Godzillah Afunguka Mapenzi Yake kwa Halima Mdee.

Msani wa muziki wa hipo-hop nchini Godzillah amefunguka na kuelezea mahusiano yake na mwanasiasa anaefanya vizuri kutoka chadema Halima Mdee ambae amekuwa akimu-insipire sana katika kazi zake za sanaa na hata kumsifia kila anapotoa wimbo hasa huu wimbo wake mpya wa stay.

Godzillah alipoulizwa kuhusu maoni ya halima katika muziki wake alijibu “kazi nzuri ya sanaa hugusa nafsi ya kila mtu” akimaanisha kuwa kutokana na uzuri wa kazi zake na ndio maana hata mbunge huyo amekuwa akimsifia kwa sababu anajua kile anachofanya katika muziki wake.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu kuchekewa kutoka kwa video yake ya wimbo wa Stay, Godzillah anasema kuwa  wimbo huo una maudhui yanayoishi na ndio maana hata hakuwa na wasiwasi wa audio yake kuchoka na ndio maana anaamini kuwa hata kama video imechelewa lakini bado video inaweza kufanya vizuri.

Ninaweza Kuoa Kimyakimya kama Alikiba;-Godzillah

Msanii wa muziki Godzillaha mefunguka na kusema kuwa mahusiano yake ya mapenzi siku zote yamekuwa ya siri na wala sio kla kitu kinapswakuongelewa katika mitandao yakijamii lakini yuko sawa katika mahusiano yae.

Akiongea na clouds e ya clouds tv, godzillah anazungumzia wimbo wake mpya ambao unaitwa stay , wimbo ambai baadhi ya watu wamekuwa wakihisi labda anazungumzia mahusiano ayke kutokana na kwamba wimbo huo unazungumzia mwanaume aliyepo katika mahusiano na mwanamke mwenye options nyingi za wanaume wengine.

Hata hivyo Godzillah anasema kuwa wimbo huo ni maisha ya watu wanayaishi lakini sio kweli kwamba hayo ni mahusiano yake kwa sababu upande wake mahusiano yake yako sawa wala hana kinachomsumbua na kwasema kuwa wasije wakashangaa hata yeye akafunga ndoa kama ilivyotokea kwa Alikiba.

Ndoa ya Alikiba imkuwa inspirationkubwa sana kwa wasanii wengi waliopo katika mahusiano na hata wale wasiopo katika mahusiano kutokana na mahusiano hayo kuwa na usiri mpaka sio ya ndoa.

Nay wa Mitego Kajibu Povu la Godzillah

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nay wa Mitego, amejibu rasmi povu lililotolewa na msanii mwenzake wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana Godzillah.

Nay wa Mitego ameachia rasmi ngoma yake jumatatu hii inayoitwa Mikono Juu cha ajabu kilochotokea hapo ni kwamba Nay alipoweka wimbo ule kwenye ukurasa wake wa Instagram Godzillah aliibuka na kudai wimbo ule mbaya lakini hata alipohojiwa na kituo kimoja cha redio alisema Tena kuwa wimbo huo ni mbaya.

Baada ya povu hilo kila mmoja alitegemea Nay wa Mitego atapanick na kumtolea povu zito lakini imekuwa tofauti sana kwani alipohojiwa alisema haoni shida kwani kila mtu ana mtazamo wake binafsi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Nay alifunguka yafuatayo:

Kwanza kwa nini nipanick kisa kaniambia ngoma mbaya? Huo mtazamo mtu anatoa ule anaoona yeye huwezi kupanick utakuwa sio mtu unayefanya kitu kwa ajili ya watu na ukipeleka kitu kwa watu wengi sio kila mtu atapenda alafu mimi nafanya kitu kwa ajili ya watu wengi and then mimi nawajua watu wangu ninaowaimbia lakini pia naamini kizuri hakipendwi na kila mtu asikwambie mtu Yesu mwenyewe alipingwa itakuwa mimi NAy wa Mitego?”.

Lakini pia ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Godzilla na kuna nyimbo zake nyingi anasikiliza pia amesisitiza hana muda wa kukaa na kutengeneza bifu na mtu yeye yupo kikazi kwaiyo anachukulia comment ya Godzilla kama ya shabiki yoyote.

Godzillah ‘Amchokonoa’ Ney wa Mitego

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya hip hop Godzillah ameibuka na kumchimba Msanii mwenzake wa Bongo fleva, Nay wa Mitego baada ya kumwambia nyimbo yake aliyoitoa ni mbaya.

Nay wa Mitego amaechia nyimbo yake mpya na video yake ya wimbo unaoitwa ‘mikono juu’ lakini kitu cha ajabu kilitokea pale ambapo Godzillah alienda kukomenti kwenye page ya Nay na kusema nyimbo mbaya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego aliandika maneno haya ili kutambulisha ujio mpya wa video ya wimbo wake wa Mikono juu:

Video ya wimbo wangu wa mikono juu inatoka kesho jumatatu Subscribe kwenye account yangu ya YouTube #Mr Nay uwe wa kwanza kutazama video yangu”.

Baada ya kuweka posti hiyo cha ajabu Godzillah aliibuka na kwenda kuandika kwenye page ya Nay maneno haya:

Wimbo mbaya Emanuel”.