Snura Aibuka Kudai Haki Zake Mahakamani
Mwanamama anaendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na uchezaji wake katika video zake na kufanya vizuri katika stage za muziki Snura Mushi maarufu kama Snura Majanga ameibuka na kwenda mahakamani kudai haki zake za malipo kwa kampuni moja nchini baada ya kampun hiyo kutumia wimbo wake wa Majanga katika tangazo lao bila kuwa na idhini yoyote kutoka kwake kama mmiliki wa nyimbi hiyo.
Snura anasema kuwa kampuni iyo inayoshughulika na bidhaa za unga imetumia wimbo wake wa majnaga katika matangazo yao lakini yeye hakuwa na taarifa zozote kama mmiliki hiyo inabidi kampuni iyo imlipe fidia kwa kosa ilo.
Akiongezea , anasema kuwa tayari alishatafuta mwanasheria na mwanasheria huyo alishawatumia ‘notice’ kampuni hiyo ya unga kuwa ndani ya siku saba wawe tayari wameshamlipa fidia yake inayokadiriwa kuwa ni bilioni 2.1 kwa kutumia wimbo huo.
Hata hivyo Snura anasema kuwa kesi hiyo imesota kwa muda wa zaidi ya mwaka sasa na ameshaangaika sana na kutafuta wanasheria mara tatu zaidi, na alitumia baadhi ya mamalka husika na bado hakuweza kufanikiwa kwa chochote.
kwakweli nimesumbuka kwa muda mrefu sana,tangu mwaka 2015 nimetafuta wanasheria zaidi ya mara tatu ikashindikana, na bado nilienda mpaka COSOTA nako hakuna kilichoeleweka lakina kwa sasa nimepata mwanasheria mwingine ambae naamini kuwa atanifanikisha na nitapata haki zangu kama ilivyokuwa maana ushahidi na kila kitu kipo
Snura hatokuwa msanii wa kwanza kupeleka kampuni mahakamani, hivi karibuni kulikuwa na kesi nyingine mahakani iliyohusisha kampui ya tigo na wasanii Ay na Mwana Ka kutokana na kutumia nyimbo zao kwa miito ya simu kwa wateja bila kuwa na ridhaa yao.
Makampuni na vyombo vingi vimekuwa vikitumia nyimbo za wasanii katika shuguli zao bila kuwa na hati miliki kutoka kwa msanii husika , ambapo hii ni moja ya kukandamiza na kuwaburuza wasanii kwa sababu wanapotoa ngoma zao moja ya vitu vinavyotakiwa viwape faida ni matumizi ya nyimbo hizo katika matangazo na shughuli mbalimbali za kiofisi kwa sbabu hata wao kuna faidia wanaingiza wanapotumia nyimbo hizo.