Stanbakora Ajitolea Kulipa Deni la Tunda Kwa Aunty Ezekiel

Msanii wa maigizo ya vichekesho  Stan Bakora ameingilia kati ugomvi kati ya Aunty Ezekiel na video queen Tunda baada ya kuona kuwa ugomvi huo umeendelea kwa muda mrefu na hakuna muafaka wa kizuri kitakachoendelea.

Tunda na Aunty Ezekiel jana waliingi aktika ugomvi mkubwa baada ya Aunty Ezekiel kudai kuwa Tunda alikopa pombe yake dukani na kisha kushindwa kulipa ela hiyo.hata hivyo ugomvi huo ulieindelea na mzazi mwenzie na aunty ezekiel (Mose Iyobo) aliingilia kati ugomvi huo na kisha kuingia tena katika bifu hilo.

download latest music    

Hata hivyo Tunda leo alipopata nafasi ya kusimulia tukio hilo alikataa kudaiwa na aunty na kusema kuwa pombe hiyo aliichukua kwa Mose Iyobo na walikubaliana kuwa Aunty Ezekiel hasijue chochote kuhusu deni hilo lakini anashangaa kwanini hayo yote yanatokea.

Msanii wa maigizo ya vichekesho Stan Bakora katikaukuasa wake wa instagram alisema kuwa anamjua na kufahamiana na tunda kwa muda mrefu hivyo anajua Tunda hawezi kufanya jambo kama hilo hivyo yeye atajitolea kulipa deni hilo kama atapata uthibitisho wa kuwa deni hilo lipo.

“Tangu nimeanza kujuana na Tunda sijawahi kuishi nae vibaya, hivyo @auntyezekiel na @moseiyobo kama mnamdai hiyo pesa basi nitalipa mm”.

                                                              

Hata hivyo bado Tunda hataki kukubali kosa hilo na kusema kuwa Aunty Ezekiel amekuwa akitafuta kiki kupitia yeye na ameona kuwa hajaongelewa kwa muda mrefu katika mitandao na ndio maana ameanza kwa kumchokoza ili apate cha kuongelewa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.