Faiza Amshauri Diamond Kuachana Na Zari Ili Apate Muda Wa Kula Ujana.

Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa msanii mkubwa wa muziki bongo na mzazi mwenzie Zari The Bossy wanawezekana kuwa katika mgogoro mzito kutokana na tetesi zinazoenea kuwa msanii huyo kwa sasa anatoka kimapenzi na video queen Tunda , Faiza Ally amemshauri Diamond kuachana na stress za kuachana na mzazi mwenzie na kama anataka kumuacha amuache tu kwa sababu yeye bado ni kijana sana bado anahitaji kula ujana.

Faiza anamwambia Diamond kuwa aache kujibebesha mizigo ya kuwa na familia wakati yeye bado ni kijana na anahitaji kutumia ujana wake vizuri kabla umri wake wa kujibebesha majukumu haujafika.

Diamond ni kijana mdogo sana anahitaji kuhave funny na watoto wenzie sio wadada watu wazima, lazima tuangalie watu wa kutembea nao.go baba enjoy the World have funny ndio useto down.jiachie uwe huru ikibidi usiwe na mahusiano kabisa.bado ujaona Dunia hata robo, wewe ni star ela ipo . there is a lot to see nasema with a clean hate no hate  kwa zari na kwa yoyote.

Sio kwa mara ya kwanza Faiza amekuwa akitoa ushauri kwa Diamond kutokana na matatizo yanayomkumba hasa kwa mambo ya mahusiano na jinsi wanawake alionao katika mahusiano wanavyokuwa wanampelekesha.

Itakuwa ni mara ya pili sasa Diamond na Zari wanaingia katika mpasuko wa kimapenzi baada ya kuwa natetesi nyingi zinazokuwa zikisambaa kwamba mwanaume huyo yupo katika mahusiano ya kimapenzi na watu wengine.Mara ya kwanza ilikuwa Hamisa Mobeto na sasa ni mrembo Tunda.

Wizara Ya Afya Waongelea Picha Ya Utupu Ya Faiza Ally

Baada ya kusambaaa kwa picha ya msanii wa bongo movie Faiza Ally ikimuonyesha yupo leba akijifungua na yeye mwenyewe akionekana kusherekea kutimiza kwa miezi minne ya kujifungua mtoto wake huyo wa kiume wizara ya afya waongelea swala hilo.

Faiza Ally ambae baada ya picha hiyo kupostiwa katika ukurasa wake wa Instagram watu wengi walionekana kutokupendezwa na kitu hicho na kujia juu alionekana kutokujali maneno ya watu  na hata kuingia katika ugomvi na baadhi ya wasanii wenzie kutokana na swala hilo,Hata hivyo picha hivyo ilifutwa baada ya muda mfupi kuwekwa na wamiliki wa mtandao wa instagram kutokana na kuripotiwa kuwa ilikuwa haina maadili kwa jamii na kuwa ilikuwa ikiwadharirisha wanawake.

Kampuni ya  GPL iliamua kuwatafuta wahusika wa afya kuzungumzia swla hilo ambalo kwa namna moja ama nyingine linawza kuwahusu ambapo juhudi za kumpata Waziri wa Afya zilishindikana lakini alipatikana msemaji wa wizara hiyo Ndugu  Nsachris  Mwamwaja na kusema kuwa sio vizuri kitendo kama kile kufanyika na wala hairuhusiwi kabisa , lakini pia hata katika maadili ya kitanzania jambo kama hilo haliwezi kuruhisiwa lakini kwa sababu ameposti katika mitandao ya kijamii, wizara inayohusika na mambo ya mitandao wanatakiwa kufatilia swla hilo.

Lakini kwa kuwa aliweka katika mitandoa ya kijamii basi  watu wa sheria za mitandao wanapaswa kufuatilia swala ilo kwa undani zaidi na kwa namna gani wanaweza kuthibiti swala kama hilo lisiweze kutokea tena. maana ni baya na halifai kabisa.

Hata hivyo mwenyewe Faiza Ally alipotafutwa kuulizwa kuhusu hilo alisema kuwa  kwa iyo picha kwake ni jambo la kawaida tu kwa sabau kila mtu anazaa na kuzaliwa tangu enzi za bibi zeu walikuwa wanafanya kitendo hicho kuhusu kujifunza bado sijajua maana bado sijachukuliwa hatua yoyote ila nina jivunia kwa sababu nimeingia leba.

Snura Ajikuta Matatani Baada Ya Kutoa Maoni Kuhusu Faiza Ally.

Baada ya Faiza Ally kuweka picha yake ya utupu ikimuonyesha alivyokuwa leba kipindi anamzaa mtoto wake wa pili wa kiume, baadhi ya watu walishikwa na hasira na wengine waliona kuwa kitendo hicho ni kitendo cha kudharirisha wanawake.Moja ya wasanii wa bongo movies anaefanya vizuri na anaesifika kwa kukata viuno anaejulikana kama Snura Majanga alifunguka na kuongelea swala la Faiza kutuma picha hiyo ni kudharirisha wanawake waliokwend leba tayari.

najua wengi watasema mbona na yeye hana adabu ,ila ukichunguza utagundua sehemu yangu ya kiuno tu ndio inayoniweka matatani, sinaga mambo mengi ya ajabu na sitakuja kuwa nayo kamwe.faiza hii umepitiliza TUSITIRI WANAWAKE WENZIO.. mwanamke anapotaka kuzaa hata kama ni barabarani utafutwa nguo na kuziba …leba ni siri yetu kuna mengi tunayafanya kule ambayo hayapaswi kujulikana nje,ni wengi wanashoot hata video lakini huwa inabaki kumbukumbu yao,na sio kuweka hadharani kila mtu akaona, inakuwaga aibu hasa kwa sisi wanawake, tunadharirika na kupoteza heshima kabisa ya mama, tunadharauliwa sanakwa mtindo huo.hata ndugu zetu wakija hawaruhusiwi kuingia leba zaidi ya manesi na  madaktari  na kama ni private ataruhusiwa kuingia mumeo tu, hizi ndizo tamaduni zetu tusijikatae sana tukaendekeza uzungu, mengine tuwaachie wenyewe sisi tubaki kuwa sisi.#niliemkwazapole -Aliandika Snura katika ukurasa wake wa instagram.

Lakini baada ya posti hiyo ya snura nae faiza aliamua kumjibu na kumjia juu snura kwa kuandika,

Video yako ya Chura na picha ya mimi leba bora nani,na mauno kutwa kucha kuhamasisha ngono kupitia musiki kweli, hebu jiongeze bwana nimezaa hiyo ni natural  mama, wanangu watakuwawasomi hawatakuwa na mawazo ya kipuuzi hivyo, kama za kwako na wengne…so stupid of you kama wewe na mziki wako tu  #postiyamudamfupi @snuramushi. Aliandka Faiza kumjibu Snura.

Hata hivyo posti hiyo iliyokuwa ikimuonyesha faiza yupo leba ilifutwa dakika chache baada ya kuwekwa kutokana na sheria za mitandao  na watu wengi kuiripoti picha hiyo kuwa haina maadili.

 

Faiza Ally: Gabo Sio Aina Ya Mwanaume Naweza Kuwa Naye

Mwanamitindo na muigizaji wa bongo movie asiyeishiwa vituko Faiza Ally ameibuka na kudai kuwa muigizaji wa bongo movie Gabo siyo aina ya mwanaume anayeweza kutembea naye wala kuzaa naye.

Baada ya Faiza kuzaa mtoto wake wa pili anayeitwa Li bila kumtambulisha baba mzazi wa mtoto huyo watu wengi wamekuwa wkijiuliza je ni nani baba mtoto wake? Moja kati ya watu ana ukaribu nao ni mwigizaji Gabo ambaye hata amewahi kuigiza naye filamu inayoitwa ‘baby drama’ na zaidi ya hapo amewahi kusema huko nyuma kuwa amewahi kuwa mpenzi wake hivyo watu wengi hasa mashabiki zake kwenye mtandao wa jamii instagram wamekuwa wakimtaja mwigizaji Gabo kuwa ndiye baba wa mtoto hadi kufikia hatua ya kumfananisha na kudai kuwa wanafanana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza alifunguka kuwa Gabo sio baba wa mtoto wake na wala hajaona mwanaume wa kutembea naye Tanzania kwa hivi sasa.

Ngoja niwaambieni ukweli kuhusu Gabo naona watu wengi mmeamini kabisa kuhusu Gabo! Ni hivi tulikua na kipindi cha Family love kinachorushwa na Clouds Tv na mimi na Gabo ni wanafamilia na mtoto wangu Li ilitakiwa akizaliwa iwe moja kwa moja familia ya ukweli hata ile posti niliyosema kama Gabo ndiye baba wa mtoto ilikuwa ni kukitafuta kipindi namna ya kujulikana, ukweli ni kwamba mimi na Gabo kwanza ni marafiki, pili ni kaka na dada, tatu ni tumefanya kazi mbili pamoja kwa hiyo katika mapenzi mimi na yeye hatujawahi wala hatutowahi zaidi ni mtu mwenye familia yake ana mke na watoto siwezi especially kwa mtu maarufu! kwa hiyo naombeni mtoe fikra zenu mana naona naitwa mrs Gabo na mtoto wangu juu mnamsema ni wake! hapana si wake. Mimi sina bwana Tanzania niko nalea tu halafu  pia kuwa na mtanzania kwa sasa hapana labda awe na quality ninazo zitaka mimi lakini bado sijaona”.

Alimalizia kufunguka Faiza ingawa mpaka sasa amegoma kumuweka wazi baba wa mtoto wake kwa sababu zake binafsi mwenyewe.

Faiza Ally: Sugu ni Mwanaume Ambaye Hajielewi Sina Muda Wa Kumnyenyekea

Mwanamitindo na muigizaji Faiza Ally amefunguka tena kuhusiana na uhusiano wake na baba wa mtoto wake wa kwanza Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Mbunge wa Mbeya Mjini.

Faiza na Sugu wamekuwa katika mabishano ya muda mrefu sana kuhusiana na malezi ya mtoto wao huku Faiza amemshtaki Sugu kwa kukataa kutoa fedha za matunzo ya binti yao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka yafuatayo;

“Kuna wanaume wapumbavu sana mimi nitapigana mwanangu atakua lakini kumbuka sina cha kupoteza mtoto atakapo kuwa wewe ndio utakua umepoteza muda wa kumtunza mwanao kwa sababu ya kuni punish mimi na ujinga wangu! Lakini mimi ntakua nimetimiza majukumu yangu kama mzazi na huenda matusi yangu ndio yananipunguzia stress kwa namna fulani ili maisha yaendelee….sasa weweendelea kunikomesha siku hazigandi”.

Pia Faiza aliendelea kufunguka kwa kulalamika kukerwa na kilichotokea baina yao;

“Ila tu ujue nikiwa najisikia ntakuchamba tu mpaka ntakapo choka na hata nikiacha  ntakua nimeacha kwa sababu nimechoka lakini sio eti ni ache ndo umtunze mwanao, mtunze ndo niache kama humtunzi siachi nikijisikia nakupa za uso mpaka uelekee na usipo elekea basi lakini siwezi kukunyenyekea mpaka nakufa”.

 

Faiza Ally: Diamond Bado Kijana Mdogo Hayupo Tayari Kuoa

Tangu jana kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii ya kuwa Zari na Diamond wameachana habari hizo zilisababishwa na ujumbe alioweka Zari na kitendo chake cha kufuta picha zote za Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram, hii imetokea siku chache tu baada ya Zari kumsamehe Diamond baada ya kuzaa na Hamisa Mobetto ambapo watu waliamini wamesameheana na yameisha.

Muigizaji na mwanamitindo Faiza Ally amefunguka na kudai kuwa hadhani kuwa Diamond yupo tayari kuoa na kutulia chini na familia kwasababu ya umri wake kuwa bado mdogo.

Kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza ameandika yafuatayo;

“Diamond kijana mdogo sana anahitaji kuhave fun na watoto wenzie na sisi wadada tuangalie watu wakutoka nao…..nenda baba have fun ndo usettle down….jiachie uwe huru ikibidi uwe na mahusiano bado hujaiona dunia hata nusu wewe  ni star, hela ipo there is a lot to see. Naongea kwa roho nyeupe sina chuki na Zari au kwa yoyote nimezurura sana duniani kabla ya kuzaa na kutulia jiachie bwana life is today”.

Aliandika Faiza ambaye ameshawahi kuweka wazi kuwa yeye ni shabiki wa Zari.

Faiza Ally: Alikiba Anafanya Muziki Mzuri Kuliko Diamond

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Faiza Ally ameibuka tena na kudai kuwa anauelewa zaidi muziki anaofanya Ali Kiba kuliko muziki anaofanya Diamond Platnumz.

Katika mahojiano aliyoyafanya na TBC Faiza alidai kuwa wasanii wote wawili wanajitahidi katika kufanya muziki kwani wana vipaji tofauti kwani mmoja ni muimbaji na mwingine ni mburudishaji.

Faiza aliendelea kusema:

“Kwanza kati ya muziki wa Diamond na Ali Kiba , naupenda zaidi muziki wa Ali Kiba, muziki wake ni mzuri kuliko Diamond, kwani Diamond ni ile full entertainment ukimwangalia tu unatabasamu lakini Ali Kiba ana muziki mzuri. Nikizungumzia mtu aliyeutoa mziki akaupa heshima mpaka akampa changamoto Kiba na yeye akasimama mpaka tukaanza kumuona kwenye hali ya tofauti ni Diamond”.

Faiza ni moja ya watu ambao msimamo wake umekuwa ukibadilika kuhusu nani ni bora kati ya Diamond na Ali Kiba kwani mara kwa mara amekuwa akibadilika kwani leo anaweza akasema Diamond na kesho atasema kuwa ni Ali Kiba.

Lakini yote kwa yote ushindani huu ndo unafanya muziki wetu kuwa bora zaidi kwani Ali Kiba asingekuwa na changamoto kutoka kwa Diamond asinge kuwa bora alivyo sasa na hivyo hivyo kwa Diamond asingepata changamoto kutoka kwa Ali Kiba basi asingejitahidi kutupa muziki mzuri zaidi tunaopata leo hii.

Sugu Avunja Ukimya Juu ya Swala la Malezi ya Mtoto

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Mbunge wa Mbeya mjini amevunja ukimya na kufunguka kwa mara ya kwanza juu ya shutuma zinazomkabili  dhidi ya mzazi mwenzie Faiza Ally.

Faiza amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kumshutumu Sugu kwa kukataa kumlea binti yao mdogo Sasha. Baada ya juzi kumsema Sugu kuwa hamjali mtoto wake na kukataa kumlipia mtoto huyo ada ya shule hadi kufikia hatua ya Sasha kurudishwa nyumbani.

Kwa mara ya kwanza Sugu kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka na kusema anamlipia ada binti yake huyo lakini mwenye matatizo ni mama yake kwani humkataza kumuona, aliandika yafuatayo juu ya tuhuma hizo:

“Huwa sipendi kuposti hivi vitu lakini imenibidi,  hizi ni bank slips za ada ya mwisho niliyolipa kwaajili ya Sasha na ilikuwa mwezi huu wa tisa nimuanzishe shule ya Feza Nursery pale Mikocheni, lakini from no where mama yake ghafla akanizuia na kusema hahitaji nilipe ada na kunizuia nimsomeshe tena Sasha! Na kwamba ana uwezo wa kumsomesha mwenyewe shule yoyote anayotaka na ndo kumpeleka huko Hazina international ambako pia hata hivyo nilishaanza kuwasiliana na uongozi ili niendelee tu kulipa ada hata kama nimepigwa marufuku kumuona mwanangu bila sababu. Hivi kama nyie mngefanyaje?

Hata hivyo mara baada ya kusema hayo Faiza alikuja juu na kumuita Sugu muongo na amewahi kulipa ada mara mbili tu tangu mtoto wao aanze kusoma na miaka yote hiyo Faiza ndo alikuwa analipa ada.

Faiza Ampongeza Diamond Kwa Kumkubali Mtoto Wa Hamisa

Mwanamitindo Faiza Ally amefunguka na kumpongeza Diamond kwa hatua aliyochukua ya kwenda kwenye vyombo vya habari na  kuweka wazi kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wa Hamisa. Kwa muda mrefu katika mazingira mbalimbali Diamond alikanusha kuwa name uhusiano na Hamisa name pia kuzaa naye. Leo kwa kupitia kipindi cha Leo Tena Diamond amekubali kuwa shetani alimpitia na amewahi kuwa name mahusiano ya kimapenzi na Hamisa.

Baada ya mahojiano hayo kuruka hewani mwanadada Faiza kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka new kuandika yafuatayo:

“Nasikiliza Clouds FM Naseeb nakupenda wewe ni mwanaume ea maana  saana sema wanawake wa Uswahilini ni kama ile methali ya Hamisi, yaani unaweza ukamtoa Hamisi shamba lakini usilitoe shamba kichwani kwa Hamisi #hope hutarudia Tena ujinga wako”.

Inasemekana Kuwait suala la Diamond kumkubali mtoto huyo na kumuhusumia limemgusa sana Faiza kwa sababu halo aliyonayo saivi ni Kuwa baba wa mtoto wake hamuhudumii mtoto wake ipasavyo ndio maana ameona kitendo alichofanya Diamond ni  cha kishujaa.

Faiza Amtolea Povu Mzazi Mwenzie Sugu

Mwanamitindo na mlimbwende Faiza Ally asiyeishiwa na vituko mtandaoni ameingia katika ugomvi mwingine na mzazi mwenziye Mh. Joseph Mbilinyi “Sugu” mbunge wa Mbeya kuhusiana na malezi ya binti yao Sasha. Kupitia ukurasa wake wa instagram Faiza amefunguka yaliyo moyoni mwake mara baada ya kumpeleka mtoto wake shule na yeye kurudishwa getini kwa sababu ya kushindwa kulipa ada.

Faiza ameandika:

“Na hasira zangu za shule nazirudisha kwake kwa sababu na yeye ni muhusika kama mzazi! Kwanza kabisa nakuita mbunge mpumbavu sana! Inakuaje serikali inakupa madaraka makubwa kiasi hicho? Wakati unashindwa kuendesha maisha ya mtoto wako mmoja tu? Mbunge gani usie jua mwanao analipaje ada? Mbunge gani usiyejua mwanao analala wapi? Mbunge gani usiyejua mwanao ana mahitaji anakula nini? pumbavu wewe unaendekeza mbunge tu na bangi na konyagi? how? Can you call yourself mheshimiwa? Kwa heshma ipi? Hivi wewe ulilazimishwa kunipa mimba? We si ulikuwa unalialia unataka mtoto f*** wewe? Ulinizalisha ili unikomoe? Na kwambia hustahili hata kuwa na rafiki kama Msigwa, Lema sio wenzako u belong kitaa utarudi mtaani there is where u belong unaona wenzako wametupa watoto? Huna hata haya huoni hata mfano kwa Prof. Jay kwa mwanae? how can you punish Sasha for no reason ! Shame on you Joseph! na sasa nakushtaki naona punda haendi  bila mzigo! Eti Jay Z and Obama ndo role models wako how? huoi hao ma role models wako na familia zao wakoje? Sielewi how did i fall in love wewe sijielewi how did i fall in love na inakuaje bado nakupenda mtu kama wewe. Sasa naiomba serikali iingilie kati haya maswala kati ya viongozi wasiojali watoto wao!  I hate you baba jina na nikifa najua ni wewe adui wa maisha yangu!.”

Faiza Ally: Tanzania nzima na East Africa tunatakiwa tumpenda Diamond sana

Faiza Ally amedai kuwa ni sharti Tanzania na Afrika Mashariki nzima kumpenda Diamond. Mrembo huyo aliandika ujumbe wake kwenye mtandao wa Instagram.

Ally alimpigia kifua Diamond kwa kusema kuwa muziki wa Tanzania haukua na ushindani kabla ya Diamond kuingia kwenye game.

“Hivi hamjawaji kujiuliza kwamba toka zamani kabla ya Diamond kulikua na mziki mzuri lkn hakujawahi kuwa na ushindani kama changamoto alio leta Diamond kwenye game. Hivi mnajua kwamba Tanzania nzima na East Africa tunatakiwa tumpenda Diamond sana ???? Hivi hamjawaji kujiuliza kwamba toka zamani kabla ya Diamond kulikua na mziki mzuri lkn hakujawahi kuwa na ushindani kama changamoto alio leta Diamond kwenye game , sasa nasema hivi mziki mzuri peke yake hautoshi na akili kubwa inahusika , unapo kuwa huna akili ktk unalo lifanya ni sawa na mwanamke mzuri hlf hajielewi…. Leo hii kwa u star wenye akili alio uleta Naseeb wazazi wengi wanaona fursa ya mziki kupitia Diamond tofauti na miaka ya zamani, mziki ulikua unaonekana kama sio kazi lkn Leo mziki unaendesha familia nyingi, hata mm ningependa mwanangu awe mwanamziki mwenye mafanikio kama Diamond , sasa nasema hivi ku mpenda Diamond ni amri sio ombi,” aliandika Faiza Ally.

Aliandelea kwa kusema kuwa Diamond ni kama Obama:

” Diamond ni kama Obama marekani kwa watu weusi , yeye alionyesha kuwa mtu mweusi ana uwezo kwenye siasa na Diamond tanzania kaonyesha mziki unalipa na msisahau katoa vijana wengi na bado wengine wamepata ajira kupitia yeye na naona watapata wengi zaidi ! Sasa nakuomba D ufungue music school basi tuwalete watoto wetu na wenyewe wapate mkwanja kama wako maana shule sio maisha pekee mention town na vipaji navyo ni sehemu ya mafanikio ktk maisha a special kwa maisha tunayo elekea , mm nakupendaga sana na zaidi ni jitihada zako kwenye kazi ! Keep it up dogo ? #ZILIPENDWA”

 

Faisal Ally asisitiza lazima afanye upasuaji wa matiti ili aonekane sexy

Faisal Ally ambaye anajulikana sana kwa sababu ya movie zake za Bongo na pia mitindo yake ya kimavazi, alifunguka na kusema lazima afanye upasuaji wa matiti kuwa binti mdogo.

Faiza ambaye ako na wawili kwa sasa, alisema kuwa akimaliza kunyonyesha mtoto aliyemzaa hivi karibuni ataenda kufanya operesheni ya matiti kuyarudisha ndogo.

Soma pia: Faiza Alley ajifungua mtoto wa pili (video)

“Unajua kila kitu ni kupanga kwa sababu huyu baba wa mtoto wangu wa pili ni Mmarekani na hatukuwahi kupanga kuishi pamoja zaidi ya kuja labda kwa mara moja kuona mtoto wake basi. Kwa sasa sina mpango wa kuongeza mwingine tena nikimaliza kunyonyesha nitaenda kufanya operesheni ya matiti kuyarudisha saa sita yaani nirudi msichana kabisa labda,” alisema Faiza katika mahojiano na Ijumaa.

 

Faiza Ally amchana Hamisa Mobetto

Faisal Ally ambaye anajulikana sana kwa sababu ya movie zake za Bongo na pia mitindo yake ya kimavazi hivi karibuni alifunguka kuongelelea ujauzito wa Hamisa Mobetto ambaye ni video vixen na model kutoka bongo.

Hata hivyo hii ndio mara ya kwanza Faiza Ally kutoa maoni kuhusu mrembo huyu tangu isemekane kuwa anamtarajia mtoto wa Diamond Platnumz ambaye ni mume wa Zari Hassan.

Akizungumza na 3 Tamu, Faiza alisema kuwa, yeye Kama mwanamke hajafurahishwa na maneno yale ikiwa ni kweli kuwa Hamisa Mobetto ana ujauzito unaodaiwa ni wa msanii wa CEO wa Wasafi Records. Ally alisema,

Unajua wasichana wengi hawajithamini wanafanya vitu bila kufikiria, kama huyo Hamisa nasikia ana ujauzito wa huyo msanii (jina kapuni) na kama ni kweli mimba ni ya huyo mtu, kakosea sana, napenda kuongea kitu kinachonigusa kwenye nafsi yangu akichukia atajijua.

Hata hivyo Diamond aliweka wazi hivi karibuni kuwa yeye na Hamisa Mobetto hawamtarajii mtoto pamoja na kuwa uhusiano was ni wa kibiashara tu.

“Alikuwa na pesa nyingi, lakini ameshindwa kununua uhai” Waigizaji wa Bongo Movie waongea matope kuhusu kifo cha Ivan

Tofauti na wasanii wengine ambao walitoa salamu za rambirambi kufwatia kifo cha Ivan Ssemwanga, Steve Nyerere and Faiza Ally wameeleza hisia kali kuhusu kifo cha aliyekuwa mume wa Zari.

Waigizaji hao wa Bongo Movies wameongea matope kuhusu kifo cha Ivan, hisia zao kuhusu kifo cha mwenda zake zinaonyesha uadui tu.

“Alikuwa na pesa nyingi, alikuwa na uwezo wa kufanya chochote, alikuwa na uwezo wa kununua chochote lakini ameshindwa kununua uhai. Nimejifunza kitu kupitia wewe, tuishi vizuri na watu maana hakuna ajuaye kesho,” Steve Nyerere aliandika.

Steve Nyerere

“Binaadamu akikuchukia hata zuri kwake ni baya na ndio maana huwa na maisha yangu tu kama mimi bila kutaka kuwa yoyote, hakuna zuri mbele ya mtu mbaya. Unajua nini wala sijali naona upuuzi tu kama ya kipuuzi mengine yote yalio pita.

“Maisha yangu na wanangu yako kwenye mikono salama hata kushinda mikono yangu, yako kwenye mikono ya Mungu mwingi wa rehma. Leo Ivan na matajiri wengine wako wapi? Mali sio kila kitu kwenye maisha yetu tunahitaji amani, mapenzi, maelewano makubaliano.

Faiza Ally

“Nimetoka kwenye kutokua na mlo mpaka sasa namiliki milo, huo ni utajiri mkubwa maana kwanza ni kushiba akili ikae sawa ndio upange habari zingine, so at the end my heart is pure and that what give me amani ya moyo, hayo mengineyo tena yako nje ya uwezo wangu ni mipango ya Mungu, Faiza Ally aliandika.