Shiloleh Afunguka Swala la Kumzalia Uchebe.
Mwanadad Shiloleh amefunguka na kuelezea kuhusu swala lakutaa kumzaliwa mume wake Uchebe ambae kwa sasa wanatimiza zaidi ya mwaka tangu kufungwa kwa ndoa hiyo lakini hakuna dalili ya Shiloleh kuwa mjamzito.
Hata hivyo wawili hao pamoja na kwamba wameoa , lakini tayari kila mmoja tayari alikuwa na watoto wawili hivyo kufanya familia yao kuwa na watoto wanne tayari.
Shiloleh anasema kuwa hata yeye amekuwa akitamani sana kumzalia mume wake huyo mtoto kama zawadi lakini anaamini kuwa muda utakapofika basi kila kitu kitakuwa sawa.