Shiloleh amuomba Diamond Amuoe Zari
Mwanadada Shiloleh ambae ndoa yake imedumu mpaka sasa tangu walipofunga ndoa na mume wake, amemshauri msanii mwenzake Diamond platinumz kuamua kumuoa zari ambae alikuwa mpenzi wake lakini pia ni mzazi mwenzake wa watoto wawili.
Shiloleh anasema kuwa hakuna mwanamke anaeona anamfaa diamond zaidi ya zari kwa sababu wanawake wengine hawawezi kuendana hata siku moja.
nitafurahi sana kama Diamond ataoa, lakini katika kumbukumbu zake lazima arudi nyuma, akumbuke kumuoa zari kwa sababu hata akioa mwanamke mwingine sijui ni nani atakaemfaa.
Ni zaidi ya mwaka sasa tangu msanii huyo aliachana na mwanamama huyo kutoka Uganda na kila mtu kuendelea na maisha yake huku msanii huyo akiwa anabadilisha idadi ya wanawake kila siku.