Ebitoke Amuomba Msamaha Shilole Baada Ya Kudai Sio Msanii

Mchekeshaji mwenye vituko kutoka Timami Tv, Ebitoke amesanda na kumuomba msamaha msanii wa Bongo fleva Shilole baada ya kupewa kichambo cha haja.

Siku chache zilizopita Ebitoke alitamka Kwenye Interview aliyokuwa anafanya na kusema hajui kama Shilole ni Mwanamuziki au ni mama ntiliye na hata kusema kuwa hajui nyimbo yake hata moja.

Baada ya kuongea maneno hayo Shilole alimjia juu na kumrushia maneno huku akidai hawezi kubishana na Ebitoke kwani siyo level zake kabisa kwani hadhi zao haziendani.

Baada ya kupokea kichambo hiko Ebitoke ameibuka na kumuomba msamaha Shilole na kusisitiza kuwa maneno aliyoongea yalikuzwa na watu matandoni kwani anajua kuwa SHilole ni msanii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Ebitoke alifunguka haya:

Unajua watu wanajua kukuza maneno sana ila mimi niliongea kutokana na kazi anayozozifanya nyimbo zake mbona mimi nazijua kama ile wa kigoli si wimbo wake ule? Mi naujua na ninajua ni msanii kwaiyo mimi naomba tu anisamehe tu”.

 

Shilole Amjibu Ebitoke na Kudai Sio Hadhi Yake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amemjia juu msanii wa vichekesho kutoka Timamu Tv, Ebitoke na kusema sio mtu wa hadhi yake.

Siku ya jana Ebitoke alimuongelea Shilole Kwenye Interview yake na kudai hajui nyumimbo hata moja ya Shilole kwa sababu hajui kama ni msanii au ni mama ntiliye.

Kwenye mahojiano na EATV, Shilole amesema hawezi kubishana na mtu kama Ebitoke kwa kuwa hana pesa na pia sio level zake na pia kama anatafuta kiki basi yeye hatoi kiki sahivi:

Nyumbani kwake ananitazama kila siku, wengine wanapenda wanisikie nikiongea, mimi siwezi kuongea na mtu ambaye hana hela, lakini wakati huo ananijua na ananiangalia kwenye tv sebuleni kwake, mimi sitoi kiki sasa hivi“.

Mbali na kuwa msanii Lakini pia Shilole ni mjasiriamali ambapo anamiliki mgahawa wake unaoitwa Shishi Food.

Ebitoke- Shilole Sio Msanii Bali ni Mama Ntiliye

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv, Ebitoke ameibuka na kumtolea povu zito Shilole huku akidai kuwa hamuelewi kama ni msanii au mama ntiliye maana hajui kazi yake hata moja.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Shabiki mmoja alimtaka ataje wimbo mmoja wa Shilole na kuuimba ndipo aliposema hajui wimbo wake hata mmoja kwani hajui kama ni msanii au ni mama ntiliye:

Labda unitajie nyimbo zake mimi sijui kazi zake mimi najuaga  yeye ni mpishi tu ila hapa Kwenye nyimbo mtanisamehe kwa kweli sizijui nyimbo zake…..Nisiwe muongo naongea ukweli wala sio kiki kama mlivyozoea mambo ya kiki siku hizi nimeacha”.

Shilole mbali ya kuwa msanii wa Bongo fleva Lakini pia ni mfanyabiashara ambaye anamiliki mgahawa wake unaoitwa Shishi Food ambapo anauza vyakula mbali mbali.

 

Shilole: Nikifa Sitaki Mwili Wangu Ufanyiwe Mbwembwe

Mwanamke wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kutoa sharti siku akifa kuwa hatataka mwili wake ufanyiwe mbwembwe Leaders Club.

Shilole amesisitiza kuwa hatataka mwili wake ufanyiwe mbwe mbwe Leaders Club badala yake anataka mambo yote yaishie msikitini kwa kuwa yeye ni mtoto wa kiislamu.

Wiki mbili zilizopita Mrembo Agnes Masogange alifariki dunia kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Pumu na baada ya hapo mwili wake uliagwa Kwenye viwanja vya Leaders Club.

Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Shilole amesema yeye anatoa agizo kuwa, ikiwa ametokea amefariki dunia leo au kesho, kama siyo kuagwa nyumbani kwake Gongo la Mboto, basi aagwe msikitini.

Mimi sitapenda kabisa taratibu za mazishi yangu zifanyike katika Viwanja vya Leaders, ni bora kama nyumba yangu itakuwa haijamalizika basi watu wakafanyie taratibu hizo msikitini kwa sababu mimi ni mtoto wa kiislam, siwezi kuagwa kwenye viwanja ambavyo watu wanakunywa na kuuza pombe“.

 

Shilole- Mama Yangu Alinifunza Kujitoa Kwenye Matatizo Ya Wengine

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kusema Mama yake alimfunza kujitoa Kwenye matatizo ya binadamu wengine.

Shilole ambaye alijizolea sifa kubwa Kwenye msiba wa msanii wa Bongo movie Agnes Masogange ambapo alionekana akishughulika kupika chakula na wanawake wengine Kwenye msiba.

Shilole baadae aliweka wazi kuwa alipofika tu msibani hapo badala ya kwenda kukaa pembeni na wasanii wenzake alienda jikoni kujiunga na wanawake wengine na kuanza kupika chakula.

Shilole ameweka wazi Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa hivyo ndivyo alivyo siku zote kwani mama yake alimfunza kujitoa kwa ajili ya matatizo ya watu wengine:

Kabla mama yangu hajafariki aliniambia sifa ya binaadamuu! Kujitoa kwa wenzio hasa Kwenye matatizo kwani raha zipo tu. Pumzika kwa amani mama yangu japo uliniacha nikiwa na miaka saba hekima zako bado nazifata”.

 

Shilole Achora Tatoo ya Mwisho Yenye Jina la Mumewe

Mwanamuikzi wa kike ambae pia ni mjasiriamali, Shiloleh ameonyesha tatoo aliyochora kwenye mwili wake yenye jina la mume wake mpendwa uchebe yenye jina ‘ASHRAF‘  na kusema kuwa hiyo ndio tatoo yake ya mwisho kuichora katika mwili wake.

katika ukurasa wake wa instagram , Shilole aliandika”kwa mara ya mwisho nimechora tatooo ya jina la mume wangu nampendaaa sanaaa’

                                            

Wasanii wengi wamekuwa na hiyo tabia ya kuchora tatoo zenye majina ya watu wanaowapenda hasa wapenzi wao na kisha kuangaia sana pindi wanapoachana  na hii ilishawahi kumkuta Shilole alipochora jina la mpenzi wake wa kwanza Nuh Mziwanda na walipoachana alifuta na kuweka ua, lakini shiloleh amekiri kwa hiyo ndio ya mwisho.

Lulu Diva- Sitaki Kupambanishwa na Shilole

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya muziki wa mduara Lulu Diva ‘Diva Divana’ ameibuka na kusema hataki kufananishwa na msanii mwenzake Shilole.

Lulu Diva amewataka mashabiki ambao wanafananisha rekodi zake na na miondoko ya nyimbo za Shilole waache kumpambanisha naye kwani hataki beef naye.

Lulu Diva amefunguka hayo Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, ambapo amedai anamheshimu Shilole kama dada yake hivyo hatopenda kuwa na beef naye:

Hapana Jamani hakuna mtu ambaye anapotezwa kila mmoja anaimba mziki wake na mimi Shilole namheshimu kama dada na anafanya mziki wake wa kwake peke yake yaani hata ukiangalia mziki anaofanya na mziki wangu ni vitu viwili tofauti ni watu tu wanatengeneza vitu ili waweze kutuchonganisha”.

Lulu Diva aliendelea kumwagia Sifa Shilole huku akisisitiza hataki bifu naye:

No mimi namheshimu sana as a sister she is a legend ameanza mziki kabla yangu anajua vitu vingi kwenye gemu kabla yangu kwaiyo wasitengeneze hiyo kitu mpaka mimi nikawa kuna kitu nataka kujua kuhusu mziki nikashindwa kumfuata kwa sababu ya maneno kwaiyo naomba hivyo vitu visiwepo mimi nafanya mziki wangu mimi kama mimi”.

 

Shilole Kamtosa Uchebe Karudiana na Nuhu Mziwanda

Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amedaiwa kumtosa mpenzi wake Uchebe na kuamua kurudiana na mpenzi wake wa zamani mwanamuziki mwenzake Nuhu Mziwanda.

Uhusiano wa Shilole na Nuhu Mziwanda ulipata umaarufu kutokana na tofauti kubwa ya umri kati yao. Lakini baada ya kuwa pamoja kwa kipindi kirefu waliachana na kugeuka kuwa maadui wakubwa. Baada ya kuachana walitungiana nyimbo mbali mbali huku Nuhu Mziwanda kwenye nyimbo aliomtungia Shilole iliyoitwa jike shupa alidai kuwa alipokuwa kwenye uhusiano na Shilole  alikuwa anampiga sana tuhuma ambazo Shilole alithibitisha na wala hakukataa.

Miezi michache iliyopita Shilole alianza uhusiano wa kimapenzi na kijana anayeitwa Uchebe ambaye hakuwa na umaarufu wowote nikimaanisha kuwa hakuwa msanii bali ni fundi gereji lakini Shilole alisisitiza kuwa anampenda sana hadi kufikia hatua ya kutangaza kuwa wanategemea kuoana hivi karibuni na hata kusema watafunga ndoa Ulaya. Siku mbili zilizopita Shilole alienda kupiga shoo Tabora, Igunga ambako pia ni Nyumbani kwa wazazi wake na baadae aliweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram zikimuonyesha akiwa na Uchebe na Mama yake na kuweka wazi kuwa ameenda kumtambulisha kwa wazazi wake.

Baada ya hayo yote kutokea siku ya Jana picha zilisambaa zikimuonyesha Shilole akiwa amelala kitandani kimahaba kabisa na Nuhu Mziwanda jambo liliozua tetesi kuwa Shilole karudiana na Nuhu na kamtosa mpenzi wake Uchebe.

Hizi ni baadhi ya picha zilizosamvaa mtandaoni zikimuonyesha Shilole na Nuhu kitandani:

 

 

Shilole Amchana Barakah The Prince, Huku Mx Cater Adai Ana Stress

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Barakah the Prince amezidi kuwa katika kipindi kigumu wiki hizi chache tangu atoe wimbo wake mpya ‘sometimes’.

Tangu ametoa wimbo huo, Barakah amekuwa katika headline baada ya kudai kuwa label yake ya zamani Rockstar 4000 na Mx Cater wanamfanyia hila ili nyimbo yake mpya isivume wala kupata viewers YouTube.

Mapema wiki iliyopita Barakah alidai kuwa MX cater ambaye ni meneja wa wanamuziki Aslay na Shetta alimuomba password ya akaunti yake mpya ya YouTube kwa lengo la kumfanyia uchunguzi wa nani anamfanyia mchezo huo mchafu, lakini Barakah anadai baada ya kumuamini na kumpa password hali ile ikaanza kutokea tena kwenye akaunti yake mpya.

Barakah amedai kuwa habari za yeye kufanyiwa mchezo mchafu na MX carter amepewa na msanii mwenzake Shilole, jambo ambalo Shilole amelikataa kwa nguvu zote ambapo amedai kuwa Barakah ni muongo na mchonganishi.

Lakini kwa nini huyu mtoto anapenda kugombanisha watu? Na ndio maana haelewani na watu kwa sababu ya mambo yake anayoyafanya siyo vizuri kama unataka kuongea na mtu mfuate binafsi si mpaka upitie kwa mtu mwingine, yaani sikipendi nasema ukweli halafu yule ni mdogo wangu namheshimu, yule mtoto ajipange unajua sometimes unataka kiki lakini siyo za namna hiyo, ana dharau sana yule mtoto nasema hiyo dharau haitampeleka kokote, kwangu mimi hapati kiki bali nitamuharibia sitoi kiki kishenzi”.

Pia Shilole amezidi kusisitiza kuwa hajawahi kumwambia Barakah jambo kama hilo mara ya mwisho waliongea kwenye Simu ambapo Barakah alimuomba ampostie Nyimbo yake mpya, lakini pia Baada ya tuhuma hizo MX cater alikataa tuhuma hizo alizopewa na Barakah kudai Ana stress za nyimbo yake mpya kufeli.

Sihofii Kuibiwa Uchebe, Namwamini Sana-Shilole Kaongea

Ingawa ni moja wa wasanii waliosemwa sana katika mitandao kuhusu tabia yake ya kutembea na wanaume wanaowazidi umri, Shilole hajawahi kukoma kufanya hivyo huku akisema kuwa yeye kwake anachoamini ni mapenzi na sio kitu kingine na swala la umri linabaki kuwa namba tu,Shilole ambae anasifiika kwa tabia ya kuwa na mahusiano na wanaume wadogo lakini pia ikisemekana kuwa amekuwa akiwaonea sana hata kuwapiga muda mwingine amefunguka na kusema kuwa mpenzi wake alienae sasa hivi anamuamini sana hivyo wala hana wasiwasi nae.

” Sihofii kabisa kuibiwa uchebe wangu maana ninamwamini sana, na yeye ananiamini sana hata ninpokuwa safarini  nje ya nchi huwa sina hofu yoyote maana ni mtu wa dini sana mume wangu  na huwa hana hayo mambo ya wanawake” Alizungumza shilole.

Shilole aliendelea kumsifia mpenzi wake huyo huku akisema kuwa kwa upande wao mapenzi yao huwa wanayatamguliza kwa Mungu , ndio maan awanaweza kukaa kwa amani kabisa maana bila kumshirikisha Mungu katika ilo hakuna kinachoweza kufanyika  kwa akili zao katika hilo,”mapenzi yetu tunamtanguliza Mungu zaidi  maana kwa akili zetu hatuwezi.”

Shilole na Uchebe wamekuwa katika mahusiano kwa takribani miezi kadhaa sasa imepita lakini, mwanaume huyo alienae iliwahi kusemekana kuwa alikuwa mume wa mtu wa ndoa lakini alipoingia katika mahusiano ya kimapenzi na shilole aliamua kumuacha mke wake kwa talaka kwa ajili ya kukaa na Shilole ambae pia inasemekana kuwa huwa akiwapa ela wanaume hao ili waendelee kukaa nae.

Ukiachana na Uchebe, Shilole pia alishawahi kuwa na mahusiano na msanii mwenzie, Nuh Mziwanda kwa kipindi cha nyuma lakini walipokuja kuachana Nuh Mziwanda alifunguka na kusema kuwa Shilole alikuwa alimuonea sana na kumfanya kama mtoto kwa sababu tu alikuwa akimzidi ela na umri pia, kwa kifupi Shilole anasemekana kuwa ni wamama wenye tabia ya kulelea wanaume ivyo ujiingiza kwenye mahusiano wa wanaume wenye umri mdogo ili aweze kuwamudu na kuwaendesha vile anavyotaka yeye.

 

Shilole Amponda Hamisa na Kumsifia Zari

Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole Kiuno amefungukia suala la Hamisa na Zari na kuweka neno lake. Kama ilivyokuwa kwa wasanii wengi wametoa maoni yao juu ya jambo hili Shilole pia amefunguka na kuonyesha wazi yupo upande wa Zari na kumponda Hamisa.

Kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole amefunguka kuwa kitendo alichofanya Hamisa kimewadhalilisha wanawake wote kwani  amemtumia mtoto wake kutafuta kiki.

Shilole amefunguka;

“Mwanamke asiyejielewa ndio hutumia mwili wake kujidhalilisha na kuwatumia watoto malaika wasi na kosa kutafuta kiki. Mwanaume akikupenda atakuweka ndani atakuthamini. Kinyume na hapo mtatumiana kwa maslahi yenu binafsi. Ukiwa mwizi unakuwa hata na heshima kwa mwenye mali yake ya nini mpaka udhalilishwe na mwanaume ijulikane hupendwi ila umetumiwa tu. Vinginevyo hata huduma unayopata kwa wiki utaisikia bombani. Kwani haiwezekani mwanamke kufight na kutulia na watoto wako mpaka utengeneze drama? Hebu tubadilikeni jamani huu ni u GOLD DIGGER unatudhalilisha tu. Aggh mi nakereka tu hebu niendelee na umama ntilie wangu au sijui na mimi nitafute wababa wa watoto wangu tuanza drama”.

Kwa upande mwingine Shilole amemposti Zari na kumuonyesha yuko upande wake na anamkubali yeye. Shilole kaweka picha ya zari na maandishi “Ijumaa Kareem! Mashallah umependeza wifi”.

Shilole: Naepukana na skendo yoyote kwa sasa

Ndoa ya Shilole ambayo itafanyika hivi karibuni imefanya staa huyo kubadili mienendo yake. Shilole sasa ameamua kutulia kuepukana na skendo.

Shilole ameliambia Dimba Jumatano kwamba kwa sasa ameamua kutulia na hatasikika katika skendo yoyote kwasababu anajiheshimu na ameamua kufanya maamuzi hayo kwa moyo mmoja.

Staa huyo pia alidhibitisha kuwa ndoa yake sio propaganda kama baadhi ya watu wanavyodai, alisema kuwa atakua mke wa mtu  hivi karibuni.

“Ndoa yangu si propaganda, mimi ni mchumba wa mtu na niwaambie tu kitu kimoja, nimeamua kutulia na mume wangu mtarajiwa na msitegemee tena kusikia skendo yoyote kutoka kwangu, mara leo kwa Khamis kesho kwa Juma, hapana,” alisema Shilole.

Shilole awatolea povu mashabiki zake

Shilole amekasirishwa na baadhi ya mashabiki wake wanaodai kuwa yeye bila ya kiki na kukaa mtupu hawezi kufanya vizuri katika kazi zake za kimuziki.

Hii ni baada ya mrembo huyo kuachia wimbo mpya ‘Kigori’ ambayo mbaka kwa sasa haijafanya vizuri katika mitandao ya kijamii.

Akiongea katika kipindi cha Friday Night Live ‘FNL’ cha EATV, Shilole alieleza kuwa wimbo wake haujafanya vizuri kutokana na yeye kutokata viuno kama mashabiki zake walivyozea kumuona katika nyimbo zake za awali alizowahi kufanya.

“Sikutaka skendo katika hii video, nilitaka kuwachukua wale real mashabiki zangu, nimefanya video nzuri kama mtoto wa kitanzania yenye maadili mazuri kwa ajili ya kila mtu, sijakaa utupu kabisa kwenye ‘video’ hii kama watu walivyozoea. Kwa hiyo inabidi tuwabadilishe na ndugu zetu watanzania waweze kuelewa kuwa kuna ‘video’ hii inataka iwe hivi na nyimbo hii inataka hivi ‘so’ kuna nyimbo za matashititi. Tuanze kukubali muziki kwanza siyo lazima kila siku niwe Shilole wa fujo fujo tu“, alisema Shilole.

 

Mipango ya ndoa ya Shilole sasa imeiva

Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole sasa yuko tayari kuwa mke wa mtu. Mrembo huyo sasa amebaki na miezi mbili tu afunge ndoa na mpenzi wake.

Kitu ambacho kimebaki kwa sasa ni kutoa kadi za mwaliko kwa ndugu, jamaa na marafiki kwani Shilole atafunga ndoa Oktoba, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Shilole

Msanii huyo aliambia Mtanzania kuwa anamshukuru Mungu na amewataka wasanii wenzake na mashabiki kumpa sapoti katika ndoa yake.

“Mipango ya ndoa inakwenda vizuri, hivyo Oktoba mwaka huu utakuwa mwezi wetu ambao Mwenyezi Mungu atatubariki kuunganisha familia,” alisema Shilole.

 

Shilole: Sina utata rafiki wangu kuwa na mahusiano na wapenzi wangu wa zamani

Zuwena Mohamed maarufu kwa jina la Shilole amefunguka kuhusu ishu ya rafiki zake kuwa na mahusiano na wapenzi wake wa zamani.

Shilole alisema kuwa  mapenzi ni kama ni kama daladala mtu akishuka mwenzake anakaa kwa hivyo yeye hawezi kuwa na uchungu rafiki zake wakipendana na wapenzi wake wa kitambo.

Staa huyo pia alifunguka na kusema kuwa atafunga ndoa wakati wowote kwani mpenzi wake tayari ameshatoa hela ya barua.

“Mimi kwa sasa hivi sina boyfriend kabisa, niwaambie tu nina mchumba ambaye tayari ameshanitolea mpaka barua, Mungu akijaalia harusi nitawakaribisha siku siyo nyingi. Na kuhusu wapenzi waliopita kuwa na mahusiano na marafiki zangu naona ni kitu cha kawaida kwa sababu naamini mapenzi ni kama daladala ukishuka mwenzako anakaa” Shishi alikiambia kipindi cha 5Selekt ya EATV.

 

Gigy Money aeleza sababu hampendi Shilole

Mrembo kutoka Bongo Gigy money ambaye ni star wa video za mziki amefunguka kudai kuwa yeye si shabiki wa nyimbo za Shilole wala hampendi.

Gigy alisema haya baada akisititiza kuwa yeye binafsi ni fan wa hip hop na kwa hilo jambo, yeye anamsupport Rosa Ree. Aliendelea kwa kusema yeye angepata mtu wa kumuandikia mistari, panda kufanya muziki ambao ungewavutia mashabiki wengi. Mrembo huyu alisema,

shilole
shilole

“Sina hata mpango wala sitaki, sio fun wake (Shilole), labda Rosa Ree, tatizo la watu walio up wanasumbua, so hip hop its better, mimi ningepata mtu wa kuniandikia niwe nachana ningependa, I don’t love this kind of music ambayo nafanya, nafanya ili nipate hela, mimi napenda hip hop,”

Hata hivyo Gigy anaonekana kuwa na ‘beef’ na mastaa wa kike kutoka Tanzania.