Steve Nyerere Alia na Waandaaji wa SZIFF

Msanii na kiongozi wa umoja wa bongo movie nchini amefunguka yaliyopo moyoni mwake na kusema kuwa waandaaji wa tuzo za sinema zetu iliyofanyika juzi katika ukumbi wa mlimanai city hawajafanya usawa kwa sababu wapo wasanii wengi ambao walistahili kuwekwa katika kategoria mbalimbali na wangeweza kushinda lakini wao wamebana sana.

Steve nyerere ambae pia hata hakutaka kuonekana katika tuzo hizo usiku ule huku akiwa kama kiongozi wa bongo movies anatoa sababu ya kutokuonekana pale na kusema kuwa wasanii wengi  wameachwa nyuma sana.

download latest music    

Steve anasema kuwa hajwenda kwa sababu kuna wasanii kama kina kitale, asha boko walitakiwa kutafutiwa nafasi zao ili kupata ushindi kwa sababu wanastahili lakini wao waandaaji wamechagulia watu waliokua wanawajua tu.

nitakiongea nilichokiona jana kwenye tuzo,kwani Ray, Jb, roams, aunty ezekile, Shamsa ford, Duma , Weru, Hemedi,Johari, Irene, Tausi , Batuli na hata Mainda wanaofanya vizuri wako wapi?na mbona sijawaona na kuna vijana wengi wazuri ambao ni machipukizi wako wapi

Tangu kumepita kwa tuzo hizi , kumekuwa na maneno mengi sana huku wengine wakisema kwa wasanii wengi waliopata tuzo hizo hawakustaili kuzipata kwa haki.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.