Malkia wa Taarab Khadija Kopa amwomba Diamond kusign mwanawe katika WCB

Diamond alishirikiana na Khadija Kopa kutoa ngoma kali sana unaoitwa ‘Nasema Nawe’. Wimbo huo ulipendwa sana na mashabiki kwasabubu ya wanawake wanaotingiza makalio zako kwenye video.

Akizungumza na Ayo TV, Khadija alisema Diamond atatambulisha mwanawe kama msanii wa Wasafi Classic Baby (WBC) wakati wowote.

Khadija Kopa akitumbuiza

Malkia huyo wa Taarab aliambia Ayo TV kuwa alimwomba Diamond kusign mwanawe na bado anangoja jibu kutoka kwake.

“Nilikwenda kwa Diamond Platnumz nikamwambia amsikilize mwanangu akamsikiliza na anasema amemuelewa yuko anasubiria kwani subira yavuta heri ndio riziki yake mwanangu kuimba kama isingekuwa riziki yake basi angepata label nyingine kwahiyo tutegemee muda wowote mwanangu kusainiwa WCB,” Khadija Kopa alisema.

 

Anavyo onekana Diamond baada ya kunyoa rasta zake (Photos)

Diamond Platnumz sasa hana rasta tena, hit maker huyo wa ‘Marry You’ aliamua kunyoa kwa ajili ya album yake ambayo anataka kuipromote.

Baba Tiffah alisema kuwa anatengeneza mwili wa kutolea album yake mpya kabla aanze kuipromote.

“Sasa hivi naelekea kutoa album yangu…namalizia kwa hiyo narudi kutengeneza mwili wa kutolea album alafu nianze kufanya promotion ya album yangu mpya…”Diamond aliandika kwenye Instagram.

Diamond kabla ya kunyoa rasta zake

Kuhusu kunyoa rasta yake, Diamond alieleza kuwa nyimbo zake kwenye album yake mpya zinatoa hisia ya huruma kwa hivyo ilimbidi anyoe rasta zake ile aweze kuonyesha hisia ya huruma.

“Nywele zangu nazitoa muda sio mrefu kwasababu nashoot ngoma zangu za huruma huruma zile…ukishoot na rasta unaonekan,” Diamond aliongezea.

Diamond baada ya kubadilisha muonekano wake wa nywele

“Sikuwahi kuwa mshabiki wa Diamond” Naibu Waziri wa Afya Hamis Kigwangalla atoa maoni yake kuhusu Chibu Perfume

Diamond alizindua manukato yake “Chibu Perfume” siku chache zilizopita. Staa huyo wa Bongofleva alifanya uzinduzi mkubwa, aliwaita wanahabari alipozindua Chibu Perfume.

Hatua hio ilifanya Diamond kutawala vichwa vya habari, Naibu Waziri wa Afya Hamis Kigwangalla ni miongoni mwa watu walitoa maoni yao kuhusu uzinduzi wa Chibu Perfume.

Bwana Kigwangalla alikiri hakuwa shabiki wa Diamond hapo mwanzoni lakini alianza kupenda muziki wake hivi karibuni.

Alimsifu Diamond kwa kuwa mwanamuziki timam na mwekezaji ambaye ni mfano mwema kwa vijana nchini Tanzania.

“Sikuwahi kuwa mshabiki wa msanii huyu kijana @diamondplatnumz, kama nilivyosema hapo nyuma kidogo, japokuwa nimekuwa nikifuatilia na ku-enjoy muziki wake; Ila toka nimeanza kumfuatilia nimegundua kuwa, this young man is not only a good entertainer, but also a talented entrepreneur and businessman. He does business in music, he does a business of entertainment. Sasa naona kupitia kipaji chake cha ujasiriamali, naona ameamua kuwa muwekezaji, an investor! This is incredible. Keep stepping up your game son, that’s the way to do it! Hakika wewe umetoka #NjeYaBox, na Mungu akuongoze ubaki huko huko juu, usishuke! I wish wasanii wenzako pia watoke nje ya box kifikra, wafanye biashara kwenye vipaji vyao, wageuze changamoto kuwa fursa, waache kulalamika, wapige kazi tu! #HapaKaziTu! Kwa sababu nyie watu mashuhuri mkigeuza crowds zenu kama chanzo cha solo la bidhaa zenu, kwa hakika mtafanikiwa sana! Changamoto kwenu wadogo zangu..” Hamis Kigwangalla alisema.

Jah Prayzah aingia studio na Harmonize baada ya kutoa collabo kali na Diamond

Kila mtu anakumbuka ‘Watora Mari’ – wimbo huo bado ni hit kubwa mieze nane baada ya kuachiliwa. Msanii Jah Prayzah alishirikiana na Diamond kutoa wimbo huo.

Umaarufu wa Jah Prayzah ulienea barani mzima baada ya kumhusisha Diamond kwa wimbo wake. Msanii huyo kutoka Zimbabwe alinyakulia tuzo ya Listener’s Choice Awards ya MTV MAMA mwaka jana.

Jah Prayzah sasa imeingia studio na Harmonize – ujumbe aliouandika kwa mtendao wa Instagram unashiria ujao wa collabo yake na staa huyo kutoka WCB Wasafi.

“In the studio again with another Tanzanian big star @harmonize_tz .Zimbabwe neTanzania ?,” Jah Prayzah aliandika.

 

Diamond aendelea kuwa kicheko mitandaoni kwa kuwa hawezi ongea kingereza

Diamond kwa kweli hawezi ongea kingereza ata kwa hii miaka yote ya kuwa star.

Hii ilibainiwa wazi kwa post zake kwenye instagram akitayarisha watu kwa uzinduaji wa Chibu perfume unaotarajiwa kufanyika kesho.

Also read: Tazama hii gari ya kifahari Diamond Platnumz alinunua pale kwake South Africa

Hapo ndipo alipofanya makosa mengi ya lugha iliyofanya awe kicheko kwa wengi.

Na hata baada ya hilo, bado anaendelea kufanya makosa.

Ebu tazama hapa:

 

 

Diamond araruliwa kwa kuandika Kiingereza kibovu kwenye Instagram

Diamond hana pakuficha uso wake baada ya kutumia Kiingereza kibovu kutangaza kuwa amezindua manukato yake ambayo ataanza kuuza hivi karibuni.

Staa huyo wa Bongo flava aliongelea kuhusu ujio wa Chibu Perfume akitumia Kiingera ambacho hakikuzingatia sheria ya msamiati ya lugha hio.

“I feel incompleted when am on any outfit, without wearing @chibuperfume !….. @chibuperfume by Diamondplatnumz comming out this week!” Diamond aliandika.

Maneno ‘incompleted’ na ‘comming’ ambazo Diamond alitumia kwa sentensi yake ilikua imeandikwa vibaya – hazina maana yoyote katika Kiingereza.

Wanaofahamu Kiingereza vizuri walimrarua Diamond kwenye comments zao. Wengi walimwambia atumie tu Kiswahili badala ya kujiaibisha na Kiingereza kibovu.

 

Nay Wa Mitego: Mwambieni Diamond pia awe mpole kwasasa alee watoto

Nay Wa Mitego amezua hisia tofauti baada ya kumpasha Rich Mavoko ujumbe ambao alitaka uwafikie wasanii wote wa Wasafi Diamond akiwepo.

Rich Mavoka aliandika kwa ukurasa wake wa Instagram kutambulisha wimbo wake mpya ambayo bado haujaachiliwa kwenye redio na runinga.

“Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii ? #Showme” Rich Mavoko aliandika.

Nay Wa Mitego alimjibu haraka, alimwambia asubiri mbaka mwakani 2018 ndo watoe nyimbo (wasanii wa Wasafi.) Alimwambia apitishe ujumbe kwa Diamond ambaye alimtaka alee watoto kwanza.

Nay Wa Mitego na Diamond

“”NAOMBA MUENDELEE KUSUBILI, MAY BE MPAKA MWAKANI 2018, NDO MTAANZA KUJISHUGHULISHA NA MASWALA YA KUWAIMBIA WANA NCHI. MWAMBIENI NA BABA YENU PIA AWE MPOLE KWASASA ALEE WATOTO. KAZI TULIYO NAYO IKIENDA SAWA TUTA WARUHUSU MUENDELEE KUBURUDISHA WANA NCHI. TUNATAKA MAMBO YAENDA SAWA KWANZA✊?. Wimbo wetu wa TAIFA ni #Wapo LINK ON MY BIO☝”,”Nay Wa Mitego aliandika.

Ujumbe wa Nay Wa Mitego hata hivyo ni utani tu, Diamond ni rafiki wake mkubwa ambaye alishirikiana naye kutoa ngoma kali sana ‘Muziki Gani’.  Si mara ya kwanza wawili hao kutupiana vijembe kupitia mitandao.

“Usinigeuze maji kesho, mana nakujua mzee wa single touch ukimuamulia mtu” Diamond amkejeli Askofu Gwajima

Beef kati ya Diamond na Askofu Gwajima ilianza baada ya askofu huyo kudai kuwa Diamond ni mshirika wa dini la kishetani la Freemasonry.

Askofu huyo alisema kuwa Diamond anamuimba kwa nia mbaya, aliapa kuwa angegeuza staa huyo kuwa maji lakini alibadilisha nia yake baada ya Diamond kumwomba msamaha.

“Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba?….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…

“Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi??

“Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho ?, mana nakujua mzee wa single touch ukimuamulia mtu……. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima???” Diamond aliandika kwa Instagram.

Askofu huyo alimwonya Diamond tena alipokuwa akihubiria maumini wake Jumapili iliyopita, alisema kuwa Diamond akirudia kosa lake hatamsamea tena. Tazama video hio hapo chini:

 

Diamond akutana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ofisi ya Wasafi kuzungumzia wizi wa kazi za wasanii

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alikua mgeni wake Diamond Platnumz jana Aprili 4. Makonde alialikwa katika ofisi ya Wasafi na staa huyo wa muziki.

Afisa huyo wa police alifanya kikao na wadau wakuu wa Wafasi, walizungumzia wizi wa kazi za wasanii na mambo kadha wa kadha zikiwemo changamoto mbalimbali.

Tazama kikao hicho kati ya Wafasi na Paul Makonda kwenye video hapo chini:

Meneja wa Diamond Babu Tale amrarua mmiliki wa kampuni ya Global Publishers Eric Shigongo

Eric Shigongo alianza mgogoro na Wafasi alipodai kuwa Diamond anaingizwa shimoni na Naseeb Abdul, Babu Tale na Salaam.

Soma pia: “Diamond anapelekwa kwa shimo na watu watatu” Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers aonya

Babu Tale amemjibu Eric Shigongo kwa Instagram:

“Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kwenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya… baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo insyagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako…

“Siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata..ila kesho ukawaambie vizuri waamdishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wengine na watu mbalimbali…

Babu Tale

“Tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu… Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond… ila sie kaa kimya… na kujifanya unazungaa eti unatushauri… kweli mtu unasema unampenda unamshauri instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?… Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini?…na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya Harmonize DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi “kupost tumepost… ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilika na kutak asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa…tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa…

“Hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na mashabiki zao hii ndio kuwaeka wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe… mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula madawa…yote kutafuta sababu msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kumbomoa msanii kupitia magazeti yako…tafadhali heshimu heshima yetu kwako…”Mh Magufuli tafadhali ulipo kaza legeza, ona wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoot vidogo vyao….”

Eric Shigongo na Diamond

 

 

Saida Karoli aeleza kilichompa nguvu mpya ya kurudi kwenye muziki baada ya kustaafu

Mwimbaji mkongwe Saida Karoli anayejulikana kwa hit yake ‘Maria ya Salome’ amerejea kwenye sanaa ya muziki baada ya kupotea kwa miaka kadhaa.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa iliopita, Saida Karoli alisema kuwa kurejea kwake kwenye muziki ulifanikishwa na Diamond na Belle 9.

Anadai kuwa Belle 9 na Diamond walimpa nguvu mpya ya kurudi kwenye muziki baada ya kuachia nyimbo zao walizotumia baadhi ya vitu kutoka kwenye wimbo wake wa ‘Maria ya Salome’.

“Nilishatamani kuacha muziki na nilishawahi kuhamisha baadhi ya vitu vyangu kurudi kijijini na ndiyo kipindi hiko hiko Belle Nine na Diamond walitoa nyimbo ya Chambua kama karanga, wakanirudisha maana ilikuwa safari kabisa,” Saida Karoli alisema.

Diamond and Saida Karoli

 

Tazama jinsi Diamond alivyobaki akiduwaa baadaya ya Zari kupata vipuli visivyo vyake chumbani mwao

Diamond alinaswa na mke wake Zari Hassan walipokuwa wakionyesha bidhaa za Danube kwenye tangazo.

Tangazo hilo lilikua linaonyesha bidhaa za Danube zinazouzwa GSM Mall jijini Dar es Salaam. Diamond na Zari walitumiwa kuonyesha bidhaa hizo.

Hit maker huyo wa Marry Me alibaki akiduwaa baadaya ya Zari kupata vipuli visivyo vake chumbani mwao katika tangazo hilo.

Kiswahili cha Zari kimeimarika sana; Zari, mzaliwa wa Uganda, alizungumza Kiswahili mufti alipotokea kwenye tangazo hilo.

“Diamond anapelekwa kwa shimo na watu watatu” Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers aonya

Eric Shigongo, mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, amekiri kuwa Diamond ni mfano mwema wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi Tanzania na ata duniani kote.

Shigogo amesema hit maker huyo ameweza kuvuka vizingiti vyote maishani na kuwa msanii wa kutajika nchini Tanzania na ata barani.

Lakini Shigogo ameonya kuwa Diamond anaelekea shimoni. Mmiliki huyo wa Global Publishers aliandika barua yenye ujumbe kwa Diamond kupitia mtandao wa Instagram;

“Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo.

“ Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha. Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania. Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. BRAVO! LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake. Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE. Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti.”

Eric Shigongo na Diamond

 

Diamond na Belle 9 waamua kumnurusu Saida Kalori

Baada ya kutoa ‘Salome’, Diamond alikemewa na watu wengi walio dai kuwa alitumia wimba wa Saida Kalori bila ya msani huyo kunufaika.

Saida Karoli anatajika kwa hit yake ‘Maria Salome’ ambayo ilimpa publicity sana nchini Tanzania na hata Afrika Magharibi na nchi zingine barani.

Diamond na Belle 9 sasa wameamua kumnurusu Saida Kalori, wawili hao watashiriki katika albamu yake itakayoitwa ‘Naamka’.

Diamond na Saida Kalori

Akilonga na Showbiz, Saida alisema kuwa anamshukuru Mungu amerudi tena kwenye muziki na wasanii hao wamempa nguvu ya kufanya vizuri katika albamu

“Nimeamka tena jamani nashukuru nimebebwa na wasanii wenzangu Diamond na Belle9 ambao nimewashirikisha kwenye nyimbo zangu ambazo zipo kwenye albamu itakayotoka hivi karibuni,” alisema Saida.

 

Wasafi.com yavuka border! Diamond azuru Uhispania kukutana na waekezaji wanaotaka kuekeza wasafi.com

Diamond Platnumz alizindua tovuti yake ya kuuzia muziki unaoitwa Wasafidotcom. Super star huyu amekuwa akifanya mikutano ofisini kwake na wasanii mbalimbali, kuzungumza namna ya kufanya nao kazi kwenye mradi huo. Tayari amekutana na wasanii kama Ben Pol, Barnaba, Chege na hata Willy Paul Kutoka Kenya.

Msanii huyo wa muziki ya injili – Willy Paul alikubaliana na Diamond kuweka muziki wake mpya na Alaine ‘I Do’ kwa tovuti Wasafi.com.

Diamond and Willy Paul

Jana Diamond alisafiri kuelekea Uhispania kufanya mazungumzo na waekezaji wanaotaka kuekeza wasafi.com.

Hitmaker huyo wa Marry You alisema kuwa atafanya kikao kifupi na waekezaji kabla ya kuelekea nchini Oman kufanya show yake.

“Kikao kifupi Nchini Spain kuhusu @wasafidotcom kabla ya show yangu mjini Muscat, Oman ijumaa hii… wadau natamani niwadokeze walau kidogo jinsi tasnia yetu iendapo huu mwaka…?? tafadhali msiache kuniombea?” Diamond aliandika kwenye caption ya picha yake.

Diamond amrai Ali Kiba kuweka muziki wake wasafi.com

Akiongea kwenye mahojiano ya kipindi cha 360 cha Clouds FM, Diamond Platnumz alikiri kwamba hana tatizo na Ali Kiba. Diamond na Kiba wamekuwa na beef zito sana kwa takribani miaka mitatu.

Diamond aliambia Clouds FM kwamba anaheshimu Ali Kiba, alifunguka na kusema kwamba uongozi wake uko katika mazungumzo na uongozi wa Ali Kiba ili Kiba aweze kuuza nyimbo zake kwenye mtandao wa wasafidotcom ambao ni mradi mpya wa Diamond.

Ali Kiba and Diamond TBT

Baadaye usiku kupitia akaunti yake ya Instagram, Ali Kiba aliandika caption zenye utata zilizotafsiriwa na mashabiki na wadau mbalimbali kuwa zimelenga kujibu maneno hayo ya Diamond Platnumz.

“Waambie Wasituzoee kabisa MAZOEA kuzoeana ?? @billnass #alikibaworldtour2k17 #KingKiba,” Ali Kiba aliandika.

Watu wengi wanaamini kwamba Diamond anahitaji amani na Ali Kiba kwasababu za kibiashara zaidi. Iwapo Ali Kiba atakubali kuuza wimbo zake wasafi.com, Diamond atafaidika zaidi kwasababu Ali Kiba ako na wafwasi wengi.