Sista Fey Awekwa Ndani Kwa Amri Ya Naibu Waziri
Muigizaji wa Bongo movie na msanii wa Bongo fleva Faidha Omary maarufu kama Sista Fey amejikuta katika upande mbaya wa sheria baada ya kuwekwa rumande.
Sista Fey yupo chini ya ulinzi kufuatia tabia yake ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo imempa umaarufu mkubwa na kujulikana na watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii.
Sista Fay na mpenzi wake ambaye pia ni msanii Hollystar walijizolea umaarufu baada ya kuposti video mbali mbali ambazo ziliangaliwa kama kuwa ni kinyume na maadili ya Kitanzania.
Taarifa ya kuwekwa chini ya ulinzi imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika: