Sijawahi Kulia Kuwa Nina Shida Kwa Wema- Mama Kanumba
Mama mzazi wa aliyekuwa msanii wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba, Mama Kanumba amefunguka na kusema kuwa hajawahi kulia shida kwa Wema sepetu hata siku moja.
Mama Kanumba amefunguka hayo baada ya habari kusambaa mwanzoni mwa wiki hii kuwa alienda nyumbani kwa Wema Sepetu lakini alivyofika hapo hakufunguliwa geti.
Jambo lililopelekea Mama huyo kwenda kulalamika kwenye vyombo vya habari kuwa Wema kamwambia aende nyumbani kwake akamtembelee lakini alivyofika pale akawaambia walinzi wake wasifungue geti.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Mama Kanumba amefunguka kuwa hana tatizo na Wema ila hajawahi kwenda kuomba pesa kama watu wengi walivyodhani baada ya kusikia alienda nyumbani kwa Wema:
Kusema ukweli sina bifu na Wema, na hakuna binti ninayempenda kama Wema na siku zote nimekuwa nikisema sijawahi kumsema vibaya ila hii ni stori tu inaumdwa naomba Wema popote alipo ajue mimi sina bifu naye na sina ubaya naye tukionana tusalimiane na tupendane”.
Lakini Mama Kanumba aliongelea ishu ya yeye kwenda kugonga nyumbani kwa Wema na kutofunguliwa mlango:
Unaweza ukaenda ukagonga mlango labda hakuwepo au alikuwa ana shida zake aache kunifungulia kwani mimi nilikuwa namdai au yeye alikuwa ananidai? Alafu wengine wanadai nilikuwa nataka kumuomba hela waende wakamuulize sijawahi kwenda kwake kuomba hela au kulia shida”.