Steve Nyerere Afungukia Sakata Lake na Muna Atangaza Kumsamehe
Muigizaji wa Filamu za kibongo na kiongozi wa Kamba hiyo Steve Nyerere ameibuka na kuongelea sakata lake yeye na Muna na kutangaza kuwa ameamua
Muna alipoongea na waandishi wa habari, alikanusha baadhi ya taarifa ambazo zilitolewa na Steve Nyerere zikidai kuwa muigizaji huyo amekubali kushirikiana na Mumewe Peter Komu katika kumzika mtoto Patrick ambaye Muna amekanusha kuwa sio wa Peter bali ni wa Casto Dickson.
Steve alifunguka siku ya jana Kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo ameamua kupangua hoja zote zilizotolewa na Muna ambazo zinamuhusu yeye.
Kwanza nimpe pole dada yangu Muna kwa kupita katika kipindi kigumu sana, kwa kuondokewa na mtoto. Tulikuwa tumejipanga kwenda kumuona, tukaambiwa kwa waliokoka huwa hawana 40, lakini kwa mzazi lazima kuwepo na 40. Mimi siyo mjinga wa kukurupuka tu kutangaza kuhusu msiba bila kuambiwa na wahusika wa msiba, sikukurupuka, mimi ni mtu mzima, nina familia na watoto, nilipewa maagizo hayo na Muna mwenyewe akiwa na ‘mumewe’ Joel Lwanga wakiwa Kenya, alinipigtia simu.
Nimemsikia akizungumza maneno mazito, eti nyumba anayoishi Peter haina hati, kama haina hati basi itakuwa ni ya serikali wakachukue nyumba yao. Anatukandamiza na kutoa voice, ametoa hisia zake kwa Watanzania, ametufundisha sisi vijana na wazee. Tukisema tufuatilie tutakuta mtoto uliyemsomesha hadi chuo kikuu ni wa mlinzi, mwanamke mwenye busara lazima awe na staha, ndoa siyo kitu cha mchezo jamani.
Nimemsamehe Muna kwa sababu hajui kama anachokizungumza anakifahamu. Hili liwe funzo kwa dada zetu, mimi nimemsamehe hata nikikutana naye asiogope kunisalimia, Shilole naye amemsamehe, usipoimamini biblia utamwamini sheria”.