Steve Nyerere Aongelea Tangazo Lake Kuhusu Ndoa ya Wema.

Mwanabongo movis steve nyerere aliwahi kuweka post moja iliyozua maneno mengi sana katika mitandao ya kijamii kuhusu ndoa ya mwanadada wema sepetu na mwanaume mmoja anejulikana kwa jina la rahul.

Katika posti hiyo,Steve aliandika kuwa ndoa ya mwanadada huyo na Rahul inakuja soon. lakini alipojuwa akiongea na Ayo Tv , Steve alisema kuwa alikuwa anatania kwa lengo la kuwapima watanzania na uwaona watasema nini.

Nilikuwa tu natania , nilikuwa natania kwa sababu nilitaka kuona tempe ya watu, unajua kuwa ukikaa muda mrefu bila utani au kucheka inakuwa sio vizuri na kwa watanzania wanaopedna sana umbea na ndio maana nilitaka tu kuona.Watanzania wengi wanapenda sana umbea , hawapendi kufanya kazi ,kwaio unaangalia tu temper ya watu .

 

Steve Amekuwa na Mchango Mkubwa Kwa Wasanii Hasa Muda Wa Matatizo- Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ameibuka na kumkingia kifua Msanii mwenzake Steve Nyerere dhidi ya tuhuma za utapeli na Kula pesa za Michango ya rambi rambi.

Stevw Nyerere alijikuta katika wakati mgumu baada ya kila mtu kumnyooshea kidole na kumnanga kuwa misiba ikitokea anakuwa mstari wa mbele na kuchanganya michango ambayo anaishia kuitumia.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Irene Uwoya amemtetea Steve na kudai mchango wake mi mkubwa sana kipindi cha matatizo kwani watu wanakuwa hawajui wafanye nini hivyo yeye huwapa mwongozo kama kiongozi.

Kama Steve asingekuwa mtu wa kujitoa na kusimamia hiyo misiba tusongekuwa tunatoa heshima za mwisho sasa imekuja imegeuzwa kuwa Steven anasubiria misiba ili afaidike kitu ambacho sio cha kweli kwa sababu akisimama Steve msiba umetokea anasimama kweli kwa sababu msiba ni kitu cha ghafla tunakuwa hatujajipanga kwaiyo Steve anakuwa na uwezo wa kushika simu na kufanikisha mambo mbali mbali”.

Irene Uwoya amesisitiza kuwa Steve ni mtu muhimu sana Kwenye jamii na kama akijiondoa katika shughuli za kujitolea kama hizo lazima atakumbukwa maana mchango wake ni mkubwa sana.

Wasanii Waguswa na Tuhuma Zinazomkabili Steve Nyerere.

Baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali katika tasnia ya filamu wameona kuwa jambo linaliendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu kumsema Steve Nyerere ni jambo baya na linamkosesha amani yeye na familia yake.

Lakini pia jambo hilo limemfanya Steve ukata tamaa na kupoteza tena ule moyo wa kujitolea kila linapotokea jambo, na ndipo walipoanza kufunguka na kuomba wamuache Steve kumuandama kwa tuhuma za kuwa anakula pesa za rambirambi kweny misiba.

Faiza Ally anasema , wasanii wa bongo movies wameshndea kuelewa umuhimu wa steve na ndio maana tangu tuhuma hizi zianze wamekuwa kimya bila kuongea chochote.Lakini pia yeye anamini kuwa Steve ni mtu muhimu sana katikati yao anaewaunganisha kwa moyo wake tena bila kulipwa wala kuombwa.

Faiza anasema kuwa watu wanasahau kuwa steve amewasaidia mambo mengi tofauti na misiba , amekuwa nao katika harusi, katikakazi na dili nyingi mbalimbali lakini leo hii wanasahau na kukaa wakicheka tu pale wanapoona msanii huyo anatuhumiwa vibaya.

Faiza anawaomba wasanii wote kusimama na kuungana pamoja ili kumtetea na kukanusha tetesi zinamzomkabili Steve Nyerere ili kuendelea kuweka heshima yake.

Na kwa upande wa Aunty Ezekiel, anasema kuwa wasanii wamechagua kuzikwa na steve nyerere, hivyo waache kumbeza steve nyerere.

kila binadamu huwa anapewa  karama yakekatika hii dunia, tivu  hiyo ni karama yake.jamani tuacheni tumeamua wenyewe kuzikwa na tivu….I love you tivu akee.

Kwa upande wa soudy brown anasema kuwa pamoja na kwamba hapo awali jambo hili la steve llikuwa likichukuliwa kama utani lakini ifike  sehemu waavche kuendelea kufanya utani kwa sababu inamkatisha tamaa mhusika,kwa sababu katika familia yoyote kuna mtu mmoja huwa anatokea kwa ajili ya kuwaunganisha watu wote.

 

 

Steve Nyerere Akataa Kujihusisha na Msiba wa Mzee Majuto.

msanii steve nyerere amefunguka nakuongea na waandishi  wahabari alipokuwa akiulizwa kuhusu taratibu za msiba wa mzee majuto na kusema kuwa pamoja na kwamba amepokea taraifa za msiba lakini yeye haweiz kusema chocote kuhusu swala hilo kwa sababu hausiki na chochote.

steve anasema kuwa amedhalishwa na kufedheheka sana ktaia kujitolea kwae na ndio maana kwa sasa anaona bora na yeye kuwa kama waombelezaji wengine tu.

nimeshasema siongei kitu, kuna viongozi wanaofatilia hii,nimeshatukanwa sana , nimeshasemwa sana,nimefedheshwa sana, na mimi pia nina familia  na nina watoto pia kwaio mimi sio msemaji mkuu lakini nia ni kumpumzisha mzee lakini mimi iswezi kusema chochote kile.mimi ni muombeleza kama waombelezaji wengine.

Hayo yanakuja kutokana na mitandao ya kujamii kupiti wasanii mbalimbali kuwa wakimbeza na kumtuhumu sana Steve kwa kumwambai kuwa amekuwa akisubiri misaba hili kula pesa za rambi rambi.

Steve Nyerere Agoma Kumjibu Mama Kanumba.

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini , stve nyerere amekiri kuwa kamwe hawezi kujibishana na mama wa msanii marehemu steven kanumba kwa sababu ana mheshimu sana kama mama yake.akiongea na EATV, steve amesema kuwa kamwe kwake itakuwa ni kukosa adabu kama atamjibu mama huyo.

Ameyaongea hayo ikiwa ni kukataa kujibu tuhuma na maneno aliyowahi kuyaongea mama huo kuhusu Steve nyerere hapo awali na huko akisema kuwa hamjui Steve tangu hata marehemu alipokuwepo hakukuwa na mahusiano mazuri baina yao.

Mama kanumba aliwahi kusema kuwa kwake itakuwa kitu cha ajabu kuona steve nyerere ana mpenda kwa sababu hakuwahi kumpenda hata marehemu, kauli ambayo ilizua sana utata katika mitandao ya kijamii kutoka kwa mama huyo.

Ni zaidi ya mara moja mama huyo na steve wamekuwa wakirushiana maneno katika mitandao ya kijamii  hasa kipndi mahakama ilipofanya mabadiliko ya kesi ya mwanadada lulu ambapo mama huyo aliona kama wameonewa kwa kitu hicho na ndipo walikuwa wakirumbana sana na steve.

 

Wolper Amkingia Kifua Steve Nyerere Kwenye Suala la Rambirambi

Msanii wa filamu za Bongo Movie Jacqueline Wolper ameibuka na kumkingia kifua msanii mwenzake Steve Nyerere na kumtaka asivunjike moyo kusaidia wengine.

Steve Nyerere amekuwa Kwenye headlines za mitandao ya kijamii kwa muda sasa huku skendo ambayo imekuwa ikimuandama ni ya kila pesa za rambi rambi anazokusanya Kwenye misiba ya watu.

Na ishu hii imerudi  kwa kasi Tena mara baada ya Steve Nyerere kuonekana akiwa mstari wa mbele siku ya leo kwa ajili ya kuandaa msiba wa msanii Mzee Majuto.

Wolper ameibuka na kumkingia Steve na kumpa moyo kwa kazi nzuri anayofanya ya kuwasaidia watu ambao ni wafiwa na kumtaka ayapuuze maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu yake:

https://www.instagram.com/p/BmPJJuDlj1d/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=gh0ae9yptkq7

Steve Nyerere Amfananisha Idris na Fransis Cheka.

Mchekeshaji maarufu nchini  steve nyerere amefunguka na kusema kuwa watu wanakosea sana wanapotaka kumfananisha yeye na idrisa sultan kwa sababu hawawezi kulingana hata siku moja.

Wawili hao ambao wote ni wa tasnia ya uchekeshaji wamekuwa wakifanya vizuri comedy na kila mtu kwa style yake na huku kila mmoja akiwa na mashabiki wake.

Hata hivyo kutokana na jinsi idris amekuwa akitania sana wasanii wenzie katika mitandao ya kijamii na hata kutoa kituko cha skendo zinazondelea kumkabili steve nyerere, steve nasema kuwa haweiz kujibishana na idris kwa sababu wao ni watu wawili tofauti ni sawa na van dame na fransis cheka.

siwezi kushindana na idrisa maana kushindana na idrisa ni sawa na teke la van dame na fransis cheka, hivyo ni vitu viwili tofauti.

Sikumjua Billnass, Nilijua ni Jina la Mabasi ya Lindi na Mtwara: Steve Nyerere,

Msanii wa bongo movies Steve nyerere bado anaendelea kurusha madongo kwa msanii wa bongo fleva billnass baada ya wawili hao kuwa wakijibizana kwa muda mrefu katika mitandao ya kijamii na kwa waandishi wa habari kila mtu kwa nafasi yake.

Sakata la steve na billnass lilianza baada ya billnass kulalamika kuwa wimbo wake wa labda ulikuwa umefutwa youtube ukiwa na siku mbili tu na ndipo steve alipomwambia kuwa hata kama wimbo huo ukifutwa hakuna hasara kwa sababu yeye hana mashabiki wengi anachotakiwa ni kufanya kazi sana ili kazi zake ziuze.

Wawili hao waliendelea kujibizana kwa kupigana vijembe na ndipo Steve Nyerere hivi karibuni alipopata nafasi ya kuongea na clouds media na kumtupia tena vijembe Billnass.

sisi ndio watoto wa mjini hapa, baghati nzuri kipindi anakuja dar alikuwa anauliza kla kituo bado hatujafika tu, sasa mtoto kama yule lazima tumfndishe lakini msanii ambaye kwenye you tube una followers 10  unalalamika , si unaweza kuwachukua hata wale wanafamilia nyumbani kwenu tu.

Steve nyerere anasema kuwa hakuwahi kumjua billnass mpaka alipoanza kuwasikia watoto wake wakiongea na hata hivyo alikuwa akijua kuwa ni jina la mabasi yanayoenda lindi na mtwara.

unajua mimi billnass hata nilikuwa simjui hapo awali , nikawa nasikia watoto wangu wanaongea tu baba billnass nikajua ni jina la mabasi ya kwenda lindi na mtwara.

Steve Nyerere -Hakuna Msanii Yoyote alikasirishwa na Uteuzi wa Jokate .

Msanii wa bongo movies steve nyerere amefunguka na kukanusha ttesi zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye kuwa amekasirika kwa sababu ya  kuteuliwa kwa mwanadada Jokate kuwa mkuu wa wilaya ya kisarawe na kusema kuwa yeye anamshukuru sana rais kwa sababu ameleta heshima katika tansia ya sanaa.

Steve anasema kuwa maneno yamekuwa yakizunguka mengi sana huku wengine wakipinga uteuzi huo kuwa ni wa upendeleo lakini kwake ni furaha sana kwa Jokate kuwa mkuu wa wilaya.

moja ya kazi aliyonayo baada ya kuteuliwa ni kutuwakilisha sisi vijana wenzake na ametuwakilisha sisi vijana,kwa namna moja ama nyingine hakuna msanii yoyote au msanii yoyote  alikasirishwa na uchaguzi wa ma-DC wote tuko tayari kuwasapoti katika kazi kwa namna moja au nyingine. vinavyoongelewa na kuashiriwa ni vya kwenye mitandao tu wala hakuna kitu kama icho.

Steve Nyerere Anatafuta Riziki Kupitia Sisi :-holystar.

Msanii wa bongo movies ambae pia ni mpenzi wa Sister fey, Holy star a,efunguka na kusema kuwa katika vitu mabavyo mpenzi wake sister fey amemuudhi ni kumuongelea sister fey kwa sababu steve ana tafuta riziki kupitia wao kama alivyowahi kufanya katika msiba wa Muna.

Holy star anayasema haya ikiwa zimepita siku tangu Steve Nyerere kuongelea mahusiano ya Sister fey na holystar ambapo  baada ya hapo sisterfey alimjibu na ndipo mpenzi wake huyo aliposema kuwa Sister fey hakupaswa kumjibu chochote kwa sababu steve anatafuta kiki.

kitu alichoniudhi  ni kumzungumzia steve kwa sababu mwenzetu anatafuta riziki, kama alivykuwa akitafuta riziki katika msiba wa muna pale katikati lakini riziki ikachuja na sasa hivi ameona bora atafute kupitia huku kwetu.unajua steve ameka anazungumza na kusema mke wangu afungiwe miaka 18, sasa anataka mimi niishije yaani,kwa mtoto wa kiume huweiz kukaa miaka 18 bila mwanamke.

Billnas Amtaka Steve Nyerere Afungue Biashara Ya Mambo Ya Misiba

Msanii wa Bongo fleva anayetamba na kibao chake cha Labda Bill Nas amempa ushauri wa bure msanii wa Bongo movie Steve Nyerere na kumtaka afungue kampuni yake ya binafsi itakayoshughulikia mambo ya misiba.

Steve Nyerere siku za hivi karibuni amekumbwa na skendo ya Kula fedha za rambi rambi zinazochangwa na watu kwa ajili ya kuwafikia wafiwa.

Steve Nyerere na Billnas waliingia Kwenye bifu zito mapema mwezi huu baada ya Steve kumwambia maneno kuhusu yeye na Nandy jambo ambalo halikumfurahisha kabisa Billnas.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Billnas ameibuka  kumtaka Steve kuweka ugizaji wake wa vichekesho pembeni na badala yake ajikite kwenye biashara ya kuandaa misiba maana ndio anayoiweza:

Steve badala ya kutumia pesa zake kuandaa comedy shoo kubwa sijui anaweza kufungua kampuni ya kushughulikia mambo ya misiba na inaweza kuwa kampuni kubwa tu na akatengeneza hela na akatumia mtaji huo huo mdogo akanunua magari ya kubebea maiti na akafanikiwa zaidi”.

 

Steve Nyerere Afunguka Baada Ya Kejeli za Kukosa U-DC

Msanii wa filamu za Bongo Movie Steve Nyerere amemwaga povu zito baada ya kusikia maneno ya kejeli kutoka kwa mashabiki baada ya kukosa nafasi ya kuwa Mkuu wa wilaya.

Maneno ya kumpiga vijembe Steve Nyerere yalianza kusikika baada ya Mrembo Jokate Mwegelo na Jerry Muro kuwa moja kati ya watu waliotangazwa na Rais Magufuli kuwa wakuu wa wilaya.

Mashabiki walimjia juu na kumpa pole Steve huku wakimnanga kwani Steve Nyerere  amekuwa akionekana katika matukio mengi akitetea utendaji wa Rais Magufuli hali ambayo iliwajenga picha mashabiki hao kwamba anataka nafasi ya uongozi.

Baada ya kupokea meseji nyingi za pole na kuona comments za watu wengi zikiwa za kumnanga kwa kukosa uongozi, Steve alikuja juu na kumwaga povu zito ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Mnao nitumia meseji za pole naomba iwe mwisho sasa. Sipo kwa ajili ya cheo nipo kwa ajili ya Watanzania kwanza mengine no, msinilishe maneno“.

 

Alichokiandika Steve Nyerere Kuhusu Wabaya Wake.

Hivi karibuni kumeibuka maneno mengi kuhusu Steve Nyerere kusemwa vibaya kutokana na kuonekana kuwa mstari wa mbele kwenye kila tukio la wasanii au watu maarufu linapotokea.

Kutokana na matukio hayo ya kusemwa vibaya mfululizo, Steve kupitia mtandao wa Instagram ameonekana kushindwa kuvumilia na kuamua kuandika ujumbe mzito kwa wabaya wake.

Kupitia mtandao huo Steve ameandika:

Watu wengi tunamarafiki lakini hakuna kazi ngumu kama urafiki, Rafiki wa kweli ana kazi zifuatazo atasimama na wewe kwenye baya na zuri,atakuwa tayari kunyooshewa kidole kwa ajili yako, atakutetea popote pale bila kujali madhaifu yako,kwenye magonjwa njaaa hata mitihani ya kidunia atasimama nawe,Pale unapokosea rafiki anatakiwa awe mstali wa mbele kukueleza ukweli, Apende mafanikio yako,Na asiache kukumbusha mambo muhimu ya maisha. Marafiki wengi wapo kwa watu kwa sababu ya kitu fulani, wapunguze ubaki na imani ya moyo.

Sister Fey Amtolea Povu Steve Nyerere, Amtuhumu Kwa Kula Rambirambi.

Mwanadada Sister Fey amefunguka na kumtolea povu msanii wa bongo movies steve nyerere baada ya steve kumwambia Sister fey kuwa sio msanii kutokana namambo anayoyafanya katika mitandao ya kijamii yeye na mpenzi wake ambae amemzidi umri.

Akiwajibu waandishi wa habari, Fey anasema kuwa pamoja na kwamba Steve anamsema yeye sio msanii lakini amekuwa akimshangaa yeye kama kiongozi kila siku amekuwa akituhumiwa kwa kula rambirambi na michango mbalimbali ya misiba na shughuli mbalimbali.

Mi naona sasa hivi kwa sababu misiba haijatokea tu, na kwanini yeye ana niita mimi sio msanii kwanini ananiongelea sasa , mimi kama nani akiniongelea.kama mimi sio kioo cha jamii kwani yeye ni kioo cha jamii, kwanini anakula rambirambi za watu misibani huko.anafanya mambo mengi sana ambayo unayajua lakini tunaacha.

“Mimi na Wema Tutaenda Kumtembelea Muna Labda Tufukuzwe”- Steve Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere ameweka wazi kuwa hana kinyongo na Muna hata baada ya povu alilomtolea Povu Kwa waandishi wa habari Lakini ameshapanga kwenda kumtembelea.

Sakata hili lilianza wiki chache Kwenye msiba wa mtoto wa Muna ambapo Steve alionekana kuingilia mambo ya kifamilia ya Muna na kutangaza Kwenye mitandao ya kijamii taarifa ambayo Muna amedai haikua ya kweli.

Lakini siku ya jana Steve ametangaza kumsamehe Muna na kudai anajua hiki ni kipindi kigumu kwa Muna kwani bado anamuomboleza mtoto wake hivyo haoni sababu ya kuweka kinyongo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Steve  amedai kuwa yote ambayo ameongea Muna siku ya jana kuhusu yeye sio ya kweli na tayari ameshamsaheme ambapo amepanga safari ya kwenda kumtembelea akiwa na Wema Sepetu.

https://www.instagram.com/p/BlaXDuthZLR/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1lebqzhdtqbzi

Steve Nyerere Afungukia Sakata Lake na Muna Atangaza Kumsamehe

Muigizaji wa Filamu za kibongo na kiongozi wa Kamba hiyo Steve Nyerere ameibuka na kuongelea sakata lake yeye na Muna na kutangaza kuwa ameamua

Muna alipoongea na waandishi wa habari, alikanusha baadhi ya taarifa ambazo zilitolewa na Steve Nyerere zikidai kuwa muigizaji huyo amekubali kushirikiana na Mumewe Peter Komu katika kumzika mtoto Patrick ambaye Muna amekanusha kuwa sio wa Peter bali ni wa Casto Dickson.

Steve alifunguka siku ya jana Kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo ameamua kupangua hoja zote zilizotolewa na Muna ambazo zinamuhusu yeye.

Kwanza nimpe pole dada yangu Muna kwa kupita katika kipindi kigumu sana, kwa kuondokewa na mtoto. Tulikuwa tumejipanga kwenda kumuona, tukaambiwa kwa waliokoka huwa hawana 40, lakini kwa mzazi lazima kuwepo na 40. Mimi siyo mjinga wa kukurupuka tu kutangaza kuhusu msiba bila kuambiwa na wahusika wa msiba, sikukurupuka, mimi ni mtu mzima, nina familia na watoto, nilipewa maagizo hayo na Muna mwenyewe akiwa na ‘mumewe’ Joel Lwanga wakiwa Kenya, alinipigtia simu.

Nimemsikia akizungumza maneno mazito, eti nyumba anayoishi Peter haina hati, kama haina hati basi itakuwa ni ya serikali wakachukue nyumba yao. Anatukandamiza na kutoa voice, ametoa hisia zake kwa Watanzania, ametufundisha sisi vijana na wazee. Tukisema tufuatilie tutakuta mtoto uliyemsomesha hadi chuo kikuu ni wa mlinzi, mwanamke mwenye busara lazima awe na staha, ndoa siyo kitu cha mchezo jamani.

Nimemsamehe Muna kwa sababu hajui kama anachokizungumza anakifahamu. Hili liwe funzo kwa dada zetu, mimi nimemsamehe hata nikikutana naye asiogope kunisalimia, Shilole naye amemsamehe, usipoimamini biblia utamwamini sheria”.