Steve Awaomba Wasanii Wote Wasimame na Wasanii Wenzao

Msanii wa Bongo movie na komedian maarufu Steve Nyerere ameibuka na kuwataka Wasanii Wenzake wote kuungana pamoja na kuwaombea msamaha wasanii wenzao.

Steve amewataka wasanii wote kwa jumla bila kujali wa muziki au filamu kuwa pamoja kumuombea msamaha msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama ambaye mpaka sasa yupo kituoni kwa kosa la uharibifu wa mali ya umma.

download latest music    

Maua na mtangazaji wa Clouds, Soudy Brown wanadaiwa kusambaza video mitandaoni ikionesha watu wanaokanyaga noti za shilingi elfu kumi ambalo ni kosa la kisheria.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers,  Steve Nyerere amesema  anawaomba wasanii waungane kumuombea msamaha Maua kwani ni mwenzao.

Msanii yeyote ni kioo cha jamii, chochote atakachokifanya kinaweza kuwa na faida au hasara, kwa kile walichokifanya, mimi na wasanii wote bila kujali wa muziki au wa filamu tuwaombee kwa vyombo vyote husika kwa kuwa natumaini wamejifunza na naomba tu wapewe dhamana”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.