Aunty Ezekiel Atoa Tamko, Hata Kama Wema Hataenda, yeye South Africa Ataenda Tu.

Mwanadada Aunty Ezekiel amefunga mjadala uliokuwa ukiendelea baada ya kusemwa kwa maneno ya muda mrefu kuhusu uamuzi wa Diamond kuwataka yeye pamoja na Wema kwenda afrika ya kusini katika sherehe ya Tiffah.

Tamko la kwenda afrika ya kusini lilitolewa na Diamond mwenyewe na kusema kuwa katika watu kumi watakaokwenda ni lazima awepo Wema na Zari na ndipo Zari alipoanza kuwajibu katika mitandao kuwa hataki kuona watanzania watamchafulia nyumba.

Hata hivyo wengi walihisi kuwa tamko la Zari lingeweza kubadilisha mawazo ya wahusika lakini Aunty Ezekiel ameamua kujibu na kusema kuwa hata kama Wema hatokwenda Afrika ya kusini lakini yeye ataenda kwa sababu yeye ni  moja ya wanafamilia , lakini pia Zari pia ni wifi yake.

Ifike sehemu inabidi  tufunge mjadala maana kila siku ni aunt kuwa karibu na zari,wema na kama ni bethdei nitaenda tu.Hawa wote ni marafiki zangu kwa hiyo sasa siwezi kubagua eti kwa sababu wema aliachana na Diamond  wakati pia kule kwa Diamond kuna penzi wangu Iyobo  na isitoshe kwa upande mwingine Zari ni wifi yangu.

Aunty Ezekiel Awatolea Povu Wanaohoji Ukaribu Wake na Zari Pamoja na Wema

Msanii filamu za kibongo Aunty Ezekiel amemwaga povu kwa mashabiki Kwenye mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wakimsema na kumuita Yuda kwa kitendo chake cha kuwa na ukaribu na Wema pamoja na Zari.

Mashabiki Kwenye mtandao wa Instagram ambao wamegawanyika Kwenye team Wema na Team Zari wamekuwa wakimpiga majungu Aunty na kumuita Yuda msaliti baada ya kutangaza kwenda nchini South Africa kushiriki birthday ya Tiffah.

Kwenye mahojiano na gazeti la na Amani, Aunty alisema majungu hayo yameanza mitandaoni baada ya kusikia amealikwa kwenda kwenye bethidei ya mtoto wa Zari, Tiffah inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao lakini kamwe majungu hayo hayamsumbui.

Ifike mahali tufunge mjadala, kila siku ni Aunt kuwa karibu na Zari, Wema kama ni bethidei nitaenda tu. Hawa wote ni marafiki zangu sasa siwezi kubagua kwa kuwa eti Wema aliachana na Diamond wakati kule kwa kina Diamond pia kuna mpenzi wangu Iyobo na isitoshe Zari ni wifi yangu kwa upande mwingine“.

Kwa miaka mingi Zari na Wema wamekuwa kama paka na panya kwa ajili ya kugombea penzi la Diamond kwaiyo kitendo cha Aunty kusema anaenda Kwenye sherehe ya mtoto wa Zari kiliwashangaza watu wengi hasa kwa sababu Aunty rafiki yake kipenzo ni Wema.

Aunty Ezekiel- Sipendi Kuishi Maisha Ya Kuigiza Mitandaoni

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Aunty Ezekiel amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi kuishi maisha ya kuigiza tajiri kwenye mitandao ya kijamii wakati hana kitu.

Aunty amefunguka hayo baada ya hivi karibuni kusemwa Kwenye social media baada ya kuonekana amerudia nguo aliyovaa Kwenye msiba wa mtoto wa  Muna ambayo alishavaa Kwenye misiba kadhaa siku za nyuma.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Amani, Aunty Ezekiel, amesema anawashangaa watu wanaomjadili kuwa anarudia nguo na kumtaka anunue nguo kila siku kitu ambacho yeye anaona hakina maana.

Eti kila sehemu niende na nguo mpya au hata msibani nibadili nguo ina maana nitakuwa sina vitu vingine vya kufanya vya maendeleo zaidi ya kununua nguo kwa ajili ya maonyesho? Watu wasinijadili, sina muda huo wala kufuata wanayotaka wao”.

 

Aunty Ezekiel Amwaga Povu Baada Ya Tuhuma Za Kurudia Nguo

Muigizaji wa filamu za Bongo Movie na mfanyabiashara Aunty Ezekiel ameibuka na kumwaga povu kwa watu waliokuwa wanamsema amerudia nguo aliyovaa Kwenye msiba wa mtoto Patrick.

Siku ya Jumamosi Aunty Ezekiel aliungana na Familia ya Muna na ndugu jamaa na hata wasanii wenzake katika mazishi ya Mtu Patrick yaliyofanyila katika viwanja vya Leaders na kuzikwa Makaburi ya Kinondoni.

Lakini mara tu baada ya kupigwa picha akiwa amevaa gauni lake jeusi  mjadala mzito uliibuka Kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu walimtuhumu kwa kurudia nguo ile aliyokuwa amevaa Kwenye msiba.

Baada ya kuona mjadala huo mtandaoni Aunty alitumia ukurasa wake wa Instagram kumwaga povu ambapo aliwataka watu wasimfatilie kuhusu mavazi yake na ni uamuzi wake kurudia nguo kwani hakuna anayejua maisha yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Aunty Ezekiel aliandika:

Naomba niseme hivi mimi huwa sifanyi maisha ya maigizo 

Baada Ya Kunusurika Kifo, Aunty Ezekiel Arudi Kanisani

Staa wa filamu za kibongo mwanamama Aunty Ezekiel Grayson amerudi kanisani baada ya kunusurika kuchungulia kaburi baada ya kuumwa sana.

Siku chache zilizopita picha zilisambaa zikimuonyesha Aunty Ezekiel akiwa amelala Kwenye kitanda cha hospitali huku akiwa hoi taabani.

Baadae taarifa zilisambaa kuwa Aunty Ezekiel anasumbuliwa na ugonjwa wa Malaria ambao ulimfanya mpaka alalazwa.

Lakini tangu janga hilo litokee Aunty Ezekiel anafunguka na kudai kuwa aliumwa kiasi cha  kudhani kuwa angekufa.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Aunty Ezekiel amekiri kuwa tangia amepona ameamua kwenda kanisa la Katoliki la Kisarawe mkoani Pwani, mahali ambapo alikulia.

Mungu alinitendea makuu kwa kuniinua tena kitandani na kuweza hata kuzungumza hivyo sina budi kumshukuru”.

Aunty Ezekiel alikiri kufanya hivyo kwa sababu alipokuwa akiumwa hakujua kama ataweza kuinuka tena na kuzungumza kama zamani kwani alishakata tamaa, lakini Mungu akamponya hivyo hana budi kumrudishia shukurani.

Aunty Ezekiel: Sioni Tatizo Kuvaa Nguo Niliyoshonewa na Mobetto

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amewatolea povu zito watu wote waliomkoso kwa kuvaa nguo aliyoshonewa na Mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Siku ya uzinduzi wa filamu yake fupi ya Mama Aunty alivaa nguo nzuri nyekundu na kupendeza kupita kiasi ambapo baadae aliweka wazi kuwa aliyemshonea nguo ile ni Hamisa.

Mashabiki wengi walimjia juu Aunty kwa kuvaa nguo ya Hamisa huku akijua wazi yule ni adui namba moja wa Zari na pia adui wa shoga yake Wema Sepetu.

Kwenye mahojiano na gazeti la  Amani, Aunty amekiri kutowaelewa wanaoshangaa ishu hiyo kwa sababu yeye na Mobeto hawana ugomvi wowote na wala hajawahi kukosana naye, sasa kitakachomfanya ashindwe kuvaa nguo aliyomshonea ni kitu gani?.

Mimi ninawashangaa sana wanaoongea kuhusiana na kuvaa nguo ambayo nimeshonewa na Hamisa. Sioni tatizo kwani tofauti zake na mtu mwingine mimi hazinihusu“.

Mashabiki ambao ni Team Zari wamekuwa wakimtolea maneno Aunty kwa usaliti aliofanya kwa Zari kwani wengi waliamini kuwa ni rafiki yake lakini kama utakumbuka siku za nyuma Aunty alishasema kuwa hana urafiki na Zari wala Hamisa.

Hii Ndio Sababu Iliyomzuia Wema Kufika Kwenye Uzinduzi Wa Filamu Ya Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kutaja sababu iliyomfanya mpaka asiweze kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya Aunty Ezekiel.

Siku ya Jumapili Aunty Ezekiel alikuwa anafanya uzinduzi wa filamu yake fupi ya dakika 20 inayoitwa MAMA pale Kwenye ukumbi wa Cinema Mlimani City.

Wema Sepetu ambaye mwanzoni alitoa taarifa ya kuthibitisha kuwa atakuwepo eneo la tukio kumpa sapoti Aunty Ezekiel ambaye pia ni rafiki yake kipenzi kabisa hakuonekana mpaka shughuli inaisha.

Siku ya jana Wema aliweka wazi kuwa sababu kubwa iliyomfanya mpaka asihudhurie shughuli hiyo ilikuwa ni kucheleweshwa na Mama yake mzazi ambaye alikuwa naye na hivyo kujikuta kapitisha muda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema aliandika:

I was soooo Ready for MAMA Short Film But My MAMA Took my Time aswell… Nikachelewa…???,”

Hata hivyo Aunt Ezekiel alipohojiwa na Mwananchi Digital sababu za Wema Sepetu kushindwa kufika katika uzinduzi huo alisema ni kutokana na gauni la mrembo huyo alilotakiwa kuvaa kwenye uzinduzi huo lilikuwa bado lipo kwa fundi halijamalizika kwa sababu ya kukatika kwa umeme.

Uzinduzi wa Filamu ya Mama(+picha)

Taher 13 May mwaka huu Aunty Ezekiel aliamua kuweka historia katika maisha yake baada ya kufanya uzinduzi wa filamu yake mpya inayojulikana kwa jina la mama huku mhusika mkuu akiwa ni aunty ezekiel pamoja na mtotowake mdogo wa kike Cookie Iyobo.

Aunty ezekiel akiwa na Nice chande

 

 

 

Zamaradi Mketema akiongea na waandishi wa habari

 

Diamond platinumz alikuwepo kutoa sapoti yake.

 

 aunty ezekiel akiwa na cookie pamoja na mume wake moze iyobo.

 

moze iyobo akiwa na mtoto wake cookie ambae ni mhusika mkuu katika filamu hiyo.

Diamond akiwa pamoja na mama yake mzazi 

Aunty na Rammy Wajibizana kwa Sababu ya Rambirambi ya Agness

Kumekuwa na figisu figisu nyingi kuhusu rambirambi ya mwanadada agness masogange aliyefariki wiki chache zilizopita huku wakimtuhumu  kiongozi wao  steve nyerere ambae anasemekana kuwa ndie aliyekula  pesa hizo.

Ingawa Steve Nyerere  aliwajibu na kusema kuwa rambi rambi ya marehemu haitakabithiwa kwa ndugu wa marehemu kwa sababu marehemu alikuwa na mtoto aliyekuwa anamtegemea na alimwacha akiwa anasoma hivyo pesa hiyo atakabithiwa mtoto na sio ndugu wa marehemu ikifika 40.

Sasa sakata lingine linakuja baada ya aliyekuwa ex wa Masogange( Rammy Galis)  kuamua kuto ayake ya moyoni kuhusu swala hilo la rambi rambi na kusema kuwa anasikitika sana kuona kuwa michango hiyo haijafikka kwa walengwa na kusema kuwa atajitahidi filamu waliocheza wote inaawanufaisha familia yake.

@rammygallisofficialsintofahamu ya michango ya msiba wako zinanisikitisha sana , namuomba Mungu anisaidie ili niweze kutoa kile  kitaachobarikiwa kwa kazi ya mikono yako na wangu (HUKUMU) , Sania yupo kwa niaba yako.

Baada ya kuandika hivyo Aunty Ezekiel nae alionekana kukwera na maneno hayo na kuamua kumjibu Rammy kwa kusema kuwa aache tabia ya kuwa  na drama na kuwahumiza wafiwa.

Wewe ulitoa shingapi kwenye huo msiba , punguzeni drama basi kwenye mambo ya familia za watu  tena wenye majonzi bado.

 

 

Aunty Ezekiel- Zari na Hamisa Sio Marafiki Zangu

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kuweka wazi kuwa hana urafiki wowote na Mama watoto wa Staa Diamond, Zari na Hamisa Mobetto.

Kwa muda mrefu inajulikana kuwa Aunty Ezekiel ana urafiki na Wema Sepetu kwaiyo siku ambayo alionekana na Diamond na Zari visiwani Zanzibar wakila bata watu wengi walichukulia kama usaliti kwa rafiki yake.

Hivi sasa Tetesi zinadai kuwa Diamond yupo Kwenye Mahusiano na Hamisa Mobetto ambaye ni adui namba moja wa Wema Sepetu hivyo Kolabo mtu amekuwa akihoji Aunty atakuwa upande gani kama ni Hamisa au Wema?.

Lakini Aunty ameshaweka wazi kuhusu hilo na kudai hahitaji kuchagua upande kwa kuwa Zari na Hamisa sio marafiki zake bali Wema ndiye rafiki yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Aunty ameweka wazi kuwa Diamond sio bosi wake bali ni mshkaji wake wa siku nyingi kabla hata hajaanza Mahusiano na Moses Iyobo.

Naseeb is not my boss, Naseeb mimi ni rafiki yangu na mshkaji wangu ni mtu ambaye nimejuana naye kabla ya kujuana na hawa watu wengine wote yaani tumejuana kivyetu na sio Kupitia Mahusiano yetu.

Hamisa sio rafiki yangu na wala Zari sio rafiki yangu na hata mwanamke mwingine wa Diamond sio rafiki yangu lakini Wema mimi ni rafiki yangu”.

 

Uchungu Upo Ila Inabidi Kuacha Kumlilia-Aunty Ezekiel

Staa mkubwa wa filamu za bongo Aunty Ezekiel amesema kuwa hakuna sababu ya kuendelea kumlialia staa mwenzao wa filamu aliekuwa gwiji steven kanumba zaidi ya kumuombea na kufuata nyayo zake ili kukuza kazi za sanaa.

Aunty anasema kuwa uchungu na kumbukumbu yake badio itaendelea kuwepo ila kwa heshima kubwa ya kumuonyesha steven ni kuiga mambo mazuri aliokuwa akifanya ili kuendelea kumuenzi.

Aunty anasema kuwa wasanii wengi wamekuwa wakilia sana inapofika siku ya kukumbuka siku ya kifo chake,kitu ambacho yeye anaamini kuwa inarudisha tasnia ya filamu nyuma kwa sababu ya kusononeka kwao.

Najua uchungu upo lakini inabidi sasa tuache kulia,badala yake tujitahidi kufika pale ambapo na yeye alitaka tufike na tusonge mbele lakini tukisema kuwa kila siku tubaki tunasononeka hatuwezi kufika tunapopataka hata siku moja.

 

Aunty Ezekiel Awataka Wasanii Wenzake Waache Kumlilia Kanumba

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kuwaasa wasanii wenzake wa Bongo movie waache kumlilia msanii mwenzao Steven Kanumba na badala yake waenzi kazi zake.

Steven Kanumba alikuwa msanii wa Bongo movie ambaye alikuwa ni mfano wa kuigiza na kila msanii kwani uwezo wake wa kuigiza na ubunifu ili we za kwa kiasi kikubwa kuifikisha tasnia hiyo mbali.

Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu tasnia hii imkumbuke siku ya kifo chake ambayo inaitwa Kanumba Day, Aunty Ezekiel amefunguka na kusema sasa kuomboleza kifo chake tu kumetosha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Aunty Ezekiel amesema kuwa  mara nyingi wasanii wanapoadhimisha kumbukumbu ya kifo chake, wanakuwa wanalia au wengine wanasononeka mara kwa mara hiyo inakuwa inazidi kurudisha tasnia nyuma badala yake wasanii wakaze buti waweze kufika alipokuwa amefika yeye.

Najua wazi uchungu upo lakini inabidi tuache sasa kulia badala yake tujitahidi kufikia pale alipotuacha ili tuzidi kusonga mbele maana tukisema kulia kila siku hatuwezi kufika tunapotaka hata siku moja”.

 

Sitokaa Nigombane na Ex- wa Moze Iyobo.:-Aunty

Msanii wa bongo movie ambae pia ni fanya biashara Aunty Ezekiel, amekiri na kusema kuwa alikuja kukaa na kugundua kuwa kugombana na aliyekuwa mwanamke wa baba wa mtoto wake kwa sasa ni jambo lilisilokuwa na maana na kusema kuwa hatokaa afanye jambo hilo tena.

Aunty ana sema kuwa hata kama wangekuwa wanagombana miaka yote isingeweza kubadilisha majina ya watoto wao au kuvunja uhusiano wa baba na mtoto na pia isingeleta picha nzuri kwa mtoto baadae hivyo aliona bora kuachana na mambo hayo.

katika vitu ambavyo vilipita na nikaandika , nilisema sitakaa nigombane na mwengi hata siku moja., tena kwa sababu nimekuja kugundua kuwa ni ujinga tu na kla kitu kina mwisho na katika kugundua kwangu nilijua kabisa yule mtoto hatokuja kubadilisha jina lake la mwisho kuwa ni wa moze.kwa sababu miwsho wa siku ataitwa fuani fulani iyobo na ndivyo itakavyokuwa na kwa cookie m na sasa hivi mitandao ni mingi mwisho wa siku wamekuja kukua waje waone kuwa mama wa huyu na yule walikuwa wanagombana , haitaleta pcha nzuri.

Baba wa mtoto wa Aunty Ezekiel ambae pia ni mcheza dansa maarufu wa Diamond Platinumz amekuwakatika mapezni na aunty kwa zaidi ya miaka minne sana na kupata mtoto wa kike mmoja lakini kabla ya hapo mwanaume huyo alikuwa katika mahusiano na mwanadada  mwengi na kubahatika kupata mtoto wa kiume na amekuwa akimuweka sana katika mitadano ya kijamii ambapo hapo awali Aunty alikuwa akitukanana sana na mwanamke huyo.

Uoga kwako ndio kufeli kwako:Ujumbe wa Aunty Ezekiel kwa Diamond

Mwanadada Aunty Ezekiel arusha kombora kwa waliofungia nyimbo za wasanii !!. Muigizaji huyo wa filamu ameandika haya katika ukurasa wake wa instagram huku akimtaja diamond platinumz kama shujaa katika kusimama imara ili kutetea muziki huo.
.
Uoga wako ndio kufeli kwako…..diamondplatnumz Am so proud of u kiukweli unajua unachokifanya haijalishi anaetaka kukukatisha Safari yako ni Nani na ana cheo gani ! Ilimradi unajua haki yako basi weka uwoga pembeni na kutetea haki yako….SAFI SANA ….Ktk kazi hizi kwa asilimia kadhaa hawa watu wamekuwa wakichangia kufeli kwa kazi zetu tena Mbaya zaidi hutokeza baada ya kuona kuna baadhi ya mafanikio kupitia fani hiyo Ila wakati mkihangaika kusukuma gurudumu huwa wamekaa kimya kama hawapo. Mnakosea Sana tena Sana mnakatisha tamaa, mnafelisha watu Pamoja na Maisha yao bila kufikiri kuna watu wangapi Nyuma yake ambao anawabeba na kufanya Maisha yaende….Nashindwa kuandika sana lakini natamani tuu wajue kuwa WANATUKOSEA SANA SANA SANA……Wasanii tuinuke na kuwa na Uthubutu wa kusema yote yale ambayo tunaona tunaonewa na sio kukaa kuongea chini chini haitatusaidia na tutaendelea kufeli na wao wakifaulu kwa kuonekana wafanyakazi Bora kumbe hamna lolote Uonevu tuu…

Hata hivyo baada ya mwanadada huyo kuongea hivyo diamond platinumz alimjibu na kusema:

Ni muda wa kujenga Sanaa iliyo kubwa na yenye kuleta mafanikio kwa wasanii na serikali….sio kuleteana figigufigisu kisa eti una mamlaka kutafuta eti Kiki ama eti uonekane we flani uogopewe HELL NO !

Aunty:Mose Hashangai Picha Zangu za Uchi.

Msanii wa bongo movies na mjasirimali Aunty ezekie marufu kama Mama cookie amefunguka na kusema kuwa mzazi mwenzie huwa hashangai waa kushtuka na picha za nusu uchi anazokuwa anapiga kwa sababu anajua kabisa ni za matangazo na zipo kwa ajili ya kutangaza biashara.

Aunty Ezekiel ambae amekuwa katika mahusiano na moja ya madancr wakubwa tanzania kutoka kundi la wcb amesema kuwa  hata mara nyingi picha hizo anazokuwa anapiga zenye kumuonyesha yuko uchi zinakuwa znapigwa na mume wake huyo akiwepo kwaio haina madhara yoyote kwa sababu anakuwa anajua kitu anachokifanya ni kwa ajili ya biashara.

Iyobo hawezi kushangaa hata siku moja kuona picha ninaopiga na kuziweka katika mitandao kwa sababu anajua ni za matangazo,anajua kabisa kuwa ni za matangazo na ni kazi kwaio haina shida  na kuna muda mwingine hata yeye mwenyewe anakuwepo na anakuwa anatoa kabisa ushauri  na mawazo kuwa zinapigwaje.

Picha hizo tata za aunty ezekiel amekuwa akiztupia katika mitandao ya kijamii kwa kutangaza biashara yake ya sabuni ya murua mabapo baadhi ya mashabiki walitaka kumuonya mwanadada huyo kaucha kuweka picha hizo ili yasije yakatokea yake ya wasanii wengine waliofungiwa kazi zao.

 

 

 

Aunty Awashushua Wanaomsema Anakaa Nyumba Ya Kupanga.

Msanii mkongwe  wa bongo movies na mjasiriamali  Tanzania Aunty Ezekiel, amefunguka na kuwashushua watu wanaomsema kuwa tangu ameanza kuwa maarufu mpaka sasa hivi bado anaishi katika nyumba ya kupanga na hajafanikiwa kuwa na nyumba yake wakati ana jina kubwa na amekuwa akitengeneza ela inayoweza kumfanya kujenga nyumba yake.

Hata hivyo aunty amejitetea na kusema kuwa anakaa katikati ya mji kjitonyama kwa sababu ni karibu na anakofanya shughuli zake nyinginlakini ana nyumba ya kwake mwenyewe Kigamboni lakini hawezi kwenda kukaa huko kwa sababu ni nje ya mji na ni mabli na nyumbani kwake.

Nawashangaa sana wanaosema  hivyo kuwa sina nyumba sijui wamejualiwa wapi hayo yote,mimi nimeamua kupanga katikati ya mji ili niweze kufanya kazi zangu kwa urahisi zaidi na kama ni nyumba mbona ninayo huko kigamboni ? –Aliongea Aunty Ezekiel

Aunty Ezekile ni mamam wa mtoto mmoja wa kike aliyezaa na mcheza dancer maarufu kutoka katika lebel kubwa nchi ya Wasafi chuni ya bosi wao Diamond Platinumz.

Maneno haya yanakuja baada ya wasnaii wengi tanzania kuwa wakiishi maisha ya juu huku wakiwa hawana sehemu za kukaa zaidi ya kupanga nyumba zenye gharama na baada ya muda wanapopata matatizo wanashindwa pa kujistiri na kuanza kuomba msaada kitu kinachofanya kupotosha kazi ya sanaa na watu wengine kuona kama haina faida yoyote.

Lakini bado watu hawapaswi ku-judge na kuongea maneno bila kuwa na uhakika wa kile wanachokuwa wakikiongea kwa sababu sio kila mtu anapenda kuweka maisha yake hadharani.