Madee Ali – Ni Ruksa Mwanangu Kufananishwa na Mai

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Madee Ali amedai ni ruksa kwa watu kumfananisha mwanaye mdogo anayejulikana Kama ‘Chonge’ na Mtoto muigizaji Mai Zumo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Madee amesema kuwa hana neno pale anapoona watu wanafananisha Mtoto Wake na Mai Zimo kwani duniani wawili wawili.

Nimekuwa nikiona mara nyingi watu wakimfananisha binti yangu Chonge na huyu mtoto mchekeshaji Mai Zumo, ni kweli wanafanana na huwa sichukii kwa sababu ni jambo la kawaida.

Lakini Pia duniani watu wawiliwawili, hivyo Mungu akitujalia, basi itabidi wafanye kitu cha pamoja ili tutengeneze pesa.”

Mtoto wa Madee, Chonge na Mai Zumo mara kadhaa wamekuwa wakifananishwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na sura zao kufanana.

Madee Afungukia Furaha Yake Kuwa Mzazi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Hamadi Ali ‘Sheneida’ ‘Madee’ amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu kinachompa furaha kama vile kuwa mzazi.

Madee ambaye ni baba wa watoto wawili wa kike amefunguka kuwa endapo watu watamuona kitaa akiwa amembeba binti yake wasije kudhani kasusiwa na mama yake la hasha ila ameamua mwenyewe.

Wakati wanaume wengi wakisifika kwa kukwepa kulea watoto wao Lakini  Madee ameibuka na kudai kuwa kwake hiyo wala si ishu, anapenda kinoma kulea Watoto Wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Madee ameweka wazi Furaha anayopata kuwa karibu na Watoto Wake na hasa kuwapa malezi ya baba.

Hakuna kitu kinanipa raha kama ninavyomlea mtoto wangu, yaani nikimuona ananipa nguvu nyingi ya kutafuta pesa ili aweze kukua katika maisha bora yeye na dada yake.”

Madee amewashauri wanaume wenzake kuwepo kwenye maisha ya Watoto wao ili kuvunja Imani za kuwa wamama peke yao Ndio Walezi.

Madee Aweka Wazi Ndoto Yake Ya Kumiliki ‘Private Jet’

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva ameelezea ndoto yake juu ya kumiliki ndege yake binafsi (Private jet) siku moja katika maisha yake.

Madee ameweka wazi kuwa ana ndoto ya kumiliki ndege katika maisha yake kiasi cha kumnyima usingizi wake kila siku.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Madee ameandika, “ndoto inayosumbua usingizi wangu,” huku akiwa katika picha inayomuonesha akitembea kuelekea kwenye ndege ndogo.

Kauli hiyo ya Madee kuhusu kumiliki ndege inakuja miezi michache baada ya nyota wa soka nchini anayechezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta kueleza matamanio yake juu ya kumiliki ndege yake binafsi.

Septemba 12, Samatta katika ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Ndoto za kumiliki ‘Private Jet’ zimeanza baada ya kupiga picha hii, sio kila ndoto inaweza kutimia ila acha vita ianze”.

 

Kilio Cha Madee Kwenda Kwa Waziri Mwakyembe

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba na miondoko yake ya kuchana Madee Ali ‘Rais wa Manzese’ ametuma ujumbe mzito kwa Waziri Mwakyembe.

Madee amemtumia ujumbe  Waziri wa Habari, Sanaa, utamaduni na Michezo Dkt Harison Mwakyembe wa kumtaka kuliangalia suala la uchezwaji wa nyimbo za wasanii Kwenye vyombo vya habari.

Madee ameonekana kusikitishwa na vitendo vya asilimia kubwa ya vyombo vya habari kucheza ngoma za nchi za nje kuliko ngoma za wasanii wa Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Madee amemuomba Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo Dkt Harison Mwakyembe kuliangalia swala hilo huku wengi wakiamini kuwa linashusha hadhi ya muziki wa Bongofleva pia inawakatisha tamaa wasanii.

Mh Waziri wa habari na Utamaduni baba yetu Harrison Mwakyembe ngoma zetu hazionekanai kwenye television za nyumbani tunaangalia mangoma ya nje tu yanayopigwa na television zao tafadhali chezesha baba”.

 

Dogo Janja Ataja Ngoma Ambayo Haikubali Kutoka Kwa Madee

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kuanika jina la ngoma kutoka kwa Msanii mwenzake Madee Ali.

Dogo Janja ameitaja ngoma ya Madee ‘Hip Hop haiuzi’ kama moja ya nyimbo za Msanii huyo ambazo hajawahi kuzikubali kabisa.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kwetu Flavor cha Magic Fm Dogo Janja ametaja ngoma ya Madee ‘Hip Hop Haiuzi’ kama wimbo ambao hakupendezwa nao kabisa pindi ulipotoka.

Kipindi hiyo unatoka nipo chuga, nachana sana na masela. Nikaona huyo vipi, masela wanasema huyu waki labda hasije chuga, tutamfanyia kitu mbaya”.

’Hip Hop haiuzi’ ni nyimbo ya Madee ambayo ilizua gumzo sana miaka ya nyuma ambapo wasanii wenzake ambao wanafanya muziki wa Hop Hop walimjia juu MAdee baada ya kuuponda muziki wao wa hip hop.

 

Belle 9- Dogo Janja Ndio Anatakiwa Kuchapwa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Belle 9 ameibuka na kudai kama kuchapwa anatakiwa kuchapwa Dogo Janja sio yeye.

Wiki iliyopita Dogo janja Kwenye Interview yake alisema Belle 9 anahitaji kuchapwa viboko 70 baada ya kusema Hamuelewi na hata nyimbo zake anzoimba huwa hazielewi.

Kwenye mahojiano na Enews ya EATV, Belle 9 amemjibu Dogo na kusema inabidi achapwe yeye kwani nyimbo yake mpya ya ‘Banana’ ni ngoma ya kihuni na hajaielewa:

Nilivyosema msanii ambaye simuelewi ni Madee sikuwa na maana mbaya na samahani kama wamekasirika lakini niliongea kwa uzuri maana ni msanii ambaye huwa namuangalia.

Kusema ukweli nilivyosikia anasema nichapwe viboko nilicheka sana na huenda tunatofautiana kufikiria na labda kwa mazingira aliyokulia yeye anaona kuchapwa viboko kunaweza kumbadilisha mtu ila sio pointi sana maana mambo yamebadilika.

Halafu kama ni viboko anatakiwa achapwe yeye kwa nyimbo anazoimba zenye  utata kwani nyimbo iliyopita alivaa kama mwanamke na nyimbo yake mpya ya Banana anaimba sijui your my Banana na wote tunajua Banana ina maana gani”.

 

Dogo Janja- Belle 9 Amemkosea Sana Madee

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Dogo Janja anayefanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Banana’ amedai kuwa Msanii mwenzake Belle 9 amemkosea sana Madee hivyo anahitaji kuadhibiwa.

Wiki chache zilizopita Kwenye mahojiano na Jembe FM ya jijini Mwanza Belle 9, alimtaja Madee kama rapa wa Tanzania ambaye haelewi nyimbo zake kabisa anaona kama mzugaji kwani anaona ni msanii ambaye anatoa ‘beat’ tu na sio wimbo.

Katika interview na Enews ya East Africa Tv, Dogo Janja amemjia juu Belle 9 kwa kumwambia kuwa amekosea sana kumbeza msanii mkongwe kama Madee ambaye ameshawahi kutoa ngoma kali nyingi hata kabla ya Belle 9 kujulikana kwenye muziki.

Kitu cha kwanza hata yeye Belle 9 kuna vitu anafanya kuna watu huwa hawamuelewe, hata mimi mwenyewe kuna wanangu kibao huwa wananiambia bora Nuruely. Alichokifanya Made kwenye muziki, Belle 9 hata robo hajafikia.. Respect a legend, waheshimu wakongwe, waheshimu wazee sio busara kutukana wakongwe.

Kakosea amemkosea mzee, anatakiwa apigwe 70 bomani (wamasai hapo wamenielewa) ukivunja sheria au ukimkosea mkubwa au mzee unatakiwa uchapwe fimbo 70 mbele ya wanabomani wote.. Madee mpole sana ndio maana wanamuonea. ni mkongwe anayezeeka na heshima zake”.

 

Madee Hana Mpango Wa Kusaini Msanii Wa Kike Kwenye Label Yake

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Madee Ali almaarufu kama Raisi wa Manzese amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kumsaini msanii wa kike kwenye label yake.

Madee ni mmiliki wa label ya muziki inayojulikana kama  Manzese Music Baby (MMB)anayo Mpaka sasa ina wasanii wawili ambao ni Dogo Janja na Gaza.

Madee amefunguka hayo Kwenye Interview na Clouds Fm ambapo amedai sababu pekee ya kufikia uamuzi huoni kuogopa usumbufu unaoletwa na watoto wa kike.

Hapana, sipendi tu mambo hayo namwachia Daxo Chali, ndio anayaweza. Siwezi tu kukaa na watoto wa kike kwa sababu jinsia tofauti tutapishana maneno ataona nimemuonea”.

Kama utakumbuka producer wa muziki kutoka MJ Records Daxo Chali aliingia Kwenye skendo nzito baada ya wadada wawili aliokuwa anawasimamia Nini na Haitham kudai aliwataka kimapenzi na walipomkataa akawatimua.

 

Belle 9- Siuelewi Kabisa Muziki wa Madee

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva aliyetamba na kibao chake cha ‘Masogange’ Belle 9 amefunguka na kumrushia Dongo Zito msanii mwenzake Madee Ali Raisi wa Manzese.

Belle ameweka wazi kuwa Madee ni mmoja kati ya wasanii wa Bong fleva ambaye haelewi muziki wake anaoufanya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na  JJ wa Jembe FM, Belle 9 amesema kuwa kutokana anasikiliza wachanaji wengi wanaofanya vizuri anahisi kuna kitu anakikosa kutoka kwa Madee.

Honesty, let me be honesty, Madee huwa simuelewi. I don’t know, ujue kuna wasanii inafika kipindi unasikiliza unasema huyo mtu ana-release beat sio wimbo tena.

Labda kwa vile nasikiliza rappers ambao wanajua sana au kuna kitu nakitegemea kutoka kwake kutokana muda mrefu yupo kwenye game, kuna kitu nakimisi, so naona kama nikimsiliza na lose”.

Baada ya kimya cha muda mrefu Belle 9 amerudi kwa kasi ya ajabu ambapo kibao kipya cha ‘Dada‘ kimeendelea kufanya vizuri katika vituo mbali mbali vya habari Lakini pia hata mitandao ya kijamii kama Youtube ambapo umeshika nafasi za juu.

Mwanangu Akitaka Kuwa Mwanamuziki Ruksaa-Madee Ali

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika kundi la Tip Top Connection, Madee Ali amefunguka na kudai endapo binti yake atakuwa na ndoto ya kuwa msanii hawezi kukataa.

Madee Ali amesema atamruhusu binti yake huyo anayeitwa Aimal Hamad kuwa msanii kwa sababu yeye alivyokuwa mdogo alifuata nyayo  za Baba yake na kuingia kwenye sanaa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo5 hivi karibuni Madee alisema licha ya mara nyingi kuwa na wanae hata studio hajui iwapo atapenda muziki lakini yeye kama mzazi hawezi kumuwekea mipaka.

Tunashauriwa tuwaangalie watoto wafanye kile ambacho wanapenda kwa sababu anaweza kuwa anapenda mpira mimi nikamzuia nikamwambia afanye kitu kingine na asifanikiwe, nitakuwa nimepata lawama.

So akielekea huko mimi sina tatizo kwa sababu hata mimi mwenyewe nimemfuata baba yangu alikuwa ni mwanamuziki wa Western Tabora Jahazi Band wala hakutegemea nitakuwa mwanamuziki, so sitaona maajabu sana kwa sababu Waswahili wanasema maji hufuata mkondo”.

Kuna wasanii wengine wengi ambao wana maoni tofauti ambao wanaweza wazi kuwa hawataki watoto wao wake kuingia kwenye sanaa hapo baadae.

“Muziki Ndio Maisha Yangu Sina Mpango Wa Kustaafu”-Madee

Msanii mkongwe kutoka Tip Top Connection Madee Ali amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kustaafu kama habari zinavyodai kwa sababu mziki ndio maisha yake.

Kuna habari zilienea kitaa kuwa Madee anampango wa kustaafu kufanya mziki ndio maana anaelekeza nguvu zake zote kwenye kuwasimamia wasanii wake wawili Gaza na Dogo Janja walio kwenye uongozi wake wa ‘Manzese Music Baby’ (MMB).

Lakini Madee amekana taarifa hizo Kwenye Interview aliyofanya na Sam Misago na kuziita taarifa zakinafki na kusema hawezi kuacha mziki na wala hana mpango huo kwa kuwa mziki ni maisha yake:

Hapana watu wanatengeneza tu habari unajua siku hizi habari zimekuwa chache na zimekuwa biashara so hiko ni Kitu ambacho mimi sijawahi kukisema ndio kwanza nakisikia kwa watu na mimi mziki ndio maisha yangu, mimi baba yangu mpaka anazeeka anakaa chini bado anapiga gitaa kwa sababu anapenda mziki.

Mimi sina elimu yoyote ya kusema itaweza kuendesha maisha yangu zaidi ya music so nitaacha muziki ntakula nini? Yaani mziki ndio kila kitu mziki ndio kama na mziki ndio baba na mama yangu kwaiyo maisha yangu yote yanategemea mziki wangu kwaiyo siwezi kuacha mziki”.

 

Madee Amefungukia Tuhuma za Babu Tale Kuitelekeza Tip Top Baada ya Kuhamia WCB

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Madee Ali amefunguka na kutoa mtazamo wake juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikienea kwamba Babu Tale ameitelekeza Tip Top Connection na kuhamia WCB.

Tangu zamani Babu Tale alijulikana zaidi kwa kuwa meneja wa wasanii wa kundi la Tip Top Connection lililoundwa na wasanii kama Madee, Tundaman, Kassim Mganga, Keisha na wengineo.

Lakini baadae alianza kumsimamia staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na label nzima ya WCB na kuanzia hapo akaanza kutuhumiwa kwa kuitelekeza Tip Top baada ya kuona anapata mafanikio zaidi WCB.

Madee amefunguka juu ya hilo alipokuwa anafanya mahojiano na Sam Misago na kudai sio kweli hajawatekeleza kwani bado wanafanya naye kazi:

Babu Tale bado tunafanya naye kazi Tip Top Connection na bado anaangalia kila kinachotokea Tip Top na hapo hapo bado Babu Tale ni meneja wa WCB”.

Madee amekiri kuwa maneno maneno yanayosemwa mtaani hayana ukweli wowote watu wanazusha hayo kwa sababu wanataka kusikia kuwa wana ugomvi lakini hakuna bifu wala hakuna tatizo kazi inaendelea kama kawaida.

“Siwezi Kukurupuka na Kufunga Ndoa”- Madee

Msanii mkongwe wa mziki wa Bongo fleva Hamad Ali maarufu kama Madee Ali kutoka Tip Top connection amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kufunga ndoa kwa muda wowote kuanzia sasa.

Madee amefunguka na kusema hawezi kukurupuka na kufunga mkumbo wa kufunga ndoa kisa mastaa kibao wanafunga ndoa ila amesema anachotaka kufanya ni ndoa ya siri siri watu watashangaa tu ameshafunga ndoa.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Madee amefunguka haya:

Unajua suala la ndoa sio la kukurupuka tu unaenda kufunga. Ndoa ni kitu binafsi kabisa na maamuzi ambayo yanachukuliwa kwa mara moja halafu huwezi kuwa na maamuzi tena kwa hiyo mimi kama mimi kufunga ndoa ni mipango yangu na familia yangu ambayo siwezi kuiweka wazi lakini muda wowote naweza kufunga ndoa”.

Madee pia amefunguka kuwa ameamua kuwa makini na label yake inayojulikana kama Manzese Music Baby (MMB) ambayo anataka iweze kutanuka zaidi na kukua kwani ameshafanikiwa na wasanii wawili ambao ni Dogo Janja na Gaza.

Madee- Dogo Janja Aliandaliwa Kukabiliana na Changamoto za Ndoa

Mwanamuzi mkongwe wa Bongo fleva Madee Ali amefunguka kuhusiana na drama zinazoendelea mtandaoni hivi sasa kati ya Dogo Janja na mke wake Uwoya.

Madee ndiye alichukua nafasi ya kumlea Dogo Janja tangu akiwa mdogo alipoanza kuimba miaka michache iliyopita na hata baada ya kuoa juzi Madee nsiye aliyesimama kama baba wa Dogo kutokana na ukweli kuwa baba mzazi Wa Dogo Janja alifariki.

Baada ya sakata lililotokea weekend iliyopita la picha za kitandani zilizomuonyesha Irene Uwoya akiwa amelala kimahaba kabisa na mtangazaji wa East Africa Tv , Tbway 360 Madee amesema Dogo Janja alisahandaliwa kama mwanaune kukabiliana na matatizo kwenye ndoa yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Madee alifunguka yafuatayo kuhusiana na ishu hiyo:

Dogo Janja anaendelea vizuri kwenye ndoa yake tunashukuru Mungu ambacho tulijaribu kumuhusia ni kutohusisha ndoa yake na mambo ya muvi na muziki mkeo afanye muvi zake na wewe ufanye muziki wako kwa sababu wakianza kufata Maliki basi hiyo ndoa haitadumu kwasababu wote niwatu maarufu na pia wana marafiki ambao nao ni maarufu”.

Lakini pia Made ameweka wazi kuwa anafyrahushwa na jinsi amvavyo Dogo Janja anavyo handle matatizo na majaribu yanayowatokea kwenye Ndoa yao na tofauti na fikra za wengi na jinsi anavyoweka ndoa yao mbali kabisa na mitandao ya kijamii.

Madee Amefunguka Kuhusiana Na Kitu Kinachomkera Zaidi Kuhusiana na Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya

Msanii mkongwe wa Bongo fleva kutoka Manzese Madee Ali amefunguka kuhusiana na ndoa iliyozua gumzo na kufunga mwaka kati ya Dogo Janja na Irene Uwoya ambapo amedai hakuna kitu kinachomkera kuhusu ndoa hiyo kama wait kudhani au kuhisi ni kiki.

Madee ambaye anajulikana kama baba mlezi wa Dogo Janja tangu alipomchukua kutoka Arusha na kumleta Dar es Salaam kwa ajili ya kusimamia kazi zake muziki pia aliendelea kuwa na ukaribu naye pale Dogo Janja alipofiwa na Baba yake mzazi hivyo Madee alichukua jukumu la kumlea Dogo Janja.

Kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa, kupitia kipindi cha Friday Night live, Madee amesema kuwa kitendo cha watu kuhisi kuwa kila kitu ni kiki kitu kibaya sana kwani kuna uwezekano kuwa msanii anaweza akawa anahitaji msaada wa haraka na watu wakachukulia jambo hilo kama kiki;

Kitu ambacho nimekigundua na ni kibaya na kinaendelea kutokea ni watu kuamini katika kiki, hata Leo ikitokea mimi nimegongwa na gari na kuumia watu bado wataamini ni kiki na kushindwa kunisaidia. Kwaiyo kama hili suala lingekuwa la kumsaidia Dogo Janja ili aokike kwenye jambo fulani ambalo ni baya basi tungekuwa tumeshamuumiza kwa sababu watu wote wanaamini kwenye kiki  hadi sasa bado kuna watu hawaamini bado eti Dogo Janja kamuoa Uwoya haya mambo ya kiki tuyaache”.

Pia Madee alifunguka kuwa kitu ambacho watu wengi hawajui ni kuwa Dogo Janja alimficha sana juu ya uhusiano wake na Irene kiasi ya kwamba siku anamwambia kuwa anataka kumuoa alishtuka sana lakini pia amewahakikishia watukuwa ndoa ile niya kweli wala haikuwa na longo longo lolote.

Madee Ajibu Kashfa Za Dudubaya Kuhusu Muziki Wake

Ikumbukwe kwamba kipindi cha nyuma kidogo katika kipindi cha Friday Nite Live kinachorushwa na East Africa Television , msanii mkongwe wa muziki nchini  Dudu Baya aliongelea baadhi ya nyimbo za wasanii nchini , na katika nyimbo izo  alipata nafasi ya kuongelea wimbo mpya wa msanii Madee aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria Tekno unaojulikana kama ‘Sikila’ huku video ikiwa katika mfumo wa vikatuni(amination) wakimtumia Jackline Wolpre kama Video queen.

Dudubaya ambae alionekana kuipondea kidogo video iyo na kusema kwamba video ilikuwa mbaya, hata audio ilikuwa mbaya, jinsi alivyopangilia mashairi na jinsi alivyoyawakilisha pia ilikuwa ni vibaya na kumwambia kuwa hata muziki wenyewe ameiga kwa sababu wimbo ulikuwa na maadhi ya kinigeria na sio ya kitanzania, hivyo Dudu Baya alisema kuwa wimbo ule wa ‘Sikila’ haupo kama vile ambavyo yeye amemzoea made katika kufanya kazi zake.

Hivi karibuni Madee ametoa ngoma mpya aliomshirikisha mwanadada Nandy, na unafanya vizuri unaoitwa  ‘Sema’. Akijibu tuhuma hizo Madee alisema kuwa labda kwa kuwa yeye ni msanii mkubwa ndio maana maneno hayo yameweza kusikika sana katika mitandao”unajua labda kwa sababu Dudu Baya ni msanii mkubwa, lakini hayo ni maneneo yanayozungumzwa na kila mtu kwamba huwezi kutoa wimbo alafu watu wote wakausifia,au wakasema ndio au wote wakasema mbaya,lazima kuna watu wa ‘yes’ or ‘no’, kwaiyo Dudu Baya nae ni moja kati ya watu wa ‘no’ kwaiyo sio kitu kibaya,na pia ni ruksa kumpa mtu nafasi kusema maono yake hata mimi  ningeweza kusema nyimbo ya flani ni mbaya , kwaio kwangu ni kawaida tu, hivyo ndo vitu tunavyotamani kuvipokea kila siku ili tuwe wakubwa , changamoto zinapotufika ndio tunaongeza vitu zaidi’ alifunguka Madee

Madee aliendelea kusema kuwa yeye hajali sana pale watu wanapomuongelea maana hiyo ni moja kati ya vitu wanavyokumbana navyo wasanii” mimi napenda kuongelewa sana, ndo aana hata wewe umenitafuta baada ya kusikia nimeongelewa, hicho kwangu ni kitu kizuri” aliongezea. Imekuwa kama desturi kwa baadhi ya wasanii kusema nyimbo za wasanii wenzao, lakini kwa msanii kama Dudu Baya ambae ni msanii mkongwe yeye atakuwa ameona mengi.