Shiloleh Amkumbuka Sharo Millionea
Mwanadada Shiloleh amefunguka na kusema kuwa moja kati ya watu anaowakumbuka sana katika maisha yake ni msanii sharo millionea ambae amefariki miaka mingi nyuma kuwa ndio alikuwa alimpenda na kumchukulia kama ndugu yake katika sanaa.
Shiloleh ambae aliongea na ilifika sehemu alishindwa kuendelea kuongea anasema kuwa , Sharo Millionea alikuwa hawezi kukaa mbali na yeye kiasi kwamba hata alipokuwa akitaka kwenda kulala alikuwa radhi alale sebleni .
Ikumbukwe kuwa shilole na Sharo Milionea walikuwa marafiki sana kiasi kwamba ikifikia hatua baadhi ya mashabii walikuwa wakihoji sana mahusiano yao kutokana na ukaribu wao.