Dogo Janja Akiri Ndoa Yake Imeupendezesha Muziki Wake Zaidi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Dogo Janja amefunguka na kudai ndoa yake na staa wa Bongo movie IreneUwoya imezidi kupendezesha muziki wake anaofanya sasahivi.

Dogo Janja anafanya vizuri hivi sasa na wimbo wake mpya unaoitwa ‘Banana’ ambao umezidi kushika chati nyingi za juu Kwenye redio stesheni mbali mbali Lakini pia unashika namba moja YouTube.

Dogo Janja aliyefunga ndoa na Uwoya mapema mwaka jana amedai ndoa yake ndio imempa mzuka wa kuwa anafanya muziki mzuri zaidi kuanzia ngoma yake ya ‘Wayu wayu’ mpaka ‘Banana’.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Dogo Janja amefunguka haya kuhusu ngoma yake mpya na mchango wa ndoa yake:

 Kikubwa nimebadilika, naimba staili tofauti kabisa zikiwa na mchanganyiko wa ragga f’lan na hata kwenye ngoma yangu hii ya Banana utaona utofauti.

Kwa upande wangu ndoa imefanya muziki wangu kuwa muruaa, nina ndoa na muziki kama kawa ngoma zinatiririka tu”.

 

Dogo Janja Atangaza Nia Ya Kuoa Mke Wa Pili

Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa ana mpango wa kuongeza mke wa pili baada ya kumuoa star wa Bongo movie Irene Uwoya mwaka jana.

Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja ilikuwa moja ya stori zilizoongelewa sana mwaka jana ambapo ilikuwa ngumu kwa watu wengi kuamini kuwa Irene Uwoya anaweza kuolewa na kijana mdogo kama Dogo Janja hasa ukizingatia tofauti zilizopo baina yao.

Dogo Janja amefunguka kuhusu mipango yake ya kuongeza mke wa pili Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm Kupitia kipindi cha The Playlist ambapo alimsanua Lil’Ommy kuhusiana na mipango yake.

Dogo Janja alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa yeye kuoa mke wa pili kwa sababu ni Sunnah kwa yeye Muislam kwani alipata baraka sana baada ya akufanikiwa kumuoa Uwoya ambaye alimbadilisha dini kutoka kwenye Uislam mpaka ukristo.

Inshalllah kuongeza wa pili wa tatu wa nne, hapo ukishakaa vizuri kiuchumi na mwenzako aweze kuridhia, hata kuoa wake wanne sio mbaya hapa tunaongelea Mwenyezi Mungu akitujalia uhai labda baada ya miaka kumi naweza kuongeza wa pili ikipita miaka kumi tena naongeza yaani mpaka nikifika miaka hamsini nakuwa nimekamilisha wake nne”.

 

Dogo Janja- Nitaua Mtu Kwa Ajili Mke Wangu Uwoya

Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja ametoa bonge la mkwara kwa watu wote wanataka kuingilia penzi lake na mke wake muigizaji maarufu wa Bongo movie Irene Uwoya.

Tangu Dogo Janja na Irene Uwoya wamefunga ndoa mwaka jana mwishoni bado imekuwa ngumu kwa watu kuwazoea kama wapo pamoja kwani ni jana tu ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa Dogo Janja kurusha picha mtandaoni wakiwa pamoja.

Lakini kumekuwa na maneno mengi ambayo yamekuwa yakiongelewa juu ya ndoa hiyo hasa kwa familia ya Uwoya ambapo Mama yake mzazi ameshaweka wazi kuwa hamtambui Dogo Janja kama ni mume wa mwanaye.

Lakini pia wasanii wengine na mashabiki wamekuwa wakiwapa wakati mgumu kuhusiana na Mahusiano yao ni siku chache zilizopita tu kuna msanii alimrushia dongo Dogo Janja kwa kudai kuwa ameolewa na Irene Uwoya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dogo Janja ametangaza vita na kudai yupo tayari kumwaga damu kwa mtu yoyote atakayejaribu kuingilia penzi lake na mkewe Uwoya:

Ni bora umwage damu mbele ya adui kuliko kumwaga chozi, My beautiful wife, Atadondoka mtu, mazoea na mke wangu sitaki”.

Baada ya Dogo Janja kuposti picha hiyo, Irene Uwoya alienda aka comment “ Una mkwara Baba….ila usiua utaenda jela”.

 

Irene Uwoya na Dogo Janja Waanika Ratiba ya Chumbani Mtandaoni

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya pamoja na mume wake Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja wameachana za watu wengi baada ya kuweka mambo yao binafsi ya chumbani kwenye mtandao.

Tukio hilo lilitokea siku ya jana baada ya Dogo Janja kuposti kipande cha karatasi kilikuwa kimeandikwa na kusainiwa na Irene Uwoya huku kikimuelekeza Dogo Janja siku atapewa na siku gani hapewi.

Of course hawakuandika wanapeana nini lakini mara moja kila mtu alianza kudhani kupeana mambo ya chumbani maana ujumbe ulianza na maneno “ Ratiba ya kukupa Mume wangu”. na kisha kaweka siku zote kuanzia jumatatu mpaka jumapili na kamwambia siku anazompa na siku ambazo hatompa.

 

Dogo Janja na Uwoya wametoka mbali sana tangu wafunge ndoa yao ya siri mwkaa jana ndoa iliyokuwa ndoa ya mwaka maana walitengeneza headlines vibaya mno maana hakuna aliyetegemea Dogo Janja angeweza kumpata Uwoya.

Madee Amefunguka Kuhusiana Na Kitu Kinachomkera Zaidi Kuhusiana na Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya

Msanii mkongwe wa Bongo fleva kutoka Manzese Madee Ali amefunguka kuhusiana na ndoa iliyozua gumzo na kufunga mwaka kati ya Dogo Janja na Irene Uwoya ambapo amedai hakuna kitu kinachomkera kuhusu ndoa hiyo kama wait kudhani au kuhisi ni kiki.

Madee ambaye anajulikana kama baba mlezi wa Dogo Janja tangu alipomchukua kutoka Arusha na kumleta Dar es Salaam kwa ajili ya kusimamia kazi zake muziki pia aliendelea kuwa na ukaribu naye pale Dogo Janja alipofiwa na Baba yake mzazi hivyo Madee alichukua jukumu la kumlea Dogo Janja.

Kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa, kupitia kipindi cha Friday Night live, Madee amesema kuwa kitendo cha watu kuhisi kuwa kila kitu ni kiki kitu kibaya sana kwani kuna uwezekano kuwa msanii anaweza akawa anahitaji msaada wa haraka na watu wakachukulia jambo hilo kama kiki;

Kitu ambacho nimekigundua na ni kibaya na kinaendelea kutokea ni watu kuamini katika kiki, hata Leo ikitokea mimi nimegongwa na gari na kuumia watu bado wataamini ni kiki na kushindwa kunisaidia. Kwaiyo kama hili suala lingekuwa la kumsaidia Dogo Janja ili aokike kwenye jambo fulani ambalo ni baya basi tungekuwa tumeshamuumiza kwa sababu watu wote wanaamini kwenye kiki  hadi sasa bado kuna watu hawaamini bado eti Dogo Janja kamuoa Uwoya haya mambo ya kiki tuyaache”.

Pia Madee alifunguka kuwa kitu ambacho watu wengi hawajui ni kuwa Dogo Janja alimficha sana juu ya uhusiano wake na Irene kiasi ya kwamba siku anamwambia kuwa anataka kumuoa alishtuka sana lakini pia amewahakikishia watukuwa ndoa ile niya kweli wala haikuwa na longo longo lolote.

Dogo Janja: Nilisota Sana Mpaka Kumpata Uwoya, Haikuwa Kazi Rahisi

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka mambo mazito siri juu ya uhusiano wake  mkewe mpya Irene au Sheila Uwoya.

Wiki hii nzima Dogo Janja na Uwoya wameshika vichwa vya habari kwa wingi baada ya kufunga ndoa wiki iloyopita siku ya Ijumaa, huku wengi wakikataa kuamini kuwa mtoto mdogo kama  Dogo Janja anaweza kumpata mtoto mzuri kama Uwoya, leo kwenye mahojiano aliyofanya na clouds Fm katika kipindi cha Leo tena Dogo Janja amefunguka yafuatayo kuhusiana na mkewe Uwoya na ndoa yao kwa ujumla:

Kwanza kabisa hakuna kitu kinanisikitisha kama watu kuifananisha ndoa yangu na mimi kutafuta kiki na ndio maana tulifanya haya mambo kwa siri kubwa, kwa sababu sikutaka haya mambo yawe hivi kwani na mimi inaniumiza sana ninachotaka watu wajue kuwa nimeoa kweli , alafu isitoshe familia yangu imetoa baraka zote kwasababu kwanza kabisa nilishawahi kumpeleka Uwoya  nyumbani na kusema ukweli mama alimfurahia sana na walicheka sana na nikamwambia mama basi mi nampenda sana huyu mwanamke na ntamuoa ili uendelee kufurahi zaidi kwaiyo nina baraka zote za mama yangu”.

Pia Dogo Janja amefunguka zaidi kuhusu uhusiano wake;

Unajua watu wengi wanaona kama mimi sistahili kuwa na Irene labda kutokana ni watu wawili tofauti lakini mimi Irene nimeanza kumpenda tangu zamani yaani nilikuwa nikimuangalia navutiwa naye yaani nimeamini kuwa ndoto huja kutokea kweli kitu kikubwa ni kuthubutu na kuvaa ujasiri yaani mpaka nampata Irene nimesota sana yaani haikuwa kazi rahisi mara ya kwanza alikuwa hataki hata kuniona lakini kutokana na nilimpenda nilivumilia mpaka leo hii tumefunga ndoa”.

Dogo Janja amesema ndoto yake siku moja wawili hao wawe na familia kwani anaamini Uwoya atakuja kuwa mama bora kwa familia yao.

Irene Uwoya: Nimeolewa na Mwanaume Wa Ndoto Zangu, Nakupenda Dogo Janja

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya hatimaye amefunguka asubuhi hii na kukiri kuwa ameolewa na mwanamuziki wa Bongo fleva, Dogo Janja.

Tangu ijumaa ndoa hiyo ifungwe kumekuwa na utata wa nani ni mume wa Uwoya huku wengi wakiwa hawataki kuamini kuwa mwanamke mrembo kama Uwoya anaweza kuolewa na kijana mdogo kama Dogo licha tu ya utofauti katika umri pia ni kipato.

Leo hii kama dakika ishirini zilizopita kupitia ukurasa wake wa Instagram, Irene Uwoya amemweka wazi mume wake aliyemuoa siku mbili zilizopita ambapo ameandika maneno yafuatayo:

I married the man of my dreams @dogojanja I am still crying happy tears I love you and I am excited to spend the rest of my life with you”.

Kwenye ujumbe huo wa hadhara Uwoya kamfungukia mumewe Dogo Janja kuwa anashukuru amepata mume wa ndoto zake mwanaume aliyekuwa anamuota kila siku na mpaka sahivi akimfikiria bado anatokwa na machozi ya furaha na pia ana hamu kubwa ya kuona maisha yao pamoja yatakavyokuwa pia watakavyoishi pamoja milele mpaka pale kifo kitakavyo watenganisha.

Uwoya amemweka wazi mumewe baada ya watu kuanza kuzusha kuwa ameolewa na kigogo ambaye ana mke na watoto, lakini mpaka sasa bado hajaweka wazi picha zao hizo za harusi zinazowaonyesha wakiwa kwa pamoja.

Tetesi za Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja Zazidi Kushangaza Wengi

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya, amezidi kushika vichwa vya habari mwishoni mwa wiki hii baada ya habari kuenea kwa kasi kuwa anaolewa na mwanamuziki wa bongo fleva Dogo Janja.

Tetesi za Uwoya na Dogo Janja zimekuwa zikisambaa kwa muda sasa huku kila mmoja akikataa kuwa na uhusiano na mwenzie. Siku ya Ijumaa oktoba 28 taarifa zilienea kuwa Uwoya anaolewa lakini bwana harusi hakuwekwa wazi kuwa ni nani na inasemekana kuwa ndoa hiyo ilifanyika kwa siri kubwa sana kwani habari za chini chini zinadai wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hiyo hawakuruhusiwa hata kupiga picha na wengine walilazimishwa kufuta picha hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya aliweka wazi kuwa amebadilisha dini na kuwa muislamu na kubadili jina na kuitwa Sheila. Uwoya aliweka picha zake za harusi lakini picha za bwana harusi hazikuonekana.

Habari za Dogo Janja na Uwoya kufunga ndoa ziliwashangaza wengi kutokana na tofauti kubwa ya kiumri iliyopo baina yao. Siku ya jumamosi mastaa mbali mbali ambao ni marafiki wa Dogo Janja na Uwoya waliwapongeza wawili hao kwa kufunga ndoa, mastaa hao ni kama vile Zamaradi, Madee,Shetta na wengineo.

Picha zilisambaa pia zikimuonyesha Dogo Janja akiwa amevaa khanzu huku wengi wakidai kuwa ametoka kuoa.

Baadhi ya habari pia iliyosambaa ni kuwa Uwoya ameolewa na kigogo ambaye hataki ajulikane hivyo kamtumia Dogo Janja kama kuuwa soo jambo ambalo binafsi sidhani kuwa ni kweli kwani ukiangalia kwenye sehemu zote ambazo Uwoya amepongezwa kwa kuolewa na Dogo Janja hakuna hata sehemu moja aliyokataa kuwa mumewe siyo Dogo Janja.

Kama kweli Uwoya atakuwa ameolewa na Dogo Janja basi atakuwa amedhihirisha ule usemi usemao kuwa umri si kitu chochote mbele ya mapenzi kuwa mapenzi hayachagui. Pia ifahamike kuwa sababu kubwa ya Irene kubadilisha dini na kuwa muislamu ni kwa sababu kisheria na kidini ni mke wa mtu kwani ameolewa ndoa ya kanisani na mumewe wa zamani na baba wa mtoto wake Kataut Ndikumana hivyo asingeruhusiwa kuolewa tena kanisani hicvyo akafikia uamuzi wa kubadili dini.

Je nini maoni yako unadhani Uwoya na Dogo Janja wameoana tafadhali tiririrka maoni yako hapo chini.