Barakah The Prince alaumu siasa kwa kusababisha wimbo wake kutofanya vizuri

Barakah The Prince anadai kuwa siasa Tanzania ni moja ya vitu ambavyo vinasababisha nyimbo za wasanii kutofanya vizuri.

Muimbaji huyo amekiri kuwa wimbo wake mpya ‘Acha Niende’ aliyowachia miezi mitatu iliyopita uliathirika na kipindi cha mpito ambao umebadilisha hali ya muziki nchini.

Akiongea katika kipindi cha Enewz cha EATV, Barakah The Prince alisema kuwa ‘Acha Niende’ haukufika malengo ambayo alijiwekea wakati alitoa wimbo huo.

“Hali ni ngumu kweli kwa wasanii, nyimbo nyingi ambazo zimetoka hivi karibuni zimeshindwa kufanya vizuri kusema kweli hata wimbo wangu haujafikia kwenye malengo ambayo nilijiwekea wakati natoa au hata nikilinganisha na nyimbo zangu zilizopita,” Barakah The Prince alisema.

https://www.youtube.com/watch?v=IKjVsyA77II

Barakah the Prince amjibu Ben Pol baada ya kudai walimpunguza kwenye show

Msanii kutoka Tanzania Barakah the Prince amefunguka kwa mara ya kwanza kumjibu Ben Pol ambaye alidai hivi karibuni kuwa msanii huyu alipunguzwa kwenye show ambayo alitakiwa kutokea na wasanii wenzake Kama Juma Jux.

Akizungumza kwenye interview mpya na kipindi cha XXL cha Clouds FM Barakah alisema kuwa wake Ben Pol alichozumgumzia kwenye interview yake ni uongo, huku alisema;


“Mimi sipunguzwi, nilijitoa nikawaambia nina menejiment ambayo ina utaratibu wake, ninapofanya kazi lazima kuwe na makubaliano na mkataba kwa sababu wao walishindwa kufuata utartibu nikajitoa kwenye hiyo show yao.”

Aliendelea kwa kusema,

“Hatukuwa na muungano wowote kusema kwamba tulikuwa na tour, tulifanya show moja tu ile, show iliyofuata uongozi wangu ukataka utaratibu wa hizo show waliposhindwa nikawaambia mimi sitaweza kufanya. Sema nyimbo yake ni mbaya asitafute sababu ya kujitetetea… utovu wa nidhamu yule (Ben Pol) baba yangu?”

Barakah The Prince awararua mashabiki wake ambao walimuita msaliti

Barakah The Prince hatambui kwamba mashabiki wake ndo wanachangia yeye kufauli kimuziki – mwimbaji huyo alikerwa sana baada ya kuitwa msaliti.

Siku chache baada ya kuonekana kwa picha na Babu Tale ambaye ni meneja wake Diamond Platnumz, baadhi ya mashabiki wake walimkosoa kwa kile walitaja kama usaliti.

Babu Tale na Barakah The Prince

Barakah The Prince na Alikiba wako katika lebo inayoitwa Rock Star 4000. Mashabiki wa Barakah walimwita msaliti kwasababu Diamond and Alikiba ni maadui.

Hit maker huyo hata hivyo hakufuraishwa kuitwa msaliti, aliwaonya mashabiki wasimpangie maisha yake binafsi. Aliwaambia kwamba wao kinachowahusu kutoka kwake ni muziki mzuri tu.

“Wewe kama ni shabiki wangu wa muziki haimaanishi pia ni shabiki wa maisha yangu binafsi, maisha yangu binafsi mniachie. Shabiki wewe ni nani sasa mpaka unipangie maisha? kama mtu niliyepiga naye picha ni binadamu siyo shetani lakini cha ajabu mashabiki ndiyo wanaonitukana na kuongea hivi na vile wakati uongozi wangu haujasema kama nakosea,” Barakah The Prince alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.