Darasa Ajipanga Kutoa Album, Msanii Avril Kutoka Kenya Ndani.

Habari zinazosambaa katika mitandao ni kwamba pamoja na kwamba msanii wa hip hop nchini, Darasa kukaa kimya lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa hivi karibuni anategemea kutoa album yake ambayo itasambaa mitandaoni.

katika album hiyo amabyo alianza kuiandaa tangu mwaka 2017 inawasanii wengine wakubwa lakini pia kwa habari za kuaminika ni kuwa pia kutakuwepo na mwanadada Avril kutoka Kenya ambae anafanya vizuri nchini humo.

pamoja na kwamba mashabiki wa Darasa wamekuwa wakilalamika kla siku kuhusu ukimya wa mwanadada huyo lakini hii inaweza kuwa ni habari njema na ya kufurahishwa kwa mashabiki hao hasa kutokana na ujio wake mpya ambao utakuwa mkubwa.

Alichokisema Zaiid Kuhusu Darasa

Msanii wa muziki wa bongo fleva Zaiid anaetamba kwa sasa na wimbo wake wa picha amefunguka na kusema kuwa watu wasikae wakimsema vibaya Darasa kwa kitendo cha kukaa kimya  na kumsema kuwa amefulia lakini kitu cha kuzingatia ni kwamba kuna wimbo mmoja ambao msanii yoyote anaweza kufanya vizuri kuliko mwingine.

Darasa alichofanya katika wimbo wa muziki ni muziki mzuri kwaio haikuwa raisi , ku-hiy isiwe sababu ya kumshusha mtu vyeo hata siku moja , kuhit ni matokeo tu , kuna watu hawajui hata kuimba lakini wanaweza kutoa wimbo uka-hit.

ku-hit saa zingine kunaendana na matukio na kiki pia,kunaendana na vitu vingi sana , ukiona wimbo wako umefanya vizuri bila changamoto yoyote ujue kuwa wewe ni msanii mzuri na mkubwa sana.

Ikumbukwe kuwa baada ya Darasa kutoa wimbo wa muziki alitoa wimbo wa hasara roho na kisha kukaa kimya kabisa na hii iliwafanya mashabiki kuuliza sana huku wengie wakisema kuwa amefulia.

Hanscana Amtetea Darasa, Asema Maneno ya Mashabiki Yanam-panikisha Darasa

Muandaaji wa video bongo Hanscana amefunguka na kumtetea Darasa kwa kuzingatia kuwa yeye ni moja ya watu wa karibu sana na msanii huyo na alikuwa nae kwa kipindi chote ambacho aliweza kufanya nae ngoma za huko nyuma ambazo zilifanya vizuri sana,

Akiongea na Shadee wa Clouds E ,Hanscana anasema kuwa ni kawaida kwa wasanii kukaa kimya kwa muda ili kujipanga na sio Darasa tu ambae amekaa kimya bila kutoa ngoma mpya lakini kwa nini watu wamekuwa wakimkomalia sana Darasa.

Akitolea mfano wa wasanii wengine kama Bob Junior, hanscana ansema kuwa wapo wengi wamekaa kimya lakini hiyo inakuwa ni umauzi wa mtu kujipanaga ili kurudi upya hivyo watu wasihofie swala la Darasa kukaa kimya.

Hanscana anasema kwa jinsia mbayo mashabiki wamekuwa wakiongea katika mitandao ya kijamii kuhusu Darasa , kama msanii huyo asingekuwa jasiri basi angekuwa amesha-panic sana na hata kuamua kuwaridhisha mashabiki kwa kutoa ngoma mpya lakini kwa kukurupuka kitu ambacho baadae wangesema tena ameharibu.

HLlakini pia , hanscana anasema kuwa anachoamini ni kwamba mashabiki wanampenda sana Darasa na ndio maana wamekuwa wakimsumbua yeye sana na wala sio wasanii wengine lakini pia Darasa kwa sasa anapaswa kuwa imara sana ili kuosikiliza maneno ya mashabiki na kujikuta anakurupuka na kutoa ngoma bila kujipanga vizuri.

Maneno ya Hanscana yanakuja baada ya watu wengi kusema kuwa msanii Darasa amekuwa kimya sana na wanahisi kuwa msanii huyo anaweza kuwa na matatzo au ameharibikiwa kabisa na kwamba amefulia hawezi kufanya tena kama mwanzo,hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Hanscana kuongea hayo kuhusu Darasa huku akisema kuwa msanii huo anajipanga ili kutoa kivingine tena.