“Siwezi kutoa nyimbo mpya kila siku”-Lady Jay Dee
Msanii mkongwe kabisa wa kike kutoka tanzania ambae alianza muziki na bado anaendelea nao kwa mud amrefu pamoja na kuwa game linazidi kubadilika lakini bado yuko imara katika kazi zake mwanadada jay dee amefunguka na kusema kuwa hawezi kuwa anatoa nyimbo mpya kila siku kwa sababu anaamini kuwa nyimbo zake ni nyimbo zenye hisia sana na huishi muda mrefu hivyo si lazima kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja.
Mwana dada huyo ambae hivi juzi ametoa wimbo mpya unaokwenda na jina la ‘i miss you’ ambao umetengenezwa na producer man water ambae pia ametengeneza nyimbo zake nyingine nyingi ikiwepo ule wa ndindindi anasema kwa sasa wasanii wengi wamekuwa wakitoa nyimbo mfululizo bila kujali kuwa wimbo uliopita umekaa kwa muda gani,”siwezi kuwa natoa nyimbo mpya kila siku ,kwa sababu nyimbo zangu ni za hisia sana ambazo zinaweza kukaa hata miaka kumi.Ni bora nitoe wimbo mmoja kwa mwaka lakini uwe unaishi miaka mingi kwa ladha ile ile siku zote‘ amesema jay dee
Akizungumza na kipindi cha planet bongo cha East Africa Radio ,pia lady jay dee amepata nafasi ya kuzungumziz kwa ufupi hali ya usalama inayoendelea nchi ikiwepo kuuawa na kutekwa kwa baadhi ya watu maarufu akiwepo msanii wenzio roma mkatoliki lady jay dee anasema “kitendo cha mtu kuweza kupigwa risasi hadharani inatishia amani sana, vilevile kuna wasanii walikuwa wametekwa,unaogopa,sehemu yenye amani vitu kama hivi haviwezi kutokea,ninaweza nisiwe na maneno ya kusema nikabaki kusikitika tu kwasababu sio mambo mazuri haya yanayotokea,na yanaonyesha kuwa sio kuzuri tunakoelekea” ameongezea dada mkubwa.
Lady jay dee ni moja kati ya wasanii wakongwe kabisa wenye mchango mkubwa katika kukuza sekta ya muziki wa bongo fleva Tanzania na amekaa katika kazi hii zaidi ya miaka kumi na bado nyimbo zake zimekuwa ni nyimbo zenye kupendwa na mashabiki sana ,kiasi kwamba hata zile za zamani bado zinapendwa na watu .