Nay wa mitego :Sina Tatizo na Alikiba na U-team wao Haunihusu.

Msanii wa  bongo fleva ambae  muda mwingi ujikuta katika vita na wasanii wenzake kutokana na tabia yake ya kutoa makavu kwa wasanii wenzao kwa kile wanachokuwa wanakifanya ,Ney wa Mitego amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake hana bifu wala ugomvi na msanii wenzake  Alikiba kama watu wanavyokuwa wanatangaza na kuzasha katika mitandao ya kijamii kuhusu swala hilo.

Nay wa Mitego anasema kuwa yeye ana Alikba walishawahi kutoa wimbo huko miaka ya nyuma kipindi wote wawili walikwa bado hawajapata majina makubwa ya kuwafanya aanze kujulikana sana katika kiwanda cha muziki, hata hivyo Ney wa Mitego anasema kwa upande wake huwa afatilii sana maswala ya teams kwa sababu hazimuuhusu kitu lakini wanatakiwa kujua kuwa hata yeye pia na team yake.

sina shida wala tatizo na alikiba nahata hzio team zao mimi hazinuhusu,mimi mwenyewe nina team true boy watu hawajui tu na nilishawahi kufanya kazi nzuri tu  na Alikiba kitambo sana hata kabla sijawa mkubwa kiashi hiki na hata alikiba baso alikuwa hajawa alikiba huyo wa sasa alikuwa Alikiba wa sinderela, na kipindi hicho nilitoa wimbo unaitwa watafahamika.-Alisema Ney wa Mitego.

Ney wa mitego wiki za nyuma alisikika akisema kuwa kwa sasa hataki kubishana kuhusu swala la muziki na mtu yoyoye zaidi sana anajikita katika kufanya kzi kwa sabau amegundua kuwa watu wanakaa wakimpotezea muda katika kubishana nae huku wenzao wanatafuta kiki.

 

Nay wa Mitego ni Bingwa wa Kukata Mauno

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Nay wa Mitego amedaiwa mbali ya kuwa na kipaji cha kuimba na kuchana lakini pia ni fundi mkubwa sana wa kukata mauno.

Ney wa Mitego aliyetoa ngoma yake mpya siku ya jumatatu inayoenda kwa jina la ‘Mikono juu’ ameonekana kwenye video  ya nyimbo hiyo akikata mauno balaa ambayo yamezoeleka kuonekana kwa msanii kama Bob Junior lakini sio msanii mgumu wa hip hop kama Nay wa Mitego.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Nay amesema yeye ndio aliyemwambia director ashoot hiyo sehemu anayokata mauno maana ni lazima ufanye kitu tofauti kila siku:

Mimi ndio nilimwambia Nicholaus achukue kile kipande nikiwa napiga uno kidogo lazima ufanye kitu ambacho mtu hatarajii kama utafanya ili mradi kilete utofauti na ndio maana leo hii tupo hapa tunazungumzia vile viuno vyangu kwenye video unajua siku nyingine huwa tunafanya chumbani lakini sahivi tumeamua kuvileta huku ili angalau watu nao wajue sio kwamba hatuwezi hapana tunaweza kujaribu na kufanya utofauti kidogo inaruhusiwa ili kusaidia katika kuleta chachu na kachumbari kwenye kazi na ndio maana sahivi tunazungumzia kile kitu ambacho kipo kwenye ile kazi ni cha tofauti na hakuna mtu aliyekuwa ametarajia kuona mauno yangu”.

 

Nay wa Mitego Kajibu Povu la Godzillah

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nay wa Mitego, amejibu rasmi povu lililotolewa na msanii mwenzake wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana Godzillah.

Nay wa Mitego ameachia rasmi ngoma yake jumatatu hii inayoitwa Mikono Juu cha ajabu kilochotokea hapo ni kwamba Nay alipoweka wimbo ule kwenye ukurasa wake wa Instagram Godzillah aliibuka na kudai wimbo ule mbaya lakini hata alipohojiwa na kituo kimoja cha redio alisema Tena kuwa wimbo huo ni mbaya.

Baada ya povu hilo kila mmoja alitegemea Nay wa Mitego atapanick na kumtolea povu zito lakini imekuwa tofauti sana kwani alipohojiwa alisema haoni shida kwani kila mtu ana mtazamo wake binafsi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Nay alifunguka yafuatayo:

Kwanza kwa nini nipanick kisa kaniambia ngoma mbaya? Huo mtazamo mtu anatoa ule anaoona yeye huwezi kupanick utakuwa sio mtu unayefanya kitu kwa ajili ya watu na ukipeleka kitu kwa watu wengi sio kila mtu atapenda alafu mimi nafanya kitu kwa ajili ya watu wengi and then mimi nawajua watu wangu ninaowaimbia lakini pia naamini kizuri hakipendwi na kila mtu asikwambie mtu Yesu mwenyewe alipingwa itakuwa mimi NAy wa Mitego?”.

Lakini pia ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Godzilla na kuna nyimbo zake nyingi anasikiliza pia amesisitiza hana muda wa kukaa na kutengeneza bifu na mtu yeye yupo kikazi kwaiyo anachukulia comment ya Godzilla kama ya shabiki yoyote.

Godzillah ‘Amchokonoa’ Ney wa Mitego

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya hip hop Godzillah ameibuka na kumchimba Msanii mwenzake wa Bongo fleva, Nay wa Mitego baada ya kumwambia nyimbo yake aliyoitoa ni mbaya.

Nay wa Mitego amaechia nyimbo yake mpya na video yake ya wimbo unaoitwa ‘mikono juu’ lakini kitu cha ajabu kilitokea pale ambapo Godzillah alienda kukomenti kwenye page ya Nay na kusema nyimbo mbaya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego aliandika maneno haya ili kutambulisha ujio mpya wa video ya wimbo wake wa Mikono juu:

Video ya wimbo wangu wa mikono juu inatoka kesho jumatatu Subscribe kwenye account yangu ya YouTube #Mr Nay uwe wa kwanza kutazama video yangu”.

Baada ya kuweka posti hiyo cha ajabu Godzillah aliibuka na kwenda kuandika kwenye page ya Nay maneno haya:

Wimbo mbaya Emanuel”.

Ney wa Mitego Amchana Diamond Baada ya Kuachwa na Zari

Msanii wa Bongo fleva Ney wa Mitego amemtolea povu zito msanii mwenzake Diamond Platnumz baada ya mpenzi wake Zari kutangaza rasmi kuwa amemuacha kutokana na michepuko kuzidi.

Jana usiku Zari aliwashtua watu wengi baada ya kuweka wazi kuwa ameamua kimya cha Diamond kutokana na kuzidi kudhalilishwa na taarifa za yeye kuwa na michepuko mingi huku mambo yaliyokuwa yanatokea kwenye mitandao ya kijamii yalikuwa yanamuumiza.

Kumekuwa na skendo nyingi mtandaoni za Diamond kuchepuka na wanawake kadhaa huku pia kumekuwa na uthibitisho wa vitendo hivyo lakini kwa muda mrefu Zari alionekana kuvumilia na kumsamehe mpenzi wake huyo lakini safari hii inaelekea maji yalimfika shingoni.

Baada tu ya Zari kutangaza kumwaga Diamond mashabiki walianza kumlaumu Diamond kwa kumuacha mrembo kama Zari aende kwa tabia yake ya kuendekeza michepuko moja kati ya watu hao ni msanii Ney wa Mitego.

Nay kumtolea povu zito Diamond kwa kumuacha mtoto mzuri kama Zari ambaye ana pesa zake na badala yake kuendekeza michepuko ambayo hainam maana ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego alitoa povu hili:

Wanasema chozi la aliyetendwa haliendi bure mwanangu Diamond, Omna sana Mungu akuonyeshe njia la si hivyo utapotea… umempoteza mwanamke ambaye hana njaa ana maisha yake binafsi alichokuwa anataka ni mapenzi yako tu sikatai kuwa hakuna mwanaume asiyekuwa na tamaa lakini ulifeli kufanya uchafu wako wazi wazi”.

Baada ya kutoa povu hili imeonyesha wazi kuwa Nay wa Mitego na Diamond hawana urafiki mzuri kama waliokuwa nao mwanzoni ambapo siku za nyuma kulikuwa kuna habari zikidai kuwa wamekorofishana.

Ney wa Mitego Awashangaa Wasanii Wanaotumia Uchawi Kwenye Sanaa

Msanii wa Bongo fleva Ney wa Mitego ameibuka tena na kusema kuwa anashangaa sana pale anaposikia wanamuziki wanatumia ndumba kwenye kazi zao.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Clouds FM kupitia kipindi cha XXL msanii huyo amefunguka yafuatayo kuhusiana na suala hili;

“Umefika muda Tanzania nzima inaamini katika kile ambacho ninafanya, hii ni ndele tosha ni zaidi ya ndele sijui mtu ambaye anaamini hivyo, halafu ndele huwa zina mwisho ukifika muda maana wewe ndo umemaliza hata uimbe vipi hata umshirikishe Yesu bado watu hawaelewi’.

Pia msanii huyo anayetamba na wimbo wake wa ‘Makuzi’ ameongeza kuwa msanii yoyote anayeamini kwenye uchawi huishia katikati ya safari na hupotea katika ramani ya muziki. Nay amekana vikali kujihusisha na ushirikina wa aina yoyote na kudai kuwa kwake kipaji alichojaaliwa na Mungu kinaongea chenyewe.

Wasanii wengi wa Tanzani wamekuwa wakijihusisha na imani hizo za kishirikina kwa hofu ya kupotea kisanaa ingawa wengi wao hukana hadharani lakini inasemekana wengi wao hutumia waganga wa kienyeji ili tu wakae kwenye sanaa hiyo kwa muda mrefu na kufnya kazi ambazo mashabiki watazipokea.

 

Nay Wa Mitego: Nliumizwa sana na maneno ya Roma Mkatoliki

Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay Wa Mitego amefunguka kuhusu bifu yake na Roma Mkatoliki iliyoonza baada ya Roma kutekwa nyara miezi kadhaa iliyopita.

Roma aliongea maneno ya kumkashifu Nay Wa Mitego mara baada ya yeye kuachiliwa na watu waliomteka nyara akiwa na wenzake kwa studio yake.

Nay Wa Mitego

Nay ata hivyo hana machungu na Roma, rapa huyo alisema yeye bado anamtakia mema Roma hata kama maneno aliyosema juu yake yalimuuma sana.

“Roma anatakiwa ajue kwamba mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao walishinda kutwa nzima kwenye studio yake ya Tongwe Records na kituo cha polisi, toka siku aliyotekwa hadi siku aliyopatikana, lengo likiwa ni kutaka kujua tunasaidiana vipi ili aweze kupatikana. Akitaka kuthibitisha hilo amuulize mkewe, lakini nikashangaa baada ya kupatikana eti akanikashifu, kila nikikumbuka inaniumiza, sema mimi ni mwanaume siweki vitu rohoni, na pia nimeipenda sana ngoma yake ya Zimbabwe, Roma ni rapa mkali, sina kipingamizi juu ya hilo,” amesema Nay Wa Mitego.

Roma Mkatoliki

 

Malkia wa filamu Shamsa Ford amaibisha mpenzi wake wa kitambo – Nay wa Mitego

Rapper Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameaibishwa hadhani na Shamsa Ford – mpenzi wake wa kitambo.

Apo awali ilisemekana kuwa Shamsa Ford atakuwepo katika show ya ‘Wapo Tour’ ya rapper Nay wa Mitego itayofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, May 20 2017.

Nay wa Mitego ndo alisemekana kuwa chanzo cha habari kuwa mpezi wake wa kitambo Shamsa Ford atakuwepo katika show ya ‘Wapo Tour’

Shamsa Ford na Nay wa Mitego walipokua bado wanapendana

Malkia huyo wa filamu hata hivyo amemkana Nay wa Mitego na kumaibisha hadharani. Akiongea na Bongo 5, Shamsa Ford alisema kuwa hajui chochote kuhusu show hiyo kwasababu Nay wa Mitego hajawai mwambia lolote kuhusu show hilo.

“Kusema kweli sina show yoyote na mtu na wala sijazungumza na Nay wa Mitego kuhusu show ya Dar Live. Hajaniambia chochote siwezi kudanganya, ndio kwanza hizo taarifa naziona katika mitandao ya kijamii. Kama kweli na mimi nitakuwepo ungeona hata nikipost. Kwahiyo sitakuwepo kwenye hiyo show kwa sababu sina taarifa yoyote,”alisema Shamsa Ford.

 

Yusuph Mlela atoboa siri kali kuhusu msanii Nay wa Mitego

Na kwa kweli hii wiki si ya Nay wa Mitego hata kamwe.

Baada ya mama ya mtoto wake kutokea mitandaoni na kueleza Nay hashughuliki na mtoto wake na ila anatafuta kiki naye, muigizaji mkali Yusuph Mlela pia amejitokeza kukashifu Nay wa Mitego.

Akizungumza na global TV alieleza ya kwamba Nay wa Mitego alikuwemo Chokoraa miaka iliyopita na kuna mambo mbalimbali ya aibu iliyotokea wakati humo ambayo utayapata kwenye hii video:

Nay wa Mitego azindua msanii wake wa kwanza kwenye label yake mpya

Free Nation 966, label mpya ambayo Nay wa Mitego alizindua imefahamisha msanii wa kwanza.

Ni rapa anayejulikana kama B Gway atakaye fuatwa na mwimbaji hivi karibuni.

“Leo label yangu ya ‘Free Nation 966’ imemtambulisha kijana wake wa kwanza ‘B Gway’,” alisema Nay. “Ni msanii mkali sana, sikutaka kumchukua msanii ambaye anatanisumbua, tena wimbo wake wa kwanza ‘Sijachukua’ amenishirikisha,”

Aliongeza, “Kwahiyo ningependa kuwaambia mashabiki wasubirie mambo mazuri kutoka ‘Free Nation 966’. Pia siku chache zijazo tutamtangaza msanii mwingine wa kuimba,” Nay wa Mitego alieleza Bongo 5.

 

Nay wa Mitego amjibu Skyner Ally baada ya kudai ameshindwa kuwa baba bora kwa mtoto wake

Mwanamuziki wa Tanzania Nay wa Mitego hivi karibuni aliiabishwa na muigizaji wa filamu Bongo, Skyner Ally baada ya kumchana kwa kumwambia kuwa hajakuwa akimtunza mtoto wao kama anavyostahili.

Skyner na Nay wakona mtoto wa kike pamoja lakini muigizaji huyo wa filamu amedai kuwa Nay hajakuwa akimsaidia mwanae. Hii ilikuja baada ya Nay alipoweka picha ya mtoto wao mtandaoni wa Instagram huku akimsifu kwa uzuri wake.

Hata hivyo Skyner hakupendelea kwani Nay hajakuwa akihusika na mambo ya mwanae kwa muda mrefu sasa. Kilicho muuma zaidi ni kwamba Nay alikuwa anawadanganya mashabiki wake kuwa anawatunza wanawe vyema ilhali alikuwa ameshindwa kuwa baba bora kwa mtoto wa Skyner ambaye alizaa na yeye.

Inaonekana kuwa Nay aliweza kuiona post ya Skyner na kupitia mtandao wake wa Instagram, Nay aliandika kusema…

“Si kwa kichambo kile jamaniiiiii huh??! Jamani inatosha basiii Povuuu. Nitapeleka Matumiziiiii???. Nawapenda sana awa Watoto Wanguu?. Wasiopeleka Matumizi ya Watoto?? #Wapo,”

Haya basi, wacha tutazame watakacho kifanya hawa wawili sasa.

Skyner amchanwa na Nay baada ya kuposti picha ya binti yao

Skyner aliyekuwa mpenzi wa msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego, hivi karibuni aliamuaibisha baada ya kuweka picha ya binti yao mitandaoni huku akijisifu kwa uzuri wa mwanae.

Hata hivyo Nay wa Mitego hakukipata alichotarajia kutoka kwa Skyner ambaye alimchana kupitia Instagram huku akifunguka kuwa Nay hajakuwa baba kwa manae kwa miaka ilhali anawadanganya watu mitandaoni.

Ujumbe na Nay wa Mitego ulisema,

Skyner ambaye alikasirishwa na ujumbe huu aliandika ujumbe akimshangaa Nay ambaye anasemekana kuwa hataki kutoa huduma kwaajili ya mtoto. Aliandika kusema,

“Thats face you make when you see your ‘daddy jina’ anakufanyia promotions na kudanganya Watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi unayovaa hajui thamani yake maskini. Nimevumilia sana it’s 5 Years now nimejiskia kutapika na nimetapikaa. Am done Mungu wa mbinguni nakuomba unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki….. uzima wa afya nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake”

Aliendelea kwa kusema…

“Endelea na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki…Please unapost picha za mtoto wangu za nini…shobo dundo zanini? Sitaki shobo na mwanangu koma kama ulivyo komaaa…Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done”

Aliendelea kwa kuonyesha binti yake alivyokuwa muhimu katika maisha yake alivyoandika kusema…

“Hakuna anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba’ko hana analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy Birthday My Happiness,” alisema Skyner.

Hata hivyo rapa huyo bado hajazungumza chochote kuhusu sakata hilo, Bongo5 bado inafanya jitihada za mtafuta.

“Nay nataka round 3 tu za boxing kwenye stage”Muigizaji Yusuph Mlela aomba kupigana na Nay wa Mitego

Nay wa Mitego  alitumia ukurasa wake wa Instagram kukosoa baadhi ya  wasanii wa Bongomovie huku akiwataka wafanye kazi bora pia.

Nay alidai kuwa wasanii wa Bongomovies wanapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya kwa lengo la kutaka wafanyabiashara wanaouza filamu za nje ya nchi wafungiwe kwani hawafuati  taratibu ambazo wasanii wa bongomovie wanazifata wakati wa usambazaji wa kazi zao.

Muigizaji Yusuph Mlela alikerwa na maneno aliyosema Ney na kuamua kumjibu kwa hasira –alimtukana na pia kuomba apigane naye ngumi.

Yusuph Mlela na Nay wa Mitego

“Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa wewe leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa waigizaji\wanamuziki wakubwa….acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi… sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la maandamano.

“Nay wa Mitego acha kutafuta sifa… nakushangaa kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe siyo msanii…halafu huwezi kufananisha filamu na muziki….. Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu….. This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ********** kuongea sana tabia za kike wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale” Yusuph Mlela alisema.

 

Nay Wa Mitego: Mwambieni Diamond pia awe mpole kwasasa alee watoto

Nay Wa Mitego amezua hisia tofauti baada ya kumpasha Rich Mavoko ujumbe ambao alitaka uwafikie wasanii wote wa Wasafi Diamond akiwepo.

Rich Mavoka aliandika kwa ukurasa wake wa Instagram kutambulisha wimbo wake mpya ambayo bado haujaachiliwa kwenye redio na runinga.

“Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii ? #Showme” Rich Mavoko aliandika.

Nay Wa Mitego alimjibu haraka, alimwambia asubiri mbaka mwakani 2018 ndo watoe nyimbo (wasanii wa Wasafi.) Alimwambia apitishe ujumbe kwa Diamond ambaye alimtaka alee watoto kwanza.

Nay Wa Mitego na Diamond

“”NAOMBA MUENDELEE KUSUBILI, MAY BE MPAKA MWAKANI 2018, NDO MTAANZA KUJISHUGHULISHA NA MASWALA YA KUWAIMBIA WANA NCHI. MWAMBIENI NA BABA YENU PIA AWE MPOLE KWASASA ALEE WATOTO. KAZI TULIYO NAYO IKIENDA SAWA TUTA WARUHUSU MUENDELEE KUBURUDISHA WANA NCHI. TUNATAKA MAMBO YAENDA SAWA KWANZA✊?. Wimbo wetu wa TAIFA ni #Wapo LINK ON MY BIO☝”,”Nay Wa Mitego aliandika.

Ujumbe wa Nay Wa Mitego hata hivyo ni utani tu, Diamond ni rafiki wake mkubwa ambaye alishirikiana naye kutoa ngoma kali sana ‘Muziki Gani’.  Si mara ya kwanza wawili hao kutupiana vijembe kupitia mitandao.

Video ya WAPO itatokea rasmi siku hii kulingana na Nay wa Mitego

Nay wa Mitego ambaye amekuwa zungumzio kubwa Tanzania hivi karibuni baada ya wimbo wake mpya Wapo leo alitoa rasmi siku ambayo video ya wimbo huo itatokea.

Na alitoa ujumbe kwenye instgram yake.

hivi ndivo alivysema: