Steve Nyerere Akubaliana na Uamuzi wa Katibu Kuhusu Wasanii Kutotumika Katika Kampeni

Msanii wa maigizo na vichekesho nchini, steve nyerere ameongelea majibu ya kile kilichosemwa na katibu mkuu wa CCM hivi karibuni kuhusu wasanii wa muziki  nchini kutotumika katika kampeni za CCM kama ilivyokuwa hapo awali .

Mwaka 2015 kipindi cha kampeni wasanii wa bongo movies na wasanii wa bongo fleva walitumiwa katika kampeni  katika mikoa mbalimbali lakini katibu mpya wa CCM anasema kuwa wamemaua kwa sasa wasifanya hivyo kutokana na heshima ya wasanii katika kufanya kazi zao.

download latest music    

Akiongea na EATV, steve nyerere anajibu kuwa  hawezi kuonelea chochote kuhusu swala hilo kwa sababu katibu mkuu ana nafasi kubwa sana katika chama na kama ameamua hivyo basi hawawezi kupinga kitu.

swala la  Bashiru siwezi kuliongelea kwa sasa , licha ya kuwa amesema hivyo lakini walifanya kazi kubwa sana na ndio maana tunawathamini, , siwezi kubishana na katibu mkuu kwa sababu yeye ana nafasi kubwa sana katika chama.

Hata hivyo steve anasema kuwa kwa sababu wanaheshimu sana maamuzi hayo wao kama wasanii hawatafanya lolote mpaka pale watakapoambiwa  cha kufanya hivo anawaomba wasanii wenzake wakae kimya na kuacha kujibizana na watu ambao wanaweza kuwabeza.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.