Belle 9- Dogo Janja Ndio Anatakiwa Kuchapwa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Belle 9 ameibuka na kudai kama kuchapwa anatakiwa kuchapwa Dogo Janja sio yeye.

Wiki iliyopita Dogo janja Kwenye Interview yake alisema Belle 9 anahitaji kuchapwa viboko 70 baada ya kusema Hamuelewi na hata nyimbo zake anzoimba huwa hazielewi.

Kwenye mahojiano na Enews ya EATV, Belle 9 amemjibu Dogo na kusema inabidi achapwe yeye kwani nyimbo yake mpya ya ‘Banana’ ni ngoma ya kihuni na hajaielewa:

Nilivyosema msanii ambaye simuelewi ni Madee sikuwa na maana mbaya na samahani kama wamekasirika lakini niliongea kwa uzuri maana ni msanii ambaye huwa namuangalia.

Kusema ukweli nilivyosikia anasema nichapwe viboko nilicheka sana na huenda tunatofautiana kufikiria na labda kwa mazingira aliyokulia yeye anaona kuchapwa viboko kunaweza kumbadilisha mtu ila sio pointi sana maana mambo yamebadilika.

Halafu kama ni viboko anatakiwa achapwe yeye kwa nyimbo anazoimba zenye  utata kwani nyimbo iliyopita alivaa kama mwanamke na nyimbo yake mpya ya Banana anaimba sijui your my Banana na wote tunajua Banana ina maana gani”.

 

Dogo Janja- Belle 9 Amemkosea Sana Madee

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Dogo Janja anayefanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Banana’ amedai kuwa Msanii mwenzake Belle 9 amemkosea sana Madee hivyo anahitaji kuadhibiwa.

Wiki chache zilizopita Kwenye mahojiano na Jembe FM ya jijini Mwanza Belle 9, alimtaja Madee kama rapa wa Tanzania ambaye haelewi nyimbo zake kabisa anaona kama mzugaji kwani anaona ni msanii ambaye anatoa ‘beat’ tu na sio wimbo.

Katika interview na Enews ya East Africa Tv, Dogo Janja amemjia juu Belle 9 kwa kumwambia kuwa amekosea sana kumbeza msanii mkongwe kama Madee ambaye ameshawahi kutoa ngoma kali nyingi hata kabla ya Belle 9 kujulikana kwenye muziki.

Kitu cha kwanza hata yeye Belle 9 kuna vitu anafanya kuna watu huwa hawamuelewe, hata mimi mwenyewe kuna wanangu kibao huwa wananiambia bora Nuruely. Alichokifanya Made kwenye muziki, Belle 9 hata robo hajafikia.. Respect a legend, waheshimu wakongwe, waheshimu wazee sio busara kutukana wakongwe.

Kakosea amemkosea mzee, anatakiwa apigwe 70 bomani (wamasai hapo wamenielewa) ukivunja sheria au ukimkosea mkubwa au mzee unatakiwa uchapwe fimbo 70 mbele ya wanabomani wote.. Madee mpole sana ndio maana wanamuonea. ni mkongwe anayezeeka na heshima zake”.

 

Sio Rahisi Kusaini Wcb:-Belle 9

Msani wa bongo fleva Belle 9  amefunguka kuhusu kusaini katika lebel ya WCB ,mwanamuziki huyo anaetamba na wimbo wa dada  ameiambia The play List ya   Times fm  amesema kwa anaweza kuwa katika lebel hiyo lakini anaona kuwa  ni vigumu sana kusaini katika lebel hiyo.

ikitokea  tunaweza kusainiwa basi tunaweza kufanya kazi lakini nadhani kuna condition za kusainiwa sio rahisi tu kusainiwa hapo inabidi tupate muda kuiangalia mikataba hiyo kwanza na kuifikisha kwa wanasheria wang kwanza waiangaliae

unajua kwa muda ambao nilikuwa mimi mwenye nilishajua nini ninahitaji ili kutoka hapa kwenda mbele,na kuna jinsi ninavyotaki hii safari iwe.

Siku hapo nyuma karibuni Belle 9 alionekana akiwa na bendi ya wasafi akiwa anafanya mazoezi hata hivyo yeye mwenyewe anasema kuwa alikwenda hapo kwa ajili ya mkataba na bado haujakamilika.

Belle 9- Siuelewi Kabisa Muziki wa Madee

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva aliyetamba na kibao chake cha ‘Masogange’ Belle 9 amefunguka na kumrushia Dongo Zito msanii mwenzake Madee Ali Raisi wa Manzese.

Belle ameweka wazi kuwa Madee ni mmoja kati ya wasanii wa Bong fleva ambaye haelewi muziki wake anaoufanya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na  JJ wa Jembe FM, Belle 9 amesema kuwa kutokana anasikiliza wachanaji wengi wanaofanya vizuri anahisi kuna kitu anakikosa kutoka kwa Madee.

Honesty, let me be honesty, Madee huwa simuelewi. I don’t know, ujue kuna wasanii inafika kipindi unasikiliza unasema huyo mtu ana-release beat sio wimbo tena.

Labda kwa vile nasikiliza rappers ambao wanajua sana au kuna kitu nakitegemea kutoka kwake kutokana muda mrefu yupo kwenye game, kuna kitu nakimisi, so naona kama nikimsiliza na lose”.

Baada ya kimya cha muda mrefu Belle 9 amerudi kwa kasi ya ajabu ambapo kibao kipya cha ‘Dada‘ kimeendelea kufanya vizuri katika vituo mbali mbali vya habari Lakini pia hata mitandao ya kijamii kama Youtube ambapo umeshika nafasi za juu.

Belle 9 Kuimba Gospo.

Mwanamuziki kutoka katika tasnia ya muziki Belle 9 maefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba amepitia magumu mengi yenye kukatisha tamaa katka muziki lakini bado anaona kuwa tasnia ya mzuki bado inamuhitaji na ndio maana hajakata tamaa hata kidogo.

Belle 9 ambae kwa sasa ametoa wimbo wake wa dada anasema kuwa pamoja nakwamba alikaa kimya kidogo kwa muda lakini anashukuru mungu kwa sababu muziki huo umepokelewa vizuri sana kumekuwa na muitikio chanya katika hilo.

Akiendelea kuongelea kuhusu muziki wake , Belle 9 anasema kuwa anataka kufanya kazi za gopso kidogo ili aweze kuweka historia kuwa alishafanya aina zote za muziki katika tasna yake ya muziki,

kitu ambacho sijakifanya katika katika muziki ni kumuimbia mungu , nataka kufanya wimbo wa dini na kikishafanya hilo nitakuwa nimeshafanya kila kitu.

 

Belle 9 Akana Tetesi za Kukimbia Mjini Baada Ya Kufulia

Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Masogange’ Belle 9 amekana tetesi zinazodai kuwa amefulia.

Belle 9 alipata shavu la kusainiwa na label ya ‘Vitamin Music’ ambayo ilimuhamisha kutoka Morogoro na kumleta Dar kwa ajili ya kufanya Muziki lakini baada ya kuoa  Belle 9 alipotea kidogo.

Baadae zilizuka stori kuwa Belle 9 ameamua kurudi nyumbani Morogoro kutokana na kukosa shoo na kufulia hapa Dar kiasi ya kwamba Ana kosa hata pesa ya kulipia kodi ya nyumba.

Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Belle 9 amekana tetesi hizo za kufulia na kusema hajahama Dar bado yupo mjini:

Dah Hapana muda mrefu sijafika Morogoro mi Nipo Dar, hizo ni rumors tu zinazosambazwa na watu Lakini pia naona wanasema hivyo kwa sababu sionekani Kwenye maeneo ya starehe mengi.

Belle 9 amerudi upya na kazi yake mpya aliyotoa siku chache zilizopita inayokwenda kwa jina la ‘Dada’.

Sijaongea na Familia ya Masogange , Sina Ukaribu Nao

Mwanamuziki Belle 9 amefunguka na kusema kuwa hajaongea na famila ya marehemu Masogange kwa sababu hana ukaribu na familia hiyo , lakini anawaza jinsi  kumsaidia mtoto wa marehemu katika maswala ya masomo.

Belle 9 aliongea hayo alipouwa akiongea FNL ya EATV, na kusema kuwa tanfu kumetokea msiba wa mwandada huyo hajapata nafasi kutokana na ukweli kamba hawakuwa karibu na famialia sana kama ilivyokuwa kwa marehemu mwenyewe.

sijapata nafasi ya kuongea chochote kwa sababu hatukuwa na ukaribu mkubwa na watu wa familia yake,kwaio sijapata kuongea kitu na familia  juu ya jinsi ya kumsaidia yule mtoto.

Belle 9 anakiri kuwa aliumizwa sana na msiba wa mwanadada huyo kutokana na ukweli kwamba mafanikio makubwa ya muziki wake yalitokana na masogange aliyenogesha vyema wimbo wake.

Belle 9- Ndoa Haikwamishi Muziki Wangu

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Belle 9 amefunguka na kuweka wazi kuwa kufunga kwake ndoa hukujawahi kukwamisha jitihada zake za kimuziki.

Belle 9 aliwahi kufanya vizuri na ngoma zake kama Masogange miaka ya nyuma alifunga ndoa ya kisirisiri mapema mwaka jana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Friday Night Live ya East Africa Tv, Belle 9 amesema mabadiliko yaliyotokea baada ya kufunga ndoa ni ya kawaida lakini sio ya kukwamisha muziki kabisa:

Kwa kusumbua sanaa hapana, lakini maisha binafsi inakuchukua kidogo.

Kama kijana zaidi ni usiriazi na familia kwa sababu vitu vimebadilika, kabla ya kufanga kuna vitu nilikuwa sivifahamu sasa navifahamu”.

Ni jambo la kawaida kwa wasanii wengi kupunguza kasi ya kimuziki baada ya kuingia kwenye ndoa kutokana na kupata majukumu mapya ya kifamilia tofauti na ilivyokuwa kabla ya kuingia kwenye ndoa.

Belle 9 Akiri Kunyooshwa na Maisha Ya Ndoa

Msanii wa Bongo fleva Abednego Damian maarufu kama Belle 9 amekiri kabisa kunyooshwa na maisha ya ndoa na kukiri tangu ameoa amebadilika sana.

Belle 9 alifunga ndoa mwaka jana mwishoni lakini mpaka mwaka huu mwezi huu ameshainyoshea mikono juu ndoa.

Belle 9 amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda ambapo amekiri kuwa ndoa imemnyoosha tofauti na alivyokuwa mwanzo kabla ya ndoa:

Kiukweli ndoa imenibadilisha sana kwa sababu maisha niliyokuwa ninaishi kabla ya ndoa ni tofauti kabisa na ya sasa.

Kwenye ndoa kuna vitu vingi nimejifunza, nimekuwa ni mtu mpya katika maisha yangu mapya, kwa sasa ninaangalia zaidi familia yangu kwa jumla.”

Belle 9 yupo Kwenye listi ya wasanii wengi masupastaa kama AY, Ali Kiba ambao wameamua kuukimbia ukapera na kufunga ndoa.

Belle 9 Akiri Alishawahi Kufumaniwa.

Msanii wa bongo fleva Belle 9 amefunguka na kuweka wazi kuwa alishawahi kufumaniwa na mpenzi wake akitoka na mwanamke mwingine lakini sababu kubwa anasema kuwa wasanii wengi wa kiumewamekuwa wakitongozwa na wanawake hivyo kuna muda hata wao wanashindwa kujizuia.

Belle 9 ambae alifunga ndoa mwaka jana na mpenzi wake wa muda mrefu na kuamua kufanya siri bila ya watu kujua mpaka pale alipoamua kuweka picha katika mitandao anasema kuwa ni vigumu sana kuepuka maswala ya kufumaniwa kwa sababu wasanii wengi wanakuwa wanatakwa kimapenzi na wanawake.

Nilishawahi kufumaniwa ingawa ni mara chache sana,wanawake wengi huwatamani wanaume wasni kimapenzi, na hii utokea kutokana na ushawishi wa wasanii.lakini mimi nataka mwanamke wangu ajitambue kabisa-Alifunguka Belle 9 alipokuwa akiongea na radio Kings FM.

Vishawishi vinavyotoka kwa wanawake kwenda kwa wasanii vimekuwa b=vingi na wasanii wengi wamekuwa wakikiri kutongozwa na wanawake katika mitandao ya kijamii, hata hivyo kwa sasa Belle 9 ameoa.

 

BASATA na Waziri Wake Wanatafuta Kiki:-Belle 9

Kumekuwa na wimbi la wasanii na wadau mbalimbali wa muziki wakijaribu kutoa maoni yao kuhusu swala la naibu wa ziri mh juliana shonza kufungiwa wasanii wa muziki wa bongo nyimbo zao kwa madai ya kuwa nyimbo hizo hazina maadili.

Msanii Belle 9 nae pia ameibuka na kuongelea swala hilo na kusema kuwa kitendo hicho kwa mara ya kwanza alpokisia hakuchukulia kama jambo baya lakini kwa jinsi siku zinavyoenda na kuona hali inavyokuwa amegundua kuwa naibu waziri na BASATA wanatafuta kiki kupitia wasanii.

Naibu waziri ambae hivi karibuni aliongea na waandishi wa habari juu ya swla hilo, alikuwa akishindwa kujibu baadhi ya maswali ya msingi kutoka kwa wadau wa muziki kitu kilichowafanya watu na wasanii waone kuwa naibu waziri hana sababu ya msingi ya kufanya hivyo.

Belle 9 Amefunga Ndoa Ya Kimya Kimya (picha)

Mwanamuziki wa Bongo fleva Belle 9 ametawala vichwa vya habari weekend iliyopita baada ya picha kusambaa mtandaoni zikimuonyesha akifunga ndoa ya kimya kimya.

Mwaka 2017 ulikuwa mwaka mzuri sana kwa mastaa wengi kwani kuna ndoa kibao zilizofungwa na kuweka headlines kwenye mitandao ya kijamii ndi hizo ni Kama ndoa ya Joti, ndoa ya Uwoya na Dogo Janja, ndoa ya Shilole na Uchebe na nyinginezo.

Inavyoelekea Belle 9 hajataka kufunga mwaka huu bila kufanya na yeye yake kwani siku ya Jana picha kibao zilisambaa mitandaoni zikimuonyesha akiwa na mwanamke ambaye inasemekana ni mama watoto wake au mzazi mwenzake wakiwa katika mavazi yao ya harusi kabisa wamependeza.

Lakini muda mfupi tu baada ya picha hizo za maharusi kusambaa mtandaoni ndipo na tetesi za utata zilianza kusambaa kuwa ile haikuwa harusi ya kweli Bali ni shooting tu nyimbo yake mpya huku wengine wakidai kuwa ni ndoa ya kweli ilyofungwa kwao Morogoro na ilipaswa iwe ya siri sana miongoni mwa familia tu .

Hizi ni baadhi tu ya picha zilizo onekana mtandaoni:

 

 

 

 

Belle 9 mpaka hivi sasa hajasema kitu chochote kuhusiana na ndoa hiyo au sababu zipi zilimfanya afanye ndoa yake iwe ya siri .

Belle 9 Amefunguka Baada ya Video Kuvuja Akiwa na Mchepuko Wake

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Belle 9 ameamua kuongelea video ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa na mwanamke mwingine mbali na mama watoto wake.

Watu wengi hawajamzoea Belle 9 kuwa aina ya msanii ambaye anapenda kiki kwaiyo kitendo cha video iliyomuonyesha Belle 9 akiwa na mwanamke mwingine katika pozi la kimahaba kuashiria kabisa wana uhusiano wa kimapenzi liliwashtua watu wengi.

Inafahamika kuwa Belle 9 anaishi na familia yake na kwa sasa ana watoto watatu na anaishi na mama watoto wake sasa video ike  iliposambaa akiwa na mwanamke mwingine ambaye anasemekana ni mchepuko wake ilisababisha minong’ono mikali mtandaoni.

Belle 9 Alipopiga stori na kituo cha televisheni cha East Africa kupitia kipindi cha Enews alikataa kata kata taarifa kuwa mrembo yule ni mchepuko wake bali alidai kuwa ile video ni ya zamani ila aliwahi kuwa mpenzi wake hapo nyuma.

Of course ile video clip ni ya muda mrefu na huwezi ukazuia matumizi ya mtu anavyotumia Simu yake mtandao wake kwaiyo ni kitu ambacho kimetokea au naweza kusema ile video ni ya muda mrefu sana lakini imekuja kuvuja siku za hivi karibuni na make wangu anajua hilo hasa kwa sababu mimi ni msanii kwaiyo nakuwa name zungukwa na watu tofauti lakini sina mtu mwingine wa kumlaumu zaidi ya mimi mwenyewe kwa sababu kitendo kile kilitokea wakati mimi nipo kwaiyo sina mtu mwingine wa kumlaumu”.