Mtitu Akataa Kanumba Kuondoka na Bongo Movies

K wa muda mrefu sana bongo movies imekuwa ikisemwa kuwa imekufa na kwamba aliekuwa akiifanya sanaa hiyo kuendelea ni msanii Kanumba ambae ameshafariki dunia.

Ni muda sasa tangu msanii huyo amefariki na kumekuwa na utoaji wa kazi mpya za filamu na movies na hata pia kuibuka kwa wasanii wapya chipukizi ambao wanafanya vizuri katuka tasnia, na hii inaweza kuwa ndio sababu kubwa ya  moja ya wadau wa bongo movies kukataa kuwa Kanumba ameondoa na bongo movies.

Akiongea na waandishi wa habari, Mtitu anasema kuwa sio kweli kuwa Kanumba ameondoka na bongo movies kwa sababu kila siku kazi mpya zinatoka na wasanii wapya na vipaji vipya vingi vimekuwa vikiongezeka.

 

Shif akubwa iliyop katika bongo movis kwa sasa ni kukosa ushindano na umoja katika kufanya kazi na kukosoana kwa upendo wapi alipokosea mwingine ili mwingine ajifunze kuanzia pale.

Steve Nyerere:Tunaongoza kwa Kuonyesha Tamthilia Zenye Ubora.

Siku za nyuma kidogo Steve Nyerere alikuwa ni moja ya wasanii wa bongo movies ambao walikuwa wakilalamikia sana tasnia hiyo na kusema kuwa kwa muda mrefu tasnia hiyo imekuwa ikifanya kazi na wasanii wale wale na kurudia makosa makubwa kila siku kiasi kwamba watu wamechoka kuona wakifanya hayo  hivyo hiyo ni sababu kubwa ya kufakwa bongo movies.

Lakini siku za hapa karibuni msaniii huyo ambae ndio amekuwa kama baba katika bongo movies anasema kuwa kwa sasa kazi za tamthiliya zimekuwa zikifanya vizuri sana kiasi kwamba inawezekana kabisa kuwa Afrika Mashariki ikawa ndio inaongoza kwa tamthiliya nzuri na zenye ubora kuliko sehemu nyingine yoyote ile.

Steve Nyerere anasema kuwa kwa sasa wasanii wameanza kujirekebisha na kutaka kuinuka tasnia hiyo , hivyo wameanza kujituma na kujitutumuanili kufanya kazi itakayowalipa lakini pia kuwaweka mashabiki wao katika nafasi nzuri ya kuangalia tamthiliya.

Tumesimama sana kwa afrika mashariki na hata magharibi sisi ndio tunaongoza kwa kuonyesha tamthiliya zenye ubora ,inaonyesha ni kwa jinsi gani Tanzania kuna vipaji.

 

 

Monalisa Kutangaza Tamasha la Filamu Nchini Marekani.

Mwanadada mkongwe katika tasnia ya filamu na vipaji vvya utangazaji Tanzania Vyonne  Cherrly maarufu kama Monalisa amechaguliwa kuwa mtangazaji wa tamasha kubwa la filamu litakaoanza kufanyika June mwaka huu kuanzia tareh 29 mpaka July 3 huko Dallas nchini Marekani.

Monalisa ambae amechaguliwa yeye pamoja na msanii maarufu kutoka nchini Nigeria  anaejulikana kama David Wandy  wanatarajiwa kuwa watangazaji katika tamasha hilo linalojulikana kama The African  Film Festival  (TAFF) .

Akielezea kwa kina kuhusu kuchaguliwa kwa wasanii hawa wakubwa Afrika muandaaji wa tamasha hilo Kelechi Eke anasema kuwa kutokana na Cv ya wasanii hao ndio kitu kikubwa kilichowavutia wao kufanya uchaguzi huo kwa sababu wanaamini mengi waliyoyafanya katika tasnia za filamu nchi mwao zinawapa sifa za kuchaguliwa kuonekana huko.

Katika tamasha hilo mambo mablimbali yatafanyika ikiwa ni pamoja na kuonyeshwa na kutangazwa kwa filamu za Afrika , kutoa mafunzo na semeina mbalimbali kuhusu filamu za Afrika, na pia kutakuwepo na wasanii mbalimbali kutoka Afrika kama wakina Uche Jumbo ,Dontoh dikeh ambao watakuwepo kutoa fursa mbalimbali juu ya filamu.

Msanii Bongo Movie Auza Figo Ili Kupata Ela ya Kurekodi

Msanii wa maigizo na filamu Tanzania antokea mkoani Iringa anaejulikana kama  Erasto Kilowoko maarufu kama Magumashi amekaririwa kusema anauza figo kwa sababu  hana ela ya kurekodi ilhali ndoto zake ni kufanya vizuri kumuziki.

Magumashi anasema kuwa lengo lake kubwa la kuuza figo ni kupata ela itakayomwezesha kurekodi movie yake  mpya ambayo ina lengo la kuwaelimisha vijana kuhusu maisha katika jamii kuhusu uzalendo na uwajibikaji.

Msanii huyo ambae kwa sasa kazi yake kubwa ni kinyozi mjini iringa amesema kuwa anauza figo yake kwa sh.milion25 na ameaidi kuwa kwa kuwa serikali inakusanya kodi kwa ajili ya mapato absi na yeye atatoa milion 5 kwa ajili ya kulipa kodi.

nimekuwa nikiomba viongozi na makampuni mbalimbali wanisaidie kutimiza ndoto zangu lakini naona kimya,nataka kuwa kioo cha jamii kwa kutoa elimu kuoitia sanaa.ninauza fiigo milioni 25 na kama serikali inataka mapato nitawapa milioni 5, shida yangu kubwa sio kujenga nyumba au kununua gari ila kutimiza ndoto zangu.

Magumashi anasema kuwa soko la filamu Tanzania ana uhakika sasa hivi litakaa vizuri kwa sabau anaeongoza nchi Mh.Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuthibiti kazi za wasanii .

Mkude Simba:Bongo Movie Imekufa ,Wasanii Wanakimbilia Filamu.

Msanii wa maigizo na vichekeshoo  nchini  Mkude Simba ansema kuwa kwa sasa tasnia ya bongo movie imekufa kabisa na wasaini wengi sana wamekimbilia katika kufanya kazi za filamu ilhali wakiacha upande wa pili uindelee kudidimia.

Mkude Simba anasema kuwa hofu yake kubwa ni kwamba wasanii wengi sasa wanategemea kutengeneza filamu na tamthiliya lakini ikitokea hata upande huo pia utakufa basi hakutakuwa na pa kukimbilia tena kwa sababu hakuna wa kupainua upande huo wa pili.

biashara kubwa ya  wasanii ilikuwa ni bongo movies lakini sasa hivi bongo movies imekufa kabisa,na sanaa sasa hivi inayumba kabisa,na mwokozi mkubwa aliebaki kwa sasa ni tamthiliya ambapo kila mtu anakimbilia huko.sasa sijui itakuwaje kama na huko kutaharibika.

Mkude simba anasema kuwa wasiwasi wake unakuja kwa sababu wasanii hao ambao wanashindwa kuigiza movies za dakika 60 watawezaje kuigiza filamu mabayo inahitaji miezi hat mitatu kwa filamu moja.

Ombi kubwa alilotoa mkude simba kwa wasanii wenzake ni kupigana kwa nguvu kuinua tasnia hiyo na sio kukimbilia kwingine kwa sababu kuna kizazi pia kinategmea kazi za sanaa zinazofanywa sasa.

 

Steve Nyerere Akiri Kuzichoka Sura za Bongo Movies.

Msanii mkongwe wa maigizo ya bongo movies ambae pia ni mshekeshaji maarufu bongo amekiri kuwa uweo wa wasanii walewale kila siku  kunafanya bongo movies ichokwe na kila mtu kwa sababu ladha ya maigizo inakuwa haibadiliki bali kila siku ni walewale.

Msanii huyo ambae ameluwa akipigania kuinuka kwa bingo movies kila siku anasema kuwa inabidi kuwepo na wasanii wapya ktaika tasnia ili kuleta ladha mpya ya uondo wa bongo movie lakini kitu cha ajabu hakuna wasanii wapya katika maigizo.

Akitolea mfano alipokuwa akiongea na  Ijumaa wikienda , Steve Nyerere anasema kuwa inawachosha watu wengi kama kila siku wanakuwa wakiona sura za Kajala Masanja , Shamsa Word au wolper kila siku  na ndipo linpotokea anguko la sinema za bongo kama ilivyotokea sasa hivi.

Akiendelea kuongezea Steve anasema kuwa ifike mahali wasanii wakubwa na wakongwe wabaki kupewa heshima yao kama wasanii wakongwe na kuwaibua wasanii wapya ili kuleta ladha tofauti na zile za zamani ili kuifanya tasnia kuwa na mabadiliko kidogo.

ninachokipigania mimi ni kuwa wasanii wasanii wakubwa wabaki kuwa na hati miliki zao,lakini sura za mastaa hao hao kila siku katika kioo zinachsha kabisa, maana hata mimi nimezichoka.

Rado Amtolea Uvivu Ray Kigosi na Monalisa

Ray na Monalisa wamepata nomination ya tuzo nchi Ghana , lakini baada ya kupostiwa kwa post hiyo kwa ajili ya kuomba kura hakuna aliyekuwa na muhamuko wa kure-post tena kwa ajili ya kuwasapoti wasanii hao wawili , cha ajabu ni kwamba baada ya msanii  Ray juzi kuweka kwa mara ya kwanza picha ya mtoto wake wa kiume kwa mara ya kwanza karibia kila msanii aliweza kure-post na kumpongeza msanii huyo kwa mtoto wake huyo.

Baada ya muda maneno yaliendelea kusambaa katika mitandao kwamba kwanini walipoweka post ya kuomba kula  hakuna aliewasapoti kwa kuiweka tena  katika akaunt zao ili kuwaombea kura kwa mashabiki lakini alipopostiwa mtoto kila mtu akionekana kuvutiwa na picha hiyo na hata kurudia kuipost tena?

Rado, msanii wa muziki na bongo movies pia aliamua kuvunja ukimya na kuwajibu mashabiki lakini pia kutoa ujumbe mkali kwa kuwalipua wasanii hao (Ray na Monalisa) ambao ndio wanawania tuzo hizo nchini Ghana.

Rado ameonekana kukwaza na tabia za wasanii hao wawili ambao ni wakubwa lakini hawana ushirikiano na wasanii wenzao kwa mujibu wa Rado ni kwamba Monalisa na Ray wamekwa hawahudhirii kazi za wasanii wenzao na hata hawatoi sapoti kwa wasanii wenzao,

Kwa kutolea mfano, Rado analalamika kuwa hata kipindi cha uzinduzi wa filamu yake wasanii hao wanaojiita wakubwa na ambao kwa sasa wanataka sapoti walishindwa kuwepo katika uzinduzi wa filamu hiyo.

Kuhusu Ray na Monalisa tunashindwa kusema ukweli kuwa hata wao ni wabinafsi sana,nakumbuka pale Mlimani City nilifanya uzinduzi wa filamu yangu ya  Bei kali kati yao wengine wengi hawakuja katika uzinduzi hasa wanaojiita mastaa ingawa walipata kadi ya mwaliko mapema wiki mbili kabla.monalisa alisema anakwenda Zanzibar kutembelea kiwanda na Rich.Niva na Chiko waliamua kulala nyumbani, Ray alimzuia hata mke wake kuja katika uzinduzi.

Kwa muda mrefu wasanii wa bongo movies wamekuwa wakilaumiana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya kukosa ushirikiano na kujituma katika kukuza tasnia hiyo, ingawa wamekuwa wakikanusha kufa kwa tasnia hiyo Tanzania lakini sanaa ya bongo inaonekana kufa.

Duma:Kuomba Omba Kunaua Sanaa ya Filamu Bongo.

Msanii wa filamu za bongo Daudi maarufu kama Duma amefunguka na kusema kuwa filamu za bongo zinakufa kwa sababu wasanii wengi wamekuwa ni omba omba na kujali maslahi yao zaidi kuliko kujali tasnia ya filamu kwa ujumla.Duma ambae kwa muda amekuwa akipiga kelele hasa kwa wasanii wenzake  kuweza kujituma ili kukuza filamu bongo.

Akiongea na GPL, Duma amesema kuwa wasanii wnegi bongo wakubwa wamekuwa wakipata bahati ya kuonana na matajiri wakubwa ambao wana uwezo wa kusaidia kukuza tasnia hiyo lakini kitu cha kushangaza ni kwamba wasanii hao wamekuwa hawasema shida zinazozoikumba tasnia bali wanatoa matatizo yao binafsi na kujisaidia wenyewe, ambapo duma amewafananisha wasanii hao na ombaomba.

sanaa yetu imekufa kwa sababu  kwa sababu wasanii wengi  wamekuwa omba omba kwa ajili ya matatizo yao binafsi tu,ingawa wangekuwa wanaelezea matatizo ya filamu za Tanzania kwa matajiri wanaokutana nao wala filamu bongo isingekufa kabisa. Alifunguka Duma

Hivi karibuni msanii mkubwa kutoka nigeria ramsey noauh alikuja tanzania lakini alipata bahati ya kukutana na wasanii wa boingoi movies  na wakafanukiwa kuongea nae na kuweza kupanga jinsi ya kuweza kuinua  sanaa ya bongo.

Bado kumekuwa na changamoto sana katika kuinua tasnia ya bongo movies ingawa wapo wanaojitahidi kuinua lakini umoja wa wasanii na kujitolea kunahitajika ili kuweza kutatua changamoto hizo.

Wakina Mama Bongo Muvi Waanzia Mashuleni, Ni Kuhusu Elimu Ya Ushoga

Wana mama kutoka Bongo movies kupitia katika foundation yao  inayojulikana kama  Malezi Daima Foundation wameungana na kuanza kutoa elimu mashuleni  hasa katika shule za sekondari huku elimu yao ikijikita kuwafunza wanafunzi wa kike na wa kiume kuhusu usahgaji na ushoga na athari zake.

Bi Sonia ambae ni mwenyekiti wa foundation hiyo amesema kuwa wazazi hao wameona ni bora kujitolea kuzunguka katika mashule mbalimbali ili kuwasaidia watoto ambao wanakutana na vishawishi vingi  na kujikuta wakiingia katika tabia hizo.

Bi Sonia mbele ya wanafunzi.

Kama wamama wa bongo muvi tumeona ni bora tuungane na kutoa hii elimu mashuleni ili kuwanusuru  na mimba za utotoni, ndoa za utotoni, magonjwa ya ajabu,matumizi ya madawa ya kulevya, usagaji na ushoga pia kuondokana na malezi mabaya nje na ndani ya shule .hadi sasa tumeshatembea shule kama tano hivi dar na mikoani pia.lengo letu ni kuwapa watoto malezi mazuri ambayo kama wanayakosa nyumbani basi wayapate shuleni.

Wamama wa bongo muvi wanaounda foundation hiyo ni pamoja na Bi Sandra, Natasha,Asha Boko, Herieth Chumillah, Grace Mapunda,Daina Njaidi, Mama Teckla Mjata,Mama Nyamayao na wengine wengi.

Wamama kutoka Bongo movies wakiongea na wanafunzi wa shule ya sekondaro buza jijini dar es salaam.

Bi. staa akitoa zawadi kwa wanafunzi.

Sanaa Kumtenganisha koletha Na Mwanae

Akiwa kama mmoja wa wasanii walioanza kufanya kazi za filamu miaka mingi iliyopita Koletha Raymond sasa hivi ameanza kuona kazi ya mikono yake kwa mafanikio aliyoyapata hivi karibuni,mwanadada huyo ambae ameshinda hivi karibuni katika shindano lilikuwa likiendelea la kusaka vipaji vya sauti lilikuwa likiendeshwa nchini  ameweza kuwabwaga washiriki wengine na kuweza kushinda nafasi hiyo.

Hata hivyo mshindi wa shindano ilo alipata mkataba wa kufanya kazi nchini China katika mji wa Beijing kwa zaidi ya mwaka mmoja na Koletha ndio amechukua nafasi hiyo , lakini changamoto ilikuwa pale ambapo Koletha anatakiwa kumuacha mtoto wake mdogo mwenye umri kama miezi nane hivi ili aweze kwenda kufaikisha ndoto zake na kuwakilisha tasnia ya filamu Tazania  nchini China.

Akijibu kwa ufasaha kabisa kuhusu swala hilo , Koletha anasema kuwa  ni kweli ataenda nchini China kufanya kazi hiyo lakini mume wake na familia yake yote ilisha kubali na mtoto atamuacha kwa mama yake mzazi lakini mumewe ameridhia na jambo ilo ilo hivyo anaomba baraka tu kutoka kwao

Mume wangu amenipa ruhusa kwa sababu ni baba muelewa sana,ni mwanaume anaenisaidia katika kila kitu ninachokifanya na tumekuwa tukishikamana sana kwa kila jambo na kwa sasa ameridhika kabisa mimi niende kufanya kazi huko  na nitaondoka mtoto nitamwacha kwa mama yangu.nimefurahi sana kwa ushindi huu kwa sababu umenipa fursa  ambayo sikuitegemea.-Alithibitisha koletha

Ushindi wa Koletha utasaidia pia kuleta mapinduzi katika tasnia ya filamu ukizingatia kazi yake anaenda kufanyia nchini China hivyo itakuwa pia ni fursa kuitangaza sanaa ya Tanzania mahali pengine kwa sababu huko ataenda na kukutana na watu wengine wenye vipaji pia.Tuanmtakia kila lenye kheri katika kuipeperusha tasnia ya filamu Tanzania na bendera ya Tanzania,tunaamini ataiwakilisha vyema.

Odama Akana Kujitenga Na Bongo Movies

Kumekuwa na maneno mengi kuwa bongo movie ya sasa sio kama ile ya zamani, kwamba bongo movies imekufa na wasanii wengi wameanza kutoka katika tasnia iyo na kujikita katika shughuli nyingine za kujikwamua kimaisha huku wanaofanya kazi wa sasa ni wale tu wasanii wapya .Ingawa bado kuna wachache wameng’ang’ania na kujitahidi kuinua tasnia hii lakini bado nguvu kubwa inahitajika  ili kuilinda tasnia hii.

Kumekuwa na tetesi katika mitandao ya kijamii kuwa  moja ya wasanii wa kike wa tasnia ya bongo movies Jenipher Kyaka maarufu kama  Odama amekuwa  akituhumiwa kujitenga na tasnia hii na kuwa amekuwa haonekani katika baadhi ya matukio ambayo wenzake wamekuwa wakikusanyika kwa pamoja.Hata hivyo wapo baadhi ya mashabiki walimtuhumu na kusema kuwa inawezekana ameachana na bongo movies.

Mwanadada huyo amefunguka na kusema kuwa sio kweli kuwa tuhuma hizo anazopewa na mashabiki wake kuwa ni kweli bali kuna muda kunakuwa na vitu vingine vya kufanya,na hii ni kwa sababu maisha yanakwenda yanabadilika hivyo lazima kufanya vitu vyake binafsi na sio kukutana kila siku kama ilivyoeleka kwa watu hapo kipindi cha nyuma.

Unajua watu hawaelewi tu,mtu anapobadili mfumo kidogo wansema ameanza kujitenga lakini sio kweli.wakati huu wa sasa sio wa kuwa tunakutana kila mara kwa sabau muda mnaokuwa mnakutana kuna vitu vingine vinakuwa haviendi kabisaa, kwa sababu  wote mnakuwa mnakutana sehemu moja.

Odama ni moja ya wasanii wa kike waliobuka na kufanya vizuri kabisa katika tasnia ya filamu huku filamu yake kubwa iliyomtambulisha ilikuwa na jila la  Veronika  ikifatiwa na ile ya Odama iliyoendelea kumpa jina ziadi.

Ifike mahali wasanii wa bongo movie inabidi wakae na kukubaliana kuungana na sio kila moja kukaa na kusema anaangaika na maisha yake kwa sababu kila kitu ili kiwe kizuri ni lazima nguvu ya ziada ya watu ni lazima ifanyike kwa juhudi na pia ili ionekana. Wanapotokea  watu wenye nia njema na kitu hicho huku wakifanya kwa umoja na kwa kujitolea kwa pamoja watasaidia kuinua tasnia hiyo.

JB Kuacha Kufanya Kazi Za Filamu

Msanii wa bongo movies aliyejizolea umaarufu wake nchini kutokana na kufanya kazi ya filamu kwa ufasahaa na umakini mkubwa  Jacob Steven ambae watu wengi umfananisha na mwigizaji wa filamu za kihindi anaejulikana kama  Amithabh Bhachchan amefunguka na kuongelea mpango wake wa kuacha kabisa kufanya kazi za  filamu hivi karibuni.

Katika mahojiano yake na chombo kimoja cha habari siku za nyuma JB alisikika akisema kuwa anakaribia kuacha kuigiza na hatakuwa mtu anaetokea nyuma ya kamera tu, hivyo alipokuwa anahojiwa kwa mara nyingine tena  JB alisema kuwa ni kweli kabisa kwa sasa anatarajia kucha kufanya movie lakini hii haimaanishi kuwa ataaga kabisa tasnia ya filamu nchini.

JB anasema kuwa kwa kuwa anauwezo wa kuongoza na kuandaa movies basi atakuwa amejikita sana katika kazi hizo mbili kwa sana, lakini filamu alizofanya bado zitaendelea kufanya vizuri sokoni hivyo bado yupo pamoja na mashabiki wake.

“Nategemea kuacha movies lakini bado sijaacha,lakini movie yangu ya mwezi ujao itakuwa ya mwisho kuigiza na ili kuwaaga mashabiki na sapotaz wangu movie hii nitaifanya kwa premire,” Alifunguka JB

Hata hivyo akifunguka zaidi kuhusu sababu ya kwanini anaamua kucha kufanya movies Jb anasema kuwa amejikuta kuwa ana mambo mengi ya kufanya hivyo anahitaji kujikita huko kwanza”Ni kweli tasnia bado inanihitaji,lakini sio kwamba hata ninaitupa, taste zangu bado zitaendelea kuwepo sana , kuhusu kwanini nimefikia uamuzi huo ni kwamba  nimejikuta nina mambo mengi sana ya kufanya, kwaiyo nimeona bora nizame huko, kwenye movies na tamthilia niwaachie na wengine” aliongezea JB

Hata hivyo akiweza bayana mambo yanayomfanya yeye kuwa busy Jb anasema kuwa “makampuni ninayofanya matangazo yana ziara zinanihitaji,nahitaji kuandaa muvi, kampuni yangu ya Jerusalem, bado kmapuni ya barazani inanihitaji pia maana nina hisa hapo, lakini pia mimi ni bosi kwenye kitengo cha masoko kwaiyo unaona jinsi gani nilivyo-busy” aliongezea zaidi.

JB  ni moja ya wasanii waliofanya vizuri sana katika movies kama Dj ben, Nakwenda kwa mwanangu, Taxi driver, Signature ambazo zilimfanya kutamba sana katika filamu.

 

Pesa Inaleta Dharau Bongo Movies-Cloud

Msanii mkongwe wa bongo movies nchini Cloud, amefunguka na kuongelea sababu ya kuwa na mikwaruzano mingi  ndani ya bongo movies.Kwa kipindi kirefu baadhi ya wasanii wa bongo movies wamekuwa wakirushiana maneno  binafsi ambayo kwa namna moja au nyingie hayajengi kabisa tasnia hiyo, moja ya wasanii hao ni Duma pamoja na Gabo ambao wamekuwa  wakipeana maneno ya kashfa kuhusu maisha binafsi,

Akiongea na eNews ya EATV, Cloud amefunguka na kuweka bayana baadhi ya mambo yanayovuruga bongo movie, ambapo anasema kuwa zamani kulikuwa na upendo na umoja kwa sababu watu walikuwa wanafanya maigizo bila kulipwa lakini baada ya kuanza kuigiza filamu watu wanajipatia vipato wanaanza kuonana mmoja ni mkubwa kuliko mwingine.”zamani wakati watu wanaigiza alafu hawalipwi pesa pale umoja ulikuwa unapatikana, watu walikuwa wanalipiana hadi nauli  ya daladala,lakini baada ya kuanza kufanya filamu watu wameanza kupata hivi visenti watu vimeanza kuwatia dharau, lakini baada pesa zikaanza kuwatoka kwaiyo mtu akawa akipata deal hataki kumshirikisha mwenzie kwa sababu ya wivu”

Clouds anafunguka na kudai kuwa bongo movie watu wengi sana ni maadui na hawapatani kabisa , kumekuwa na uadui mkubwa na anakiri hata yeye wapo watu wanaomchukia sana anawajua lakini anawaombea kheri tu,”kuna vitu vingi vipo ndani ya pazia kuhusu bongo movies,ni vigumu kuelezea kwanini watu hawapatini, na ni kweli watu hawapatani , hata mimi nina maadui wengi katika bongo movies” aliongezea Cloud

hata hivyo katika kumalizia kwake, clouds alitoa ushauri kuwa inabidi watuwaanze kujielewa na kujikubali ilikutatua matatizo yaliyopo katika bongo movies,”tatizo kubwa mbali ya yote niliyoyaongea ni kwamba tunakosa elimu ya kazi tunayoifanya, na tunakosa uelewa wa position tulizonazo, lakini kama tutapata elimu ya kazi na position tulizonazo nina imani izi figisu figisu zinazokuwepo hazitakuwepo tena” aliongea Cloud

hata hivyo Cloud anasema kuwa umaski wa wasanii wengi ndio unaofanya bongo movies kuvurugika, na umasikini ndio unaofanya watu kuoneana wivu na kuchukiana katika tasnia.

 

Nawapenda Wanawake Waliokaza,Sio Wema -Rado

Msanii wa maigizo nchi ambae pia alishawahi kujaribu upande wa  muziki na akafanya vizuri anaejulikana kama Rado, amefunguka na kusema sifa za mwanamke anaempenda lakini amekanusha kabisa kuwa yeye hawezi kutembea na mwanamke anaetoka Bongo Movie au Bongo Fleva.Msanii huyo ambae alikuwa akiongea na waandishi wa habari na kuulizwa kuhusu kazi yake iliyo toka kipindi cha nyuma kidogo , filamu ambayo alicheza na Tanzanian Sweetheart Wema Sepetu  iliyojulikana kwa jina la “Madame’ ambayo pia ilizua maneno na  tetesi za msanii huyo wa kiume kutoka kimapenzi na Wema Sepetu, Rado alifunguka na kusema hawezi kutembea na Wema hata kidogo.

‘Sijawahi kumpenda msanii yeyote wa Bongo Movies au wa Bongo Fleva wa kike na siajwahi tu kuvutiwa nao  hata kidogo, sijawahi  kuvutiwa na Madame Wema Sepetu kwa sababu naona yupo nje ya wanawake ninao wapenda” alifunguka rado, lakini pia msanii huyo wa  alitoa sababu za yeye kutokuvutiwa kimapenzi na msanii wa kike akiwemo madame Wema Sepetu au wanawake wote kutoka Bongo Movie na Bongo Fleva na kusema kuwa “unajua mimi ni mchanganyiko wa Usukuma na Unyakyusa, kwaiyo wanawake wa kudeka  muda wote siwapendi, napenda  wanawake fulani hivi waliokaza” ameongezea Rado

Akielezea experience aliyoipata kutoka kwa Madame Wema wakiwa katika kuigiza filamu ya ‘madame’ , Rado anasema kuwa Wema Sepetu anaonekana mwanamke wa kudeka sana kwaiyo mtu kama huyo hawatawezana kwabisa,” kwa jinsi alivyokuwa mlegevu Madame, sina hata uhakika  hata kama anaweza kufua , kutokana na kudeka kwake” anaendelea Rado

kwa upande wa Bongo Movies, Rado anasema kuwa kwa sasa tasnia  ya filamu inaendelea kufanya vizuri kutokana na jitihada zinazofanyika ili kulinda vipaji vya wasanii ambapo kumekuwa  na kampeni mbalimbali ikiwemo ile ya kusimamisha uuzaji wa filamu fake mitaani na anasema kwa sasa vilio wa wasanii wa filani  vinaelekea kuisha na wataanza kuona maslahi ya kazi wanazofanya na kuna baadhi ya makampuni yamejitolea ilii kusimamia kazi za wasanii katika uuzaji.

 

Richie Amlilia Dk.Cheni Juu Ya Filamu

Muigizaji mkongwe wa filamu Tanzania Single Mtambalike anaejulikana sana kwa jina la Richie ni moja kati ya waigizaji wa zamani na wakongwe walikuza vipaji vya wasanii wadogo wengi chipukizi na tasnia ya Bongo Movies kwa ujumla ameelekeza kilio chake kwa msanii mwenzie mkongwe Dk. Cheni na kumtaka arudi katika tasnia ya filamu

Dk. Cheni ambae kwa muda alisimama kufanya shughuli za uigizaji na kujikita katika shughuli za ushereheshaji (Mc)  ni moja kati ya wasanii wa kwanza walioanza kuigiza maigizo na ana mchango mkubwa sana katika kukua kwa tasnia ya filamu na hata katika kusaidia wasanii wadogo kuingia katika tasnia hiyo na kufanya vizuri kwa sababu ya usimamizi wake mzuri.

Richie anamshauri Dk. Cheni kurud katika tasnia kwa sababu anaamini kuwa sababu kubwa iliyomfanya Dk. Cheni atoke katika sanaa ni soko la filamu na anasema kwa sasa wameshalitatua  tatizo ilo hivyo anamuomba kurudi na kuendelea.

Akizungumza na eNewz ya EATV , Richie anasema anajua kilichomfanya Dk. Cheni kusimama ni sababu soko la filamu lilikuwa si zuri  Tanzania

“Nataka nimwambie Dk. Cheni kwamba ni yeye  mzuri kwenye uigizaji na soko linamuhitaji.Kilio alichokua nacho  kila siku akilia tumekipatia ufumbuzi.Tumekuja na hii project ya Barazani na tunashukuru EATV mnatusapoti naamini tutawafikia watu wengi zaidi kwa mfumo huu, kwaiyo ndugu yangu Cheni usikate tamaa wewe  unaweza njoo tuendeleze tasnia”

Pia katika mazungumzo yake Single Mtambalike anawatoa mashaka waigizaji wote  wa tasnia iyo ya filamu kuwa project yao mpya ya Barazani ina lengo la kutouza ‘master’ za movie zao kama jinsi walivyokuwa wanauza hati miliki za filamu na badala yake wanakuja kuwakomboa wasanii wa filamu kwa sasa.

Tasnia ya filamu imekuwa kimya huku baadhi ya wasanii wakiamua kufanya biashara na kujiingia katika mambo mengine tofauti, filamu zimekuwa hazitoki kama zamani,huku wasanii wengi wakilalamikia soko la filamu kuwa baya hivyo kazi haziwalipi wasanii ,ivyo kutafuta njia nyingine ya kujikwamua.

Alichosema Chuchu Hans kuhusu ndoa yake.

Msanii wa Bongo Movie Chuchu Hans amefunguka na kuongelea swala la ndoa yake na msanii mwenzie vicent Kigosi maarufu kama Ray , wawili hao wamekuwa katika mahusiano zaid ya miaka mitatu sasa na ni miezi kama minane tu imepita tangu Chuchu  ajifungue mtoto wao wa  kiume anayeitwa Brian.Hata hivyo msanii huyo wa kike alipokuwa akihojiwa aliongelea swala la yeye kufunga ndoa na baba mzazi wa mtot wake huyo.

Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa tetesi za yeye kuolewa na ray kabla ya kubeba mimba ziliishiwa wapi alijibu kuwa ni kweli  lakini mipango iyo kwa sasa haipo tena,na alipoulizwa sababu kubwa ya yeye kutaka kuhaishirisha jambo ilo Chuchu anasema kuwa inawezekana kwa sababu yeye na baba wa mtoto wake wamezoeana sasa ivyo kwakwe ni kawaida ila hakuna sababu yoyote ya yeye kukataa kuolewa nae.

Kuhusu maisha yake ya ulezi na mtoto wake  mrembo huyo alisema kuwa kwa sasa wanaendelea vizuri na maisha ya ulezi na baba wa mtoto anafanya majukumu yake kama baba na yeye pia anafanya majukumu yake kama mama mzazi.Kwa mujibu wa Chuchu  mahusiano yao yanaendelea vizuri na ndio maana aliamua kumpa baba mzazi huyo zawadi ya mtoto, kwa sababu umri pia unakwenda ivyo ni wakati sahihi yeye kumzawadia mpenzi wake huyo.

Hata hivyo Chuchu  Hans anasema kuwa kwa sasa hivi bado hajafikiria bado kuongeza mtoto wa pili, na kuhusu kumuonyesha mtoto wao wa kiume sura ambae mpaka sasa mtoto huyo ana miezi nane lakini bado hawajaamua kumuonyesha katika mitandao, amesema kuwa huo ni uamuzi wa baba wa mtoto.

Chuchu  Hans ni moja kati ya mastaa wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu,, ukiachana na kuzaa na Ray mtoto mmoja Chuchu tayari alikuwa na watoto wawili  kabla ya kukutana na baba mzazi wa mtoto wake huyu mdogo. Lakini kwa sasa amejikita katika tasnia ya filamu na wanakampuni  yao  ambayo inasimamiwa na yeye mwenyewe.