Alikiba aeleza kwanini Barakah The Prince alitemwa na lebo ya Rockstar4000

Barakah The Prince alikua amesainiwa Lebo ya kimataifa la Rockstar4000 kabla ya kuihama lebo hio. Alikiba ni mmoja wa wakurugenzi katika lebo hio la Rockstar4000.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio, Alikiba alifunguka na kusema kwa Barakah The Prince alitoka Rockstar4000 kwasababu ya utovu wa nidhamu.

Barakah The Prince na Alikiba

Kiba alieleza kuwa hakufurahishwa na vitu ambavyo Baraka alikuwa akifanya kwani aliona kuwa mwimbaji huo hakua na heshima kabisa.

“Baraka hayupo Rockstar, alitoka sababu za kukiuka vitu ambavyo hakutakiwa kufanya, Baraka nimemjua baada ya kuwa naye Rockstar400, lakini kiukweli sikufurahishwa na vitu ambavyo alikuwa akifanya, nadhani nilikuwa nikiona kama ni utoto lakini si utoto tena, ni kutokuwa na heshima nikaona haina haja, na mimi nikiwa kama mtu mzima sitakiwi kugombana na mtu mdogo inatakiwa umuache dunia imfunze kidogo, au kama kuna kitu ambacho amefanya au kalishwa sumu basi akapewe dawa itoke,” alisema Alikiba.

 

Barakah the Prince afungua YouTube mpya baada ya kuvurugana na lebo linaloongozwa na Alikiba

Alikiba alipandishwa cheo na kuwa mkurugunzi wa label ya RockStar4000 iliyokua imemsimamia Barakah the Prince kabla ya msani huyo kuondoka hivi karibuni.

Barakah The Prince alianza maisha yake mapya akiwa na label yake ya Bana Music baada ya ndoa yake na kampuni ya RockStar4000 kuvunjika.

Staa huyo ametangaza kwa mtandao wa kijamii kuwa anafungua akaunti mpya ya YouTube na kuiacha ile ambayo aliyokuwa akiitumia akiwa katika label ya RockStar4000.

“Ndugu zangu nitawatangazia soon YouTube channel yangu mpya kuna zawadi zenu kama 5 hivi…basi na hii itadondoka ndugu zangu,” aliandika Barakah Instagram.

Hatua hii ya Barakah the Prince imezua madai kuwa RockStar4000 imekataa kupea Barakah akaunti yake ya YouTube ya zamani.