kati ya jambo lililozua gumzo ni kuwa inaemekana kuwa Wema alikubali kirudi CCM kwasababu serikali imetishia kuvunja nyumba yao ya familia lakini pia inasemekana kuwa amehaidiwa kuwa kesi yake inayoendelea kuunguruma mahakamani kufutwa na kama angekataa kurudi CCM basi alitishiwa kwenda jela.
Rafiki wa karibu wa Wema na mwenzake kwenye mambo ya siasa Steven Nyerere amefunguka kuhusu tuhuma hizo za kuvunjiwa nyumba alipofanya mahojiano na Millard Ayo Tv:
Habari hizo sio za kweli na ukitaka kujua kuwa habari hizo sio za kweli utaona kuwa Wema bado ana kesi yake mahakamani hayo ni maneno tu ya mjini ambayo watu wanayaongea ambayo hawakatazwi kuyaongea kwani Watanzania sahivi wanacheza na mitandao wanapoteza muda mwingi na kubuni habari zitakazoleta uchochezi ambao hauna tija kwanza ile nyumba ipo miaka nenda miaka rudi leo hiiiwe hivyo kwa sababu gani mbona kuna watu wamefanya makubwa zaidi ya Wema na hawajavunjiwa Nyumbani zao huyo Wema avunjiwe kwa kubwa lipi alilokosa kwaiyo utaona habari hizi ni za uongi na uchochezi Wema amerudi mwenyewe CCM ameona jua linavyowaka ameamua kurudi nyumbani ili ajipange”.
Muigizaji wa Bongo movie na mwanasiasa maarufu, Steven Nyerere ameibuka na kudai kuwa kilichomtokea muigizaji Lulu Michael ni fundisho tosha kwa wait wote hivyo wajifunze kutokea kwake.
Alipofanya mahojiano na Millard Ayo, Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa kifungo alichopokea Lulu ni fundisho tosha kwa kila mtu hivyo kilichobaki ni kungoja muujiza kama itatokea wa kumuonea huruma na kumuachia huru.
Kusema ulweli nimejisikia huzuni Sana kwa sababu bado ni binti mdogo aliyepita katika misuko suko ya kiutu uzima ambayo hakustahili kwaiyo mimi nimevaa uhusika wa Lulu ili niangalie ingekuwa mimi ningefanyaje lakini nimeishia kuona kuwa hili ni jambo linalo huzunisha sana kwa familia zote mbili lakini kijana wa familia moja ameshapotea hatutamuona tena lakini huyu wa kike na yeye anaenda lupango kwa miaka miwili kitu ambacho sisi kama wananchi hatuwezi kuzuia kwa sababu mahakama imeshaamua lakini tusiache kumuombea ili Kama itatokea miujiza basi mwenzetu anusurike “.
Lakini pia Steve ameongeza kuwa kesi ya Lulu inatakiwa ichukuliwe mfano kwa vijana wengi ili owe fundisho kwa vitu wanavyofanya kwani kupigana na makosa mengine yanaweza kuwafikisha mbali hivyo ni muhimu kujifunza mapema.
Diamond Platnuz, Alikiba na Ommy Dimpoz wamekua wakitupiana maneno yenye mafumbo katika mitandao ya kijamii tangu Diamond aliposhirikishwa katika remix ya ngoma ya Fid Q ‘Fresh’.
Diamond alisema kwa wimbo huo kuwa hawezi kulinganishwa na Alikiba kisha Kiba naye akamjibu kwa fumbo kuwa yeye bado ndo mfalme.
Diamond tena aliweka wimbi nyingine kwenye account yake ya Instagram ambayo aliwachimba Alikiba na Ommy Dimpoz. Baada ya Diamond kuweka wimbo huo kwa Instagram, Ommy Dimpoz pia aliweka picha Instagram akiwa na mama mzazi wa Diamond na kuandika ujumbe wenye utata:
Ommy Dimpoz na mamake Diamond
“BARUA YA WAZI KWA BINTI YANGU MALKIA WA NGUVU
Salam zako nimezipata mwanangu Hivi kweli ww wa kukosa Adabu na kuamua kunichamba mimi Baba yako? Sasa kosa langu mimi nini???? Kwani kuna Ubaya kumtandikia Kitanda Baby wako King?
#UnanioneaKwaKuaSijuiKurap?
#SijuiNaMimiNimkatae??
#KamaYeyeAlivyomkataaWaMobeto
#YaniUnamkataaMjukuuWangu??
#UnakubaliKuleaWatotoWa5SioWako
#UmerogwaWWSioBureMwanangu
#NilikuwaNajuaNimezaaSIMBA
#KumbeNimezaaKIMBA
#DavidoNaeAnalalamiKuhusuENEKA
#UmeletaJanjaJanjaKwenyeFallOnU
#NnaedhalilikaMimiBabaYaKo??
#UtakujaKuniuaKwaPreshaJomoniiii?
#HayaNendaKatungeVesiNyingine?
#RahaYaVitaUsichagueSilaha
#BABAMALKIA
Steve Nyerere sasa ameingilia kati na kutoa ushauri wake, somo ujuembe aliondika kwa Instagram hapoo chini:
“NIMEKAA NIMEJIFIKIRIA NIMEONA NISEME KIDOGO, DUNIA MAMA ANA HESHIMA YAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE, MAMA NI KIOO CHA FAMILY MAMA NI NGUZO YA FAMILY MAMA NI KIMBILIO LA FAMILY , TUNAWEZA KUKOSEA KOTE LAKINI SI KWA MAMA NDOMANA AMNA LAANA YA BABA ILA LANA YA MAMA IPO NA INAFANYA KAZI HARAKA KULIKO KITU CHOCHOTE, SIZANI KAMA TUNA ELIMISHA JAMII KUPITIA MATUSI YA KUZALILISHA WAZAZI, NYINYI NI KIOO CHA JAMII, LAZIMA MUWE NA KIFUA CHA KUBAKISHA MANENO , MIMI NILIZANI HIZI NGUVU MNAZOTUMIA MNGEWEKEZA KWENYE MZIKI WENU TUNGEFIKA MBALI SANA , MMEJIJENGEA HESHIMA NA MMELITAFUTA JINA KWA SHIDA , ILA MNASAHAU JINA HILO LINAWEZA POTEA KWA SEKUNDE, NAWASHAULI NA NAKUSHAULI WEWE UNAYEZARAU WAZAZI FUTA KAULI NA OMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI ZAKO USUSANI KINA MAMA WOTE AMBAO NAAMINI NI MASHABIKI WAKO NA NDIO WALIOKUFANYA UKAFIKA HAPO, HATUKATAI NYINYI NI BINADAMU INAWEZEKANA MMEPISHANA KAULI ILA KWENYE KUPISHANA WEKENI AKIBA YA MANENO, KUNA KESHO HUJUI ATAKAYE KUSTILI, HAKIKA BUSARA ITUMIKE , YANI NINGEKUWA MIMI NDIO UMEMGUSA RITA WANGU IVO DOOOO, MJINGA HAJIBIWI, KICHAA HAKIMBIZWI , MWIZI SI RAFIKI, NANI KAMA MAMA, ESHIMA ITAWALE ASANTE BY #####UZALENDO KWANZA.”
Rafiki wa karibu wa Wema Sepetu amefunguka kudai kuwa hataki watanzania wamuhusishe na audio ambayo Mrembo huyo anasikika akiongea na Mbowe.
Steve Nyerere ambaye ni mchekeshaji anayejulikana sana Afrika Mashariki alitaka Watanzania wajue kwamba hawezi kumfanyia rafiki wake wa karibu jambo kama hilo alipokuwa akizungumza na Bongo 5. Steve alisema,
“Sio mimi yule na siwezi kufanya kitu kama kile, Ile sauti ukiisikiliza kwa makini utajua sio mimi na siwezi kufanya hivyo,”
Mbowe hata hivyo amekana kuwa sauti hiyo sio yake lakini kwa sasa watalaamu wanafanya uchunguzi kujua nani aliyesambaza audio hiyo.
Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai na Wema Sepetu wamekua wakitawala vichwa vya habari tangu sauti (voice note) ambazo zinadaiwa kuwa zao kuenea kwenye mitendao ya kijamii.
Voice note hio inaashiria kuwa Freeman na Wema Sepetu wana uhusiano wa kimapenzi lakini wawili hao walikana dhana hii.
Mchekeshaji Steve Nyerere amejipata pabaya kuhusu sakata ya Wema Sepetu na Freeman Mbowe. Mashabiki wa Wema na Freeman wanadai kuwa sauti ya kiume iliyoskika kwenye voice note hio ya utata ni ya Steve Nyerere.
Steve Nyerere na Wema Sepetu
Nyerere ako na kipaji cha kuigiza sauti mbalimbali za viongozi wa kisiasa na watu wengine mashuhuri; na hii ndo sababu ya watu kumlimbikizia lawama.
“Sio mimi yule na siwezi kufanya kitu kama kile. Ile sauti ukiisikiliza kwa makini utajua sio mimi na siwezi kufanya hivyo,” Steve Nyerere alijitetea kwenye mahojiano na Bongo 5.
Tofauti na wasanii wengine ambao walitoa salamu za rambirambi kufwatia kifo cha Ivan Ssemwanga, Steve Nyerere and Faiza Ally wameeleza hisia kali kuhusu kifo cha aliyekuwa mume wa Zari.
Waigizaji hao wa Bongo Movies wameongea matope kuhusu kifo cha Ivan, hisia zao kuhusu kifo cha mwenda zake zinaonyesha uadui tu.
“Alikuwa na pesa nyingi, alikuwa na uwezo wa kufanya chochote, alikuwa na uwezo wa kununua chochote lakini ameshindwa kununua uhai. Nimejifunza kitu kupitia wewe, tuishi vizuri na watu maana hakuna ajuaye kesho,” Steve Nyerere aliandika.
Steve Nyerere
“Binaadamu akikuchukia hata zuri kwake ni baya na ndio maana huwa na maisha yangu tu kama mimi bila kutaka kuwa yoyote, hakuna zuri mbele ya mtu mbaya. Unajua nini wala sijali naona upuuzi tu kama ya kipuuzi mengine yote yalio pita.
“Maisha yangu na wanangu yako kwenye mikono salama hata kushinda mikono yangu, yako kwenye mikono ya Mungu mwingi wa rehma. Leo Ivan na matajiri wengine wako wapi? Mali sio kila kitu kwenye maisha yetu tunahitaji amani, mapenzi, maelewano makubaliano.
Faiza Ally
“Nimetoka kwenye kutokua na mlo mpaka sasa namiliki milo, huo ni utajiri mkubwa maana kwanza ni kushiba akili ikae sawa ndio upange habari zingine, so at the end my heart is pure and that what give me amani ya moyo, hayo mengineyo tena yako nje ya uwezo wangu ni mipango ya Mungu, Faiza Ally aliandika.
Professor Jay alitetea haki ya wasanii wote Bungeni aliposimama kuchangia mapendekezo yake katika bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mbunge huyo wa Mikumi alisema TRA na mamlaka zingine za serikali zinawanyanyasa wasanii kwa kuwatoza kodi na ada zingine ambazo wasanii hawazi kumudu.
Tazama video hapo chini:
Kufwatia hatua ya Professor Jay kupigania haki za wasanii Bungeni, muigizaji wa filamu za Bongo – Steve amesema aliamua kummiminia sifa mbunge huyo.
“Mwenye akili anaanza kuelewa nalilia nini kwenye sanaa yetu..Sina haja ya kutukanana ni wajinga wanao tukana. Ukweli unadumu kuliko kitu chochote, ukweli huzaa amani..Asante Mhe. Haule kwa kuongea ukweli”. Alisema Steve kupitia ukurasa wake wa instagram