Aunty Ezekiel Kufunga Ndoa Na Iyobo.

Moja ya wasanii kongwe nchini katika tasnia ya filamu, eunty ezekiel amefunguka na kusema kuwa kwa muda ambao amekaa na mzazi mwenzie ni wakatiu mufaka kwao sasa kufung ndoame  na mwanau yme huyo.aunty ezekeiel ambae amekuwa na uhusiano na mwanaume huyo kwa zaidi ya miaka mitatu na kuweza kubahatika kuzaa mtoto mmoja ya kike amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa siku yoyote.

aunty na moze iyobo amabe ni moja ya madansa maarufu tanzania akiwa katika kundi moja la madansa kutoka wcb kwa msanii diamond platinumz  wamekuwa ni moja ya watu maarufu walidumu katika mahusiano na kufanya mapenzi yao kuwa pendwa kwa mashabiki wao.

Akizungumza na moja ya gazeti pendwa nchini, Aunty Ezekiel amesema kuwa anaona kabisa kuwa kwa muda aliokaa na Iose iyobo  unatosha kabisa kufunga nae ndoa kwa sababu wameshajuana vya kutosha ingawa mara ya kwanza hakuwahi  kufikiria kama hatafunga ndoa hivi karibuni.

Unajua huko nyuma nilikuwa sian wazo kabisa  nilikuwa sina wazo kabisa na ndoa  lakini sasa niko tayari, na kuanzia sasa au wakati wowte watu watasikia tu kuhusu ndoa yangu. Alifunguka Aunty.

Hata hivyo hii itakuwa ni ndoa ya pili kwa Aunty Ezekiel ambapo ndoa ya kwanza aliyofunga miaka ya nyuma kidogo kuvunjika.

Kwa hivi karibuni, Aunty Ezekiel atakuwa msanii wa pili kutangaza habari za ndoa ambapo msanii wa kwanza ni Shilole ambae mpaka sasa vikao vya maandalizi ya harusi yameshaanza kufanyika.

Waigizaji Wa Bongo Movie Kukimbilia Siasa Ni Kukosa Kazi- Aunty Ezekiel

Muigizaji wa tathnia ya Bongo Movie, Aunty Ezekiel amefunguka na kudai kuwa kitendo cha wasanii wengi kujiingiza katika masuala ya siasa ni matokeo ya wao kukosa kazi za kufanya.

Kwenye uchaguzi wa uraisi wa mwaka 2015, tulijionea jinsi gani wasanii mbalimbali wa Bongo movie walivyojitokeza na kujiunga na vyama mbalimbali vya siasa lakini pia wengine si kujiunga tu walifikia hadi hatua ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kama vile udiwani na ubunge. Wasanii kama Wema Sepetu na  Irene Uwoya walijaribu nafasi zao na kugombea nafasi za ubunge wa viti maalumu ingawa walikosa.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Times Fm, Aunty Ezekiel alifunguka kuwa sababu kubwa inayopelekea wasanii hao kujitosa kwenye mambo ya siasa ni kwasababu za wao kukosa kazi zakufanya pamoja na umaarufu unaopelekea msanii akifanya kidogo tu anaonekana kama amejitoa sana upande huo.

Hii yote inatokana na kukosa kazi kwa sababu mwisho wa siku kazi zetu zimekuwa hazina ushindani yaani tumesimama katika Kazi zetu wenyewe kwaiyo tunajikuta hata kwenye yale ambayo hayatuhusu tunaenda kuyaingilia , na kwanini unaona bongo movie tu ndio wanashiriki kwenye mambo ya siasa , sio wao tu unaweza ukakuta wananchi wengi wanashiriki lakini kwa kiwa sisi ni public figure ukishiriki hata kidogo unaonekana umeshiriki pakubwa, lakini kwangu mimi kwa sasa nimejitenga na siasa”.

Mwaka 2015 kipindi cha uchaguzi mkuu Aunty Ezekiel na Wolper waliingia katika skendo mara baada ya kuhama Chadema na kuhamia CCCM ambapo baadae ilikuja julikana kuwa walilipwa donge nono la pesa kitendo kilichopelekea kubatizwa majina ya Yuda lakini Aunty amekiri kuiweka siasa pembeni kwa sasa.

Bongo Movie Nzima Hakuna Mwanamke Aliyetulia Kama Aunty Ezekiel- Steven Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie na mdau Mkubwa wa siasa, Steven Nyerere aliye maarufu zaidi kwa uwezo wake Mkubwa wa kuigiza sauti ya Marehemu baba wa taifa, Julius Nyerere amefunguka na kudai hakuna mwanamke aliyetulia kama Aunty Ezekiel.

Siku mbili zilizopita mkongwe mwingine wa Bongo movie Adam Haji au maarufu Kama Baba Haji alidai kuwa Aunty Ezekiel amepitiwa na wanaume wengi Kama Kanumba lakini yeye ndo alikuwa ana uhusiano naye wa kweli akimaanisha yeye ndo mwanaume pekee aliyetulia Nate ingawa wanaume wengi kwenye maarufu walimpitia.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Star Mix, Steven Nyerere alidai kuwa mwanamke anayemheshimu hivi sasa kwenye bongo movie ni Aunty Ezekiel kutokana na kuwa ni mwanamke ambaye hajajibweteka na amejitahidi sana kukusanya pesa anazozipata kufanya mambo ya maana kama alivyojenga nyumba maeneo ya Kigamboni tofauti na mastaa wengine hasa wanawake:

Yaani kusema ukweli kwa bongo movie kwa Bongo movie nampa sana heshima Aunty Ezekiel ni mdada aliyetulia na mzazi mwenzie amepata mtoto lakini bado ni mtafutaji tofauti na wanawake wengine hasa mastaa lakini pamoja na hayo yote ameweza kujitumia na kujenga nyumba tofauti na mastaa wengi wa Bongo Movie”.

Alichokiongea Baba Haji Kuhusu Aunt Ezekiel,Kanumba Nae Atajwa

Msanii wa filamu bongomovies Haji Adam amefunguka na kuongea kuhusu mahusiano yake na msanii mwenzie Aunty Ezekiel kipindi cha nyuma ambapo kwa sasa yuko katika mahusiano na mnenguaji kutoka wasafi.

Akiongea na Global Tv baba haji ansema kuwa yeye na Aunty Ezekiel walikuwa  na mahusiano ya mapenzi kwa muda mrefu na walikuwa karibu sana , hata hivyo yeye ndie alikuwa na ataendelea kumjua Aunty Ezekiel kuliko mtu mwingine yeyote yule kwa sababu amekaa nae muda mrefu.Baba Haji anasema kuwa hata kama wamegombana lakini hawawezi kuacha kuongea na Aunty Ezekiel kwa sababau wanaheshimiana sana.

Mrs Iyobo mimi alikuwa mtu wangu kabisa, na ni mtu ambae mimi ninamfahamu kuliko muigizaji yeyote yule anavyomfahamu yeye,na tumebaki na heshima hiyo na tulikuwa na uhusiano wa kimapenzi kabisa.na ninamjua sanaa, watu wengine wanakuja na kupita tu juu juu lakini mimi namjua sana kuna nani sijui kapita na nani na nani .” alifunguka Haji Adam

Hata hivyo katika maongezi yake alisema kuwa anatambua wanaume wengi wamepita na mwanadada huyo lakini katika hao ni yeye tu ndo aliyekuwa akimjua vizuri , hata hivyo ameongezea na kusema kuwa anajua kuwa Aunty pia alishawahi kutoka na Kanumba.

wengine wanakuja na kupita tu, kanumba alikuja akapita ila mimi namjua sana na ni mtu ambae katika maisha yetu mimi na yeye haitakaa kutokea siku moja  iwe tunaugomvi kwa sababu kuna kitu kikubwa sana Aunty Ezekiele alinifanyia kitu kikubwa sana

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameonekana kukwazika na kitendo hicho cha msanii huyo kuongelea mahusiano yake na msanii huyo ambae sasa hivi anafamilia yake na mume wake pia, hata hivyo wengine waliendelea kuchukizwa na tabia ya Haji Adam kuanza kutaja wanaume aliotembea na dada huyo maana hayo ni maisha yake binafsi.

Aunty Ezekiel kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja na amekuwa na mahusiano ya muda mrefu na baba mzazi wamtoto wake huyo anaejulikana kama Moze Iyobo.

Aunt Ezekiel aeleza sababu zake za kutotokea kwenye Bongo Movies

Aunt Ezekiel ambaye ni muigizaji wa movie za Bongo hivi karibuni amefunguka kueleza mbona haonekani kwenye movie hizi Kama kitambo.

Mose Iyobo na Aunty Ezekiel

Mrembo huyo ambaye ni mama ya mtoto mmoja na mpenzi wa dancer kutoka Wasafi Records hivi karibuni alifunguka kudai kuwa anapumzika kwa sasa lakini hivi karibuni. Aunt Ezekiel alikiambia kipindi cha Twenzetu cha Times FM.

“Bongo Movie tunaweza kusema ni kama maisha ya binadamu, kuna time analala, anaamka, anapika, so kunakuwa na kazi tofauti tofauti. Naweza kusema kwa sasa hivi Bongo Movie ni muda wetu wa kurelax kwanza kwa hiyo tumepumzika, tumelala tukishaamka nadhani tutakuja na vitu vingi vya tofauti.”

Aliongeza,

“Sio kwamba tukilala ndio hakuna kitu ambacho kitakuja kikubwa zaidi au hakitachukua akili za Watanzania tena, hapana kulala kwa Bongo Movie ni kulala kwa kujipanga ili tunapokuja kurudi tena turudi vizuri, so mimi siamini kama Bongo Movie imekufa, tumerelax tu,”

Hata hivyo aliyekuwa rafiki yake wa karibu Wema Sepetu amekuwa akiachia projects zake mpya pole pole.

Mchumba wa Aunty Ezekiel aeleza mbona hawezi kuwa muimbaji wa Wasafi records

Moses Iyobo ambaye ni dancer maarufu wa Diamond Platnumz amefunguka kwa nini hawezi kuwa muimbaji ataiwapo angepewa fursa hiyo.

Akiongea na gazeti maarufu la Dimba, Mose alisema kuwa hana mipango ya kuingia katika muziki na kuwa kwa hivi sasa lengo lake ni kuwa dancer ambayo ni kazi anayoifanya kwa hivi sasa.

Mose Iyobo na Aunty Ezekiel
Mose Iyobo na Aunty Ezekiel

Kiluingana na yeye, kuwa muimbaji inatakiwa mtu kuwa na kipaji ambacho yeye mwenyewe hana kwa hivyo si kitu ambacho anaweza kufanya na kufanikiwa. Alisema,

“Unajua kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe, sasa kwa upande wangu sitaweza ni bora nibaki huku huku ndio pananifaa zaidi,”

Ata hivyo Mose Iyobo alisema kuwa angependa kuwa mwalimu wa kuwafindisha vijana kuwa dancer kama yeye. Kuna watoto ambao wangependa kuwa dancers wakiwa wakubwa kwa hivyo ni heri yeye kuanzisha shule ambayo atawafundisha ili hapo mbeleni waweze kutambulika kama yeye.