Shilole afunguka kwanini hataki wanawe wavae kama anavyo vaa

Shilole anajulikana kwa kuvaa mavazi za nusu utupu. Mara nyingi mavazi anayovaa Shilole huzua utata kwani watu wengi huseme yeye (Shilole) ni Muislamu na anafaa kuvaa mazazi ya kiheshima kulingana na dini hilo.

Shilole ata hivyo hataki wanawe kuiga mavazi ya nusu utupu anayovaa kwenye shoo zake wala maisha ya sanaa anayoishi yeye.

Katika mahojiano na Mtanzania, Mrembo huyo alisema kuwa anawalea watoto wake kuligana na maadili yanayokubalika na jamii. Alisema kuwa wanawe wanatambua kwamba mama yao ni msanii hivyo hawataiga anachofanya.

Shilole na mwanawe

“Watoto wangu nawalea katika maadili kama mama, siwezi kuwalea maisha ya kistaa kama ninavyoishi mimi na wanatambua kwamba mama yao nipo kazini kwa ajili yao na pia hawana ndoto za kuishi maisha yangu ya kisanii,” alieleza Shilole.

 

Shilole ametaja sifa za Mwanaume anaempenda

Kuna fununu zinazodai kuwa Shilole amepata mpenzi ambaye anataka kumuoa lakini jambo hili halijamsimamisha kutaja sifa ambazo anazozipenda kwa wanaume.

Akizungunza hivi karibuni msanii huyu wa nyimbo za Bongo alisema kuwa yeye anawapenda wanaumbe ambao wanajitambua na ambao ni warefu ikiwa ni jambo la muonekano. Ingawa aliendelea kusema kila mtu ameumbwa vitofauti, Shilole aliweka wazi kuwa hawezi kutoka na mtu ambaye ni mfupi. Alisema,

“Mimi napenda mwanaume yoyote yule ilimradi anajitambua basi, suala la muonekano hilo linatengenezwa ila kiukweli kabisa mimi napenda mwanaume mrefu, mwanaume mfupi kwangu hapana,Sipendi Wanaume wafupi, Barnaba yeye ni mfupi na kila mmoja ameumbwa na Mungu tofauti, ila sasa hivi vigezo na masharti kuzingatiwa“

Shilole alisema haya kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV huku akiongezea kuwa anatamani kuoleka kwani hii ni ndoto ya kila mwanamke.

“Hamna mtu asiyependa kuolewa, ndoa ni heshima ndiyo maana unasikia watu wanasema mke wa fulani yule, muwe wa fulani yule lakini siyo aah yule si mwanamke tu kwa hiyo ndoa ni heshima”

Mwanafunzi aliyeshtakiwa kwa kumkashifu Shilole afikishwa mahakamani

Mwanafunzi wa Chuo cha Bandari alifikishwa mahakani jana Jumatano kujibu shtaka ya kumkashifu Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole.

Thomas Lucas mwenye umri wa miaka ishirini anakabiliwa na shtaka la kumkashifu Shilole kupitia kwenye mtandao wa Instagram.

Upande wa mashtaka unadai kuwa mshtakiwa alifanya kosa hilo wakati akijiua ni kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya mtandao namba 14 ya 2016.

Shilole hata hivyo hakuweza kufika kotini kutoa ushahidi katika kesi inayomkabidhi Thomas Lucas; ilisemekana mrembo huyo hakuweza fika kotini kwasababu alikuwa anaumwa.

Kesi hiyo ya matumizi mabaya ya mtandao ilihahirishwa hadi Mei 17,2017 ambapo itaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

 

Shilole afunguka kuhusu sababu zilizopelekea yeye kushindwa kutoa wimbo na Jennifer Lopez

Shilole anasema kuwa alikutana na meneja wa Jennifer Lopez aliposafiri kuenda Marekani  – sababu ya mkutano wao ulikuwa kuwezesha kolaba kati ya J-Lo and Shilole.

Akiongea kwenye kipindi cha Kikaangoni, Shilole alisema alishindwa kufanya kazi na Jennifer Lopez kwasababu hakuwezi kuridi Marekani tena.

Shilole alieleza kuwa mambo ya familia na shuguli zake za kimuziki hapa Tanzania zilimuzuia kurudi Marekani kufanya kolabo na J-Lo. Alisema sasa anamtafuta Nicki Minaj kufanya kazi naye.

“Aisee ilishindikana maana mimi sikupata muda tena wa kwenda Marekani kwani kuna mambo yangu nilikuwa nafanya hapa nyumbani ya kimuziki na familia, hivyo muda ukawa unanipita hivi na ukiangalia Jennifer mwenyewe naye ndiyo kwanza alikuwa katoa ule wimbo  ‘Ain’t Your Mama’ nikaona tusisumbuane sana mwache tu aendelee na mambo yake mimi nitamtafuta Nick Minaj popote alipo” alisema Shilole.

Jennifer Lopez

 

Shilole: Mimi namkubali zaidi Diamond Platnumz kuliko Ali Kiba

Shilole ameeleza sababu ya kumkubali Diamond Platnumz kuliko Ali Kiba – wawili hao (Ali Kiba na Diamond) ni maadui wakubwa kimuziki.

Nani kati Diamond na Ali Kiba ndo mfalme wa muziki Tanzania? Mjadala huu huzua utata kila mara unapoulizwa. Mashabiki wa Diamond watasema Simba ndo anaweza na wale wa Ali Kiba watasema yeye ndo bingwa.

Zuwena Muhamed alimaarufu kama Shilole amesema yeye ni Team Diamond Platnumz. Akiongea kwenye kipindi cha Kikaangoni live kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Shilole alisema yeye anamkubali sana Diamond.

“Mimi namkubali zaidi Diamond Platnumz kuliko Alikiba, nampenda Diamond kutoka na mambo yake na vile alivyo, kwa hiyo kila mtu ana watu anaowakubali na kuwapenda” alisema Shilole.

Shilole afunguka kuhusu sababu ya kuficha mahusiano yake na mchumba wake mpya

Shilole atakua mke wa mtu hivi karibuni – staa huyo wa Bongofleva tayari ameshamtambulisha mchumba wake kwa wazazi wake.

“Nimepata mchumba mwenyeji wa Arusha na tayari nimeshatambulishwa ukweni. Soon dada Mwajuma naenda kuvaa shela. Nataka ndoa yangu kila mtu ahudhurie, nijaze uwanja wa Taifa. Ndoa itafungwa juu ya ndege tutashukia uwanja wa Taifa,” Shilole alisema kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM.

Mrembo huyo pia alifunguka kuhusu sababu ya kuficha mahusiano yake na mchumba wake mpya. Shilole alisema anahofia kuyaweka mahusiano yake wazi kwasababu mahusiano yake ya awali yalivunjika kutokana na kuwekwa zaidi hadharani.

“Mahusiano yangu ya nyuma yalivunjika kwa sababu niliyaweka wazi kwa watu wa karibu. Kwa sasa, namficha mume wangu mtarajiwa,”  Alisema Shilole.

 

Shilole aeleza kwanini hakujaliwa kumzalia mtoto ex wake Nuh Mziwanda

Staa wa Bongo Movies Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameeliza kwanini hakumpa mtoto ex wake Nuh Mziwanda.

Wawili hao, Shilole na Nuh, waliwapa watu sababu ya kuwazungumzia baada ya kuonekana katika mapozi ya kimapenzi.

Soma pia: Hawa watarudiana tu! Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva Shilole apatikana akiwa katika mapozi ya kimapenzi na ex wake

Nuh alimuoa Nawal na ata kuzaa naye mtoto wa kike baadaya ya uhusiano wake na Shilole kuvunjika. Ata hivyo Shilole na Nuh bado ni marafiki.

Alipoulizwa kwanini hakumpa mtoto Nuh kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio hivi karibuni, Shilole alisema kuwa hakujaaliwa tu kupata mtoto kwa uhusiano wake na Nuh. Alisema pia bado yupo single kwa sasa.

Shilole na Nuh Mziwanda

R.I.P English! Shilole sasa asema kuwa hapendi kuzungumza lugha ya Kiingereza pasipo sababu

Msanii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameoneka akizungumza Kiingereza kibovu kwenye video ambayo imesambaa sana kwenye mtendao wa kijamii.

https://www.youtube.com/watch?v=p9KUgS4_oOY&feature=youtu.be

Lakini ata hivyo msanii huyo amedhibitisha kwamba ako na umaarufu wa kuzungumza lugha ya Kiingereza. Shilole anasema kuwa yeye hawezi kuzungumza Kiingereza pasipo na sababu.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Shilole alisema watu wanaomtaka yeye kuzungumza Kingereza wanapoteza muda wao kwa kuwa yeye alijifunza lugha hiyo kwa ajili ya maslahi yake binafsi hasa katika biashara zake.

“Mimi lugha naijua sana, nimesoma kozi ya miezi mitatu, mwalimu alikuwa anakuja nyumbani kwangu kunifundisha, ukitaka kujua mimi najua kuzungumza lugha hiyo unikute kiwanja cha ndege nimechelwa ndege halafu nina show au ninapokuwa mezani nataka kuzungumza na wazungu kwa ajili ya kusaini mikataba lakini siwezi kuongea kwa kila mtu ili kudhihirisha kama naweza kwakuwa hakuna aliyenisaidia kulipa ada”, alisema Shilole.

Hawa watarudiana tu! Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva Shilole apatikana akiwa katika mapozi ya kimapenzi na ex wake

Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aliachana na mpenzi wake Nuh Mziwanda karibu miaka mitatu iliopita. Shilole alidai kuwa wivu ndiyo uliosababisha yeye na mchumba wake kuachana.

Shilole na Nuh walijibizana kwa maneno mazito mazito kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya kuachana.

Lakini sasa dalili zaonyesha Shilole and Nuh wako tayari kurudiana. Hii ni baada za picha zinazowaonesha wakiwa pamoja katika mapozi ya kimapenzi kutokea kwenye mitandao ya kijamii.

Shilole ata hivyo amewataka watu kuacha tabia ya kueneza uvumi baina yake na Nuh Mziwanda, msanii huyo anasema watu ndiyo wanavumisha habari potovu kumhusu yeye na Nuh.

“Mimi na Nuh ni washikaji tu, halafu Mwanza hatujakatana katika ‘show’ ila kila mtu alikuwa kwenye mishe zake hivyo sijaona tatizo la mimi kusalimiana naye pamoja na kupiga picha kwa kuwa alikuwa ‘Ex boyfriend’ wangu na nimeishia naye takribani miaka 5 watu waache tabia ya kukuza vitu ambavyo hawana uhakika navyo”. Alisema Shilole kwenye kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio.

 

Mwanamuziki mashuhuri Shilole ajiaibisha wakati video yake akishindwa kuongea kingereza yaibuka mitandaoni

Mwanamuziki Shilole amekuwa kicheko cha wengi mitandaoni leo wakati video yake akijaribu kuzungumza kingereza ilipo ebuka kwenye mitandaoni.

Video hiyo inaonyesha mwanamuziki huyu akitamka lugha bila uwakilifu wowote ama ustaarabu.

Kwa mwamuziki huyo mwenye kutambulika sana Tanzania na ambaye anajiona kama mwanamuziki wa kimataifa, video hiyo ni ya iabu sana.

Hata kuwa wa kwanza kwa sababu ata Diamond mwenyewe alijiaibisha wakati mmoja akihojiwa na mwanahabari huko Afrika kusini.

Mtazame Shilole kwenye video hiyo:

Bongo ni movie tuuuuuuu hadi huruma?

A post shared by nelson (@nelyhassan) on