Sijawahi Kuacha Kumpenda Dogo Janja- Irene Uwoya
Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ameibuka na kudai kuwa pamoja na yote yaliyotokea lakini bado anampenda aliyekuwa mume Wake Msanii wa Bongo fleva Abdul Chende ‘Dogo Janja’.
Baada ya kufunga ndoa mwishoni mwa mwaka jana Irene na Dogo Janja walifikia tamati ya mahusiano yao mapema mwaka huu Baada ya Penzi Lao kugubikwa na wingu la usaliti wa kimapenzi.
Baada ya ndoa hiyo kuvunjika kumekuwa na maswali mengi ya tamati ya ndoa hiyo kwani hivi karibuni Uwoya amesikika akisema yeye hakubadilisha dini ili kufunga ndoa na Dogo Janja.
Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Irene Uwoya alipohojiwa endapo ameshapewa talaka yake na Dogo Janja Msanii huyo alijibu
Sijapewa talaka na Dogo Janja na sijawahi kuacha kumpenda hata siku moja, lakini maisha mengine lazima yaendelee na ndiyo maana nikasema sasa hivi niko bize kufanikisha ndoto zangu nyingi nilizokuwa nimejiwekea kwa muda mrefu.
Mambo hayo ya kuolewa niwaachie wengine mimi sitaki tena ndoa”.
Lakini pia Uwoya ameongelea utajiri ambao amekuwa akiuonyesha kwenye mitandao ya kijamii katika siku za Hivi karibuni:
Jamani tatizo la watu wengi wanapenda sana kuwaangalia watu kwa wasiwasi na wengi wanapenda sana kujua mtu anafanya nini au amepata wapi fedha. Sidhani kama ni sawa kuweka wazi kila kitu ambacho mtu anakifanya, kuna wakati mtu unakuwa kimya wao wanaona mambo yako tu yakinyooka”.