Hemed PHD Adaiwa Kuwa Kicheche Bongo Movie

Msaniii wa filamu za Bongo movie na msanii wa Bongo fleva, Hemed Suleiman ‘PHD’ amejikuta ndani ya skendo nzito ambapo wasanii wenzake wamemnyooshea kidole kwa kuwa hajatulia na kuwa kiwembe.

Global Publishers wanaripoti kuwa wasanii wengi wa Bongo nmovie wamekuwa wakilalamika kuwa msanii huyo hajatulia kwani amekuwa akitembea na wengi wao kisha kuishia kuwatosa na hata kumtuhumu kwa kuringa na kujisikia.

Unajua wadada wengi wa Bongo Muvi, hasa mastaa wanampenda sana Hemed, lakini mara nyingi yeye anakuwa hana muda nao kabisa hivyo akiona wanamsumbua, anachofanya ni kutembea na staa kisha anambwaga wala hana muda wa kuendelea naye tena kwa sababu ana mwanamke ambaye amezaa naye na wanaishi wote,” kilisema moja ya vyanzo hivyo na kuongeza: “Sasa unaambiwa kuna mastaa ukiwatajia jina la Hemed hawana hamu naye kwa sababu walishatendwa na kuachwa solemba”.

Baada ya madai gazeti hilo lilimsaka Hemed ambaye baada ya kusomewa mashtaka yake hakusita kabisa kuanika ukweli wote;

Mimi sijawahi kumtaka mtu Bongo Muvi labda wenyewe ndiyo wananitaka, lakini siyo mimi ninawatokea wanakuja wenyewe na Mimi kazi yangu ninabutua, nasepa zangu halafu mimi sina mpango wa kutoka na staa wa Bongo Muvi”.

Lkaini pia msanii huyo ameweka wazi kuwa yupo kwenye mahusiano na mwanamke mwingine ambaye hana ustaa bali ni mwanamke anayejiheshimu tofauti na wasanii wengi.

 

Gelly Wa Ryhmes: Nilimgonga Demu Wa Hemedy PHD

Mwanamuziki wa Bongo fleva Gelly wa Ryhmes ametoa siri ambayo ilikuwepo kati yake na rafiki yake na mshkaji wake msanii wa Bongo fleva na Bongo movie Hemedy PHD ambaye amekiri kumchukulia demu wake.

Gelly wa Ryhmes alifunguka hayo alipokuwa anafanya mahojiano na LilOmmy ambapo alifunguka kuhusu historia ya urafiki wao na vikwazo ambavyo wamepitia kwa kutegemea wote wawili ni mastaa.

Hemedy PHD na Gelly wa Ryhmes

Gelly alifunguka yafuatayo kuhusiana na urafiki wake na Hemedy kwenye kipindi cha The Playlist;

Mimi na Hemedy tumekuwa wote Tanga shule tulizokuwa tunasoma zilikuwa karibu kwaiyo tulikuwa washkaji ambao tulikuwa tunaonana onana tu kwa juu juu lakini kila mtu alikuwa ana mishe zake lakini kilichofanya mpaka tukawa marafiki sana ni mwaka 2009 au 2008 nakumbuka ilikuwa shoo ya Ali Kiba iliyofanyika Zanzibar tulikutana kwenye boti njiani yaani from nowhere tukajikuta tunapiga stori alafu tumeendana wote tunafanya mziki basi tukawa washkaji kupitiliza mpaka sahivi tumeshavuka steji ya urafiki sahivi ni kama ndugu na ninavyokwambia tumepitia misala kibao tumekula goodtimes nyingi tumeshagombana sana always sisi hazipiti wiki mbili hatujazinguana lakini uzuri wetu mimi na Hemedy kati yetu hakunaga unafki mwenzako akikosea unamchana live”.

Lakini pia Gelly pia amefunguka kuhusu tetesi zinazosambaa kuwa yeye na Hemedy wanatabia ya kubadilishana mademu na hata kuna msala ulitokea kuwa Gelly alitembea na msichana wa Hemedy;

Stori yenyewe ilikuwa kwa kipindi kile nilikuwa sijatulia na demu wangu ambaye niko naye sahivi kwa kipindi kile kutokana na mambo ya ujana tu, lakini nakumbuka nilikuwa na msichana wangu nilikuwa namuelewa sana ile tunaanza mapenzi nikasikia Hemedy kamgonga nikimuuliza anakataa aisee ilikuwa bonge la ugomvi hadi Instagram huko watu walijua mwaka mzima hatukuongea kwaiyo na mimi nilichofanya ile tumekaribia kupata tu na mimi nikamgongea demu wake”.