Kuonekana na Zari Au Hamisa Isiwe Big ishu , Wote ni Washkaji Zangu;-Diamond .

Msanii Diamond Platinumz amfunguka na kuwataka wazazi wenzake kuwa na ushirikiano baina yao na kuondoa matabaka kati yao ili kuleta ushirikiano mzuri kati yao na watoto pia, Diamond anasema kuwa inabisdi ifike sehemu wazazi hao waweze kuwa pamoja katika baadhi ya mambo muhimu ya kifamilia .

Diamond anasema kuwa zari na hamisa wote ni washkaji zake tu na hakuna  anataka ibaki hivyo ili hata inapotokea anapokuwa karibu na mmoja wapo isiwe swala la kuzua gumzo bali ionekane kama washkaji lakini pia kama wazazi.

Nawapenda sana watoto wangu na mama zao watabaki kuwa tu washkaji zangu,sitaki ple ninapoonekana na hamisa au zari basi inaonekana big ishgu hapana wote ni wazazi wenzangu.na nataka hata inapotokea kuna birthday ya familia moja basi pande zote mbili ziwepo.

nawashukuru sana kwa malezi yao mazur lakini pia wanapaswa kuwajengea watoto upendo sio tu kwangu mimi ila hata kwa bibi yao na ndugu zao wengine maana maisha yenyewe mafupi.

Diamond Awaomba Wazazi Wenzie Kutoweka Matabaka kati ya Watoto Wao.

Msanii Diamond Platinums  hivi karibuni amekuwa akisistiza sana familia yake kuwa na upendo na amani ili kuondoa matabaka kati ya afmilia zake na hasa upande wa watoto wake ambao amezaa na wanawake tofauti.

Kwa kukumbuka hivi juzi katika kumtakia sikukuu ya kuzaliwa mama yake diamond alimuomba mama yake kuacha kuwabagua watoto wake na kuwapenda wajukuu zake wote kama vile yeye anavyowapenda kwa sababu anajua kuwa ni damu yake.

Lakini pia hakuacha kuwa nyumba hivi karibuni kuzngumza na wazazi wa watoto hao ( zari na hamisa0 kuwa anawaomba watoto wake wapendane na watu wa kuwaunganisha ni wao sio watu wengine.Diamond anawashukuru kutokana na wamama hao kuwa na malezi mazuri kwa watoto wao lakini sasa ana sisitiza upendo.

Nawashukuru wazazi wenzangu wanalea watoto vizuri lakini pia tumekuwa tukishirikiana sana katika kuakikisha hilo,pia tu nataka niwaombe kwamba wajitahidi sana wasitengeneze chuki baina ya watoto wa huku na wa huko.na mimi kama mzazi ninawapenda watoto wangu wote na at the end of the day we are familiy.

Daimond ansema kuwa inapotokea kuna kitu chochcote katika familia hizi mbili basi ni lazima kuwe na ushirikiano na  mahudhurio mazuri kwa pande zote mbili sio mwingine anakuwepo hapa mwingine hayupo.

huwezi jua nani atakuwa nai kesho kwaio ukisiaki leo kuna birthday ya huyu  na huyu yupo na yule yupo , wasitengeneze matabaka kati yao na ninawashukuru sana na nina waombea kwa mwenyezi mungu waendelee kuwa na moyo huo huo.

Wafahamu Wasanii na Watu Waliopo Nyuma ya Mafanikio ya Diamond

Mwanamuziki mkubwa Duniani Diamond Platinumz amefunguka na kueleza ni wasanii gani na watu gani maarufu  aliowahikuwaangalia na kuwasikiliza kwa kufuata ushauri na mawazo yao mpka kufikia hapo alipo.

Diamond katika ukurasa wake wa instagram aliweka picha za watu mbalimbali wakubwa katika muziki na wengine wakiwa nje ya muziki na kuandika kuwa ukitaka kujua diamnd ni  nani basi unaweza kumjua kupitia watu hao.

katika list hiyo kuna mama yake mzazi,yupo msanii kama Ay, Q-chillah wote kutoka Tanzania lakini pia yuko Jayz, P-diddy hao ni wasanii kutoka nje , lakini pia yuko boss wa Clouds Media bwana Joseph kusaga.

Katika ukurasa wake baada ya kuweka picha hiyo aliandika caption”just incase somone ask about definition of Diamond platinum, that is it…””

Mwalimu Aliyemfundisha Diamond Kingereza Afunguka, Aliwafundisha WCB Nzima

Mwalimu alyemfundisha msanii mkubwa tanzania diamond platinumz kingereza maefunguka na kusema kuwa yeye ndie alimfundisha diamond kingerza na alikuwa mwanafunzi mzuri na mwenye jitihada sana alipokuwa akisoma kozi hiyo.

Hata hivyo mwalimu huyo amefunguka na kusema kuwa kwa sababu ya kufanya vizuri kwa diamond, alijikuta anapewa tenda ya kuwafundisha wasanii wengine wa wcb akiwemo harmonize.

Diamond platinumz, Diamond he was very smart na kuna muda mwingine alikuwa akiwa ananirudisha nyumbani tukiwa kwenye gari unakuta ameshika na kitabu huku anasoma.

Hata hivyo, mwalimu huyo alipoulizwa kuhusu kingereza cha harmonize iliyofanyika hivi karibuni alipokuwa Nigeria alijibu na kusema kuwa mambo haya kwenda vizuri kidogo lakini kila kitu kitakuwa sawa.

Alishawahi kunipa deal nikafundisha WCB wote, nilimfundisha Momo,Nikamfundisha Harmonize,Rich , Rayvany.kuhusu mahojiano ya harmonize ni kwamba darasa lilikuwa gumu kidogo.

Sallam k Atoa Siri ya Diamond Kununua Viewers Youtube

 

Katika ukurasa wake wa instagram, Diamond Platinumz aliweka picha akiwa katika makao makuu ya youtubu ambapo diamond wikiend hii alikuwa nchini mareknai alikopata  nafasi pia ya kutembelea huko.

Katika picha aliyokuwa ameweka, Diamond alindika kuwa amefanikisha kikaa na watu wa you tube lakini baada ya picha hiyo katika upande wa maoni alikuja Sallam k na kuandika kuwa  wanamjua kazi yake ni kwenda huko na kununua viewers na hiyo so siri kwa sababu wanamjua.

Ikiwa ni kwa muda sasa wasanii wa WCB wamekuwa wakituhumiwa kwa kufanya hivyo, bado haijulikani kama Sallam k aliandika hivyo kama utani kutokana na maneno mengi yaliyowahi kusambaa katika mtandao wa kijamii kuhusu tabia hiyo ya Diamond.

 

Diamond Aahidi Kubadilisha Maisha ya Wasanii.

Mwana muziki Diamond Platinumzamefunguka na kuwahakikishia wasanii wote watakao pata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha la Wasafi Festival linaloaanza mwaka huu kwamba atawapa ela nzuri na kwamba atajitahidi kuyainua maisha yao kupitia hilo.

Diamond ameyasema hayo alipokuwa akizindua chaneli ya wasafi tv katika kingamuzi cha star time  jijini dar june 19 mwaka huu na kupata fursa ya kuongea na waandishi wa habari.

Diamond anasema kuwa tamasha hilo halina haja ya kuua au kushindana na matamasha mengine yoyote yaliyowahi kuanzishwa huko nyuma,lakini lina lengo la kuinua wasanii na kutoa burudani.

Tamasha hili litakuwa likifanyika kila mwaka lakini nitakuwa nina hakikisha kila msimu unapoisha wasanii wanakwenda nje ya nchi au wanaanzisha mradi kutokana na kile wanachokipata.

Tunaomba makampuni yajitahidi kujitokeza ili kutusapoti vijana ili kutia chachu katika tamasha hili liwe na manufaa kwa vijana wanapopata malipo .

Alichoandika Rama Dee Kuhusu Diamond

Msanii wa Muziki Rama Dee ameonyesha hisia zake za furaha kwa mafanikio makubwa yanayoendelea katika tasnia ya muziki hasa pale anapoona kuwa kuna wasanii wamekuwa huru kuzungumza kile wanachokiona katika tasnia.

Maneno ya Rama Dee yanakuja baada ya kuona leo msanii Diamond Platinumz akiongea na waandishi wa habari na kuzngumza mengi na kumpongeza Diamond kuwa msanii wa kwanza kuwa huru na kuongea kile anachotaka kuongea katika media.

msanii wa kwanza Tanzania kupata freedom,nasikia furaha kuona msanii anaongea kama msanii na sio mtumwa wa fikra,big up Nasibu , mungu akuongezee maisha.

Diamond akiwa kama msanii anaetambulika afrika na karibia dunia nziam sasa , amekuwa msanii wa kuigwa na kufungua njia za wasanii wengine wengi bongo na kila mmoja amekuwa akifurahia mafanikio hayo wakiamini kuwa ni mafanikio ya wengi.

 

Naogopa Kwenda Wasafi ni Ma-freemasons-G.Bway

Msanii G-bway kutoka arusha amefunguka na kudai kuwa hata siku moja hawezi kufikiria kwenda katika level ya wasafi kwa sababu hawaelewi wasanii wa kundi hilo hata bosi wake akiaamini kuwa wanajishirikisha na mambo ya kishirikina.

G-bway ambae kwa sasa hana uongozi wowote zaidi ya kusaidiwa katika kazi zake za muziki na afisa wa utamaduni mkoa wa arusha anaejulikana kama meneja maneno anasema kuwa anajua kuwa kuna manejement nyingi lakini hawezi kwenda wasafi kwa sababu wapo kama ma-freemasons.

kwa wasafi naogopa kwenda kwa sababu wasafi mi naona kama ma-freemasons vile,ukangalia hata style zao wanazokaa, jinsi wanavyovaa kwa mfano ukiangalia kamabraza mond , yule braza ni muislamu lakini ukimuangalia muda mwingine unaona kavaa msalaba.

Maoni ya Viongozi Kuhusu Mkono wa Eid wa Diamond Kwa wana Tandale.

Wiki iliyopita kulikuwa na sikukuu ya Eid , sikukuu ambayo ilimaliza mfungo wa Ramadhani kwa waislamu Duniani, msani mkubwa tanzania na Duniani kote aliamua kutoa mkono wa  Eid na kuamua kusherekea sikukuu iyo na watu aliokuwa nao huko tandale.

Watu wengi walifurahi na kumuomba mafanikio kwa kila analofanya hasa kwa kitendo cha kuamua kukumbuka kwao, lakini baadhi ya viongozi wa dini wansema kuwa hiyo haikuwa sawa kwa sababu Diamond alijionesha sana hata kurekodiwa na vyombo vya habari.

Moja ya mashehe katika msikiti wa makongo juu alisema’sadaka siku zote inabidi itolewe kwa siri na ndio maana tunasema ikiwezana unatoa kwa mkono wako wa kulia basi ue wa kushoto haupaswi kujua,mimi nimeona alichofanya diamond lakini kiimani hayuko sahihi kwa sababu pale kuna wengi watamsifia lakini kwa mungu hana chake , ile tunaita ria.’

       Icho ndo alichofanya Diamond, kwamba hangekuwa amefanya kwa siri na kubabatizwa na waandishi hapo ingekuwa sawa lakini unaona kabisa mpaka televisheni yake ilikuwepo.

Kiongozi mwingine wa dini ana sema”sio huyo diamond tu , sasa hivi wasanii wakienda hata katika vituo vya watoto yatima wanakusanya  wana habari wanaweka picha katika mitandao ya kijamii , angepata thawabu sana kama swala lile la kuwapangisha watu foleni lingekuwa kwa siri.

 

 

Diamond na Familia Yake Wagusa Familia Nyingi Siku ya Eid

Msanii mkubwa wa bongo fleva Diamond Platinumz  wikiend iliyopita alifanya jambo lilioshukuriwa na watu wengi baaada ya kukusanyika na familia nyingi katika mtaa alikulia jijin dar huko tandale na kutoa mkono wa Eid kwa kila aliefika nyumbani kwao hapo.

Diamond na familia yake na watu kutoka ofisini kwao waliamua kufanbya hivyo ikiwa i moja ya njia ya kujiweka karibu na watu aliokuwa akiishi nao pindi akiwa na maisha ya chini na anaamini kuwa wanawake na mtaa huo ndio waliomlea tangu akiwa mtoto na kwa kiasi flani waliona alivyokwa akisota.

 

 

 

Daimond akiwa anaingia mtaani kwao.

Diamond akigawa mkono wa Eid.

 

Wananchi katia mtaa huo wamefurahi na kutoa shukran nyingi kwa Diamond na familia yake huku wengi wakimuombea kuzidi kufanikiwa zaidi ili kuendelea kuwakumbuka.

Nyumba ya Hamisa Yaleta Utata, Yasemekana ni ya Kupanga.

Inasemekana kuwa hiyo inaweza kuwa ni tabia ya msanii Diamond Platinumz kuwa na show-off kila anapofanya kitu na kuwaamisha watu kuwa kila anachokifanya  ni mali yake kumbe sio kweli, hii inaendelea kuonekana baada ya ku-trend sana katika mitandao ya kijamii kuhusu nyumba ambayo inasemekana kuwa ni nyumba ambayo Hamisa amenunuliwa na Diamond lakini habari za chini chini zinasema kuwa nyumba hiyo sio ya kununua ni ya kupanga.

katika moja ya kurasa za  instagram inayojulikana kama dalali kiongozi imeonyeshwa nyumba hiyo ilipokuwa katika matangaza ya kupangishwa hapo kipindi cha nyuma na hata kutajwa kiasi cha kupangishwa kwa nyumba hiyo.

Mara Nyingi Tuzo za Tanzania Zina Uchonganishi

Mwanamuziki Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba amekuwa akipigania sana watuwa tanzania kupata tuzo lakini kwake amekuwa akihangaika sana kupata tuzo za nje na kuzileta ndani kwa sababau anaona kuwa tuzo za Tanzania zinakuwa na uchonganishi sana kwaio huwa  hana mpango sana na tuzo za Tanzania.

Diamond aliongea hayo usiku wa jana alipokuwa amehudhria utoaji wa tuzo za MO awards zenye lengo la kutoa hamasa kwa club ya simba na watendaji wake pamoja na wachezaji pia.

Mara nyingi nimekuwa nikipigania tuoz kutoka nje kuja tanzania, maana tuzo za tanzqnia zina uchonganishi sana,lakini kwa hili la simba litakuwa ni kama changamoto kwa watu wengine na club zingine pia lakini hii inatia motisha sana kwa watu kufanya vizuri.

Hata hivyo katika hafla hiyo Diamond alibahatika kutoa tuzo kwa haji manara aliyekuwa moja ya washindi wa kipengere cha mnahasishaji bora wa mpiram hata hivyo Diamond amesisistiza kuwa nhata yeye ni simba damu.

Mrema Amfagilia Diamond Platinumz.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Mrema amesema msanii wa Bongo Flava anayemfuatilia kwa sana ni Diamond Platnumz.
Ameeleza sababu ya kumfuatilia muimbaji huyo ni kutokana na kujituma kwake na muziki wake unavutia.
Namfuatilia sana Diamond, ni kijana mdogo, muimbaji mahiri, yaani Diamond asaidiwe naona hatima yake katika maisha yake na nchi yetu atatufikisha mahali pazuri. Kwa muziki wake unakosha roho, hata sisi wazee, mimi naridhika sana,” Mrema ameiambia Times FM.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa serikali kuwa karibu zaidi na wasanii, hata hivyo amesema anaziona jitihada za Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe za kukutana na wasanii kila mara hasa pale wanapopata matatizo na kuwasaidia.

Mr. Blue Anyoosha Mikono kwa Diamond Platinumz.

Kwa muda mrefu msanii Kheri Sameer (Mr Blue) amekuwa yupo kwenye bifu zito na Diamond Platnumz Simbaaaaaaaa ,mara kwa mara Blue amekuwa akimponda Diamond Platnumz lakini waswahili husema jibu la mjinga ni kumkalia kimya tu ipo siku ata erevuka,na siku zote kama unajua unajua tu watu watapiga kelele mwisho wa siku watanyoosha mikono bila kupenda.

Sasa bhana Diamond a.k .a mzee wa minyoosho anazidi kuwanyoosha tu watu , na mmoja mmoja anaanza kunyooka , alianza kunyooka ,Richi Mavoko,akafuatia H-baba ,akaja Baraka the Prince sasa zamu ya Mr Blue naye kanyooka bila kupenda ,Ha ha ha ha team Kiba inazidi kusambaratika tu, hapo amebaki Tundaman na adui kuu Ally Kibanio

Yani Blue kanyooka haswaaa ,tena kasindikiza na Caption Mungu ni mwema maana alijijua alichokuwa anakifanya ni kitendo cha kijinga ,kapitwa na fursa nyingi kwa kitendo chake cha kumchukia Diamond.

Mapya Yaibuka Gari Jipya la Diamond

Inasemekana kuwa siku chache baada ya zari kuweka gar lake jipya katika mitandao ya kijaMii, mzazi mwenzie pia Diamond Platinumz alionekana ku-panic na kuamua kurushia ndinga jipya katika mtandao wa kija ii ili kuonyesha kwamba na yeye analipiza kisasi ka mwanamke wake huyo ambae wameachana.

Lakini siri imekuja kufichuka na kusemekana kuwa kumbe gari hiyo aliyoweka Diamond na kusema jipya wala halikuwa jipya bali gari hiyo ilibadilishwa tu muundo na muonekano na moja ya gereji yenye utaaramu huo jijini Dar.

Baada ya Diamond kuanika ndinga hiyo, kampuni ya gpl waliamua kuwatafuta kampuni waliotengeneza gari hiyo na ndipo walipokiri kuwa ni kweli kuwa walikuwa wakibadilisha muonekano wa gari hiyo huku wakigoma kutaja thamani ya matengenezo hayo.

Kampuni hiyo walisema kuwa kutaja bei ya mambo yote waliyofanya kwenye gari hilo ni kama kutoa siri ya mteja wao wakati sio makubaliano ya kampuni na wateja wao.

kumekuwa na ushindani mkubwa kati ya Diamond na Zari baada ya kuachana hasa katika upande wa utajiri na umiliki wa mali.

Diamond Anafanya Kazi , Sijui Kama Analala:-Master Jay

Mtayarishaji na mzalishaji wa nyimbo mkongwe Tanzania , Master jay amefunguka na kusema kuwa washngae mafanikio ya Diamond kwa sababu yanatokana na juhudi zake mwenyewe na kujituma kwingi bila kuchoka wala kukataa tamaa.

kwa wale wanaomjua diamond kwa ukaribu wanajua kabisa kuwa hivi vitu anavyopata sasa havijaja kirahisi, ni mtu ambae anafanya kazi, sijui hata kama analala , anafanya kazi kwa bidii sanaa,kwaio hata haya matunda tunayoyaona leo ni mafanikio ya juhudi zake.

Kwaio sasa hivi mimi ninaona anaanza kupata matunda ya kazi zake na ninafurahi sana na nina mshukuru Mungu.

Ukiachana na kazi za musiki ambazo diamond amekuwa akifanya lakini pia ameingiza bidhaa sokoni kama paerfum na karanga lakini pia sasa hivi yuko na wasafi Tv