Siwezi Kurudiana na Petit Hata Iweje :- Esma
Dada wa msanii Diamond Platinumz , maarufu kama Esma Platinumz amefunguka na kusema kuwa hata iweje hawei kurudiana na mzazi mwenzie petit man
Esma amefunguka hayo kufuatia kuvuja kwa video mtandaoni ikiwaone- sha wawili hao waki- wa pamoja na wadau kuanza kuwapongeza wakidhani wamerudiana.
“Hatujarudiana. Hiyo video ni ya siku nyingi, wewe an- galia hata hizo nguo tulizovaa sidhani hata kama wote tunazo hadi sasa, ni za siku nyingi sana. Kwa
sasa mimi jamani hata iweje siwezi kurudiana na Petit,” alisema Esma. Septemba, mwaka huu, Esma alitan- gaza rasmi kumwagana na Petit kwa kile ali- chodai kuwa jamaa huyo amekuwa akimkwami- sha katika mambo yake ya kimaendeleo.