T-Bway Akacha Mahusiano na Uwoya
Baada ya kusambaa na kuvuja kwa picha ikimuoyesha msanii na mjasiriamali Irene Uwoya ambae pia ni mke halali wa ndoa wa msanii wa bongo fleva Dogo Janja na mwanahabari na mtangazaji T-bway wakiwa wameonekana wakiwa kitandani faragha, mwanaume huyo ameamua kufunguka na kusema kuwa picha hiyo ni ya zamani kabla hata wawili hao hawajafunga ndoa.
Irene Uwoya mabe amekuwa akiingia kwenye skendo hivi karibuni tena hasa baada ya kufunga ndoa na Dogo Janja ambae ni mdogo kwake kiumri ameonekana kuwa ni tabia yake kutembea na wanaume walio chini ya umri wake maarufu kama vi-ben 1o kwa sabau hata huyo T-bway ni mdogo kiumri.Hata hivyo baada ya picha hiyo kuvuja katika mtandao bado ilileta tafrani kwa sababu Dogo Janja na Irene hawana muda mrefu tangu kufungwa kwa ndoa yao hivyo inakuwaje tena Irene kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine.
Akiandiak katika ukurasa wake wa instagrma Dogo Janja alionekana kutokujali kwa maneno na picha hizo na alisema kuwa hawezi kugombana na mke wake huyo mpendwa kwa sababu ya maneno ya watu kwa sababu anampenda sana mke wake,
Hata hivyo nae R-bway hakuwa wazi sana kuhusu maneno yake ila alisema kuwa wamekuwa wakimsema kuhusu picaha hiyo ilhali ni ya zamani.
when you wake up in the morning and you find out everything everything is going west but you decide to go east #YAZAMANIKABISA-Aliandika t-bway katika ukurasa wake.
Inasemekana kuwa wawili hao walikuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu zamani kabla mwanadada huyo hajaolewa na kuwa mke halali wa Dogo Janja.
Picha zilizovuja zikiwaonyesha Irene Uwoya akiwa na T-bway faragha,