Aunty Lulu Asherekea Mama Yake Kupata Mchumba

Msabii wa Bongo movie Lulu Semagongo maarufu Kama Aunty Lulu amefunguka na kutangaza furaha yake Baada ya mama yake mzazi kupata mchumba na hatimaye kuchumbiwa.

Aunty Lulu amesherehekeamama yake mzazi kupata mchumba ambaye alimvalisha pete mwishoni mwa wiki iliyopita katika kanisani moja lililopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Aunty Lulu alisema kuwa amefurahi sana mama yake kumpata mwenza kwani baada ya baba yake kufariki dunia, alikaa muda mrefu akiwa mpweke.

Unajua nina furaha kupita kiasi mama yangu kupata mwenza imenipa faraja, ninamuombea maisha mema ya ndoa kwani ni jambo ambalo limetufurahisha sisi kama familia”.

Aunty Lulu ameweka wazi kuwa mama yake hakuwa kwenye mahusiano na baba yake kwa miaka mingi hivyo vyema mama yake kuuaga upweke na kupata furaha.

Aunty Lulu Aunga Mkono Operesheni Ya Makonda

Msanii wa filamu za Bongo movie Lulu Semagongo maarufu Kama Aunty Lulu ameibuka na kudai anaunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda za kupambana na Mashoga.

Wiki mbili zilizopita Mheshimiwa Paul Makonda alitangaza rasmi vita na Vijana wanaofanya Mapenzi ya jinsia moja maarufu Kama Mashoga katika mkoa wa Dar Es Salaam.

Katika mahojiano yake na Global Publishers, Aunty Lulu amedai amefurahishwa mno na hatua aliyoichukua Makonda kwani naye ni mmoja wa mastaa waliokuwa wakiishi na mashoga, lakini Mungu akamuokoa na kuachana nao hivyo zoezi hilo litasaidia kwani mashoga hao wamesababisha hata wanawake wasiolewe.

Ninampongeza sana Makonda maana hawa mashoga ni janga la kitaifa, naomba akishawakamata wakipimwa na kugundulika wanafanya ufuska huo, wakusanywe kwenye uwanja mkubwa wachapwe viboko baada ya hapo ndiyo wapelekwe gerezani kwa sababu wanawake tunakosa kuingia kwenye ndoa kwa sababu yao”.

Lakini pia Aunty Lulu alimuomba Makonda azungumze na Rais John Pombe Magufuli ili msako ufanyike kwa nchi nzima kwani mashoga wengi wamekimbia jijini Dar na kwenda mikoani.

Aunty Lulu Amdondoshea Mate Diamond

Msanii wa Bongo movie Lulu Semagongo maarufu kama Aunty Lulu amefunguka na kudai anataka sana kuzaa na msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Aunty Lulu amesema kuwa ingawa anajua itakuwa ngumu kwa yeye kuzaa na Diamond kwa sasa kutokana na Msanii huyo kusema amejifunza kutumia kinga ili kuepuka watoto wa nje lakini yuko tayari kutafuta mganga wa kumloga.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Aunty Lulu amesema ni ndoto yake ya muda mrefu kuzaa na Diamond hivyo ili itimie atafanya juu chini mpaka ampate hata kwa kumloga ili akikutana naye asahau hata kutumia kinga aweze kumpa ujauzito.

Diamond amesema kwa sasa yuko makini ili asizae nje ya ndoa lakini kwangu mimi nitamloga mpaka aweze kuzaa nami kwa kuwa ni muda mrefu nina ndoto hiyo na hakuna kitakachonizuia maana namwamini sana mganga wangu“.

Kwenye Interview aliyofanya mwezi uliopita Diamond alidai kuzaa na Hamisa ilikuwa ni kosa hivyo amejifunza kutumia kinga anapokuwa na michepuko.

Aunty Lulu Apanga kumlonga Diamond Ili Aweze Kuzaa Nae.

Ingawa hapo karibuni mwanamuziki Diamond Platinumz alisema kuwa moja ya vitu anavyoangalia sana na kujifunza ni kutumia kinga ili kuweza kuepuka kupata watoto wa nje ya ndoa kama ilivyotokea hapo awali kwa wanawake wengine lakini bado kuna wanawake wana ndoto ya kuzaa na mwanamuziki huyo.

Moja ya wasanii wa bongo movies aunty lulu amefunguka na kusema kuwa hata yeye ataenda kwa waganaga ili amloge Diamond ili aweze kupata nae mtoto kwa sababau anatamani sana mtoto na msanii huyo.

Diamond anasema kwa sasa yuko makini sana ili asipate mtoto nje ya ndoa,lakini kwangu mimi nitamloga tu mpaka apate kuzaa na mimi, kwa kuwa ni muda sasa nina ndoto hiyo na hakuna  kitakachoweza kunizuia kwa sababu nimekuwa nikimwamini sana mganga wangu.

Diamond ambae kwa sasa amekuwa na watoto watatu wa wanawake wawili tofauti alisema kuwa hataki tena kuongeza mtoto mpaka pale atakapoamua kuoa ndipo atakapozaa tena.

WOWOWO Lampatia Aunty Lulu Wachumba Watatu

Mtangazaji na muigizaji wa Bongo movie Lulu Semagongo maarufu kama aunty Lulu amewaacha watu wengi midomo wazi baada ya kudai kalio lake kubwa limemsaidia kupata wachumba watatu nchini China.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Aunty Lulu alifunguka na kudai kuwa kwenye Safari yake ya kibiashara nchini China hivi karibuni alihudhuria kwenye ukumbi mmoja ambao kulikuwa na msanii ambaye ni Mtanzania ambaye alikuwa anapiga shoo.

Aunty Lulu amedai baada ya muziki kuanza kupigwa alianza kucheza na kukata mauno kiasi ya kwamba wanaume walianza kumtolea macho na usiku huo alipata wachumba watatu ambao wapo tayari kumuoa.

Kalio langu limenipatia wachumba wa Kichina watatu, sasa baada ya wote kuniambia wanataka kunioa, niliwatajia mahari yangu kuwa ni shilingi milioni 50 na walikubali, lakini niliwapa mtihani mwingine kwamba atakayekuwa wa kwanza kufika Bongo ndiye atakayenioa, hivyo ninasubiri na ndoa yangu itakuwa ya mkataba”.

 

Aunty Lulu Atoa Ofa Kwa Papii Kocha.

Mwanadada aliyewahi kujipatia umaarufu wake kwa kazi ya utangazaji ambae pia haachi kuwa na drama za mara kwa mara, Aunty Lulu amefunguka na kusema kuwa yupo tayari kumpa ofa msanii wa muziki papii kocha kwa muda wot mpaka asahau maisha ya jela aliyoyapitia.

Aunty Lulu anasema kuwa amemuona papii kocha na ameona jinsi ambavyo amekuwa akipendeza na kuwa mpya hivyo yuo tayari kumpa penzi litakalomfanyua asahau shida na mateso aliyokuwa ameyapitia kipindi yupo jela.

Aunty Lulu ambae amejisifia kuwa anajua sana kupenda amesema kuwa yuko tayari endapo msanii huyo atakubali kumpatia nafasi.

Unajua mimi najua kupenda,endapo nitampatia penzi papii kocha mbona atasahau kabisa alipotoka.Yeye akubali tu mbona sijawahi kuona mahusiano yake,naamini kwa kipindi alichokaa jela kama angekuwa na mwanamke angekuwa tayari ameshajitokeza siku nyingi.-Alifunguka Aunty Lulu.

Jitihada za kumtafuta papii kocha ziligonga mwamba baada ya simu ya msanii huyo kutokupatikana ili kujulishwa taarifa hizo.

Papii kocha na baba yake walikuwa wasanii wa muziki waliofanya vizuri kwa muda mrefu lakini kazi zao zilisimama baada ya kukaa jela kwa muda mrefu kwa kosa la kulawiti watoto , lakini mwaka 2017 mwishoni wasanii hao walipokea msamaha wa rais na kuachiwa huru.

wasanii hao sasa hivi wamepanga kurudi kwa kasi ya ajabu huku wakiwa chini ya studio ya Wanene Entertainment huku wakipokea msaada na uangalizi wa wizara ya habari na michezo ili waweze kuimarika kimuziki.