Diamond Kuja na Wasafi Festival

Msanii diamond platinumz ametangaza rasmi kuhusu kufanya festival kubwa mwaka huu itakayojulikana kama Wasafi Festival ikiwa ni moja ya ubunifu wake mkubwa katika biashara na kuwafurahisa mashabiki wake.

Hii ni moja ya jambo kubwa sana ambalo mashabiki wengi wa team hiyo walikuwa wakirisubiria kwa hamu kubwa givyo ujio huo umewaweka watu wengi katika hamsa ya kujua lini litafanyika swala hilo.

Katika ukurasa wake wa instagram, diamond aliandika “kama naiona wasafi festival mwaka huu itakavyokuwa , sijui hata tuanze mkoa gani “

Wasafi wamekuwa wakifanya baadhi ya matamasha ya pamoja na mshabiki ikiwa ni moja ya njia nzuri yakuwa na mshabiki wao , kama ilivyofanyika mwaka uliopita Wasafi beach party.

 

Bifu la Diamond na Mama Yake Lafika Mtandaoni.

Msanii Diamond platnumz na mama yake inasemekana hawana mahusiano mazuri kutokana na ukweli kwamba siku ya jana akaunt ya instagram ya  mama yake ilionyesha kuwa wa sasa mama huyo amfuati tena mtoto wake lakini vile vile hata Diamond amfuati mama yak.

Diamond na mam yake wanasemekana kuingia katika ugomvi huo kutokana na chuki aliyonayo mama huyo kwa hamisa mobeto na mtoto wake wa kiume aliyezaa na Diamond ambapo siku chache zilizopita Diamond alimpost mtoto wake huyo ilhali bibi wa mtoto huyo(Bi .Sandra ) hajawahi kumpost na watu kuhisi kuwa inawezekana mama huyo hampezni kabisa mjukuu wake huyo wa kiume kutoka kwa hamisa.

Kumekuwa na uendeleaji wa isri wa pnzi la Hamisa na Diamond huku tetesi zikidai kuwa ile ahadi ambayo Diamond aliiweka ya kuoa mwaka huu inawezekana kutimia kwa ailimia 90 kwa hamisa  kutokana na ukaribu wake na hamisa na penzi jipya kati yao.

 

Wema Sepetu Atoa Baraka Ndoa ya Hamisa na Diamond.

Mwanadada Wema Sepetu amefunguka kwa mara ya kwanza na kuto abaraka zake endapo kutakuwa na makubalianao ya ndoa kati ya msani Diamond na Hamisa Mobeto kwa kuwa huo ni uamuzi wake na mpenzi wake huyo.

Wema ambae hapo mwanzo walikuwa hawapiki chungu kimoja na Hamisa na kusema kuwa hamisa ni mdogo sana kwake lakini ameshindwa kumuheshimulakini pia uadui mkubwa kati ya Hamisa na Wema ulitokana na wawili hao kuwa katika mahusiano na mwanaume mmoja katika wakati tofauti.

Ni hivi watu wannapenda sana kuunganisha matukio na ndio maaana siku hile ya usiku wa sinema zetu watu waliona kama mimi nimekwzika sana kumuona hamosa akimtaja diamond kama mwanaume aliyemvutia kwa kubaa vizuri.

watu wanapaswa kujua kuwa siku ile sikukasirika na hata niliposema kuwa nitaanza kufanya kazi wasafi tv , kuna watu walainza kusema nimerudiana na diamond lakini ukweli ni kwamba diamond amebaki kuwa rafiki yangu, kaka yangu na pia bosi wangu tu.

siku zote nimekuwa nikisema kuwa mobeto ni mdogo wangu tu na nimekuwa nampenda sana na ananiheshimu sana, uhusiano wake na diamond mimi ninaona ni mzuri tu kwa sababu walishakuwa kitu kimoja kama wazazi  kwaio hata kama wataoana mi naona sawa tu kwa sababu hata couple ya ni nzuri na inafurahisha.

Ukiachana na drama zote za Diamond na wanawake tofauti tofauti lakini Wema ndio mwanamke wa kwanza katika historia ya mapenzi ya Diamond kutoka nae kimapenzi akiwa mwanamke maarufu tanzannia  na hata Diamond mwenyewe huwa ukiri kuwa Wema ndie mwanamke aliyewahi kumfanya akafanikiwa sana kipindi cha hapo nyuma.

 

Ijue Siri ya Diamond Kuchaguliwa Kombe la Dunia

Mara nyingine labda watu wamekuwa wakijiuliza kwanini Diamond achaguliwe katika Kombe la Dunia kuiwakilisha Afrika na wala sio wasanii wengine waliopo Afrika, mbona kuna wasanii wengi tu wakubwa mbao wamekuwa wakifanya vizuri sana lakini hawajachaguliwa mpaka amechaguliwa Diamond.

Raia mmoja kutoka Afrika Kusini ambae ni mdau mkubwa wa muziki barani Afrika anafunguka na kusema kuwa  yeye ndie alipwe jukumu la kutafuta wasanii watano kutoka afrika watakao shiriki kutengeneza wimbo wa kombe la dunia na  kutokana na vigezo alivyokuwa navyo diamond haikuwa rais kuacha kumchagua.

Tim Horwood anasema kuwa diamond ni moja kati ya wasanii walijenga ngome kubwa sana barani A frika kupitiamuziki wake kiasi kwamba hata alipopewa kazi hiyo hakuweza kuacha kumfikilia Diamond Platinumz.

Diamond Ahojiwa na Kuachiwa kwa Dhamana, Atahojiwa Tena.-Kamanda wa Polisi

Msanii Diamond Platinumz ambae aliwekwa kituo cha polisi kwa muda ili kutoa taarifa ya kile kilichokuwa kikisambaa katika vyombo vya habari kuhusu kuvuja kwa picha  na video chafu katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha yeye na wanawake wwili tofauti wakiwa katika hali ya usiri videoambazo hazikupaswa kuwa wazi kama zilivyosambazwa.

Diamond alimaliza mahojiano hayo siku hiyo hiyo na kuachowa kwa dhamana na polisi kuthibitisha kuwa ni kweli alikuwepo kituoni na ametoa ushirikiano uliohitajika na ameachiwa mpaka uchunguzi uatakapo kamilika na kuhojiwa tna siku watakapo mhitaji.

kamanda mambo sasa alisema kuwa diamond ameachiwa kwa dhamana”alihojiwa jana na kuachiwa kwa dhamana, lakini upelelezi unaendelea”

Diamond na Nandy walikamatwa na polisi baada ya kutuhumiwa kwa kosa la kusambaza picha chafu zisizokuwa na maadili katika mitandao ya kijamii.

 

Stamina Atamani Kuwa na Media House Kama Diamond

Msanii wa hip-hop  Stamina amefunguka na kuongelea juhudi za diamond baada ya kufungua media house yake ambayo itakuwa ni kama chachu kwa wasanii wengine kutamani kufanya kama alivyofanya yeye.

Stamina ansema kuwa anamuona diamond amepiga atua kubwa kwa sababu kitu alichokifanya hakuna aliyewahi kukifanya na kama kuna mtu atakuwa kimya bila kumpa sifa diamond basi ni mtu mwenye roho mbaya .

ni steji nzuri alichokifanya kama una roho mbaya utakiona kitu cha kijinga ila kama una roho nzuri unaachaje kumsifia mtu ambae kajitahidi na kuweka efforts zake, namsifia mimi siwezi kuacha kumsifia  , siwezi kuwa na negative though ukiona mtu anafanya vile ujue ana step anatoka hapa na anafanya vile.

Stamina ansema kuwa alichokifanya diamond ni chachu kwa wasanii wengine  na hata yeye ametamani sana kuwa na media house kama Diamond.

lazima iwe chachu msanii gani ambae hatamani, hata mimi natamani kuwa na media house yangu kwa sababu kutoka kupigwa nyimbo yako kwenye media hadi kuwa na media yake kuamua anapiga mud wowote anaotaka.

Kwangu Sio Msalaba Bali ni Alama ya Kujumlisha Yenye Siri Nzito:-Daimond

Msanii mkubwa wa bongo Diamond  amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakimsema kuwa anavaa msalaba ambao hauendani na imani yake lakini ukweli unabaki kuwa siri ya msalaba huo anaijua yeye na kwamba kwake yeye ule sio msalaba bali ni alama ya kumjumlisha ambayo kwake ina maana sana.

Diamond amesema kuwa hayo kwa sababu kuna kipindi aliwahi kuongelewa hadi  na voiongozi wa dini kuwa amekuwa haeleweki kwa sababu anavaa misalaba ambayo ni kunyume na imani ya dini yake ya kiislamu.

cheni ninayovaa na watu wanavyonidiss nimekuwa nina washangaa sana,kwa sababu watu wamekuwa wanazungumza kile wasichokijua kabisa.kwangu huu sio msalaba bali ni alama ya kujumlisha ambayo ninaiona kuwa haina tatizo lolote kwangu zaidi ya kuwa na siri nzito sana.–Aliongea Dimaond akichona na kipindi cha Mikito Nusu Nusu.

Diamond Athibitisha Zamaradi Kufanya kazi WCB

Katika usiku wa sinema zetu, Diamond Platunumz ambae alipata bahati ya kupndwa katika jukwaa hilo na kutoa tuzo kwa moja ya washindi alifunguka na kusema kuwa televisheni na radio yao zingewashwa siku hiyo na kuwapa moyo wasanii wa filamu nchi kwa kutangaza rasmi kuwa kutakuwa na kipindi kipya na kizuri kwa ajili ya kwasapoti wasanii wa filamu nchini.

Katika kutangaza huko, diamond alisema kuwa mwanadada zamaradi mketema ndie atakae kuwa na kipindi maarum kwa ajili ya wasanii wa filamu  nchi.

Zamaradi aliwashawahi kuwa na kipindi kama hicho kilicjhokuwa kikijulikana kama take one ambacho kilikuwa kikifatilia kazi na wasanii wa bongo movies wanayoyafanya na alisaidia sana kuinua sanaa ya bongo movie.

Zamaradi amabe kwa hapo mwanzo alikuwa akifanya kipindi hicho clouds tv , sasa hivi atakuwa akipatikana huko kwa ajili ya kuinua sanaa ya Tanzania.KILA LENYE KHERI KWAKE.

BASATA Wakanusha Kufungulia Nyimbo za Diamond.

Siku mbili zilizopita baada ya msanii diamond kukutana na waziri Mwakyembe na Naibu Waziri wake Juliana Shonza ambae alikuwa katika vita ya kurushiana maneno na msanii huyo walipokutana  na kuzungumza maswala yaliyokuwa yanaendelea  kuhusu kufungia nyimbo za wasanii zikiwemo hizo mbili za Diamond Platinumz  kuna baadhi ya mitandao walizusha kuwa nyimbo mbili za Diamond zimefunguliwa na kuruhusiwa kuchezwa kama mwanzo katika vituo vya habari.

katibu mtendaji wa BASATA amesema kuwa habari zinazosambaa wanatakiwa kuzipuuzia kwa sababu hazina ukweli wowote,lakini pia mngerza ameelezea kwanini msanii Diamond amekuta na waziri na wala sio wasanii wengine waliokuwa wamefungiwa.

katibu mtendaji wa BASATA  anasema kuwa sababu kubwa ya Diamond kukutana na waziri na Naibu ni baada ya kutokea kwa majibizano kati yao hivyo walitakiwa kukutana hili kuyamaliza matatizo hayo ambayo yalikuwa yanaendelea bila wao kukutana.

Hata hivyo Mngereza maesema kufunguliwa kwa nyimbo ya msanii yoyote ni baada ya msanii huyo kukamilisha vigezo vyote na masharti atakayotakiwa kuyatimiza.

Uoga kwako ndio kufeli kwako:Ujumbe wa Aunty Ezekiel kwa Diamond

Mwanadada Aunty Ezekiel arusha kombora kwa waliofungia nyimbo za wasanii !!. Muigizaji huyo wa filamu ameandika haya katika ukurasa wake wa instagram huku akimtaja diamond platinumz kama shujaa katika kusimama imara ili kutetea muziki huo.
.
Uoga wako ndio kufeli kwako…..diamondplatnumz Am so proud of u kiukweli unajua unachokifanya haijalishi anaetaka kukukatisha Safari yako ni Nani na ana cheo gani ! Ilimradi unajua haki yako basi weka uwoga pembeni na kutetea haki yako….SAFI SANA ….Ktk kazi hizi kwa asilimia kadhaa hawa watu wamekuwa wakichangia kufeli kwa kazi zetu tena Mbaya zaidi hutokeza baada ya kuona kuna baadhi ya mafanikio kupitia fani hiyo Ila wakati mkihangaika kusukuma gurudumu huwa wamekaa kimya kama hawapo. Mnakosea Sana tena Sana mnakatisha tamaa, mnafelisha watu Pamoja na Maisha yao bila kufikiri kuna watu wangapi Nyuma yake ambao anawabeba na kufanya Maisha yaende….Nashindwa kuandika sana lakini natamani tuu wajue kuwa WANATUKOSEA SANA SANA SANA……Wasanii tuinuke na kuwa na Uthubutu wa kusema yote yale ambayo tunaona tunaonewa na sio kukaa kuongea chini chini haitatusaidia na tutaendelea kufeli na wao wakifaulu kwa kuonekana wafanyakazi Bora kumbe hamna lolote Uonevu tuu…

Hata hivyo baada ya mwanadada huyo kuongea hivyo diamond platinumz alimjibu na kusema:

Ni muda wa kujenga Sanaa iliyo kubwa na yenye kuleta mafanikio kwa wasanii na serikali….sio kuleteana figigufigisu kisa eti una mamlaka kutafuta eti Kiki ama eti uonekane we flani uogopewe HELL NO !

Manara Amkingia Kifua Diamond

Moja ya watu wanaojihusisha sana na soka Tanzania Hajis Mananra amefunguka na kumkingia wa kifua msanii Diamond na wenzake ambao wamekuwa wakishinda mitandao kutwa kujaribu kutetea haki zo kwa Naibu waziri ambae ameibuka na sera ya kuwafungia wasanii kwa madai kuwa wanaimba nyimbo zisozokuwa na maadili katika jamii.

Hivi karibun Diamond aliongea katika mdia moja na kusema kuwa hata kama atatakiwa kulala jela kwa sababu ya muziki basi atafanya ilimradi kutetea haki ya muziki kwa sababu wau wanaofungia muziki huo hawajui historia ya muziki wala msanii wanaemfungia.

Hajis mManara anasma kuwa pamoja na kwamba wasanii wanwza kuwa wamefanya kosa lakini wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la pli na kwa upande wa Diamond ni msanii mkubwa mbae amekuwa akiiwakilisha nchi katika mambo mbalimbali na hata kjuitoa kwa ajili ya jamii.

ngoja na mimi nispitwe na hili..inawezekana kuwa kama binadamu anaweza kuwa amekosea , lakini inabidi tutambua kuhusu muziki wa kisasa na soko lake linataka nini..by the way diamond na wenzie tunawatumia sana katika maswala ya kijamii  na hata kampeni zetu za kisiasa,na huyu ni brand kubwa ,,,walau tufanye staa kidogo na tujitaidi tupende vya kwetu.

nb.mimi napenda muziki mzuri sina cha timu wala cha baba yake na timu….hawakawii wabongo. @diamondplatinumz

Hata hivyo bado vita kati ya Diamond na Naibu waziri katika mitadaoya kijamii ni kubwa kutokana na kurushiana kwa maneno , na pia waziri mwenye mamlaka husika anssema Diamond hapaswi kulewa umaarufu wake.

BET Waonyesha Kumtambua Diamond na Kazi Zake.

Diamond wiki yote iliyopita ameonekana kuwa  na trending kubwa katika mitandao ya kijamii hasa baada ya kufanya uzinduzi wa album yake mpya huku nchini kenya na kuzoa mashabiki kibao huku watu mbalimbali wakizidi kumuongelea katika vyombo vya habari na katika mitandao ya kijamii.

Kituo kikubwa cha habari nchi cha BET  nacho hakikuwa nyuma kuonyesha kufurahishwa na kazi za msanii Diamond kwa kumpongeza hasa baada ya nyimbo zake tano kuonekana katika list ya nyimbo bora za itune katika nchi ya Burkina Faso.

katika ukurasa wao wa twitter , BET waliandika  congratulations @diamondplatinumz for having first 5 songs  on the Burkina Faso iTunes top song list #winning.

                                                        

Wiki hii pia Diamond aliachia wimbo wake mpya wa african beauty ambao amemshirikisha Omarion ambae pia alikuwepo katika uzinduzi wa album yake huko nchini Kenya na kufanya Diamond kuendelea kuwa na trending katika mitandao.

 

Diamond Ndani ya Billboard kwa Kishindo.

Msanii Diamond Platinumz amekuwa ni moja ya mastaa ambao ndoto zao zinaanza kutimia kwa kuandikwa katika makala za mtandao wa billboard nchini.katika makala hiyo Diamond amewekwa katika picha ya pamoja na mstaa wengine wanne akiwepo Wizkid, Tiwa savage na  Davido.

Katika makala hiyo inaonyesha ni jinsi gani muziki wa Afrika unavyojitahdi kumtafuta star wa pop Dunianai kutoka afrika pia.Hii imekuja baada ya kampuni kubwa ya muziki Duniani Universal Group ambayo pia inasimamia kazi za Diamond kwa sasa  kupitia tawi lake la nchini uhalanzi ilitangaza kununua hisa za asilimia 70% za lebo ya AI records za nchini  kenya.

UMG itakuwa inafanya kazi ya kusambaza kazi mbalimbal za wasanii  kutokea AI Records  Duniani kote ikiwepo  kwenye mitandao  mikubwa tofauti tofauti Duniani.

 

 

Diamond Aacha Historia, Akabidhiwa Ardhi Kenya.

Msanii wa muziki diamond latinumz ambae ameamua kufanikisha swala la kuwa miongoni mwa wasanii ambao wametoa album za nyimbo zake  amepewa zawadi nono nchini kenya.diamond ambae amefanya uzinduzi wa album yake ya A Boy From Tandale  March 14 nchini Kenya, show ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu  na watu wa nchini humo huku wakijiona kuwa na heshina na thamanikubwa kwa msanii huyo kutokana na ukweli kwamba Diamond angeweza kufanya show hiyo nchi yoyote lakini aliamua kuifanya nchini humo.

Hata hivyo watu wa nchini Kenya pia waliamua kurudisha shukrani zao kwa msanii huyo na kuamua kumpatia zawadi ya kipande cha robo heka ya ardhi nchini humo.

Katika shoe hiyo diamond aliambatana na familia yake pamoja na team yake nzima ya wasafi huku msanii mkubwa Dunianai Omarion akija Afrika kwa ajili ya kumpa sapoti.

 

Kwa Mara ya Kwanza Tangu Kufungiwa kwa Nyimbo Zake, Diamond Awashauri BASATA,

Msanii wa muziki nchini Diamond Platinumz jana kwa mara ya kwanza amefunguka na kuongelea swala la kufungiwa kwa nyimbo zake na nyimbo za wasanii wengine wiki kadhaa zilizopita kwa madai ya kuwa nyimbo hizo hazina maadili na zimekuwa na maneno ya kupotosha wasikilizaji.

Diamond anasema kuwa  nyimbo nyingi zimekuwa zikifungiwa kwa sababu ya tasfiri binafsi na sio kwa sababu zinakuwa na matatioz kama wanavyosema.Hata hivyo Diamond anasema kuwa nyimbo nyingi za wasani wa nje zimekuwa zikipigwa katika vyombo vya habari na kuzifungia za wasanii wa ndani ya nchi.

Huwezi kuimba nyimbo ya mapezni na ukaacha kusema maneno ya kimahaba, huo ni uongo kwa sababu hautafikisha ujumbe unaokusudia.nyimbo kama waka waka na hallelujah nilizifanya nikifikiriakuwa nataka kuona na soko lingine watusikilize serikali lazima ielewei hilo. nakitu kinachoniuma zaidi ni kwamba zinafungiwa nyimbo zetu lakii za nika nick minaj zinapigwa, so ni lazima hilo nalo tuliangalie.

Diamond aliongea hayo kwa mara yake ya kwanza kufumguka tangu kufungiwa kwa nyimbo zake mbili ambazo zimetoka hivi karibuni na tena zote akiwa amefanya na wasanii wakubwa kutoka nje ya nchi,maneno hayo aliongea Diamond alipokuwa katika mahojiano na waandishi wa habari nchini kenya ambapo akikwenda kwa ajili ya kufanya uzinduzi wa album yake.

Diamond Amuhaidi Mama Yake Kuoa Mwaka Huu.

Mwanamuziki mkubwa Duniani Diamond Platinumz jana katika kusherekea  siku ya  wanawake Duniani amemtakia mama yake kheri ya siku hiyo na wanawake wengine wote Duniani huku akitoa ahadi kuwa mwaka huu kabla haujaisha atahakikisha kuwa anaoa mwanamke ambae hatomsumbua tena mama yake.

Diamond aliamua pia kutumia nafasi hiyo kumuomba mama yake msamaha kwa makwazo na magumu yote ambayo amekuwa akimpitisha  na kumdharirisha kuwa mambo mengi katika mitandao na kutukanwa kote anapokuwa anatukana.

Happy women’s day kwa mama na wanawake wote ulimwenguni,nashukuru sana kwa kunizaa na kunilea ..wewe ni nguzo na mboni ya maisha yangu mama ..licha ya shida na mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea lakina hata sasa ambapo ulitakiwa walau kupumzika nimekuwa nikikukosa  kwa kukuingiza hata kwenye matatizo yasiyokuhusu..wanakutukana ,wanakukebehi, na kukutupia kila neno lililo baya  yote kwa sababu yangu mimi , lakini siku zote umekuwa ni mwenye kunisamehe , kunipenda na kunithamini ..nakupenda sana mama , nisamehe kwa yote niliyokukosea..inshalaah mwenyezi mungu anibariki mwaka huu mwanao nifanikishe ndoa yangu na kukuoa furaha ya milele ambayo siku zote umekuwa ukiitaka…@mama_dangote.

Ingawa maneno ya diamond yamekuwa kitendawili kwa sababu hajaweka wazi ni lini au nani anategemea kumuoa mwaka huu lakini hii imekuwa ni kama ameweka larm kwa watu mbalimbali hasa mashabiki  wake.

Tangu Diamond ameachana na zari amekuwa akionekana yupo karibu sana na diamond lakini pia anaonekana kuwa ameshamaliza tofauti zake na hamisa na kukubali kulea mtoto wao.