Shiloleh Afunguka Anachopenda Kwa Uchebe

Msanii wa musiki wa bongo fleva shiloleh amefunguka na kutaja mambo anayoyapenda kwa uchebe na jinsi gani amekuwa moja ya wanaume wanaomsapoti na kumjali sana kimaisha pamoja n kwamba watu wamekuwa wakisema kuwa hawatadumu kutokana na ukweli kwamba mara nyingi  amekuwa hadumu na wanaume katika mahusiano.

Shiloleh anasema kuwa anashukuru mungu kwa sababu pamoja na skendo nyingi alizowahi kuzipitia kabla ya kumpata uchebe lakini ameweza kukubalika ukweni (kwa wazazi wa uchebe).

ninashukuru mungu sana wakwe zangu ni wacha mungu na wananielewa sana na mimi ninawaelewa sana,hawapendi kusikiliza maneno ya watu wanatambua muda wa kazi ni upi na  na muda wa nyumbani ni upi hivyo tunaishi kizungu.

Hata hivyo shiloleh anaendelea kwa kusema kuwa kipindi cha nyuma alikuwa hajatulia kwa sababu alikuwa anatafuta mwanaume wa kutulia nae ila kwa sasa anatulia kwa sababu anaamini kwa uchebe ndio amefika.

unajua kipindi cha nyuma watu niliokuwa nao wote walikuwa wanataka niendelee kujichetua,sikuwa na mtu sahihi wa kuniongoza lakini nilipompata uchebe tu alianza kuwa ananikosoa, na kunirudisha katika msati ulionyooka, na ndio maana sasa hivi nimebadilika sipo kama zamani.

nilikuwa nahitaji mtu ambae atakuwa ananikosoa pale ninapokosea kila mara,lakini pia mtu ambae atakuwa ananijali mud wote na hivyo vitu nilikuwa nakosa mara ya kwanza.

Shiloleh aliendelea kumsifia mwanaume wake kwa kusemakuwa watu wanaweza wasielewe kila kitu anachoongea lakini anapenda sana kumuona Uchebe akicheka.

macho ya uchebe mie hoi,napenda sana tabasamu lake hasa pale anapocheka meno yake yote huwa hayaonekani.kwa mtu wa kawaida hawezi kuelewa lakini napenda  macho yake akitabasamu.

Shiloleh Ajutia Vivazi vya Mitandaoni

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia , biashara nazo zimekuwa na watu wamekuwa wakiweza kuagiza bidhaa katika mitandao kwa kupitia simu na bidhaa zinakuwa zinafika pale zinapohitajika.

Msanii wa bongo fleva , Shiloleh wikiendi hii alizua gumzo katika mitandao baada ya nguo alikuwa amevaa katika special party ya WCB kumuacha maziwa wazi na kuoneka kama haijampendeza kwa tukio kama hilo.na hata katika mitandao ya kijamii watu wengi walianza kumsimanaga kwa kitendo chake cha kuvaa gauni kama hilo.

Lakini kama kawaida ya Shiloleh sio mtu wa kuficha mambo, baada ya kuona watu wamemzungumzia sana hakusita kutoa dukuduku lake kuhusu nguo hiyo ambayo iliwaacha watu midomo wazi kwa kumsema.

Shilloleh alisema kuwa nguo hiyo alikuwa ameiona katika mtandao na kuiagiza kwa lengo la kuivaa akiamini kuwa atapendeza na kutokea kama alivyoiona kwenye picha kama ilivyo kawaida ya watu wengi wakiamini kuwa nguo hizo zitawatoa kama walivyoziona katika mtandao.

Katika ukurasa wake wa instagram shiloleh aliweka picha hiyo na kuandika “yaani kama nitaagiza mimi nguo mtandaoni tenaaaa………..wallah lbda mimi sio dada Mwajuma.”

                                                  

Alichokiandika shiloleh baada ya kupokea maoni mengi juu ya muonekano wake .

                                                     

Muonekano wa Shishi baada ya kuvaa nguo aliyoiagiza mtandaoni.

Billnass Ampa Uchebe Dhana za Kupambana na Nuh Mziwanda

Msanii Billnas amemzawadia uchebe zawadi ya vifaa vya kufanyia mazoezi huku akimwambia kuwa amefanya makusudi kumleta vifaa hivyo ili aweze kufanya mazoezi na kuwa fit ili aweze kupambana na watu wanaomfatilia mkewe Shiloleh hasa msanii mwenzao Nuh Mziwanda.

Jumamosi wikiendi iliyopita Uchebe na Shiloleh walifanya weddingparty baada ya kufunga ndoa mwezi mmoja uliopita,party hiyo ilifanyika masaki jijini Dar es Salaam ilikuwa ya kufana sana na walikuwepo  wasanii wengi wakiwemo wasanii wa kundi kubwa nchini la Wasafi likiongozwa na meneja wao Diamond platinumz.

Wakati wa kuto zawadi kila mmoja alikuwa na chake mkononi lakini kwa upande wa bilnass aliona isiwe shida bali kumsaidia uchebe kuwa fit kwa kumpa  ahadi ya kumtafutia vifaa vya mazoezi huku akimwambia afanye mazoezi ili apambane na Nuh mziwanda.

najua mwanangu ashrafu anapenda nini,anapenda michezo ya ngumi kwaio na mimi kwa kulitambua hilo  na mimi nitamzawadia vifaa vya mazoezi kwa ajili ya fitness.ufanye mazoezi hata ya kupambana na kina nuh mziwanda , sisi watoto wa kiume inabidi kujilinda pale inapobidi.-Alisema Bilnass.

Ukiachna na vikwazo vingi walivyopitia shiloleh na uchebe mpaka kufikia hatua ya kukamilisha ndoa hiyo ikiwani pamoja na kukataliwana baaadhi ya ndugu na kusema sana katika mitandao, Nuh Mziwanda alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wakiliandama sana penzi la wawili hao mpka kufikia hatu ya kutaka kuwagombanisha kwa kuvujisha picha za uchonganishi.

Nuh mziwanda alikuwa mwanaume wake na shiloleh kabla ya kukutana na uchebe, nuh alikuwa ni moja ya kikwazo sana kipindi cha maandalizi ya harusi ya wawili hao kupelekea hadi kufunga ndoa kimyakimya.

Siku hiyo ilikuwa ni moja ya siku ya bahati kwa msanii shiloleh na mme wake uchebe kutokana na zawadi nyinge walizpokea kutoka kwa wasanii wenzao  ikiwemo gari,ahadi za kusaidia katika kazi na ada za shuke kwa watoto wake.Wasanii wengi waliohudhuria waliwatakia maisha mazuri na yenye baraka katika katika ndoa yao .TUNASEMA HONGERA KWAO.

 

 

 

Viongozi Wa Dini Walimshauri Shiloleh Ndoa Ya Kimyakimya

Msanii wa muziki wa bingo fleva nchini zuwena mohamed maarufu kama shiloleh amefunguka na kusema kuwa kufunga ndoa ya kimya kimya alishauriwa na viongozi wa dini na ndio maana ndoa yake ilikuwa haijatangazwa ingawa watu walikuwa wakijua kuwa atafungua ndoa.Lakini pia shilole anasema kuwa upinzani alioupata kutoka kwa dada yake ambae hakutegemea kwa sababu alikuwa mtu wa karibu nae ulimfanya kufunga ndoa kwa haraka zaidi.

Shiloleh alisema kuwa viongozi wa dini walimshauri kuwa ndoa haitangazwi kwa sababu kuna watu wanaweza kuwafanya kubadilisha maamuzi yenu na mkashangaa ndoa ikabadilika na ikashindwa kufanyika kabisa.

Niliambiwa kuwa sio kila mtu anapenda kusikia jambo jema hilo, wengine wanaweza  kukufanyia husda ili jambo lako jema lisifanikiwe  kwaio nikaamua kuwasikiliza lakini sio kwamba sitafanya sherehe. –Alifunguk Shiloleh

Akiongelea swala la dada yake kumkataza kufunga ndoa na mwanaume wa ndoto zake shilole anasema kuwa

Unajua haya mambo ni ya kifamilia, lakini mimi ninawatoto wawili kwaio hawezi kunipangia  mwanaume wakuolewa nae. Alisema Shishi baby.

Hata hivyo shiloleh anasema kuwa pamoja na kwamba ndoa ilifanyika kimya kimya lakini anatehemea kufanya sherehe kubwa itakayo kata na shoka na wale watu wake wa karibu wote watahudhuria na kufahia sherehe hiyo ambayo amehaidi kutangaza hivi karibuni huku ikisemekana kuwa sherehe ya ndoa hiyo itafanyika December 25 mwaka huu.

shilole alifunga ndoa na Uchebe , mwanaume ambae inasemekana pia kuwa alimuacha mke wake kwa ajili ya shiloleh na kuamua kumpa talaka mwanamke aliyekuwa nae kwa kipindi hicho.Hata hivyo mapenzi yao yamedumu mpaka sasa wameamua kufunga ndoa.

 

 

Shamsa Ford Ampa Darasa La Ndoa Shiloleh

Mwanadada mrembo anaejihususha na bongo movies lakini pia ni mjasiriamali maarufu baada ya kuijingiza huko baada ya kuolewa na mpenzi wake Chid Mapenzi, amefunguka na kumsahuri mwanadada Zuwena maaarufu kama Shiloleh jina la kisanii juu ya maisha ya ndoa aliyoyaanza hivi karibuni.

Shiloleh amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu kidogo anaejuliakana kwa jian la Uchebe wiki iliyopita ndoa ambayo ili-trend sana katika mitandao baada ya kuwashangaza watu wengi amabo walihisi kuwa ndoa hiyo haitaweza kufungwa kutokana na migogoro iliyojitokeza hivi karibuni baada ya kuvuja picha zikimuonyesha mwanadada huyo akiwa na mpenzi wake wa zamani ambae pia ni msanii mwenzie Nuh Mziwanda .

Shamsa Ford  akitumia uzoefu wa ndioa yake aliyofunga mapema mwaka huu amemshauri Shiloleh  kutulia katika ndoa yake  na kuachana na sifa za kuwa maarufu kutokana na usanii wake bali atulie ili kuweza kufaidi matunda ya ndoa yake.

Katika ukurasa wake wa instagram Shamsa ameamua kufunguka kuhusu swala ilo na kumpongeza kwa uamuzi aliouchukua

Hongera sana mama umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu cha muhimi uwe mke bora wa kitanzania kwa mumeo na ustar uache pembeni ‘mumuweke Mungu mbele yenu,uvumulivu na kuheshimiana Inshallah mtazikana,karibu kwenye chama mama …sasa nyie mnaosubiri matajiri wawaoe wakati matajiri wana wake zao  mtasubiri sana mpaka uso  uote sugu,uzuri  na ustar uana mwisho wake  itafika muda hata inzi hakusogelei. HONGERA MAMA

Alichokiandika shamsa ford katika ukurasa wake wa instagram

Mwisho huu w mwaka umekuwa mwaka mzuri kwa baadhi ya wasanii ambao wameamua kuachana na ukapela na kujiingiza katika maswala ya familia.PONGEZI NYINGI KWA SHILOLEH NA MUME WAKE.

 

Shilole na Uchebe Kufunga Ndoa Hadharani,Hakuna Kadi Ya Mwaliko.

Kwa muda sasa kumekuwa na  gumzo  mitadaoni kuhusu ndoa ya mwanadada Shiloleh na mumewe mtarajiwa  anaejulikaa kwa jina moja  la Uchebe. Wiki kadhaa zilizopita Uchebe alithibitisha kufanyika kwa ndoa hiyo mwaka huu mwezi Disemba na kuwa honeymoon atampeleka mke wake huyo mtarajiwa Ulaya.

Nae bibi harusi mtarajiwa amefumnguka na kusema kuwa ni kweli ndoa yao itafungwa hivi karibuni lakini haitakuwa kama ndoa zingine za wasanii ambazo ufanyika kimya kimya.Shilole ameongezea na kusema kuwa  katika ndoa yake haitakuwa na kiingilio wala mchango wowote hivyo yoyote anaetaka kuja atakuwa na uhuru wa kuhudhuria na itafanyika mahali peupe bila siri yoyote kama wanavyofanya wengine.

Ndoa yangu sitafanya ya siri kama mabvyo wamekuwa wakifanya wengine,nitafaya sehemu ya wazi kabisaa na wala hata  haitakuwa a kiingilio hata kidogo.napenda ndoa yangu ionwe na watu wote na kila mtu aweze kuhudhuria  na aoene kila kitu kinachoendelea.

Shiloleh amesema kuwa mpaka sasa ndoa hiyo  ina uhakika wa kufanyika  na amethibitisha kuwa mwanaume wake tayari ameshatoa mahali kubwa nyumbani kwao na ameshatambulika hivyo mipango ya harusi ndio inafanyika kwa sasa.

Shilole na Uchebe wamekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu wa zaidi ya miezi sita sasa ambapo Uchebe aliachana na mke wake wa kwanza wa ndoa kwa kumpa talaka kwa madai ya kuishi na Shiloleh.Hata hivyo wawili hao ambao mpaka sasa wanafanya mpango wa kufunga ndoa wamekuwa wakikumbana na mameno mengi katika mtandao kutokana na mashabiki wa mwanadada huyo kuwa wanamsema anatembea na mwanaume aliye chini ya umri wake.

Shilole ni moja ya wasanii wa kike ambao wamekuwa ni mfano wa kuigwa kupitia kazi  anazofanya.Ukiachana na kazi ya muziki anayofanya ambyao ndio ilimtambulisha kwa mashabiki wake, Shiloleh pia aliona fursa ya kufanya biashara ya mama ntilie na ameweza kujitoa kotekote kwa kuwahudumia wateja wake wa chakula na mashabiki zake katika muziki.Hata hivyo  Shilole ameweza kumudu majukumu yote kulingana na mahitaji ya watu wake.

Shiloleh Na Uchebe Kufunga Ndoa,Honeymoon Ulaya

Mume mtarajiwa wa msanii Shiloleh, mwanadada ambae amekuwa ni moja ya wanawake wapambanaji katika maisha  amefunguka na kuongelea mipango yao ya harusi inavyokwenda na jinsi harusi iyo itakavyo fanyika.Mwanaume huyo anaejulikana kwa jina moja la Uchebe amesema kuwa mpiango ya  harusi ipo karibuni lakini nia yake kubwa katika harusi hiyo ni kumpeleka mke wake huyo Ulaya kwa ajili ya honeymoon yao.

Akiongea na East Africa, Uchebe amesema kuwa ndoa yao hiyo inategemewa kufungwa mwezi wa kumi na mbili(12) mwaka huu  kwa sababu yeye na mkewe mtarajiwa wameshakubaliana kabisa na taratibu za ndoa zimeshaanza kufanyika  na wanataka kuhararisha mahusiano yao.

“Mwenyezi Mungu ameshafanya wepesi  sasa hivi tupo katika  kwenye maandalizi, na Mungu akipenda mwezi wa kumi na mbili itakuwa ndoa kamili kwani taratibu zote nishazifuata,mahari nishatoa sidaiwi kabisa na honey moon nampeleka Ulaya” amesema Uchebe ambae ndie mume mtarajiwa wa Shiloleh

Uchebe ambae sasa hivi ni mume mtarajiwa wa Shiloleh, alishawahi kuwa na ndoa kabla ya hii inayoenda kufungwa sasa, ambapo inasemekana kuwa ndoa hiyo ilivunjika baada ya mwanaume huyo kuingia katika  mahusiano  na Shiloleh.

Ingwa kwa hivi karibuni pia kulikuwa na tetesi za wawili hao kuwa wameachana baada ya Shiloleh kusema kuwa yeye na vi-ben ten sasa basi, taarifa za kuachana kwao wamezikanusha na kusema bado wanaendelea  na mahusiano yao na kwa sasa wapo katika mipango ya harusi.

Mwanadada Shilole ni moja ya wasanii wa kike wenye kupendwa na mashabiki wengi sana lakini pia ni moja ya wasanii wenye ushawishi  mkubwa sana  kwa mashabiki wake.Ukiachana na kazi ya muziki anayofanya Shiloleh pia ni mama ntilie anaepika chakula mwenyewe na kuwahudumia wateja wake mwenyewe.Amekuwa ni mwanadada anaeangaliwa sana na watu na kuwa mfano wa kuigwa kwa watu wengine.

Ingawa kumekuwa na maneno yanayomkabili kuhusu tabia yake ya kutemba na vijana wenye umri wa chini yake , lakini hajawahi kuathirika na maneno hayo zaidi ya yeye kupiga kazi ili kuwaridhisha masbabiki wake.

Shilole Kuachana Na Vi-ben Ten

Mwanadada mrembo kabisa, jasiri na mpambanaji, anefanya vizuri katika muziki wake, Zuwena Mohamed  almaarufu kama Shilole, amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hivi mapenzi na vi-ben ten anasimama kwanza kwa sababu havimpi faida yoyote.Shilole amefunguka na kusema kuwa alichogundua na kwamba hakijikita katika mapenzi hayamzalishii chochote lakini akijikita katika kazi anaona matunda yake hivyo kwa sasa bora afanye kwanza kazi.

“Jamani kwa usawa huu mtu hasipobadilika  na kuangalia kitu cha maana ni shida sana, mimi binafsi  mambo ya mapenzi sijui na vi ben ten vikae kwanza  vinisubirie kwanza huko, nifanye kazi zangu ili nipate kwanza maendelea yangu, sio mapenzi wanafaidi watu wa instagram tu,kukuangalia kila siku maisha yako.” alisema Shilole

Shiloleh ni moja wa wasanii wanaoingia kwenye kundi la wanawake wanaojiingiza kwenye mapenzi na vijana wanao wazidi umri,kwa  kipindi kirefu mwanamuziki huyo amekuwa akikumbwa na scandal za kutembea na vijana wanaowazidi umri na kuwatesa kwa sababu tu anawapa ela, mfano alishawahi kuwa na mahusiano na msanii mwenzie Nuh Mziwanda na baadae walikuja kuachana ambapo Nuh aliongea mambo mengi ya mahusiano yao ikiwa na lile la kuwa kipindi cha mahusiano yao alikuwa  hana sauti kwa mwanamke huyo.

Shiloleh  ambae kwa sasa yupo na uhusiano wa kimapenzi na kijana  Uchebe   inasemekana kuwa alikuwa  mume wa mtu lakini alikuja kumuacha mkewe kwa talaka kwa sababau ya kuishi na  Shiloleh pia ni kijana mwenye umri mdogo kuliko mwanadada huyo.Wawili hao wamekuwa wakionekana kuwa pamoja kwa muda mrefu na kusema kuwa hawategemei kuachana.

Ukiachana na kazi ya muziki, Shilole aliona fursa ya biashara ya chakula kwa upande mwingine na kuamua kuisogelea, biashara ambayo inamfanuy akukutana na mashabiki wengi zaidi na kuwa karibu na wateja wake pia.Pamoja na maneno mengi yanayozunguka mitandao juu yake Shiloleh ni mwanamke jasiri na anaeyeonekana kupitia mengi kwenye maisha kabla ya hapo hivyo kwa sasa yeye amuamua kufanya kazi tu.