Kajala Awapa Makavu Wanaofatilia Maisha Yake

Msanii wa filamu za Kibongo na balozi wa Biko nchini Kajala Masanja amewatolea povu watu wanaofatilia maisha yake baada ya kuhojiwa juu ya Safari zake za nje ya nchi za mara kwa mara.

Global Publishers wanaripoti kuwa marafiki wa Kajala wamekuwa wakihoji ni wapi Msanii huyo anapata pesa za kusafiri mara kwa mara kwenda Dubai ili hali uwezo wake wanaujua.

Kwa kweli tunashindwa kumuelewa mwenzetu hizi safari zake za kila mara Dubai, anapata wapi hii hela maana kama ni kazi za filamu tunajua sasa hivi soko lilivyo gumu. Kwa kweli mwenzetu sijui ni bwana mpya, sijui ana biashara gani inayomuingizia kipato”.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, alipohojiwa kuhusu tuhuma hizo Kajala aliweka wazi kuwa kinachompa jeuri ni ubalozi pamoja na kazi yake ya sanaa.

Wewe unajua mimi ni balozi, pia filamu sijaacha kuigiza iwe ni za watu au za kwangu, mtu anaanzaje kuhoji safari zangu za nje ya nchi?

Niwashauri wanaoibua hayo maswali kwangu wachape kazi, waache majungu“.

 

Kajala Akatazwa Kwenda Kwenye Kumbi Za Starehe

Msanii wa Bongo movie na mtangazaji Kajala Masanja ‘Kay’ ameweka wazi kuwa hivi sasa haonekana katika kumbi za starehe usiku wa manane kwa sababu yupo kwenye himaya ya mtu.

Kwa Miezi kadhaa sasa kumekuwa na tetesi nyingi kuwa Kajala yupo mbioni kufunga ndoa na mtu mmoja mwenye wadhfa wake ambaye anamuelewa kweli Kajala.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani hivi karibuni, Kajala alisema watu wengi wamekuwa wakimuuliza kwa nini haonekani kwenye kumbi mbalimbali za starehe lakini kikubwa ni kwamba anamheshimu sana mtu aliyenaye kwenye uhusiano kwa sasa na ndiyo maana ameamua kujituliza.

Unajua kuna kipindi mambo yanabadilika kabisa na unafanya vitu vingi kulingana na wakati uliokuwepo, mimi sasa hivi nipo na mtu ambaye hapendi kabisa vitu hivyo vya kutokatoka usiku lakini pia hata mimi mwenyewe nimebadilisha maisha yangu siyo yale tena”.

Kajala alikataa na kudai hamna ndoa inayofungwa hivi karibuni lakini alikiri yupo na mwanaume anayempenda na amedai huvi karibuni atamuweka wazi na kila mtu atamjua.

Wema Angeshindwa Kulipa Faini Ya Milioni 2 Ningemlipia Mimi- Kajala

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo msanii mwenzake Wema Sepetu angeshindwa kulipa faini ya milioni 2 basi angamlipia yeye.

Miaka ya nyuma Wema alishawahi kumtupia Kajala faini ya shilingi milioni 13 ambayo iliweza kumsaidia kutokwenda jela kwa miaka saba kutokana na kesi yake ya utapeli.

Lakini tangu miaka hiyo Wema na Kajala walikuja kugombana na kuwa maadui wakubwa na juzi ilikuwa zamu ya Wema ambaye alihukumiwa kwenda jela kwa mwaka mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni 2.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Kajala ambaye kwa sasa yupo nchini Dubai, alisema kuwa kama angetakiwa kusaidia kumlipia Wema faini hiyo asingekuwa na tatizo, angemlipia.

Ningejua na kuwa na hakika Wema hawezi kulipa hiyo faini, ningemlipia hata kama ni kwa kukopa hizo pesa, lakini mimi sikuwepo nchini wakati Wema anahukumiwa.

Lakini pia Kajala ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa zinazosambaa kuwa amemtelekeza rafiki yake Wema:

Jamani mimi naona watu wanasema sikuonekana mahakamani, lakini hawajui kama nipo au sipo, hata hivyo kama ingehitaji faini ambayo kubwa kwa kweli mimi nisingeshindwa hata ya kukopa ningemlipia.

Sio kwamba sikuwa napenda kwenda mahakamani kuungana naye, kulikuwa na vitu vinaendelea kwa upande wangu hivyo ikaniwia vigumu”.

 

Kajala Awatolea Povu Wanaohoji Umri Wa Mtoto Wake

Muigizaji  wa filamu za Bongo Movie Mrembo Kajala Masanja amewatolea povu zito watu wote ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhoji umri wa binti yake Paula.

Wiki iliyopita Kajala aliposti picha kadhaa Kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kusherekea birthday ya binti yake Paula lakini utata ulikuja baada ya mashabiki kuhoji umri wa mtoto huyo huku wengi wakikataa kuwa ana miaka 16.

Watu wengi walimjia juu Kajala wakimtuhumu kwa kumpunguzia umri binti yake na kudai anaonekana mkubwa kuliko miaka 16 na kudaiwa kupunguza miaka ya mtoto ili na yeye aonekane kama ana umri mdogo.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani hivi karibuni mara baada ya kumposti mwanaye huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumpongeza kufikisha miaka 16, Kajala alisema ameshangazwa na watu walioanza kumsema mwanaye kuwa ana zaidi ya miaka 16.

Mimi naona kubishana na watu wa Insta ni kujisumbua kwa sababu mtoto nimemzaa mwenyewe lakini wanaibuka watu wanajifanya wanajua umri wake kuliko mimi, basi waendelee kuamini ni mkubwa zaidi”.

 

Kajala- Sina Urafiki na Wema, Nina Marafiki Wapya

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amefunguka kuhusu urafiki wake na msanii mwenzake Wema Sepetu na kudai kwa sasa hawana urafiki tena.

Wema na Kajala walikuwa marafiki wakubwa sana mara baada ya Wema kumlipia Kajala shilingi milioni 13 katika kesi yake lakini urafiki huo ulivunjika baada ya Kajala kumsaliti Wema na kumuibia mwanaume wake.

Baada ya uadui wa miaka kadhaa mwaka jana Wema na Kajala walionekana kulimaliza bifu lao baada ya Wema kumtumia Kajala salamu za siku ya kuzaliwa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers  Kajala anaweka wazi kuwa hana urafiki na Wema na kusisitiza ana rafiki yake mwingine ambaye amemtaja:

Kuhusu suala la urafiki wangu na Wema yameshapita hayo na mimi kwa hivi sasa nina marafiki zangu wengine kabisa na rafiki yangu kipenzi ambaye anajua mambo yangu yote ni Lamata”.

Lakini pia Kajala alikataa Tetesi za kutaka Kuolewa na Kigogo hivi karibuni lakini amekiri ana mpango wa unalipa Kwenye mjumba wake wa kifahari.

Kajala- Sijavunja Ndoa Ya Pfunk

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Kajala Masanja amekana tetesi zinazodai kuwa yeye ndio kapelekea ndoa ya Baba wa mtoto wake Pfunk kuvunjika.

Kajala na Pfunk walikuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa miaka mingi na kuzaa mtoto mmoja lakini baadae walikuja kuachana.

Siku za hivi karibuni wamedaiwa kurudiana licha ya kwamba Pfunk tayari ana mke na mtoto na mwanamke mwingine.

Kajala amekana kabisa kurudiana na Pfunk licha ya ukaribu wao waliounyesha siku za hivi karibuni hadi kupelekea kuambiwa amevunja ndoa ya Pfunk na mama watoto wake Samiraa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Kajala amesema hajavunja ndoa ya watu Lakini pia hawezi kuacha kuwa karibu na Pfunk kwa sababu ni Baba wa mtoto wake na hayupo tayari kumtesa mtoto wake.

Mimi sijavunja ndoa ya P Funk, yule ni mzazi mwenzangu, nimeishi naye miaka tisa, nimezaa naye mtoto (Paula) ambaye sasa hivi yupo kidato cha nne na ana miaka 16, si kosa mimi kupiga picha na mzazi mwenzangu“.

 

 

Ndoa Ya Kajala Yadaiwa Kupamba Moto

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja ‘Kay’ amedaiwa kuwa mbioni kufunga ndoa hivi karibuni na kigogo mmoja wa serikalini.

Global Publishers wanaripoti kuwa Kajala yupo katika harakati za kufunga ndoa na Kigogo ambaye ana mpunga  mrefu ambapo inadaiwa Kajala kabadilisha kabisa mfumo wa maisha yake ili kujiandaa kuwa mke wa mtu.

Mtu wa karibu wa Kajala ametoa habari hizo kuhusu Msanii huyo na kuigungukia Global Publishers:

Kajala siku hizi kumuona ni shughuli kwa sababu muda si mrefu anaolewa na kigogo mmoja ambaye amembadilisha maisha yake. Ndiyo  maana siku hizi huwezi kumkuta akijichanganya hata kidogo kama ilivyokuwa huko nyuma.

Sasa hivi huyo kigogo anayemuoa anadai ndiye mtu anayeweza kuishi naye muda mrefu. Hata hivyo, ndoa yao hiyo bado imefanywa kuwa  siri“.

Baada ya Habari hiyo gazeti hilo lilimtafuta Kajala ili kujua ukweli wa mambo ambapo alikataa kuthibitisha au kukataa habari hizo:

Ndoa gani au unanichuria? Kwa nini mnapenda kusikiliza maneno ya waongeaji? Kama kuna mtu anataka kunioa si mtaniona ndani ya shela tu? Hilo ni jambo jema, kama lipo nitaliweka wazi siku si nyingi.

Kajala Athibitisha Kuvunjika Kwa Ndoa yake.

Msanii wa bongo movies Kajala Masanja amethibitisha kuvunjika kwa ndoa yake na mume wake  ambae walikuwa nae katika ndoa kwa miaka mingi lakini walikuja kutenganishwa na matatizo yaliyowafanya kusekwa jela wote wawili lakini yeye aliwahi kutoka baada ya kusaidiwa kupata ela ya kulipa mahakama baada ya Wema Sepetu kumsaidia.

Kajala amesema kuwa anaamini kuwa ndoa hiyo haipotena hasa baada ya mwanaume huyo kutoka gerezani na kushindwa kumtafuta ilijali yeye alikuwa akienda kumjulia hali gerezani kila siku lakini cha kushangaza tangu mwanaume huyo ametoka hajataka kumtafuta kajala wala familia yake kwa ujumla.

Kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita kajala  na mume wake walipata kesi ya kuiba ela za ofisini na kusekwa gerezani baada ya kukutwa na hatia lakini walikosa ela kwa ajili ya kulipa, lakini baada ya marafiki zanke wa bongo movies akiwepo Wema Sepetu walimsaidia na kuweza kutoka gerezani na kumuacha huko mume wake.

Hata hivyo Kajala anasema kuwa hata baada ya mumewe huyo alikuwa amefunganane ndoa alipotoka gerzani alishindwa kumtafuta wala kutaka kujua kuhusu familia yake aliyoiacha.

Kajala Na Zari Wasemekana Kuwa Na Siri Nzito

Ikiwa ni kama wiki imeshapita tangu kufanyika kwa harusi ya  Rommy Jons ambae ni Dj  wa msanii maarufu na mkubwa Tanzania Diamond Platinumz  ambae pia ni ndugu yake ambae wamekuwa wakifanya kazi pamoja , siri imevuja kuwa katika watu waliohudhuria akiwemo Kajala na mzazi mwenzie na Diamond anaejulikana kama Zari The Bossy wamekuwa wakikwepana na hilo lilionekana live siku ya harusi.

Wanawake hao ambao kila mmoja amekuwa nguli katika mitandao kwa nafasi yake na warembo wamesemekana kukwepana hasa Kajala ambae aliamua hadi kutoka kabisa katika sherehe hiyo  baada ya kuona kuwa kitendo cha yeye kwenda mbele kingemkutanisha kwa karibu na Zari The Bossy.

Katika harusi hiyo kuna wakati ambapo Mc aliwahitaji baadhi ya watu mbele kwa ajili ya ufunguzi wa champaign  mabapo kati ya watu hao walitajwa ni pamoja na Zari na baadae alimuita kajala ili aweze kujumuika pale mbele kwa ajili ya kufungua shampeni lakini kitu cha ajabu na ambacho si cha kutegemea Kajala aliamka na kupitia mlango wa nyuma na kutokomea kusiko julikana ilhali sherehe ikiwa bado haijaisha na kuwaacha watu wakisubiri kutokea kwake.

Hata hivyo baada ya kajal kutafutwa ili kuweza kuthibitisha hilo alikubali kuwa ni kweli aliamua kuondoka kwa sababu alikuwa hataki kuonana na baadhi ya watu, swali linakuja kwanini alikwenda kwenye harusi ilihali alijua hataki kuonana na baadhi ya watu na akiuja kabisa ni harusi ilipaswa kuhudhuriwa na watu maarufu, lakini pia kwanini iwe katika kipindi cha ufunguzi wa shampeni tena baada ya kuitwa mbele yeye na Zari.

ni kweli nilikwenda kwenye hiyo harusi  na nikaitwa mbele lakini niliamua tu kuondoka zangu kwa sabau sikutaka  kuonana na baadhi ya watu  .-Alifunguka Kajala.

Wawili hao hawajawahi kusikika kuwa wamegombana hata siku moja hivyo kama ni maadui basi kuna kinachoendelea kati yao ambacho hakijawahi kuweka wazi na watu hao wawili  na kuamua kufanya siri kwa maslahi yao binafsi.

Kajala Kuamua Kuongeza Mdogo Wake Paula

Msanii wa filamu na mrembo anaefanya vizuri zaidi katika filamu lakini ambae kwa sasa ni moja ya mabalozi wa mchezo wa bahati nasibu Tanzania Biko,Kajala Masanja amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuzaa tena bali ataamua kuongeza mtoto wa pili kwa kausili mtoto huyo.

Akiongea na waandishi wa habari Kajala amesema kuwa alikuwa ameshatamani kuwa na mtoto wa pili kwa siku nyingi na anaona kabisa kwa sasa ni muda muafaka wa kuasili mtoto huyo kwa sababu pia mtoto wake wa kwanza amshakuwa mkubwa.

Hata hivyo Kajala anasema kuwa kwa umri aliofikia mtoto wake itakuwa si jambo  zuri kubebea mimba kwa sasa ndio maana anaona ni kheri kwenda katika kituo cha watoto yatima kuchukua mtoto mmoja wa kulea ambae atakuwa mdogo wake paula.

Nilikuwa na wazo ilo la kuongeza mtoto muda mrefu sana,lakini kwa sasa naona ndio muda muafaka umefika kabisa.Mimi mwenyewe naona wazi kabisa siwezi kuzaa tena kwaiyo naona ni bora nichukue mtoto tu kwenye kituo cha kulelea watoto nimlee mpaka atakapo kuwa mkubwa.-Alifunguka Kajala Masanja

Kajala alibahatika kupata mtoto  wake wa kwanza wa kike  kwa takribani  zaidi ya miaka 15 iliyopita anaejulikana kwa jina la Paula ,mtoto ambae alizaa na mzazi mwenzie anaejulikana kama P-funk majani ambae pia yuko katika industry ya muziki.Lakini kutokana na mambo kutokuwa sawa wawili hao  waliachana  na kajala kufanikiwa kubaki na mtoto,hata hivyo Kajala alibahatika tena  kuolewa na mwanaume mwingine ambae pia alipata kesi na kuswekwa ndani hivyo ikawa ndio kama mwisho ya ndoa hiyo.

Siku chache zilizopia kajala alisema  kuwa hatoweza kuolewa tena lakini alishaweka lengo la kuongeza mdogo wake paula ili kutimiza watoto wawili  na  hivi karibuni ameonyesha tena nia yake kuwa ni ya dhati kuhusu  swala la kuchukua mtoto katika kituo cha kulelea watoto ambapo pia ni jambo zuri kwa sababu atakuwa anasaidia  wale watoto  wenye huitaji wa malezi bora.

 

Kajala Akanusha Kutumika Vibaya Na Wasanii

Kajala Masanja msanii wa Bongo Movie  pia ni balozi wa mchezo wa bahati nasibu wa Biko unaoendelea sasahivi kote nchi ambae hivi karibuni amekuwa akituhumiwa na tetesi nyingi ikiwepo wa kutoka na wapenzi wa wasanii wenzie , huku wengine wakimwita “nyakunyaku” , amefunguka tena na kuongelea swala ya yeye kutuhumiwa kutembea na wasanii wa Bongo fleva ambao wanamtumia vibaya  kwa ajili ya kutafuta  kiki ya kutaka kujulikana na kupata majina katika kazi zao kupitia yeye.

Katika mahojiano yake na Channel ya EATV katika kipindi cha eNews,alisema kuwa sio kwamba anatumika na wasanii bali kuna baadhi ya wasanii ni watu wake wa karibu.

Kajala  alipoulizwa kuhusu msanii Peter mc ambae aliimba wimbo na kutaja jina  la Kajala na kusema baadhi ya maneno yanaonyesha kama wapo kwenye mahusiano.  Hata hivyo Kajala alipoulizwa kuhusu msanii huyo alishangazwa kuwepo kwa nyimbo iyo  bila yeye kuijua au hata watu wake wa karibu kumwambia kuhusu  msanii huyo na wimbo wake, kwa kifupi anasema hamjui msanii wala wimbo.Kwa kuongezea Kajala alisema kuwa endapo atausikia wimbo huo atafatilia na kuongelea swala ilo.

Hata hivyo kulikuwa na tetesi za Kajala kutembea na msanii mwingine wa Bongo Fleva , Country Boy  ambapo kwa kipindi cha nyuma  msanii huyo  wa Bongo Fleva alipoulizwa kuhusu habari hizo alisema kuwa yeye na kajala ni kama mama na mtoto, kwa kulifafanua swala ilo Kajala amesema kuwa watu wanakuwa wanaongea vitu bila kujua , yeye na Counrty Boy ni kaka mama na mtoto kwa sababu alishawahi kumsaidia katika maswala yake ya muziki na uhusiano wao umebaki kuwa hivyo “Country mimi ni mtoto wangu, na huwa haniiti Kajala, ananiita mama , kitu watu hawajui ni kwamba wimbo wa kwanza kabisa wa Counrty  mimi ndio nilimpeleka kwa Lamar nikamlipia na akafanya‘ ameongea Kajala

Kajala anaonekana  kukerwa na tabia za watu kuzusha mambo , kila unaetembea nae barabarani basi ni mtu wako” watu tutashindwa kutembea na ndugu zetu , watu wanakwambia unatoka nae, basi utatembea na kila mtu humu duniani” anaongezea kajala

kajala Akanusha Tuhuma Za Kutembea Na Wanaume Za Watu

Kwa muda sasa kumekuwa na tetesi zinazomuandama msanii wa Bongo Movies Kajala Masanja , msanii mrembo mwenye mtoto mmoja wa kike na mwenye kipaji kizuri katika tasnia hiyo kuwa amekuwa akitembea na wanaume za watu na kuwapokonya marafiki zake wanaume.Kajala ameonyesha kukerwa na tuhuma hizo ambazo watu wamekuwa wakimtuhumu  na kusema kuwa ni uongo mtupu na hana tabia hiyo kabisa.Kajala anasema kuwa tuhuma hizo zinamuaribia katika kazi zake na maisha yake kwa ujumla,kwa sababu baadhi ya kiki watu wanazomtafutia hata yeye mwenyewe hazikubali.

Katika mahojianao yake na Ijumaa, msanii Kajala  amesema kuwa kwa wasanii wengine wa kike ni kawaida kutafuta kiki kupitia kufanya tabia za kuiba wanaume wa watu, lakini kwake anasema hazitaki kabisa kwa sababu ni mbaya na zinaharibu kazi zake.”kiki kama hizo sizitaki kabisa kuzisikia kwanza zinaniharibia hata hazijengi chochote  kwenye jamii yangu zaidi ya kuniletea picha tofauti  kwenye jamii yangu” anasema Kajala.

Hata hivyo Kajala  amekuwa akituhumiwa na tetesi za kutembea na wanaume za watu hata wale wa rafiki zake, miaka ya nyuma alituhumiwa kwa kutembea na bwana wa rafiki yake Wema Sepetu aliyejulikana kwa jina la Clemence aliyemsaidia  mpaka kutoka jela katika kesi iliyokuwa inamkabili, Kajala na Wema Sepetu walikuwa marafiki  wakubwa na walikuwa wakisaidiana katika shida mbalimbali lakini urafiki wao ulikuja kukoma bada ya kajal kutuhumiwa kutembea na mwanaume wa wema.hibvi karibuni tena kajala alikuwa katika tuhuma nyingine nzito ingawa hazikuwa na uthibitisho kuwa alikuwa anatoka na msanii Harmonize, msanii aliyekuwa mpezni wa Jackline Wolper ambae pia alikuwa rafiki wa karibu wa kajala.

Kajala ni mama wa mtoto mmoja wa kike  anaeitwa Paula ,aliezaa na mume wake wa kwanza P-Funk Majani  kabla ya kuolewa kwa mara ya pili na mwanaume mwingine ambae aliingia katika matatizo nae na kufanya waachane.Kwa sasa Kajala ni mmoja wa mabalozi wa mchezo wa bahati nasibu unaendelea kuchezwa nchi unaojulikana kwa jina la Biko.

Wema Sepetu awatemea mate waliokuwa mashoga zake wa damu

Muna Alphonse ‘Muna’, Kajala Masanja na Wema Sepetu walikua marafiki wa dhati lakini warembo hawa walikosana na kila mmoja kuenda zake.

Wema amesisitiza kuwa hajawahi kuwakumbuka waliokuwa mashoga wake wa damu, hii ni baada ya madai kuwa staa huyo wa filamu za Bongo anawamiss rafiki wake.

Muna Alphonse

Akiongea na Star Mix, Wema alieleza kuwa hajawahi kuwakumbuka rafiki zake hao ambao huko nyuma walikuwa kama kumbikumbi.

“Sitaki kusema dhambi jamani sijawahi kuwamisi hawa watu (Muna na Kajala) kabisa naona kama niliwafuta kwenye kichwa changu maana najikuta kuna watu nawakumbuka lakini hao hapana,” alisema Wema.

Kajala Masanja

Staa wa filamu ya Bongo Kajala Masanja afunguka kuhusu yeye kutumia bangi

Utumiaji wa bangi umepigwa marufuku Tanzania, hata hivyo bado kuna baadhi ya watu mashuhuru ambao wanatumia ama wamewai tumia bangi.

Wema Sepetu ako na kesi kotoni ambayo anashtakiwa kwa kosa la kukutwa na bangi. Mrembo huyo alikamatwa na kuwekwa korokoroni kwa siku sita baada ya polisi kumshika na bangi Februari mwaka huu.

Sasa nyota mwingine wa Bongo movies pia amefunguka kuhusu utumiaji wa Bangi, Kajala Masanja alisema aliwai tumia bangi miaka kadhaa zilizopita.

Katika mahojiano na Bongo Movies, Masanja alieleza kuwa alijikuta mikononi mwa marafiki waovu waliojihusisha na utumiaji wa bangi na kusababisha yeye pia kutumia bangi.

“Unajua inafika mahali sisi kama vioo vya jamii inatupasa kuzungumza ukweli wa maisha yetu husasan ya nyuma, ili kama ni watu kujifunza iwe hivyo, binafsi nimewahi kupitia maisha ambayo naweza kuyaita ya mpito, kipindi ambacho kila mtu hupitia katika harakati za ukuaji, kwamba nilijiingiza kwenye kampani za marafiki ambao ni watumiaji wa bangi.

“Hivyo, walinishawishi na kujikuta nikijiingiza kwenye ulevi huo, kidogo nipotee ila namshukuru sana Mungu kwani sikuwahi kuvuta madawa mengine kama cocaine, heroine sijui kujidunga masindano na mambo mengine ya kufanana na hayo, lakini ukweli kabisa huwa najuta sana kwa kuvuta bangi,” alisema Kajala Masanja.