Hii ndo sababu Mheshimiwa Goodluck Mlinga anataka serikali kujenge sanamu ya Diamond

Mbunge wa Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga amesisitiza kuwa ni lazima serikali iwatambue wasanii wanaowakilisha Tanzania vizuri nje.

Mheshimiwa huyo alisema bungeni kuwa Diamond anastahili kujengewa sanamu kwasababu anawakilisha nchi vizuri kimataifa. Mlinga alipendekeza kuwa sanamu la askari posta Dar es Salaam liondolewe na kuweka hilo la Diamond.

Akiongea na Habari Xtra ya Times FM, Mlinga alieleza kuwa Diamond ni mmoja tu ya wasanii ambaye yeye anawapigania ili serikali iwatambue kwa kazi zao nzuri.

Mheshimiwa Goodluck Mlinga alisema

 

“Na sikumtaja Diamond pekee, niliwataja wasanii wengi kama wakina Mr Nice ambao wameiwakilisha Tanzania sana nje lakini mpaka leo hii wamepotea hawana alama, inakuwa hawawezi kuwahamasisha wasanii wengine, lakini tunapoweka alama kila msanii anapofanya vizuri tunahamasisha wengine na ndiyo utaratibu katika nchi za wenzetu. Kuna mchezaji mmoja wa mpira alitoka Kenya (Victor Wanyama) kuja Tanzania siku ya pili alipewa mtaa, sasa vile vitu ndio tunatakiwa tuvifanye kwa wasanii wetu wanaoibeba nchi. Sasa wewe fikiri mtu katoka nje ambaye anawakilisha nchi nyingine tunampa mtaa, lakini kwetu ni msanii gani alishawahi kuacha alama hata akapewa Barabara, hakuna!!!,” Mheshimiwa Goodluck Mlinga alisema.

Zari abadilisha jina la mtoto wake wa kike Tiffah

Kifungua mimba wa Diamond amebadilishwa jina na kupewa jina la mamake, Zari alidhibitisha haya kwenye mtandao wa Instagram.

Mtoto wa kike wa Diamond anajulikana kama Tiffah Dangote, jina hilo la pili ni ya babake ambaye alijibandika ‘Dangote’ kwasababu ya mafanikio yake kimuziki.

Hata hivyo Zari aliwajulisha watu kwa Tiffah sasa anaitwa Tiffah Hassan na sio Tiffah Dangote. Alisema hayo kwenye comment section kwa Instagram baada ya mtu kuita mtoto wake Tiffah Dangote.

Hatua ya Zari kubadilisha mwanawe jina umezua uvumi kuwa Zari amekosana na Diamond ndo sababu aliamua kutoa jina la Diamond (Dangote) na kumpa jina yake (jina Hassan).

Wambeya wanasema kuwa Diamond na Zari walikosana kwasababu Simba hajaenda kumwona mama mkwe wake ambaye alilazwa hospitalini huko Afrika Kusini. Na mbaka sasa Diamond hajamtumia mama mkwe wake salamu za heri.

 

 

Yemi Alade akubali wimbo mpya wa Diamond

Diamond Platnumz ameachia nyimbo tatu kwa muda wa wiki mbili, nyimbo hizo ni; ‘I Miss You’, ‘Fire’ akimshirikisha Tiwa Savage na ‘Eneka’.

Kati ya hizo nyimbo tatu mpya ‘Eneka’ ndo imemfurahisha sana Yemi Alade. Mwimbaji huyo alichangamia wimbo huo kwasababu Diamond aliimba kwa lugha ya Igbo.

“Omg !you are singing in IGBO ?? @diamondplatnumz,” Yemi Alade aliandika kwenye video ambayo Diamond ameiweka kwenye mtandao wa Instagram

Tazama wimbo wa ‘Eneka’ hapo chini:

Diamond azua utata kwasababu ya zawadi aliyompa Professor Jay kwenye harusi yake

Professor Jay na mpenzi wake Grace Mkonja walifanya harusi wikendi iliyopita katika kanisa la Katoliki la St. Joseph jijini Dar Es Salaam.

Diamond alijiunga na shamrashamra za harusi ya Professor Jay kwenye ukumbi wa maakuli, staa huyo wa Wasafi aliwatumbuiza wageni kabla ya kumpa Jay zawadi aliyoleta.

Baba Tiffah aliwashangaza wengi kwa kumpa Professor Jay boksi tano za Diamond Karanga na manukato yake ya Chibu perfume kama zawadi.

Diamond akimpea Professor Jay zawadi zake

 

“Nimekuletea hizi boksi unajua uko kwenye ndoa, ndoa nayo inataka uongeze mwili ili watoto watoke wengi,” Diamond aliambia Professor Jay akimpa zawadi zake.

Tazama video hapo chini uone jinsi Diamond alitumbuiza wageni kwa harusi ya Professor Jay:

Diamond Platnumz aeleza kwanini amechelewesha uzinduzi wa headphones zake

2017 ilivyoanza Diamond alisema atazindua bidhaa kadhaa na alianza na manukato ‘Chibu Perfume’ kisha hivi karibuni alianza kuuza karanga – ‘Diamond Karanga’.

Staa huyo wa Wasafi sasa anafuata nyayo ya wasanii wa kimataifa kama Dr. Dre na 50 Cent walioingia kwenye biashara ya headphones.

Diamond alitangaza ujio wa ‘Chibu Beats’ lakini hakuweza kuzindua headphones hizo kwa sababu ya umiliki wa jina ‘beats’.

“Katika usajili wa Chibu Beats jina lilileta matatizo kidogo, ilikwamisha hapo kwa sababu neno beats mtu kashalisajili dunia nzima mtu mwingine asilitumie neno la beats, siunajua ni la Dre. Kwa hiyo tunaweka namna nyingine ambayo itakuwa nzuri, zitatoka zimeshakuwa tayari mpaka sampo, tumeshasikiliza ni fresh sound hatari” amesema Diamond akiwa katika kipindi ya XXL ya Clouds FM.

Diamond amenunua helikopta?

Uvumi umezuka mtandaoni kuwa Diamond Platnumz sasa ni mmiliki wa helicopther ya aina AgustaWestland A109S inayo gharimu TZS bilioni 14.5.

Baadhi za vyombo vya habari vilianza kusambaza habari hii baada ya Diamond kuonekana amepiga picha akisimama mbele ya helikopta hio.

Ukweli wa mambo ni kuwa ndege hio inamilikiwa na Akagera Aviation – kampuni ya ndege ya aina ya helikopta ambayo iko jijini Kigali.

Diamond alibebwa na ndege hilo linalomilikiwa na Akagera Aviation baada ya kufika nchini Rwanda. Baba Tiffah alikua anatoka Kongo ambapo alitumbuiza mashabiki jijini Goma.

Tazama video hapo chini uone jinsi Diamond aliingia Rwanda akitoka Kongo:

Diamond apigwa busu la kilazima na shabiki Rwanda

Diamond Platnumz alishambuliwa na shabiki mwanamke ambaye alimpiga busu la kilazima na kumpapasa akiwa kwa stage Kigali.

Hit maker huyo wa ‘Fire’ alikua Rwanda akiwatumbuiza mashabiki wake katika tamasha la Rwanda Fiesta ambalo lilifanyika jijini Kigali Jumapili iliyopita.

Tukio la shabiki kumbusu Diamond lilifanyika baada ya muimbaji huyo kuwaita mabinti warembo ambao wako na makalio nzito nzito kwa stage ii wacheze na yeye alipokua akiimba wimbo wake ‘Nasema Nawe’.

Mrembo aliyempiga busu la kilazima na kumpapasa Diamond alikua miongoni mwa wanadada ambao walikua kwa stage wakitingiza makalio zao.

Tazama video hapo chini:

Diamond, Victor Wanyama wamtakia AY heri ya siku ya kuzaliwa

Rapa Ambwene Allen Yessayah maarufu kama AY anasherekea siku ya kuzaliwa kwake leo Julai 2017. AY amefikisha miaka 36 leo.

Mastaa wengi wamemtakia AY heri ya siku ya kuzaliwa kwake, rafiki wake wa karibu Victor Wanyama alikua miongoni mwa wale waliomtumia jumbe mapema.

AY na Victor Wanyama

“Happy bday big boss @aytanzania have a good one bro,” Victor Wanyama aliandika.

Diamond na Rayvanny pia walimtumia AY jumbe:

“Big Birthday wish to Msoja wange @jahprayzah and my Legend Brother @aytanzania …. Long Life!!” Diamond Platnumz

“HAPPY BIRTHDAY KAKA LAO @aytanzania Mungu Akupe maisha marefu yenye Mafanikio zaidi,” Rayvanny

 

Diamond aachia mini-documentary ya Papa Wemba

Diamond alishirikishwa na Papa Wembo kutoa wimbo unaoitwa ‘Chacun pour soi’ (kila mtu kivyake). Papa Wemba hata hivyo aliaga dunia kabla hawajatoa video.

Papa Wemba alifariki akitumbwiza mashabiki jijini Abidjan huko Ivory Coast. Kifo chake cha ghafla kilisambaratisha mipango alizokuwa nayo Wemba na Diamond.

Diamond sasa ametoa mini-documentary ya Papa Wemba; video hio inaonyesha jinsi Diamond and Wemba walitunga wimbo wao ‘Chacun pour soi’.

Tazama video hapo chini:

Ujumbe wa Wolper kwa Diamond yawasisimua watu mtandaoni

Muigizaji wa filamu ya Bongo Jacqueline Wolper ametuma ujumbe kwa Diamond ambaye anasherekea siku ya kuzaliwa kwake leo.

Mrembo huyo alimsifu sana Diamond kwa kuinua sanaa nchini Tanzania kwa kuwasaidia wasanii wengine kunawiri kimuziki.

Jacqueline Wolper na Diamond

Ujumbe wa Wolper kwa Diamond uliwasisimua watu wengi mtandaoni, soma ujumbe huo hapo chini:

“Natamani kila mtu ajue roho yako nzuri na mchango wako ktk nchi yetu na jinsi gani umeweza kuinua wengine tunaowajua na tusiowajua pia!kijana mdogo lkn umeweza kukubalika nje na ndani ya nchi,kiufupi jina lako linaendana na roho yako una moyo wa almasi plus dhahabu unajua kula na vipofu mpk vilema ndo maana Mungu anakufungulia ridhiki zako..Wewe ni zaidi ya Almasi buana,Endelea kutuburudisha na mziki mzuri baba Tee….Happy birthday to you baba Nillan..Sema nn birthday yako bado sana mpk mwezi wa kumi mbali kapicha nako kameshawishi alafu maneno yangu pia yata expire???Nweiiz Nimejisikia tu ndugu zangu,sio mbaya na nyie mkifunguka kwa mazuri yake bwana Ngote #myboss”

 

Diamond aisifu umbo ya Wema Sepetu kwenye wimbo wake mpya

Uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na Wema Sepetu uliisha miaka kadhaa zilizopita lakini wawili hao bado ni marafiki wa kawaida.

Wiki moja iliyopita Diamond alizua utata baada ya kufunguka kuwa yeye na Wema bado huwa wanaongea na kukutana bila ya vyombo vya habari kupata uhondo wowote.

Soma pia: Diamond: Watu hawajui mimi na Wema Sepetu tunaongea sana lakini sio kwenye media

Diamond alisifu umbo wa Wema Sepetu kwenye wimbo wake mpya ‘Fire’ aliyomshirikisha mrembo kutoka Nigeria – Tiwa Savage.

“Sura Zari nadhani (ayaya) shape Sepetu Wema (ayaya) Ooh, I say, you fire baby oh (Fire fire fire fire) baby…” Diamond aliimba kwa wimbo wake.

Soma mistari ya ‘Fire’ hapo chini:

 

Diamond Platnumz – ‘Fire’ lyrics  Feat : Tiwa Savage

 

[Intro – Tiwa Savage]

It’s Tiwa Savage yeah

 

[Verse 1 – Diamond Platnumz]

Aga, you’re my sexy arose eh

Utamu zaidi ya varila

Yaani cookei wa mose

Kama pochi na ngawila

Sa nipatie dose eh

Kasi itaja nipalila

Usinifanyie ya jose eh

Tange tange kajamila

 

[Hook/Chorus – Diamond Platnumz]

I say, you fire baby

Fire fire fire fire baby

Fire oooh

(Fire fire fire fire) baby

Your love is sweet oh

(Fire fire fire fire) baby

Tamu mpaka mwisho

(Fire fire fire fire) baby

Ah ah, fire ooh

(Fire fire fire fire) baby

Fire baby (Fire fire fire fire) baby

Akicheka sura ya kitoto

(Fire fire fire fire) baby

Akinigusa kabisa ndo moto

(Fire fire fire fire) baby

 

[Verse 2 – Diamond Platnumz]

Wasi wasi ndo akili

Na kwako sina

Nyota njema alfajili

Kesha na uzima

Wanakesha kulitabiri

Pendu kuchina, baby

Tena wengine

Wakubwa mili

Watu wazima

Tanga kunani

Vurugu mechi mkwakwani

Mtoto hatari wakadada

Samba chumbani

Ye ndo messi uwanjani

Msiniibie simba, yanga

Nyuma kama sunami (ayaya)

Jinsi kunatetema (ayaya)

Sura zari nadhani (ayaya)

Shape sepetu wema (ayaya)

 

[Hook/Chorus – Diamond Platnumz]

Ooh, I say, you fire baby oh

(Fire fire fire fire) baby

Fire oooh

(Fire fire fire fire) baby

Akicheka sura ya kitoto

(Fire fire fire fire) baby

Akinigusa kabisa ndo moto

(Fire fire fire fire) baby

 

[Verse 3 – Tiwa Savage]

Let me tell you something ’bout this bobo oh (fire fire)

Love I get for him big pass orobo oh (fire fire)

Come and see the way the love dey make me to jaire (fire fire)

I swear na only him go fit enjoy my figure 8 oh

The way you shut my brain

I cannot explain

Fall for you with no shame

Baby walahi talahi eh (ayaya)

I love you no be lie eh (ayaya)

Your love dey sweet me die (ayaya)

I swear I no go lie

I say

 

[Hook/Chorus – Diamond Platnumz & Tiwa Savage]

I say, you fire baby oh

(Fire fire fire fire) baby

Aga, fire oooh

(Fire fire fire fire) baby

Your love is sweet oh

(Fire fire fire fire) baby

Tamu mpaka mwisho

(Fire fire fire fire) baby

Ah ah, fire ooh

(Fire fire fire fire) baby

Fire baby (Fire fire fire fire) baby

Akicheka sura ya kitoto

(Fire fire fire fire) baby

Akinigusa kabisa ndo moto

(Fire fire fire fire) baby

 

[Verse 4 – Diamond Platnumz & Tiwa Savage]

Tena waambie wasikunyatie darling

(Fire fire)

Hili penzi moto wakilivamia chali

(Fire fire)

Sa nipe kidogo (nitekenye)

Aga polepole (nitekenye)

Ah ah mpaka chini (nitekenye)

Ak inuka kidogo (nitekenye)

If I give it to you (nitekenye)

Will you give me sugar (nitekenye)

Oya give give (nitekenye)

Come and give me sugar (nitekenye)

Tiwa Savage aeleza vitu 3 kuhusu wimbo mpya aliyoshirikishwa na Diamond

Diamond alimshirikisha Tiwa Savage kwenye wimbo wake mpya ‘Fire’. Staa huyo aliachia wimbo huo kwa YouTube siku mbili zilizopita.

Tiwa Savage amefunguka kuhusu wimbo huo ‘Fire’, mrembo huyo alisema aliongea na Diamond kuhusu kushirikiana kutoa wimbo pamoja wakati walikutana wakifanya wimbo wa ‘Africa Rising’ ambayo iliwashirikisha Davido, Tiwa Savage, Diamond ,Micasa na Lola R.

Tiwa alisema kuwa walirecord wimbo huo ‘Fire’ miaka mitatu iliyopita. Alisema pia kuwa ‘Fire’ imeanza kushika Nigeria na barani nzima.

“2014 on the set of the Africa rising project in Ghana @diamondplatnumz and I talked about doing a collaboration and somehow it has taken 3 years but I am so excited that we finally made it happen. The result is another MASSIVE African record. No wonder the title of the record is #FIRE because it has started catching FIRE across the continent” aliandika Tiwa Savage.

 

 

Diamond: Ilibidi nipunguze kasi nyimbo zangu zisiwaue kina Harmonize, Rayvanny

Diamond ameeza kwanini alikosa kupata uteuzi wa tuzo la BET mwaka huu. Hit maker huyo wa ‘Marry You’ amewahi kuteuliwa mara mbili (2014 na 2016) kuwania tuzo hilo kwa kitengo cha Best International Act: Africa.

Akiongea katika kipindi cha XXL ya Clouds FM jana, Diamond alieleza kuwa alipunguza kasi yake kimuziki mwisho wa mwaka jana ili akuze kina Rayvanny, Harmonize na wasanii wengine.

Alieza kuwa msanii kupata uteuzi wa BET ni lazima aachilie nyimbo mfululizo na yeye aliwacha kutoa ngoma nyingi kwani kama angefanya hivyo nyimbo zake zingewaua kina Harmonize, Rayvanny na wengine.

“Mwakani lazima niingie, unajua kuna kitu kimoja…lazima uishi kwa plani na malengo…Na ukiangalia mwaka juzi mwishowe mbaka mwaka jana ulikua ni mwaka kuhakikisha nawashika vijana wa Kitanzania nao wasikike katika muziki. Na ili wasikike ilibidi mimi nipunguze kasi yangu kwasababu mimi naachilianga tu mawe, ilibidi nipunguze mawe niwashindirie tu hao mawe kina Harmonize, sijui kina nani Ray… wote…kwasababu nikiingia itakua ni mtafaruko. Ukiangalia mitaa ingine nimeanzisha lebo kuna nyimbo kama tatu, nyimbo zangu zingine ni mishirikisho tu. Ilibidi nipunguze kwasababu mimi najua nikiweka nyimbo na hawajakua na nguvu nyimbo zangu zitawaua. Na zile nomination zinataka mtu aachilie ngoma mfululu,” Diamond alisema.

Tazama mahojiano hayo hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=K_fRN6xFS8o

Diamond afunguka kuhusu mimba ya Hamisa Mobeto na vita yake na Zari

Ujauzito wa Hamisa Mobeto umezua utata kwani wambeya wanadai kuwa Diamond Platnumz ndo amempachika mimba mrembo huyo.

Wiki jana mbeya Soudy Brown alimpigia simu mamake Diamond Sanura ‘Sandra’ Kasim kudhibitisha kama ni ukweli kuwa Hamisa Mobeto amebeba mtoto wa Diamond tumboni.

Soma pia: “Napatana na Zari aliyeniletea watoto hao wengine siwajui” Mamake Diamond amkana Hamisa Mobeto

Akiongea katika kipindi cha XXL ya Clouds FM jana, Diamond alikana kuwa yeye ndo baba wa mtoto aliye tumboni mwa Hamisa Mobeto.

“Hizo zote ni za uongo, mama T pia anajua ni story ya uongo. Naskia kwamba ni mjamzito, sasa mjamzito pia watu wameunganisha hio story ikawa ni mimba yangu. Story zinazungumzwa mimi siwezi kufanya kitu chochote,” Diamond alisema.

Staa huyo pia aliguzia ishu ya Zari kuonekana akiongelea kwa spa na mwanaume aliyekuja kugunduliwa kuwa binamu wa Ivan Ssemwanga.

Diamond alieleza kuwa alikusudia kuweka picha ya Zari na Edwin Lutaaya kwenye Instagram kwani alidhani kuwa mkewe ako na uhusiano wa kimapenzi na Edwin.

“Nlikua nimekusudia, unajua…upande mwingine mimi ni binadamu kama binadamu wa kawaida mimi pia nakua naskia uchungu na maumivu. Na katika mahusiano yangu yote nshakuwa nayo basi mahusiano ya Zari nimejitahidi kujitoa sana kwa kila hali na mali. So nlikutana na ile picha kwenye mtandao sikuelewa…mi kwanza nkajua ime editiwa. Ehh nkampigia simu nikamwambia “mbona kuna picha nimeiona hivi na hivi”. Akaniambia “bwana huyo ni shemeji wangu, hapo pia tulikua na wife wake lakini kutokana na kwasiko kwa maji inaonekana kama kanikumbatia lakini haikua hivyo”. Mi nikapanic nkaona kama huyu mchongo tu yani ni kama anajifanya, anajitetea. Nkamwambia “kwa hio mbona hujaiposti kwenye account yako imetokea kwa watu wengine tu, imekuaje?”. Nkamwambia “ulikua unataka boost, unataka kiki au vipi kwasababu mimi ntakupa kiki ntakupost kabisa ili isambazike mtu aone dunia, si unataka kila mtu aone?” Kwa hivo nkaposti, kwa hivyo baada ya kuposti alikua ofisini akarudi haraka amekuja amepagawa ndo kaja na zile picha “ si unaona nlikua na huyu wife wake na nini na nini…na huyu wife wake ndo alinipiga picha kwa hivyo na hivi na hivi…. Baada ya kunionyesha ndo nkatoa ,” alisema Diamond.

Tazama mahojiano hayo hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=xnxcRkq6_34

Diamond aeleza kwanini ameachia nyimbo mbili mara moja

Diamond amemshirikisha Tiwa Savage kutoa wimbo mpya unaoitwa ‘Fire’. Ameachia wimbo nyingine pia  ‘I Miss You’ wakati huo huo.

Katika mahojiano na kipindi cha XXL ya Clouds FM, Diamond alisema kuwa alitaka kutangaza kwa redio kuwa anatoa nyimbo mbili badala ya mashabiki wake kuenda YouTube na kushangaa kuwa ameachia nyimbo mbili wakati walikua wanatajaribia wimbo moja.

“Siku ya muziki leo duniani… hapo mwanzo tulikua tunatoa wimbo moja alafu mtu akienda YouTube anashangaa kuna nyingine. Mi naweza sema tu kwanini nisitoe zote hapa badala mtu kuenda kuskia kule,” Diamond alisema.

Tazama nyimbo zake hapo chini:

 

Ujumbe wa Eddy Kenzo kwa Diamond baada ya Rayvanny kupata uteuzi wa BET award

Rayvanny ameteuliwa katika kitengo cha ‘Best International View’s Choices’ akiwa ni msanii pekee kutoka Afrika katika kitengo hicho.

Diamond na wasanii wengine wamekua wakiwarai mashabiki wao wampigie kura Rayvanny mbaka ashinde tuzo hilo. Walioteuliwa watatuzwa Jumapili hii tarehe 25 katika ukumbi wa Microsoft jijini Los Angeles, Marekani.

Eddy Kenzo aliweka picha ya Rayvanny kwa mtendao wa Instagram kuwaomba mashabiki wake wampigie kura Mtanzania huyo.

“Attention East Africa!!!!??? Our Brother @rayvanny needs our support by just commenting with #pickrayvanny on any picture of your choice on social media we need another #BET in eastAfrica asap 2015 and 2017 will be remembered ??? Alhamdulillah ?? congratulations #Tanzania Bless up @rayvanny #ipickrayvanny ????” Eddy Kenzo aliandika.

Mganda huyo amewahi kushinda tuzo la BET, alishinda tuzo hilo 2015 katika kitengo cha ‘Viewer’s Choice Best New International Artist’, kitengo sawa ambacho Rayvanny anawania mwaka huu.

Eddy Kenzo akionyesha tuzo la BET aliyoshinda 2015

Diamond Platnumz alimshukuru sana Eddy Kenzo kwa kumpigia upato Rayvanny kushinda tuzo hilo la BET.

“Kenzooooooooooo!!!!! ????” Diamond aliandika kwa comment.

Eddy Kenzo alimjibu na kumpongeza kwa kukuza talanta nchini Tanzania.

“@diamondplatnumz I see you my bro??? you are great?? thank you for showing us these talented yut of our generation may God reward you 100% blood???” aliandika Eddy Kenzo.