Aikah Afunguka Kukosa Raha Kisa Ubonge

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika Kundi la Navy Kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuweka wazi Jinsi miwili mkubwa unavyokuwa unamnyima raha hasa stejini.

Aikah ambaye ameonekana kukosolewa sana na mashabiki zake hasa katika Mitandao ya kijamii amefunguka na kukiri kuwa anajua kabisa ameongezeka sana lakini anafanya jitihada za kupungua.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Aika alisema amekuwa akiteseka na ubonge alionao kwa sasa kwani haupendi na watu mbalimbali wamekuwa wakimshangaa na kumtaka aanze kufanya mazoezi kwani anapoteza mvuto.

Siupendi ubonge nilionao kwa sasa, mashabiki wangu kibao wamenitaka nianze kufanya mazoezi kwa sababu kunenepeana huku napoteza mvuto. Nimepokea maoni yao na nitaya fanyia kazi maana nimejikuta nanenepa kutokana na uzazi”.

Aikah ambaye ana Mtoto wa mwaka mmoja na Mpenzi Wake Nahreel ameweka wazi kuwa alizidi kuongezekabzaidi Baada ya kujifungua mwaka jana.

Aikah Afunguka Kuhamia WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Kutoka katika kundi la Navy Kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuongolea taarifa za kuhamia WCB.

Baada ya kutoa hit single ambayo inaendelea kufanya vyema mpaka sasa ‘Katika’ waliomshirikisha Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuliibuka tetesi kuwa Nahreel na Aika wamehamia chini ya WCB.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers , Aika  amesema kuwa, amekuwa akisikia kwa watu wengi juu ya kuhamia WCB mara baada ya kuachia wimbo wao  na Diamond jambo ambalo halina ukweli.

Yaani watu wengi wanasema nimehamia WCB lakini ukweli ni kwamba tuna meneja anayetokea huko anaitwa Sallam na amekuwa akitusimamia sasa sijui hayo mengine yanatokea wapi.

Nilikaa na mwenzangu tukatunga Wimbo wa Katika tukaona ni vizuri tukamshirikisha Diamond ndiyo ikawa hivyo sasa nashangaa hao wanaoungaunga maneno”.

Tetesi hizo za Kuhamia WCB zilipamba moto mara baada ya Msanii kutoka WCB Harmonize kusema wazi kuwa wasanii hao wanahamia Kwenye Label yao taarifa ambazo Navykenzo walidai ulikuwa ni utani.

Aikah Aandaa Navykenzocup Kwa Ajili Ya Watoto Wa Mitaani

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika kundi la Navykenzo, Aikah Mareale amefunguka na kuelezea jinsi alivyosaidia watoto wa mitaani baada ya kuwakusanya na kutengeneza Navykenzo Cup.

Aikah ameeleza hayo wakati akiwa anatamba kuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja na si kutegemea muziki tu.

Katika mahojiano na Ijumaa Wikienda, Aika alisema kwa sasa anafanya kazi tofauti za kijamii kama kuwakusanya watoto wa mitaani ambao wanaweza kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu.

Pamoja na kuwa mimi ni mwanamuziki na mama pia namuomba Mwenyezi Mungu anisaidie jukumu hili lingine la kuchukua watoto wa mitaani na kuunda timu ili waweze kushindana na kuonesha vipaji ili baadaye wacheze kwenye timu kubwa“.

 

Aikah Navykenzo Afungukia Ndoa na Nahreel

Mastaa wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika kundi la Navy kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ wana mipango ya ndoa.

Wasanii hao ambao wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa zaidi ya miaka 10 walibahatika kupata mtoto wao wa kwanza mapema mwaka huu anayeitwa Gold Navykenzo.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Aikah amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kwamba wameshazaa nje ya ndoa lakini anaona ni jambo la kawaida na wana mipango ya ndoa.

Kwangu ninaona ni kawaida. Sisi siyo watu wa kwanza kupata nje ya ndoa mtoto, lakini mipango ya kufunga ndoa ipo na muda ukifika tutafunga ndoa.

Lakini pia Aikah ameanika changamoto wanazopitia katika kulea mtoto wao na kufanya muzikI katika wakati mmoja:

Kuna changamoto sana na si jambo rahisi hata kidogo kulea mtoto na kufanya muziki. Tangu tupate mtoto mambo mengi yamekwama kiasi kwamba kuna ‘interview’ nyingi tumezipiga chini ili tu kudili na mtoto. Unajua sisi ni wazazi wapya kwa hiyo mambo mengi tunajifunza“.

Aikah Afunguka Mpango Wa Kuzaa Mtoto Mwingine

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika kundi la Navy Kenzo Aikah Mareale amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kuzaa mtoto mwingine na mpenzi wake Nahreel.

Aikah alijifungua mtoto wake wa kwanza anayeitwa Gold Navykenzo mapema mwaka huu na mpenzi wake wa siku nyingi Emmanuel Mkono maarufu kama Nahreel.

Lakini Gold akiwa na Miezi michache tu Aikah amefunguka na kusema yupo mbioni kutaka kuongeza mtoto mwa pili.

Kwenye mahojiano na Risasi Vibes, Aika amesema kuwa tangu amezaa mtoto mmoja ameona raha kuwa mama hivyo basi hana muda wa kujishauri tena bali ni kumleta mdogo wa Gold, mapema wala hana muda wa kupoteza.

Najisikia furaha sana kuwa mama hata wa watoto watano hivi nimeona raha ya kuzaa na hivi sasa niko njiani kuleta mtoto mwingine mambo ya kupishana muda mrefu sio sawa kabisa”.

Aikah na Nahreel wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka zaidi ya kumi Lakini hivi karibuni walisema hawana haraka ya kufunga ndoa kwani kuwa na bond ni muhimu zaidi.

Tazama Video na Picha za Baby shower Ya Mtoto Wa Aika na Nahreel

Mwanamuziki Nahreel na mpenzi wake Aikah wanaounda kundi Kali la mziki Navykenzo ambao wamewahi kutamba na vibao vyao vilivyofanya vizuri kama kamatia chini na game, wamesheherekea baby shower kwaajili ya kumkaribisha mtoto wao.

Wiki chache zilizopita Nahreel na Aikah waliweka wazi kuwa wanategemea ujio wa mtoto wao wa kwanza wa kiume atakayeitwa jina la Gold. Siku ya jumapili Wazazi hao watarajiwa walifanya bonge la sherehe kwenye jumba lao jipya la kifahari wanaloliita CasadeKenzo.

Hizi ni baadhi tu ya picha zilizopigwa kwenye sherehe hiyo.

Aikah na Nahreel wakifurahia jambo