Sitaweza Kupata Ajira Kwa Ajili Ya Umbo Langu – Poshy Queen
Socialite maarufu kwenye mitandao ya kijamii mwenye umbo la kipekee Jacqueline Obeid maarufu kama Poshy Queen amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuajiriwa.
Poshy Queen aliyemaliza Stashahada ya Insurance and Risk Management katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar, amesema hataki kuajiriwa kwani anajua atakavyosumbuliwa.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Poshy Queen alifunguka kuwa anamshukuru Mungu kwani hata alipokuwa chuoni alikuwa ameshaanza kufanya biashara hivyo baada ya kumaliza chuo atajiari mwenyewe.
Sitaki kuajiriwa maana najua nitakayokutana nayo. Ni bora kujiajiri mwenyewe nitakuwa huru na umbo langu”.
Poshy Queen pia amefungukia tetesi za kuwa na shepu feki ambapo ameweka wazi kuwa shepu yake ni origino kabisa.