T.I.D- Kutoa Nyimbo Mara Kwa Mara In Ushamba na Uroho Wa Kutaka Kusikilizwa

Msanii mkongwe wa Bongo fleva T.I.D ameibuka na kudai kuwakuwa wanamuziki kutoa nyimbo mara kwa mara ni uroho wa kutaka kujulikana wenyewe tu.

T.I.D aliyasema hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na Lilommy ambapo alidai kuwa wasanii wanaotoa nyimbo kila siku ni washamba, hwajiamini na wana uroho wa kutaka kusikilizwa.

download latest music    

Kwenye Mahojiano hayo T.I.D alifunguka yafuatayo:

“To me ukiniambia kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja I don’t think kwamba ni kitu cha maana kwanza msanii unakuwa unajiangusha kwasababu in one way or another humpatii mtu nafasi, hapa sio Marekani huko mziki ni kazi kubwa sana people have a lot of time technology kwao imefika mda mrefu alafu wapo wengi kiasi cha kwamba unaweza ukatoa nyimbo mbili kwa wakati mfupi sasa Tanzania bado ni ndogo sana ukitoa nyimbo moja kali alafu ikapigwa mara mbili tatu ikapata airtime nzuri alafu ukatoa nyimbo nyingine hapo hapo utakuwa umepoteza pesa ya nyimbo ya kwanza, watu wengine wanakuwa na haraka kutaka kusikilizwa sana kwangu Mimi naweza kutoa nyimbo moja ikakaa ikauza kutoa nyimbo nyingi ni kushindwa kujiamini unakuwa Una hamu ya kukaa kwenye masikio ya watu huwapi nafasi wengine soko letu ni dogo sana”.

Kumekuwa na mjadala mkubwa Kama ni sawa kwa msanii kutoa  nyimbo mara kwa mara au wasubiri muda mrefu, msanii Kama Diamond anasifika kwa kutoa nyimbo zake kila baada ya muda mfupi lakini Alikiba hukaa muda mrefu halafu huja kutoa nyimbo zake.

Je unahisi ipi ni sahihi kutoa nyimbo mara kwa mara au kusubiri mda upite?

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.