Sister Fey Aelezea Jinsi TCRA Walivyomshugulikia Baada Ya Kuachia Picha Chafu
Muigizaji wa Bongo movie na msanii anayefanya muziki wa Bongo fleva Faidha Omary maarufu kama Sister Fey amefunguka na kueleza Jinsi TCRA walivyomshughulikia baada ya kuachia picha chafu kwenye mitandao ya kijamii.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Sister Fay alisema tangu walipokamatwa na polisi na mumewe Holy Star mwezi wa tisa kutokana na kutumia mtandao vibaya kwa video zao tata, wamekuwa wakihenyeka na hawapo mtandaoni kutokana na simu waliyokuwa wanaitumia kushikiliwa polisi mpaka sasa.

Tuliingia matatani kwa sababu ya video na picha tulizokuwa tunawekakwenye Mitandao na tukaamuriwa kuacha simu zetu pamoja na laini kule polisi huku tukipigwa marufuku kutumia mitandao mpaka tutakaporuhusiwa na TCRA kwa hiyo ndiyo maana tupo kimya“.
Sister Fey na mume Wake Msanii Hollystar walijizolea umaarufu kwenye mitandao ya kijamii Baada ya video za vituko kuvutia wengi lakini waliingia matatani Baada ya kuachia video zenye utata.