Sina Tatizo Wala Ugomvi Wowote na Barakah the Prince- Ommy Dimpoz

Msanii wa Bongo fleva Ommy Dimpoz amefunguka na kukataa kuwepo kwa bifu lolote baina yake na msanii mwenzake Barakah the Prince.

Tetesi za wawili hao kuwepo na bifu zilienea baada ya Barakah kujitoa kwenye Label iliyokuwa inamsimamia ya Rockstar 4000 na baada ya muda mchache Ommy kujiunga, Label hiyo ambayo pia inamsimamia msanii Alikiba. Kutokana  na kitendo hicho cha Barakah kujitoa na muda huo huo Ommy kujiunga kilitafsiliwa na wengi kama walijiona hawataiva kwenye chungu kimoja hivyo mmoja wao akaamua kujitoa kwenye label hiyo.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka yafuatayo;

“Sidhani kama Barakah labda alitoka sababu mimi nimekuja hapana, kwanza naamini mi na Barakah tunafanya miziki tofauti yaani hatuna sehemu yoyote tunayoweza kusema hii inaweza ikatokea mkwaruzano, na tunaheshimiana yule ni mdogo wangu namkubali naamini ni moja ya watu wenye kipaji kukubwa kwa hapa Tanzania na kapambana kutengeneza jina lake”.

Ommy Dimpoz pia aliendelea kufunguka;

“Kilichomfanya aondoke Rockstar siwezi kukizungumzia na siwezi kujua ni nini, nafikiri yeye mwenyewe na label wana majibu sahihi zaidi. Siwezi kusema kama nahisi kuna pengo sababu wakati yeye yuko Rockstar mi sikuwepo kwaiyo wenyewe ndo wanaweza kujibu kama kuna pengo la Barakah au hakuna na pia mahusiano yangu mi na Barakah ni ya siku nyingi kabla hajaenda Rockstar yaani tupo sawa tu hatuna tatizo hata kidogo”‘

Ommy Dimpoz kwa sasa anatamba na nyimbo yake ya Cheche ambayo inashikilia namba moja kwenye stesheni za redio mbalimbali na pia kwenye mtandao wa youtube.

Ommy Dimpoz: Siruhusiwi Kumuongelea Mama yake na Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ommy Dimpoz amefunguka kuwa hawezi kuzungumzia tena ishu yake inayomhusu mama mzazi wa mwanamuziki mwenzake Diamond Platnumz.

Ommy Dimpoz na Diamond ambao walikuwa marafiki wazuri mwanzoni hadi kushirikishana kwenye kazi zao mbalimbali waliingia kwenye vita kali ya maneno wiki chache zilizopita huku Alikiba naye akiwa katika timbwili hilo ambapo inasemekana kuwa ugomvi huo unatokana na wivu wa kikazi kati ya wasanii hao huku kila mmoja akijaribu kwa namba moja kwa nafasi yake.

Ugomvi huo uliishia kuzua makubwa kwani Ommy dimpoz kumuingiza Mama yake na Diamond kwenye sekeseke hilo kwa kudai kuwa ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama huyo na kumwambia Diamond amuite Baba kitendo ambacho kilimuumiza sana Diamond na kuishia kwenda kumripoti polisi na Ommy kuitwa kwa mahojiano.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka haya kuhusu kesi hiyo;

“Kuhusu ilo swala tulishasema tukiongelea tunakuwa tunarudisha mambo nyuma so hata management imesema bwana hayo mambo usizungumzie tena na wewe ujiulize tangia nimetoka safari mpaka nimerudi nimeshakutana na vyombo vya habari vingapi lakini hujaona nikizungumzia kwani nikiongelea tutaamsha hisia za watu kwaiyo inakuwa haijakaa sawa lakini yaliyopita yamepita”.

Lakini pia Ommy aliongezea:

“Central police nilienda kwa vitu vingine ndo maana polisi walisema kama kuna mtu anataka kujua tulikuitia nini aje atuulize mwenyewe hivyo siwezi kuzungumzia kwani ni vitu vya kisheria kwaiyo na mimi saivi sitaki tena kuvunja sheria, lakini hayo mambo yameshaisha lakini nilichoitiwa bado naenda polisi kuripoti kama kawaida lakini hatuko kubaya sana”.

Ommy Dimpoz anafanya vizuri na wimbo wake wa cheche , pia anafanya vizuri kwenye fiesta zinazoendelea kwa kufanya shoo kali.

Dimpoz Akanusha Kuwa Na Mtoto Marekani

Msanii wa bongo Fleva ambae saivi anafanya vizuri na kibao chake cha ‘Cheche’ kilichoshika namba moja katika channel ya Youtube, amekanusha taarifa zinazosambaa kuwa ana mtoto mdogo na mwanamke nje ya Tanzania (Marekani) . Hata hivyo kuna baadhi ya mashabiki  wamefikia hatua mpaka ya kumtuhumu kuwa mwanamke aliyezaa nae mtoto sio yule aliyekuwa anaonekana nae katika picha ziliyovuja kipindi cha nyuma ikimuonyesha yuko na mwanamke faragha.

Akiongea na kipindi cha eNews cha Televisheni ya EATV, Dimpoz alikanusha taaarifa hizo na kusema hawezi kuwa na mtoto alafu aache kutangaza ,akionyeshwa kushangazwa na taarifa hizo Ommy alianza kwa kuuliza “mtoto  yupi tena’  hata hivyo taarifa za Ommy Dimpoz kuwa na mtoto zilianza kuenea pale ambapo Ommy aliposti picha katika ukurasa wake wa instagram ukimuonyesha amemshika mtoto wa kiume

“Yule ni mtoto wa rafiki yake  , ni  Promota ,mimi ni kama Godfather, wa yule mtoto anaitwa Liber,ni mtoto wa promota anaitwa DMK, sema nilivyopost watu waliona sura zetu kama zinafanana watu wakasema mtoto wa Dimpozi , lakini kweli siwezi kujisingizia mtoto,lakini Mungu akijalia,  mimi sitaleta konakona kama wangu nitambandika tu watu wamuone “anasema Dimpoz

Imekuwa ni kama tabia kwa baadhi ya wasanii kutokuwa  wazi kusema idadi ya watoto walionao  au kuwakata kutoka kwa mama zao,huku kwa bongo msanii Hemed Phd pia anaonekana kuwa ni moja ya wasanii wenye watoto zaidi ya mmoja lakini amekuwa akimpost na  akimtumia mmoja tu katika umaarufu wake.

Hata hivyo Dimpozi alipoulizwa kuhusu kesi yake inayoendelea ambapo siku chache zilizopita alionekana  kituo cha polisi ,Ommy alikataa kuongelea swala ilo na kusema kama wanaitaji taarifa izo waende kituo cha polisi.Ommy alioneakana kituo cha polisi zaidi ya mara mbili kwa mahojiano huku sababu yeye kuwepo kituoni hapo  bado haijajulikana. Kumekuwa na tetesi ambazo hazijathibishwa kuwa ni kutokana na yeye kuposti picha ya mzazi wa msanii mwenzie ambae hawaelewani na kuandika maneno yasiokuwa na heshima.

 

Ommy Dimpozi aonekana kituo cha polisi cha kati

Msanii wa bongo fleva Ommy Dimpozi anaetamba na nyimbo zake kama kajiandae aliomshirikisha alikiba lakini pia ametoa wimbo mpya hivi karibuni unaojulikana kwa jina la ‘cheche’  ameonekana maaeneo ya polisi kituo cha kati alipokwenda kwenye mahojiano kwa takribani zaidi ya saa tano.

Ommy Dimpozi jana septemba 13 alionekana kituo cha polisi majira ya saa tano asubuhi akiingia kituoni hapo huku akiwa ameongozana na watu wawili  katika gari aliyokuja nayo, hata hivyo kwa zaidi ya masaa matano Ommy Dimpozi hakuonekana kutoka mpaka mida ya saa 10:30 jioni , kwa mujibu wa waandishi wa habari ambao walikuwa kituoni hapo kufatilia press conference ya  kamanda wa polisi Mambosasa walisema walimuona Ommy Dimpoz akiingia kituoni hapo.

Hata hivyo jitihada zilizofanywa na waandishi wa habari wa Ayo tv za kumuhoji msanii huyo kuhusu uwepo wake kituoni hapo kwa zaidi ya saa tano , Ommy Dimpoz alijibu kuwa “ni mahojiano ya kawaida tu..tutaongea ila kwa sasaivi siruhusiwi kusema chochote” alisema Ommy Dimpozi  na kuondoka.

Kwa habari ambazo hazijathibitishwa ni kwamba inawezekana sababu ya Ommy kuwepo kituoni hapo kuhojiwa ni kutokana na post yake aliyoipost siku zilizopita hivi karibuni inayomuhusu mama Diamond, na kwa kumbukumbu ni kwamba wasanii hawa wawili walikuwa katika vita ya kimtandao ambayo ilifikia hadi kumhusisha mama mzazi wa Diamond., na bado haijafahamika bado  ni nani hasa aliyepleka kesi hiyo kituoni hapo kati ya familia ya Diamond au Diamond mwenyewe, lakini ilhali amehaidi kuliongelea swala ilo tunasubiri Ommy afunguke zaidi.

Hata hivyo, baada ya press conference , mkuu wa kituo hakuongelea chochote kuhusu msanii huyo kuwepo kituoni hapo.

Ni week chache zimepita tangu kuwepo kwa mfarakano wa team kiba na team diamond ambapo Ommy ni supporter mkubwa wa team kila ilhali katika kumbukumbu za awali  ommy dimpozi alikuwa mtu wa karibu kabisa sana wa  diamond platnumz na hakuna aliyewahi kufikiria kuwa kutakuwa na bifu zito kati ya wawili hao.

Ommy Dimpoz atii onyo kali kutoka kwa dadake Diamond Platnumz

Diamond Platnumz, Alikiba na Ommy Dimpoz wamekua wakitupiana maneno yenye mafumbo katika mitandao ya kijamii tangu Diamond aliposhirikishwa katika remix ya ngoma ya Fid Q ‘Fresh’.

Bifu hio baina ya wasanii hao watatu ilifanya Ommy Dimpoz kuweka picha Instagram akiwa na mama mzazi wa Diamond na kuandika ujumbe wenye utata.

Aunty Ezekiel ambaye ni meneja wa zamani wa Ommy Dimpoz na dadake Diamond walitoa onyo kali kwa Ommy Dimpoz kukoma kumuingiza mamake Diamond katika ugomvi wake na Diamond.

Onyo hilo kutoka kwa dadake Diamond na mashabiki kadhaa ilichangia Ommy Dimpoz kuamua kuifuta post yake ya utata aliyoiweka kwenye Instagram.

Account ya Ommy Dimpoz ya Instagram ikionyesha kuwa alitoa post ya utata akiwa na mamake Diamond

 

Steve Nyerere atoa ushauri wake kuhusu bifu mpya kati ya Diamond, Alikiba na Ommy Dimpoz

Diamond Platnuz, Alikiba na Ommy Dimpoz wamekua wakitupiana maneno yenye mafumbo katika mitandao ya kijamii tangu Diamond aliposhirikishwa katika remix ya ngoma ya Fid Q ‘Fresh’.

Diamond alisema kwa wimbo huo kuwa hawezi kulinganishwa na Alikiba kisha Kiba naye akamjibu kwa fumbo kuwa yeye bado ndo mfalme.

Diamond tena aliweka wimbi nyingine kwenye account yake ya Instagram ambayo aliwachimba Alikiba na Ommy Dimpoz. Baada ya Diamond kuweka wimbo huo kwa Instagram, Ommy Dimpoz pia aliweka picha Instagram akiwa na mama mzazi wa Diamond na kuandika ujumbe wenye utata:

Ommy Dimpoz na mamake Diamond

“BARUA YA WAZI KWA BINTI YANGU MALKIA WA NGUVU

Salam zako nimezipata mwanangu Hivi kweli ww wa kukosa Adabu na kuamua kunichamba mimi Baba yako? Sasa kosa langu mimi nini???? Kwani kuna Ubaya kumtandikia Kitanda Baby wako King?

#UnanioneaKwaKuaSijuiKurap?

#SijuiNaMimiNimkatae??

#KamaYeyeAlivyomkataaWaMobeto

#YaniUnamkataaMjukuuWangu??

#UnakubaliKuleaWatotoWa5SioWako

#UmerogwaWWSioBureMwanangu

#NilikuwaNajuaNimezaaSIMBA

#KumbeNimezaaKIMBA

#DavidoNaeAnalalamiKuhusuENEKA

#UmeletaJanjaJanjaKwenyeFallOnU

#NnaedhalilikaMimiBabaYaKo??

#UtakujaKuniuaKwaPreshaJomoniiii?

#HayaNendaKatungeVesiNyingine?

#RahaYaVitaUsichagueSilaha

#BABAMALKIA

 

Steve Nyerere sasa ameingilia kati na kutoa ushauri wake, somo ujuembe aliondika kwa Instagram hapoo chini:

“NIMEKAA NIMEJIFIKIRIA NIMEONA NISEME KIDOGO, DUNIA MAMA ANA HESHIMA YAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE, MAMA NI KIOO CHA FAMILY MAMA NI NGUZO YA FAMILY MAMA NI KIMBILIO LA FAMILY , TUNAWEZA KUKOSEA KOTE LAKINI SI KWA MAMA NDOMANA AMNA LAANA YA BABA ILA LANA YA MAMA IPO NA INAFANYA KAZI HARAKA KULIKO KITU CHOCHOTE, SIZANI KAMA TUNA ELIMISHA JAMII KUPITIA MATUSI YA KUZALILISHA WAZAZI, NYINYI NI KIOO CHA JAMII, LAZIMA MUWE NA KIFUA CHA KUBAKISHA MANENO , MIMI NILIZANI HIZI NGUVU MNAZOTUMIA MNGEWEKEZA KWENYE MZIKI WENU TUNGEFIKA MBALI SANA , MMEJIJENGEA HESHIMA NA MMELITAFUTA JINA KWA SHIDA , ILA MNASAHAU JINA HILO LINAWEZA POTEA KWA SEKUNDE, NAWASHAULI NA NAKUSHAULI WEWE UNAYEZARAU WAZAZI FUTA KAULI NA OMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI ZAKO USUSANI KINA MAMA WOTE AMBAO NAAMINI NI MASHABIKI WAKO NA NDIO WALIOKUFANYA UKAFIKA HAPO, HATUKATAI NYINYI NI BINADAMU INAWEZEKANA MMEPISHANA KAULI ILA KWENYE KUPISHANA WEKENI AKIBA YA MANENO, KUNA KESHO HUJUI ATAKAYE KUSTILI, HAKIKA BUSARA ITUMIKE , YANI NINGEKUWA MIMI NDIO UMEMGUSA RITA WANGU IVO DOOOO, MJINGA HAJIBIWI, KICHAA HAKIMBIZWI , MWIZI SI RAFIKI, NANI KAMA MAMA, ESHIMA ITAWALE ASANTE BY #####UZALENDO KWANZA.”

Steve Nyerere

 

Alikiba na Ommy Dimpoz watoa ujumbe wa amani kwa Wakenya

Wakenya walipiga kura jana Agosti 8 kuchagua rais na viongozi wengine kadhaa. Uchaguzi huo umezua utata kwani upinzani umepinga matokeo yanayotolewa na tume ya uchaguzi.

Alikiba na Ommy Dimpoz wametoa ujumbe wa amani wakiwaomba Wakenya kuzingatia amani katika kipindi cha uchaguzi nchini mwao.

Ommy Dimpoz: Nawatakia Ndugu zangu Wakenya Uchaguzi wenye Amani na Upendo M/Mungu Awalinde Mmalize Salama AMEN

Alikiba: Nawatakia kila la kheri na uchaguzi Wa AMANI na SALAMA #AMEEN