“Sithubutu Kabisa Kugusa Simu Ya Mke Wangu”-Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi maisha anayoishi na Mke wake movie star Irene Uwoya.

Dogo Janja amefunguka na kuongelea ndoa yake na kuweka wazi kuwa ingawa hakuna mipaka katika ndoa yao lakini hakuna mtu kati yao ambaye anashika simu ya mpenzi wake.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Gazeti la Dimba, Dogo Janja ameweka wazi kuwa amekuwa akishirikiana kila kitu na mkewe huyo, lakini mambo ya kwenye simu hataki kuyasikia.

Yule ni mke wangu na ninaheshimu hilo…tunashirikiana vingi kwa kuwa ni zaidi ya wapenzi, lakini sitaki wala sijawahi kukagua simu yake na hata yeye ni hivyo hivyo”.

Dogo Janja amesisitiza kuwa yeye na Mke wake wamekuwa wakiheshimiana na kila mmoja amekuwa na uhuru na mwenzake, jambo ambalo anaamini litadumisha ndoa yao.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.